Featured Post Today
print this page
Latest Post

Matumizi ya baiskeli Afrika

Matumizi ya baiskeli Afrika

Nishati juu ya magurudumu mawili

 

  • Ein Kohletransporteur fährt auf einem Feldweg mit schweren Holzkohlesäcken auf dem Gepäckträger (Foto:Gerald Henzinger)
    Mkaa husafirishwa hadi umbali wa kilomita 100 kwa baiskeli na kupelekwa Beira, mji wa pili kwa ukubwa Msumbiji. Katika maeneo ya vijijini barabara nyingi ni mbovu kwa hiyo wakati mwingine ni rahisi zaidi kusafiri kwa baiskeli kuliko kwa gari. Wakaazi wengi wanawategemea wauza mkaa kwa sababu hawana uwezo wa kununua umeme au gesi.

 

0 comments

Matumizi ya baiskeli Afrika

Matumizi ya baiskeli Afrika

  • Ein Mann transportiert Holzkohle auf dem Fahrrad nahe der zentralmosambikanischen Stadt Beira (Foto: Gerald Henzinger)

    Mzigo wa kilo 300

    Hakuna jambo lisilowezekana - labda hayo yalikuwa mawazo ya bwana huyu kutoka Msumbiji. Amepakia magunia sita ya mkaa kwenye baiskeli yake. Mzigo huo una uzito wa karibu kilo 300. Hapo hakuna tena kuendesha, kinachobaki ni kuisukuma baiskeli. Amefunga kamba kwenye usukani ili aweze kuiongoza baiskeli yake vizuri.

 

0 comments

Marekani yasisitiza itaiadhibu Syria

Marekani yasisitiza itaiadhibu Syria

Marekani yasisitiza itaiadhibu Syria

Marekani imedhihirisha wazi kuwa itaiadhibu Syria kwa shambulio la Damascus ambapo zaidi ya watu 1,400 waliuawa huku wachunguzi wa umoja wa Mataifa wakikamilisha uchunguzi wao na kuondoka Syria leo (31.08.2013).
Rais wa Marekani Barrack Obama amesema hawawezi kukubali ulimwengu ambao unaruhusu wanawake, watoto na raia wasio na hatia kuuawa katika kiwango kikubwa.

Obama amesema Marekani bado inapanga hatua za kijeshi lakini hajaeleza ni lini hasa hatua hizo zitachukuliwa.Matamshi yake yanakuja huku nchi yake ikitoa ripoti ya kijasusi inayoonyesha utawala wa Syria ulishambulia eneo karibu na mji mkuu Damasacus na kuwaua watu 1,429 wakiwemo watoto 426.
Obama amesema ulimwengu una wajibu wa kuhakikisha kuwa hakuna matumizi ya silaha za kemikali na kulishutumu baraza la usalama la umoja wa mataifa kwa kushindwa kuafikiana kuhusu hatua gani ichukuliwe dhidi ya Syria.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry hapo jana alizungumza na mawaziri wenzake kutoka Uingereza, Misri, Ujerumani, Uholanzi, New Zealnd, Saudi Arabia na Milki za falme ya kiarabu pamoja na katibu mkuu wa umoja wa nchi za kiarabu.

Ufaransa imeunga mkono msimamo wa Marekani kwa kusema ujumbe mzito unapaswa kufikishwa kwa utawala wa Rais Bashar al Assad. Bunge la Uingereza lilipinga nchi hiyo kujihusisha na hatua za kijeshi dhidi ya Syria baada ya kupiga kura kupinga azma ya waziri mkuu David Cameron.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry akizungumzia hali nchini Syria kufuatia shambulio la gesi ya sumu  
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry akizungumzia hali nchini Syria kufuatia shambulio la gesi ya sumu
 
Urusi ambayo ni mshirika mkubwa wa Syria imetilia shaka uchunguzi wa kijasusi wa Marekani kuhusu shambulio hilo la tarehe 21 mwezi huu la gesi ya sumu na kuonya kutochukuliwa hatua zozote za kijeshi kabla ya kuidhinishwa na umoja wa Mataifa.

Wachunguzi wakamilisha uchunguzi Damascus
Umoja wa Mataifa hapo jana ulitangaza kuwa wachunguzi wao wamekamilisha kukusanya uchunguzi wao mjini Damascus na huenda ikachuka wiki kadhaa kwa wao kutathmini na kuwasilisha ripoti kamili kuhusu uchunguzi huo.

Kundi hilo la wachunguzi limeonekana leo likiondoka katika hoteli waliyokuwa wakikaa mjini Damascus katika msafara wa magari ulionekana katika barabara kuu inayoelekea nchi jirani ya Lebanon.
Wachunguzi hao wameahidi kuharakisha kutoa ripoti yao na wanatarajiwa kuripoti kwa katibu mku wa umoja huo Ban ki Moon ambaye amezihimza nchi za magharibi kuruhusu uchunguzi huo kutathiminiwa kwa kuwa na subira.

Kerry amesema kushindwa kuchukua hatua dhidi ya Syria kutakengeuka desturi ya kupiga marufuku matumzi ya silaha za kemikali na kuzipa nguvu Iran na kundi la wanamgambo la Hezbollah kuzitumia.

Je Marekani itaungwa mkono na nchi nyingine?
Marekani imelazimika kuangalia kwingine kupata uungwaji mkono baada ya bunge la Uingereza kupinga kujihusisha kwa nchi hiyo kijeshi na Syria. Ujerumani na Canada zimesema bayana kuwa nazo hazitashiriki katika hatua za kijeshi lakini Rais wa Ufaransa Francois Hollande amesema hatua ya Uingereza haitabadili msimamo wa serikali yake kuhusu umuhimu wa kuvamiwa kwa Syria.Uturuki nchi jirani na Syria pia inaiunga mkono Marekani.

Wachunguzi wa Umoja wa Mataifa wakiondoka hotelini mwao mjini Damascus  
Wachunguzi wa Umoja wa Mataifa wakiondoka hotelini mwao mjini Damascus
 
Urusi na Iran zimeionya Mareknai na nchi za magharibi kutochukua hatua zozote za kijeshi badala yake kutafutwe suluhu la kisiasa kutatua mzozo wa Syria.
Marekani inajikuta katika hali tete hasa baada ya vita vya Iraq na Afghanistan ambavyo kuhusika kwake kunaonekana kutokuwa na tija badala yake kuziacha nchi hizo katika hali mbaya zaidi.
Kulingana na umoja wa Mataifa,kiasi ya watu 100,000 wameuwa katika vita hivyo vya wenyewe Syria tangu vianze zaidi ya miaka miwili iliyopita na mamilioni wengine wamekuwa wakimbizi.

 

0 comments

CHELSEA YAPIGWA NA BAYERN KWA MATUTA BAADA TA SARE MYUVUBH

CHELSEA YAPIGWA NA BAYERN KWA MATUTA BAADA TA SARE MYUVUBH 

BAYERN Munich imetwaa Super Cup ya Ulaya baada ya kuifuna Chelsea kwa penalti 5-4 kufuatia sare ya 2-2 na Jose Mourinho ameshindwa kutwaa taji la kwanza baada ya kurejea darajani mbele ya Pep Guardiola.
Katika mchezo huo, ambao Chelsea ilimaliza pungufu baada ya Ramires kutolewa nje kwa nyekundu dakika ya 84, mabao ya The Blues yalifungwa na Torres dakika ya nane na Hazard dakika ya 93, wakati ya Bayern yalifungwa na Ribery dakika ya 47 na Javi Martinez dakika ya 120.
Katika mikwaju ya penalti, Ashley Cole alifunga Cech akaokoa penalti Xherdan Shaqiri. 
Penalti nyingine zilizofungwa na David Luiz, Oscar na Frank Lampard kwa upande wa  Chelsea, wakati za Bayern zilifungwa na Jerome Boateng, Toni Kroos, Philipp Lahm na Franck Ribery hivyo kuteneneza ushindi wa 5-4.

Loss: Lukaku looks on after his decisive penalty miss in Prague
Loss: Lukaku looks on after his decisive penalty miss in Prague
Champions again: Bayern celebrate the win after Neuer's penalty save
Champions again: Bayern celebrate the win after Neuer's penalty saveLevel: Javi Martinez (right) scores for Bayern in the last minute of extra time
Level: Javi Martinez (right) scores for Bayern in the last minute of extra time
Strike: Hazard scored his first goal of the season in the 93rd minute, driving low past Neuer
Strike: Hazard scored his first goal of the season in the 93rd minute, driving low past Neuer
Ahead: Hazard put Chelsea 2-1 up in extra time in Prague
Ahead: Hazard put Chelsea 2-1 up in extra time in Prague
Off you go: Ramires was sent off late in normal time for a second bookable offence
Off you go: Ramires was sent off late in normal time for a second bookable offence
In behind: Ashley Cole of Chelsea and Arjen Robben battle for the ball
In behind: Ashley Cole of Chelsea and Arjen Robben battle for the ball
Great strike: Torres wheels away after putting Chelsea 1-0 up
Great strike: Torres wheels away after putting Chelsea 1-0 upLevel: Franck Ribery scored just after half-time for Bayern with a 20-yard drive
Level: Franck Ribery scored just after half-time for Bayern with a 20-yard drive
Penalties
Fanatics: Bayern supporters paint Prague red before the game
Fanatics: Bayern supporters paint Prague red before the game
Momentum: Mourinho was looking to continue his unbeaten start as Chelsea boss
Momentum: Mourinho was looking to continue his unbeaten start as Chelsea boss
Man manager: Ribery went straight to Bayern boss Pep Guardiola after scoring the equaliser
Man manager: Ribery went straight to Bayern boss Pep Guardiola after scoring the equaliser
New venue: Stadion Eden in Prague was the stage for the final, which is usually held in Monaco
New venue: Stadion Eden in Prague was the stage for the final, which is usually held in Monaco

 

0 comments

JAMII YAASWA KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI.

JAMII YAASWA KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA    POLISI.

Na Amina Omari,Tanga
Jamii imeaswa kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi badala ya kuwaona ni kama maadui kwao hasa wanapofuatilia taarifa za uhalifu  ili kuhakikisha wanashirikina katika kulinda na kuzuia vitendo vya kihalifu  vinavyofanyika miongoni mwa jamii .
Ushauri huo umetolewa na Kamanda wa polisi mkoa wa Tanga Costantine Massawe  wakati  wa maadhimisho ya siku ya polisi ambapo kwa mkoa wa Tanga wameadhimisha kwa kutembelea kituo cha waathirika wa madawa ya kulevya  SOBAR HOUSE pamoja na kituo cha kulelea watoto yatima na kutoa misaada ya kijamii.
Alisema jamii imekuwa ikilichukulia jeshi hilo kama sehemu ya maadui jambo ambalo sio kweli kwani  nia ya uwepo wao ni kuhakikisha wanalinda mali za wananchi pamoja na kuzuia uhalifu wa aina yoyote usitokee miongoni mwa jamii na taifa kwa ujumla.
“Lengo la maadhimisho ya siku ya polisi ni kufanya kazi ambazo zitaonyesha tupo karibu na jamii ikiwemo kama kufanya usafi kwenye hospitali  kwa Tanga tumeamua kutembelea ndugu zetu walioathirika na madawa ya kulevya pamoja na watoto yatima “alisema Kamnda Massawe.
Awali akiwa SOBAR HOUSE aliwataka waathirika hao kuhakikisha hawarudi tena kwenye utumiaji wa madawa ya kulevya baada ya kupona na kuwahamasisha wenzao kutotumia madawa hayo kwa kuwaeleza madhara yatokanayo na matumizi ya dawa hizo
“Nawaomba baada ya kupona msikubali kurudi tena kwenye utumiaji wa madawa hayo kwani yanarudisha nyuma maendeleo yenu na taifa kwa ujumla kwani  mnapoteza muda mwingi kwenye matibabu yake na nguvu kazi ya taifa inapotea bure”aliwaasa Kamanda.
Hata hivyo akiwa kwenye kituo cha watoto yatima cha Abdillah bin Omari  aliiasa jamii ya wanatanga  kutowatenga watoto hao  bali  kuwatambua ni  sehemu yao   kwa kuwaonyesha upendo ili wajiihisi nao ni wajamii kama wengine
Jumla ya msaada wenye thamani ya sh Laki saba ulitolewa kwa vituo hivyo ikiwemo fedha taslim sh laki tanona katoni nne za maji ya matunda  kwa  kituo cha SOBAR HoUSE pamoja na mchele kilo 50 ,mafuta ya kupikia lita 10  na maji ya matunda katoni sita kwa ajili ya kituo cha Abdi Abdulrahmani
0 comments

TFF wasaini mkataba wa haki za kipekee za televisheni ya Azam kwa ajili ya kuonyesha mechi za ligi Kuu

TFF wasaini mkataba wa haki za kipekee za televisheni ya Azam kwa ajili ya kuonyesha mechi za ligi Kuu

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kampuni ya Azam Media leo (Agosti 30 mwaka huu) wamesaini mkataba wa haki za kipekee za televisheni (exclusive rights) utakaoiwezesha Azam TV kuonesha mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL).
Rais wa TFF. Leodgar Tenga
Mkataba huo wa miaka mitatu wenye thamani y ash. 5,560,800,000 umesainiwa kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Makamu wa Rais, Athuman Nyamlani amesaini kwa niaba ya TFF wakati aliyesaini kwa upande wa Azam Media ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo Thys Torrington.
Ligi Kuu ya Tanzania sasa itakuwa ikipatikana kupitia kisimbuzi (decorder) cha Azam TV kitakachokuwa na chaneli zaidi ya 50. Mechi hizo zinatarajiwa kuoneshwa moja kwa moja wakati wowote kuanzia mwezi ujao.
Makamu wa Rais wa TFF, Nyamlani amesema udhamini huo wa televisheni ni fursa pana kwa klabu kwani zitaweza kujitangaza zaidi huku wachezaji nao wakipata soko zaidi za mpira wa miguu.
0 comments

Francis Cheka amtandika Mmarekani Phil Williams Ukumbi wa Diamond Jubilee na kuwapa raha Watanzania

Francis Cheka amtandika Mmarekani Phil Williams Ukumbi wa Diamond Jubilee na kuwapa raha Watanzania

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BONDIA wa Tanzania, Francis Cheka, ameendeleza ubabe wake baada ya kumtandika mpinzani wake Phil Williams katika pambano lao lililofanyika usiku wa kuamkia leo katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.
Bondia wa Tanzania, Francis Cheka, pichani
Ushindi huo wa Cheka ni furaha kubwa kwa Watanzania wote, hususan wale wanaotokea mkoani Morogoro ambapo mkali huyo ndipo anapotokea kwenye mji huo.
Cheka alipata ushindi huo na kunyakua ubingwa wa Dunia wa WBU, baada ya kumpiga Williams kwa pointi kuonyesha kuwa yeye ni mkali na hana mpinzani hapa Tanzania.
Mbali na kufanikiwa kumchapa Mmarekani huyo, mara kwa mara Cheka amekuwa akiibuka na ushindi kila anapoingia ulingoni kupambana na mabondia wa Tanzania.
0 comments

KUTOKA KWENYE MAGAZETI YA MICHEZO NA BURUDANI JUMAMOSI AGOSTI 31/ 2013.

0 comments

M23 yatangaza kusitisha mapigano;

M23 yatangaza kusitisha mapigano;

m23_2fb74.jpg
Kundi la waasi wa M23 katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo limesema kuwa linasimamisha mapigano mara moja, kuruhusu uchunguzi juu ya makombora yaliyovuka mpaka na kuanguka katika nchi jirani ya Rwanda.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Lambert Mende, ameiambia DW mjini Kinshasa kuwa serikali ya nchi hiyo haijashangazwa na hatua hiyo ya M23, lakini akasisitiza kuwa wanachotaka wao ni kuona waasi hao wakiweka silaha chini, kama wanavyotakiwa na jumuiya ya kimataifa na pia serikali ya Kongo.
Jana, Rwanda ililishutumu jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa kile ilichokiita uchokozi wa makusudi, baada ya kombora linaloaminika kutoka upande wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuanguka nchini Rwanda, na kumuuwa mwanamke mmoja na kumjeruhi vibaya mtoto wake mchanga.
Serikali ya Kongo ilizikanusha mara moja tuhuma hizo, ikisema zilikuwa zikiashiria azma ya Rwanda kujiingiza waziwazi katika vita vinavyoendelea mashariki mwa nchi hiyo.
Kikomo cha uvumilivu
Kufuatia kifo cha mwanamke huyo katika mji wa Rubavu kaskazini magharibi mwa Rwanda, wizara ya mambo ya nje ya Rwanda ilitoa tangazo ambalo limesema nchi hiyo inao uwezo wa kujua yalikotoka mashambulizi dhidi yake, na kuonya kuwa haitasita kulinda eneo lake na kuwatetea wananchi wake.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Rwanda, Louise Mushikiwabo, amesema katika kipindi cha mwezi mmoja, jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo limerusha mabomu yapatayo 34 ndani ya Rwanda. ''Tumejizuia tuwezavyo kuchukuwa hatua, lakini sasa hatuwezi kuendelea kuvumilia uchokozi huu.'' Amesema Bi Mushikiwabo.
Kongo yasema ni kisingizio
Akijibu tuhuma kutoka Rwanda kuwa jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ndilo linalorusha mabomu yanayoanguka nchini Rwanda, Waziri Mende amesema tuhuma hizo zinalenga kuhalalisha kujiingiza tena katika mikoa ya Kivu. ''Inachoazimia Rwanda ni kusababisha vurugu isiyokwisha ili iweze kuendelea kupora mali katika mikoa ya kivu, kama ambavyo imekuwa ikifanya kwa miaka 15 iliyopita,'' alisema Mende.
Wakati huo huo, Umoja wa Mataifa ulisema jana kwamba unazo ''ripoti za kuaminika'' za kuaminika, ambazo zinaonyesha kuwa wanajeshi wa Rwanda wameingia katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Rwanda kuwasaidia waasi wa M23, katika vita linayopigana dhidi ya jeshi la Kongo na wanajeshi wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO.
Aidha, afisa wa ngazi ya juu wa MONUSCO, Ray Vilgilio Torres amesema vikosi vyao vimepata uhakika kuwa bomu lililomuuwa mwanamke nchini Rwanda, lilirushwa na waasi wa M23, kutoka ngome yao ya msitari wa mbele ya Kibati.

 

0 comments

Wafanyakazi wa migodi kugoma Afrika Kusini;

Wafanyakazi wa migodi kugoma Afrika Kusini; 

madinisouth_16793.jpg
Wamiliki wa migodi ya madini nchini Afrika Kusini, wamesema kuwa wafanyakazi wao wameitisha mgomo wa kitaifa kuanzia siku ya Jumanne, kutaka mishahara yao kuongezwa.
Chama cha kitaifa cha wachimba migodi, NUM kimeitisha nyongesa ya mishahara ya hadi asilimia sitini
Mapema wiki hii wafanyakazi hao walikataa pendekezo la waajiri wao la kutaka mishahara yao kuongezwa kwa asilimia sita, kiwango ambacho ni sawa na mfumuko wa bei kwa sasa nchini Afrika Kusini.
Afrika Kusini ni miongoni mwa mataifa yanayoongoza kwa uzalishaji wa dhahabu, lakini kiwango chake kimeshuka kutokana na uwekezaji duni na uhasiano mbaya kati ya wafanyakazi na wamiliki wa migodi hiyo.
Kampuni kubwa za kuchimba madini nchini humo za AngloGold Ashanti, Gold Feilds, Harmony Gold na Sibanye na kampuni zingine ndogo ndogo tayari zimepokea ilaani hiyo ya mgomo.
Chama hicho cha NUM huakilisha asilimia sitini na nne ya wafanyakazi wa migodi wapatao elfu mia moja ishirini.
Taifa la Afrika Kusini kwa sasa linakabiliana na athari za mgomo wa wafanyakazi wa secta ya utengenezaji magari, ujenzi na wale wa viwanja vya ndege.
Wafanyakazi wa secta ya kuuza mafuta vile vile wameitisha mgomo kuanzia wiki ijayo.
Serikali ya nchi hiyo imetoa wito kwa wafanyakazi hao kudumisha amani wakati wa mgomo wao.
Mwaka uliopita, wafanyakazi thelathini na wanne wa migodi waliokuwa wakiandamana waliuawa kwa kupigwa risasi na polisi wakati ghasia zilipoibuka wakati wa mgomo wao.
Wachanganuzi wa masuala ya kisiasa wanasema utawala wa rais Jacob Zuma unakabiliwa na changamoto kutoka pande zote.
Wanachama wa chama chake tawala cha African National Congress ANC wanamtaka rais Zuma, kutenda zaidi ili kupunguza viwango vya umasikini, nao wafanyabiashra wanataka serikali yake kupunguza ukiritimba ili kuvutia uwekezaji kutoka mataifa ya kigeni na kuimarisha mikakati za kufufua uchumu wa taifa hilo.

 

0 comments

Bayern ni mabingwa wa UEFA Super Cup

Bayern ni mabingwa wa UEFA Super Cup 

bayern_c69ae.jpg
Bayern Munich imeshinda taji la EUFA Super Cup kwa kuichapa Chelsea mabao 5-4 kupitia mikwaju ya penalti katika mechi iliyochezwa jana usiku kwenye uwanja wa Eden Arena mjini Prague, Jamhuri ya Cheki.(P.T)
Bayern Munich, ikiongozwa na kocha wao mpya, Pep Guardiola, imelipiza kisasi kwa kushindwa na Chelsea katika fainali ya Champions League mwaka 2012 baada ya kuifunga klabu hiyo mabao 5-4 kupitia mikwaju ya penalti kufuatia mtanange wa kuwania kombe la UEFA Super Cup kuishia sare ya mabao 2-2 baada ya muda wa ziada kumalizika.
Bao la Bayern sekunde chache kabla mchezo kumalizika, liliufungua mlango wa kuelekea ushindi kupitia penalti dhidi ya Chelsea chini ya kocha wao mpya, Jose Mourinho. Penalti zote tisa ziliutikisa wavu kabla mkwaju wa penalti wa mchezaji wa Chelsea, Romeu Lukaku, kuokolewa na kipa wa Bayern Munich, Manuel Neuer, na hivyo kuwapa ushindi mabingwa wa Ulaya, Bayern Munich, dhidi ya mabingwa wa ligi ya Ulaya, Chelsea.
Ushindi wa kwanza katika historia
Hii ni mara ya kwanza kwa Bayern Munich kushinda kombe la UEFA Super Cup katika historia yake, baada ya kupoteza fainali nyengine tatu. Fernando Torres aliifungia Chelsea bao la kwanza dakika ya nane ya mchezo, pale alipopewa mpira na Mjerumani Andre Shuerrle. Frank Ribery alisawazisha dakika ya 47 katika kipindi cha pili kupitia mkwaju mkali akiwa mita 25 kutoka lango la Chelsea, mkwaju ambao kipa wa Chelsea, Petr Cech, hakuweza kuuzuia.
"Nina furaha sana kwa ajili ya timu yangu na kocha wangu. Ilikuwa siku maalumu sana kwake katika uhasama wake wa kihistoria na hasimu wake Mourihno," amesema Frank Ribery baada ya kuinua kikombe hicho. "Tulikuwa na bahati leo. Nadhani ushindi huu utatusaidia na utatupatia motisha zaidi," akaongeza kusema Ribery.
11_cdca1.jpg
Kiungo wa Chelsea, Ramires, alitolewa uwanjani dakika ya 85 kwa kuonyeshwa kadi nyekundu baada ya kumfanyia madhambi Mario Goetze wa Bayern. Hata hivyo vijana 10 wa Jose Mourinho walifunga bao la pili dakika ya tatu ya kipindi cha kwanza cha muda wa ziada kupitia Mbelgiji Eden Hazard. Hazard aliwachenga walinzi wawili wa Bayern katika wingi ya kushoto na kuvurumisha mkwaju uliopita mikono ya mlinda lango wa Bayern, Manuel Neuer, na kuutikisa wavu. Timu ya Pep Guardiola iliendelea kukidhibiti kindumbwendumbwe hicho, kama ilivyofanya wakati ilipokuwa ikiongozwa na kocha wa zamani, Jupp Heynckes, katika fainali ya Champions League miezi 15 iliyopita, lakini juhudi zao za kufunga mabao zilikwamishwa na kipa wa Chelsea, Petr Cech, aliyekuwa macho sana kila mara akiokoa mabao ambayo yalikuwa yaingie wavuni.
12_745b3.jpg
Pep 'ampepeta' Mourinho
Ilionekana kana kwamba Chelsea wangeshinda mpambano huo kwa mabao 2-1, hadi pale Javi Martinez wa Bayern, aliposawazisha sekunde chache tu kabla kipyenga cha mwisho kupulizwa kumaliza kipindi cha mwisho cha muda wa ziada. "Wanachukua kikombe lakini timu bora imeshindwa. Wapinzani wetu wamefunga magoli mawili na sisi pia tumefunga mawili. Lakini wamefunga penalti moja zaidi kuliko sisi. Ni wazi kabisa timu bora imepoteza mechi hii," amesema kocha wa Chelsea, Jose Mourinho, wakati wa mahojiano yake na Sky Sports.
"Kwangu mimi tulikuwa timu bora zaidi. Bayern walikuwa na dakika 15 katika kipindi cha pili ambazo walitawala mchezo na kuudhibiti mpira, lakini licha ya kuwa na wachezaji 10, tulicheza vizuri sana. Tumecheza dhidi ya mabingwa wa Ulaya na wachezaji wangu walikuwa timu bora - tuna sababu za kujivunia kuamini katika siku zijazo. Napendelea kusema tu kwamba timu bora imeshindwa na nitabaki na msimamo huo," akaongeza kusema Mourinho.
Akifurahia ushindi wake wa nane dhidi ya Mourinho katika michuano 16 iliyopita, Pep Guardiola amempongeza mtangulizi wake, Jupp Heynckes, aliyeiongoza Bayern kushinda mataji matatu msimu uliopita. "Nataka kumshukuru Jupp Heynckes kwa fursa ya kucheza katika fainali hii. Ni kwa sababu ya bidii yake kwamba tuko hapa."
Maoni na hisia tofauti
Guardiola ametofautiana na msimamo wa Mourinho kwamba timu bora imepoteza mechi hiyo. "Naamini timu bora ndiyo iliyoshinda. Sisi tulitengeneza nafasi nyingi za kufunga magoli. Chelsea ina wachezaji wenye uzoefu mkubwa kama vile Petr Cech, Frank Lampard, John Terry na Ashley Cole. Walikuwa na nafasi zao, lakini tulistahili kushinda." amesema kocha huyo wa Bayern.
13_1caed.jpg
Wakati huo huo, mlinda lango wa Chelsea, Petr Cech, amesema, "Tulitaka sana kushinda kombe hili na wao pia walitaka. Walilitafuta bao la kusawazisha na sisi tulikuwa tukiwazuia na kuimarisha kwa bidii safu yetu ya ulinzi. Inauma sana jinsi walivyofaulu kukomboa." Cech ameongeza kusema, "Kila mtu anaichukulia Bayern kama timu yenye nafasi nzuri ya kushinda Champions League msimu huu na kama timu bora duniani wakati huu, lakini tumeonyesha umahiri mkubwa, wakati mambo yalipokuwa yakituendea kombo."
Ni mchuano wa kwanza kuwania Super Cup kutochezwa Monte Carlo tangu mwaka 1997 na bila shaka ndio umekuwa wa kusisimua zaidi na wenye kumbukumbu nyingi kuliko michuano mingine yote. Pia ni fainali ya kwanza ya Super Cup ambapo mshindi amepatikana kupitia penalti.


 

0 comments

Marekani yasisitiza itaiadhibu Syria;

Marekani yasisitiza itaiadhibu Syria; 

obama_d4389.jpg
Marekani imedhihirisha wazi kuwa itaiadhibu Syria kwa shambulio la Damascus ambapo zaidi ya watu 1,400 waliuawa huku wachunguzi wa umoja wa Mataifa wakikamilisha uchunguzi wao na kuondoka Syria leo (31.08.2013).
Rais wa Marekani Barrack Obama amesema hawawezi kukubali ulimwengu ambao unaruhusu wanawake, watoto na raia wasio na hatia kuuawa katika kiwango kikubwa.(P.T)
Obama amesema Marekani bado inapanga hatua za kijeshi lakini hajaeleza ni lini hasa hatua hizo zitachukuliwa.Matamshi yake yanakuja huku nchi yake ikitoa ripoti ya kijasusi inayoonyesha utawala wa Syria ulishambulia eneo karibu na mji mkuu Damasacus na kuwaua watu 1,429 wakiwemo watoto 426.
Obama amesema ulimwengu una wajibu wa kuhakikisha kuwa hakuna matumizi ya silaha za kemikali na kulishutumu baraza la usalama la umoja wa mataifa kwa kushindwa kuafikiana kuhusu hatua gani ichukuliwe dhidi ya Syria.
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry hapo jana alizungumza na mawaziri wenzake kutoka Uingereza, Misri, Ujerumani, Uholanzi, New Zealnd, Saudi Arabia na Milki za falme ya kiarabu pamoja na katibu mkuu wa umoja wa nchi za kiarabu.
Ufaransa imeunga mkono msimamo wa Marekani kwa kusema ujumbe mzito unapaswa kufikishwa kwa utawala wa Rais Bashar al Assad. Bunge la Uingereza lilipinga nchi hiyo kujihusisha na hatua za kijeshi dhidi ya Syria baada ya kupiga kura kupinga azma ya waziri mkuu David Cameron.
Urusi ambayo ni mshirika mkubwa wa Syria imetilia shaka uchunguzi wa kijasusi wa Marekani kuhusu shambulio hilo la tarehe 21 mwezi huu la gesi ya sumu na kuonya kutochukuliwa hatua zozote za kijeshi kabla ya kuidhinishwa na umoja wa Mataifa.
Wachunguzi wakamilisha uchunguzi Damascus
Umoja wa Mataifa hapo jana ulitangaza kuwa wachunguzi wao wamekamilisha kukusanya uchunguzi wao mjini Damascus na huenda ikachuka wiki kadhaa kwa wao kutathmini na kuwasilisha ripoti kamili kuhusu uchunguzi huo.
Kundi hilo la wachunguzi limeonekana leo likiondoka katika hoteli waliyokuwa wakikaa mjini Damascus katika msafara wa magari ulionekana katika barabara kuu inayoelekea nchi jirani ya Lebanon.
Wachunguzi hao wameahidi kuharakisha kutoa ripoti yao na wanatarajiwa kuripoti kwa katibu mku wa umoja huo Ban ki Moon ambaye amezihimza nchi za magharibi kuruhusu uchunguzi huo kutathiminiwa kwa kuwa na subira.
Kerry amesema kushindwa kuchukua hatua dhidi ya Syria kutakengeuka desturi ya kupiga marufuku matumzi ya silaha za kemikali na kuzipa nguvu Iran na kundi la wanamgambo la Hezbollah kuzitumia.
Je Marekani itaungwa mkono na nchi nyingine?
Marekani imelazimika kuangalia kwingine kupata uungwaji mkono baada ya bunge la Uingereza kupinga kujihusisha kwa nchi hiyo kijeshi na Syria. Ujerumani na Canada zimesema bayana kuwa nazo hazitashiriki katika hatua za kijeshi lakini Rais wa Ufaransa Francois Hollande amesema hatua ya Uingereza haitabadili msimamo wa serikali yake kuhusu umuhimu wa kuvamiwa kwa Syria.Uturuki nchi jirani na Syria pia inaiunga mkono Marekani.
Urusi na Iran zimeionya Mareknai na nchi za magharibi kutochukua hatua zozote za kijeshi badala yake kutafutwe suluhu la kisiasa kutatua mzozo wa Syria.
Marekani inajikuta katika hali tete hasa baada ya vita vya Iraq na Afghanistan ambavyo kuhusika kwake kunaonekana kutokuwa na tija badala yake kuziacha nchi hizo katika hali mbaya zaidi.
Kulingana na umoja wa Mataifa,kiasi ya watu 100,000 wameuwa katika vita hivyo vya wenyewe Syria tangu vianze zaidi ya miaka miwili iliyopita na mamilioni wengine wamekuwa wakimbizi

 

0 comments

Serikali yasalimu amri kwa wabunge;

Serikali yasalimu amri kwa wabunge; 

bunge_802dc.jpg

Muswada wa Sheria ya Taifa ya Umwagiliaji wa mwaka 2013, jana ulipita kwa mbinde bungeni mjini Dodoma, huku Serikali ikisalimu amri kwa wabunge na kukubali kurekebisha baadhi ya vifungu vyake.Bila kujali tofauti zao za kisiasa, wabunge jana walisimama kidete na kuonyesha uzalendo wa hali ya juu, wakitaka sheria hiyo imlinde mzawa badala ya mwekezaji.
Moto huo wa wabunge uliwalazimisha Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chizza na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Fredrick Werema kusalimu amri na kukubali mapendekezo ya wabunge.
Msimamo wa wabunge hao katika kuibana Serikali, pia ulililazimisha Bunge kutengua kanuni zake na kuendelea na shughuli za kupitia muswada huo hadi saa 7:35 mchana, badala ya kusitishwa saa 7:00 kwa ratiba ya kawaida.
Serikali ilikubali mapendekezo ya wabunge hao na kurekebisha vifungu ambavyo sasa vinampa mmiliki wa ardhi itakayotangazwa eneo la umwagiliaji kuwa mwanahisa na kulipwa fidia.
Awali, wabunge waliowasha moto huo ni pamoja na Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina na Suleiman Jaffo wa Kisarawe, wote kutoka Chama Cha Mapinduzi(CCM), ambapo walisema baadhi ya vifungu vya muswada huo wa sheria vilikuwa na ajenda ya siri.
Wakichangia mjadala huo wabunge hao walitaka vifungu vinavyotamka kuwa eneo litakalotangazwa kuwa la umwagiliaji litatwaliwa na Tume itakayoundwa na kupewa fidia viboreshwe, ama kama haifai, vifutwe.
Mpina alishikilia msimamo kuwa badala ya kumlipa fidia mwananchi, vifungu hivyo vitamke kuwa atalipwa fidia ama kuwa mwanahisa wa mradi ama alipwe fidia na papo hapo kuwa mwanahisa.
Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema), aliitaka Serikali itunge sheria zinazolinda wazawa na kwamba hatua ya kuacha mianya, ndiyo mwanzo wa wawekezaji kuwanyang'anya ardhi wazalendo.
Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka (CCM), alisema kuwa haihitaji kuipitia sheria yote ili kubaini maudhui yenye dhamira ovu dhidi ya Watanzania ndani yake akisisitiza kuwa baadhi ya vifungu vina ajenda ya siri.
"Vifungu hivi vina ajenda ya siri ya kuwapeleka Watanzania kwenye utumwa...Kama msipobadilisha vifungu hivi, mwondoe huu muswada maana hii ni dhambi ya mauti," alisisitiza Ole Sendeka.
Ole Sendeka alisisitiza sheria itamke kuwa kama ni kutwaa ardhi yoyote, hata kama ni Rais anataka kufanya hivyo ni lazima hilo lifanyike kwa ushirikiano na mmiliki wake, ama na wanakijiji wote kupitia mkutano mkuu.
Mbunge wa Viti Maalumu, Esther Bulaya (CCM), alisema Watanzania wameshindwa kunufaika na rasilimali nyingine na waliyobakia nayo ni ardhi hivyo hawako tayari kurudisha ukoloni mamboleo.
Mbunge wa Peramiho, Jenister Mhagama (CCM), alisema ni lazima sheria hiyo iweke sharti la lazima kwa mwekezaji kuingia ubia na mmiliki wa ardhi na kama hataafiki, ndipo apewe fidia.
Chanzo:Mwananchi

 

0 comments

IGP aibiwa upanga wa dhahabu

IGP aibiwa upanga wa dhahabu

mwema c65ff

Jeshi la Polisi limeingia katika kashfa nzito baada ya mkuu wake, Inspekta Jenerali Said Mwema, kuibiwa upanga wa dhahabu ambao ni mali ya Shirikisho la Wakuu wa Majeshi ya Polisi wa nchi za Kusini mwa Afrika (SARPCCO).
Upanga huo wenye uzito wa takriban kilo tatu na wenye thamani ya zaidi ya fedha za Tanzania Sh600 milioni, ni kielelezo kwa nchi inayokabidhiwa uongozi wa SARPCCO.

Mwaka jana Tanzania ilikuwa mwenyekiti wa SARPCCO, ambapo upanga huo ulikabidhiwa kwa IGP Mwema na Jenerali Magwashi Victoria 'Riah' Phiyega, ambaye ni Kamishna wa Taifa wa Polisi wa Afrika Kusini aliyekuwa amemaliza muda wake kwa wakati huo.
Hilo ni tukio la pili la wizi la mali zinazohusu ofisi ya IGP, ambapo mwaka jana ndani ya ofisi hiyo kuliibwa kompyuta ndogo (laptop), ikiwa na taarifa muhimu za kipolisi. Hadi sasa hakuna taarifa za kupatikana kwa kompyuta hiyo.
IGP Mwema alikabidhiwa upanga huo Septemba 5, 2012, katika mkutano saba wa SARPCCO uliofanyika Zanzibar na kuhudhuriwa na wakuu wa majeshi ya Polisi kutoka nchi 13, pamoja na mashirika ya kimataifa.
Upanga huo ambao unakwenda sambamba na bendera ya SARPCCO, ni moja ya vielelezo vya nchi iliyochaguliwa kuwa Mwenyekiti wa shirikisho hilo, ambaye moja kwa moja anakuwa ni Mkuu wa Jeshi la Polisi katika nchi husika.
Kwa mujibu wa taratibu za SARPCCO, vielelezo hivyo hutakiwa kuwekwa ofisini kwa kiongozi husika, ikiwa ni alama ya kila mgeni atakayeingia ofisini hapo kutambua uwepo wa wadhifa huo wa kimataifa.
Uchunguzi wa gazeti hili ulibaini kuwa IGP aligundua kutoweka kwa upanga huo wiki iliyopita, wakati akijiandaa kwenda kuukabidhi kwa mwenyekiti mpya wa SARPCCO, ambaye ni IGP wa Namibia.
Taarifa za ndani ya jeshi hilo zilibaini kuwa, IGP alilazimika kuondoka bila upanga huo alipokwenda Namibia wiki iliyopita kuhudhuria mkutano wa nane wa SARPCCO, uliofanyika Jumapili iliyopita mjini Windhoek.
Kwa mujibu wa uchunguzi, IGP Mwema alikabidhi upanga unaofanana na huo ambao siyo wa dhahabu, alioazimwa kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi la Namibia, Inspekta Jenerali, Luteni Jenerali Sebastian Ndeitunga, na kukabidhiwa kama ishara ya kukabidhiwa uenyekiti wa SARPCCO kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Uchunguzi ulibaini kuwa IGP Mwema alitoa ahadi ya kurejesha upanga halisi ndani ya kipindi cha mwezi mmoja, au Serikali ya Tanzania italazimika kutengeneza mwingine kulipa uliopotea.
Uchunguzi wa gazeti hili unaonyesha kuwa kashfa hiyo ametupiwa Mkuu wa Polisi Zanzibar, Kamishna Mussa Ali Mussa pamoja na dereva wake, ikidaiwa kuwa upanga huo baada ya kupokewa na IGP Mwema, Septemba mwaka jana uliwekwa kwenye gari la kamishna huyo.Kamishna Mussa ndiye alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano wa Saba, na pia ofisa mwenyeji kwa wajumbe wa mkutano huo uliofanyika Zanzibar.
Hata hivyo, taarifa zingine zilidai kuwa IGP Mwema naye analaumiwa kwa kutofuatilia kwa karibu zana za kazi, kwani baada ya kuupokea alitakiwa kuhakikisha unakuwepo ofisini kwake kama alama ya uenyekiti wake.
Gazeti hili lilipowasiliana kwa njia ya simu na Mkuu wa Polisi Zanzibar, Kamishna Mussa Ali Mussa kuhusu madai hayo alisema, kitara (upanga) hicho ni kweli kimepotea, lakini yeye hahusiki kwa kuwa kila kitu kina utaratibu wake.
"Ni kweli kitara kilikabidhiwa kwa afande IGP na mimi nilishuhudia kikikabidhiwa, na ni kweli kitara hakijulikani kiliko, lakini mimi sihusiki na kupotea kwake. Ni kweli mimi nilikuwa ofisa mwenyeji wa mkutano huo, lakini siku hiyo zilitolewa zawadi nyingi, watu walipewa mikoba, kwa hiyo mtu akipoteza mkoba wake niulizwe mimi?" alihoji Kamishna Mussa.
Alisema kila kitu kina utaratibu wake na kwamba taarifa kwamba yeye amehojiwa kutokana na upotevu wa kitara hicho au kuna kamati imeundwa, hazina ukweli.
"Sijawahi kuona kamati hiyo. Kamati hiyo kwanza imeundwa na nani na inatoka wapi? Hayo maneno yanatengenezwa na watu wa nje," alisema Kamishna Mussa.
Alisema kinachofanyika hivi sasa ni kukitafuta ili kiweze kurejeshwa kunakohusika.
Taarifa zingine zilidai hata bendera ya mezani ya mwenyekiti wa SARPCCO, aliyokabidhiwa sambamba na upanga huo nayo kuna hatihati ilipotea.
Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Advera Senso alipotakiwa kuzungumzia suala hilo alisema aulizwe kamishina wa polisi Zanzibar.
"Suala hilo muulize Kamishina wa Zanzibar ndiye anayejua," alisema Senso.
Uchunguzi unaonyesha kuwa maofisa katika ofisi ya IGP na ile ya Kamishna wa Polisi Zanzibar, wamehojiwa akiwamo Kamishna Mussa, na kwamba upelelezi mkubwa umekuwa ukiendelea ndani ya jeshi hilo.
Hata hivyo, juhudi za gazeti hili za kutaka kufahamu uamuzi wa SARPCCO katika ofisi yake ya uratibu iliyopo kwenye ofisi za Makao Makuu ya Kanda ya Polisi wa Kimataifa (INTERPOL), Harare, Zimbabwe, hazikuzaa matunda baada ya baruapepe iliyotumwa kwa ofisa mratibu wa SARPCCO ambaye pia ni mkuu wa ofisi ya Kanda ya INTERPOL, C. Simfukwe kutopata majibu.SARPCCO ilianzishwa mwaka 1995, Victoria Falls, Zimbabwe, lakini kisheria ilitambulika rasmi mwaka 2006 na lengo lake kuu ni kupambana na uhalifu wa kuvuka mipaka.
Uenyekiti wake ni mwaka mmoja, ambapo kwa sasa mwenyekiti ni Mkuu wa Jeshi la Polisi la Namibia Inspekta Jenerali, Luteni Jenerali Sebastian Ndeitunga, aliyepokea wadhifa huo kutoka kwa IGP Mwema.
CHANZO MWANANCHI.

0 comments
 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger