MAGEREZA MKOA WA TANGA YAANZA MAANDALIZI YA UKARABATI WA OFISI MPYA ZA UTAWALA, JIJINI TANGA
Mkuu
wa Magereza Mkoa wa Tanga, Naibu Kamishna wa Magereza Edither Malya(wa
pili kulia) akielezea hatua mbalimbali za Maandalizi ya ukarabati wa
Jengo la Ofisi za Utawala za Magereza Mkoa wa Tanga(wa kwanza kulia) ni
Afisa Habari wa Jeshi la Magereza, Mkaguzi wa Magereza Deodatus Kazinja
alipotembelea kujionea hatua mbalimbali za ukarabati unaoendelea leo
Februari 7, 2014 Jijini Tanga.
Muonekano
wa mbele wa Jengo la Kikoloni ambalo linalotarajiwa kukarabatiwa kwa
ajili ya Ofisi za Utawala za Magereza Mkoa wa Tanga. Jengo hilo hapo
awali lilitumika kama Kituo Kikuu cha Polisi Mkoa wa Tanga ambapo hivi
sasa Jeshi la Magereza tayari limeanza ukarabati wa jengo hilo. Wa
kwanza katika picha ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga, Naibu Kamishna wa
Magereza Edither Malya akiwa ameongozana na baadhi ya Maafisa
Waandamizi wa Jeshi la Magereza leo Februari 07, 2014 Jijini Tanga.
Tofali
ambazo zimefyatuliwa kwa ajili ya ukarabati wa Jengo la Ofisi za
Utawala za Magereza Mkoa wa Tanga. Ukarabati huo wa Ofisi mpya za
Utawala unaanza hivi karibuni Jijini Tanga na utasimamia kwa karibu na
Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga.
Mkuu
wa Magereza Mkoa wa Tanga, Naibu Kamishna wa Magereza Edither Malya
akiongoza Kikao kazi Ofsini kwake pamoja na baadhi ya Maafisa Waandamizi
wa Jeshi la Magereza wanaofanya kazi Ofisi ya Magereza Mkoa wa Tanga
leo Februari 07, 2014 alipotembelewa Ofsini kwake na timu ya Maafisa
Habari kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Dar es
Salaaam(hawapo pichani)
Mkuu
wa Magereza Mkoa wa Tanga, Naibu Kamishna wa Magereza Edither Malya(wa
tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa
Waandamizi wa Jeshi la Magereza wanaofanya kazi Magereza Mkoa wa Tanga
baada ya kutembelea sehemu mbalimbali ya maandalizi ya ukarabati wa
Ofisi Mpya za Utawala za Magereza Mkoa wa Tanga leo Februari 07,
2014(wa Nne kulia) ni Mnadhimu Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga, Kamishna
Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Augustino Mboje
(Picha zote na Lucas
Mboje wa Jeshi la Magereza).