Featured Post Today
print this page
Latest Post

TRA yashauriwa kuweka mazingira rafiki...

TRA yashauriwa kuweka mazingira rafiki...


 
 
 


MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani Tanga, imetakiwa kuweka mazingira rafiki ya kibiashara ambayo yatawafanya wafanyabiashara wasiukimbie mkoa huo.

Rai hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Chemba ya Wafanyabiashara wa Viwanda na Kilimo (TCCIA) Mkoa wa Tanga, Paul Bwoki wakati akisoma risala yake kwenye kilele cha maadhimisho ya Siku ya Mlipakodi iliyofanyika jijini hapa.
Alisema wafanyabiashara wengi wanadaiwa kuikimbia bandari ya Tanga na kutumia ya Dar es Salaam na Mombasa kutokana na huduma inayotolewa na TRA kwenye bandari hiyo.

“Chemba ya Biashara ya Mkoa wa Tanga tunaomba TRA iwe na mazingira rafiki ya kibiashara, sio kunyanyasana, lazima suala la kuheshimiana lipewe kipaumbele na kufahamu kwamba sisi tuna nia moja ya kufanya biashara na kulipa kodi kwa ajili ya maendeleo ya taifa letu,” alisema Bwoki.

Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendegu, ambaye alikuwa akimwakilisha Mkuu wa Mkoa, Luteni mstaafu Chiku Gallawa, aliitaka TRA kuboresha huduma zake ili kuwafanya walipakodi kundelea kulipa kwa hiari.

Dendegu alitumia nafasi hiyo kutangaza vita dhidi wanaokwepa kulipa kodi wakitumia bandari bubu na kulikosesha taifa mapato.

Meneja wa TRA Mkoa wa Tanga, Nyonge Mahayu, alisema TRA ilishindwa kufikia lengo la makusanyo yake kwa mwaka 2012/2013, lakini makusanyo halisi kwa kulinganisha na mwaka 2011/2012 yameongezeka kwa asilimia 13.

Chanzo;Tanzania Daima
0 comments

Kenya yazungumzia uhusiano mwema na Tanzania na kupongeza hoja za Rais Kikwete juu ya Jumuiya Afrika Mashariki

Kenya yazungumzia uhusiano mwema na Tanzania na kupongeza hoja za Rais Kikwete juu ya Jumuiya Afrika Mashariki

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akimtambulisha Mhe. Amina Mohammed, Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani) wakati wa mkutano wa pamoja na Waandishi hao kuhusu pongezi za Serikali ya Kenya kwa hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete aliyoitoa hivi karibuni kupitia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katika hotuba hiyo Mhe. Rais Kikwete alieleza msimamo wa Tanzania wa kutojitoa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Mhe. Amina Mohammed akisisitiza jambo wakati wa mkutano wa pamoja na waandishi wa habari huku Mhe. Membe akisikiliza.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. John haule (wa pili kulia) akimsikiliza Mhe. Mohammed (hayupo pichani) alipozungumza na Waandishi wa Habari kuhusu pongezi za Serikali ya Kenya kwa Tanzania. Wengine katika picha ni Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa,Balozi Celestine Mushy (kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya Afrika, Balozi Vincent Kibwana (wa pili kushoto) na Mjumbe kutoka Kenya.
0 comments

POULSEN AMTEMA IVO MAPUNDA TAIFA STARS

POULSEN AMTEMA IVO MAPUNDA TAIFA STARS


Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen amemtema kipa Ivo Mapunda katika kikosi chake.

Baada ya zaidi ya miaka mitatu, Ivo anayekipiga Gor Mahia ya Kenya aliitwa katika kikosi hicho.

Lakini baadaye Poulsen amemuondoa katika kikosi hicho kwa madai kulikuwa na ukimya.
 
"Sikusikia lolote kuhusiana na Mapunda, sifanya mkutano wa waandishi lakini ni uamuzi umepita kwa ajili huenda atakuwa na majukumu mengine," alisema.

Hata hivyo kuna taarifa zinaeleza TFF hawakupeleka barua ya kumtambulisha Ivo kuitwa katika kikosi hicho.

Ivo ni kati ya makipa wlaiong'ara katika Ligi Kuu Kenya na amesaidia Gor Mahia kutwaa ubingwa wa Kenya ambao mara ya mwisho waliubeba miaka 13 iliyopita.
 
chanzo:salehjembe.blogspot.com
0 comments

MALAIKA MUSIC BAND KUWASHA MOTO TANGA NOVEMBA 23.

MALAIKA MUSIC BAND KUWASHA MOTO TANGA NOVEMBA 23.

Na Oscar Assenga,Tanga.
BENDI Mpya ya Malaika Music Bendi inatarajiwa kufanya uzinduzi wa aina yake mkoani Tanga Novemba 23 mwaka huu katika ukumbi wa Tanga Hotel jijini Tanga ikiwa na waimbaji wake wote.
Akizungumza na blog hii,Meneja Masoko wa Bendi hiyo,Juma Abajalo alisema maandalizi ya onyesho hilo yanaendelea vizuri ambapo kabla ya kuja mkoani hapa itafanya uzinduzi wake Novemba 15 mwaka huu Mzalendo Pub Kijitonyama jijini Dar es Salaam na baada ya hapo wataelekea mkoani Morogoro na hatiamye kutua mkoani Tanga.
Abajalo alisema lengo la kuanzishwa bendi hiyo ni kuhakikisha wanakata kiu za wapenda mziki wa dansi hapa nchini kutokana na kusheheni wasanii nguli ambao wanajua kulitawala jukwaaa.
Meneja huyo alisema katika onyesho hilo,Rais wao Christiani Bella “Obama akisaidiwa na marapa pembeni Totoo Ze Bingwa,Fadii na mpiga kibodi maarufu nchini Andrew Sekedia.
Aidha aliwataka wakazi wa mkoa wa Tanga kukaa mkao wa kula ili kuweza kusikiliza masauti makali ya Christiani Bela “Obama”na wasanii wengine ambao wanaunda bendi hiyo watakaowasha moto siku hiyo.
   “Ninachoweza kusema burudani itakayopatikana hapo itakuwa sio ya mchezo hivyo nawaomba wakazi wa mkoa wa Tanga kuhakikisha wanapata nafasi ya kushuhudia uzunduzi huo ambao utakuwa wa aina yake “Alisema Abajalo.
0 comments

WATU TISA WAKAMATWA KWA KUHUSISHWA KWENYE UVAMIZI WA DR.MVUNGI

WATU TISA WAKAMATWA KWA KUHUSISHWA KWENYE UVAMIZI WA DR.MVUNGI

PIX 1



Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tukio la kuvamiwa na kushambuliwa Dk Sengondo Mvungi, Mjumbe wa Tume ya Katiba. 
Waziri Nchimbi alisema upepelezi wa tukio hilo umefanikiwa kwa zaidi ya asilimia 80 ambapo tayari watuhumiwa tisa wamekamatwa wakiwa na mapanga na simu moja ya mkononi, watuhumiwa hao walitajwa majina yao katika mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam leo. 
Hata hivyo, Waziri Nchimbi aliwaomba wananchi na waandishi wa habari wawe na subira wakati Jeshi la Polisi likiendelea na uchunguzi kwa ajili ya kuwakamata watuhumiwa wengine. Kushoto ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Pereira Ame Silima. Kulia ni Kamishna wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Suleiman Kova. PIX 3Kamishna wa Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Suleiman Kova akiwaonyesha waandishi wa habari mapanga waliyoyakamata wakati wa msako mkali wa kuwasaka watuhumiwa waliomvamia na kumshambulia Dk Sengondo Mvungi Mjumbe wa Tume ya Katiba. 
Katika msakao huo watuhumiwa tisa walikamatwa wakiwa na mapanga na simu moja ya mkononi. Katikati (waliokaa meza kuu) ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi. 
Kushoto ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Pereira Ame Silima. Hata hivyo, Waziri Nchimbi aliwaomba wananchi na waandishi wa habari wawe na subira wakati Jeshi la Polisi likiendelea na uchunguzi kwa ajili ya kuwakamata watuhumiwa wengine. 
Mkutano huo ulifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam leo.
PIX 4Sehemu ya waandishi habari waliohudhuria mkutano wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi alipokuwa anazungumza na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari vya nchini na nje ya nchi kuhusiana na tukio la kuvamiwa na kushambuliwa Dk Sengondo Mvungi, Mjumbe wa Tume ya Katiba.
 Waziri Nchimbi alisema upepelezi wa tukio hilo umefanikiwa kwa zaidi ya asilimia 80 ambapo tayari watuhumiwa tisa wamekamatwa wakiwa na mapanga na simu moja ya mkononi, watuhumiwa hao walitajwa majina yao katika mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam leo. 
Hata hivyo, Waziri Nchimbi aliwaomba wananchi na waandishi wa habari wawe na subira wakati Jeshi la Polisi likiendelea na uchunguzi kwa ajili ya kuwakamata watuhumiwa wengine. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Chanzo:Handenikwetublogspot.com
0 comments
 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger