Featured Post Today
print this page
Latest Post

Picha 19 za Nelson Mandela akiwa na watu mbalimbali maarufu duniani

Picha 19 za Nelson Mandela akiwa na watu mbalimbali maarufu duniani

nelson-david-beckham--z
 
Nelson Mandela kutokana na historia yake ya harakati za kutokomeza ubaguzi wa rangi Afrika Kusini alivutia watu wengi sana hata wale maarufu wa dunia ambao walifanya juu chini kumtembelea Mzee Mandela ambapo hizi ni baadhi ya picha zenyewe.

-9b362eff4ab20164Evander Holyfield
50 cent50 Cent
0022190dec450bb3bc9929Michael Jackson
d57bec3fNaomi Campbell
img4217-gmannelson_full  Will Smithmandela diddyP. Diddy
mandela na iverpoolLiverpool F.C
mandela-clinton-1
Bill Clinton
mandela-with-celebs-featured-obamaMichelle Obama
mjMichael Jackson
morganMorgan Freeman
Nelson Mandela's Death- Celebrities-ReactMike Tyson
nelson_mandela_meets_bill_gatesBill Gates
pelePele
pg_nelson_mandela_whitney_houston_1994_MasterWhitney Huston
ronaldo--zCristiano Ronaldo
showbiz_nelson_mandela_celebs_gallery_2Beyonce
showbiz_nelson_mandela_celebs_gallery_10Michael Jackson
0 comments

KERO YA TUTA MANISPAA YA MOROGORO KWA WALE WENYE VYOMBO VYA MOTO.

Wafanyakazi wa wakala wa barabara mkoa wa Morogoro wakiondoa vipande vya matofali vilivyojengewa tuta katika barabara ya Korogwe eneo la makao makuu ya tenesco ili kuweza kuweka tuta lingine kutoakana na tuta la mwanzo kuwa kubwa na kero kwa 
 watumiaji wa barabara hiyo mkoani Morogoro. PICHA/MTANDA BLOG
 


0 comments

KINANA AWAKONGA MOYO WAKAZI WA MBEYA.

KINANA AWAKONGA MOYO WAKAZI WA MBEYA.


Katibu wa Itikadi na Uenezi  CCM Taifa, Nape Nnauye akiwahutubia maelfu wa Wananchi wa Jiji la Mbeya katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Shule ya msingi RuandaNzovwe.
 Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Mbeya, Amani Kajuna akisalimiana na Nape katika mkutano huo.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya, Godfrey Zambi akiwahutubia wakazi wa Jiji la Mbeya waliofurika katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana katika viwanja vya shule ya Msingi RuandaNzovwe Jijini Mbeya.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro akijibu baadhi ya kero za Wananchi katika mkutano huo.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiwa amepozi baada ya kuvalishwa mavazi ya kichifu na wazee wa mila wa Mkoa wa Mbeya ambavyo ni Mkuki, mgolole na kigoda.
Mbunge wa viti maalum Mkoa wa Mbeya Mary Mwanjelwa akiwasalimia wakazi wa Jiji la Mbeya katika Mkutano huo.
Mjumbe wa Mkutano mkuu wa CCM Taifa Mkoa wa Mbeya kupitia UVCCM, Nwaka Mwakisu akiwa amebebwa juu kwa juu na vijana kwa mchango wake mkubwa kwa vijana wa Mbeya
Meza kuu wakifuatilia kwa makini baadhi ya matukio yanayoendelea jukwaani.
Vijana wa Mwanjelwa wakiwa wamembeba msombesombe mlezi wao Mbunge wa Viti maalum Mary Mwanjelwa wakimpeleka kwenye gari lake baada ya kukamilika kwa mkutano.
PICHA NA MBEYA YETU BLOG.
0 comments

MANDELA KUENZIWA KATIKA IBADA KUBWA

MANDELA KUENZIWA KATIKA IBADA KUBWA

Maelfu ya watu wameweka maua kuonyesha mapenzi yao kwa Mandela
Dunia inaendelea kuomboleza kifo cha mzee Nelson Mandela. Jana rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma alitangaza siku 10 za maombolezo kwa Mandela aliyefariki Alhamis usiku akiwa na umri wa miaka 95.
Maelfu ya watu wameweka maua kuonyesha mapenzi yao kwa Mandela
Ikulu ya Marekani imesema kuwa rais Barack Obama na mkewe Machelle watakwenda Afrika Kusini wiki ijayo kuungana na viongozi wengine wengi wa dunia, katika ibada ya kumuaga Nelson Mandela. Obama ambaye mwenyewe ni rais wa kwanza mweusi wa Marekani, ataambatana na watangulizi wake wawili, George W Bush na Bill Clinton, ambao pia watasindikizwa na wake zao.
Rais Obama ataongoza ujumbe wa Marekani kwenye ibada ya kumkumbuka Mandela Rais Obama ataongoza ujumbe wa Marekani kwenye ibada ya kumkumbuka Mandela
Mwili wa Mandela utawekwa katika jengo la serikali kwa muda wa siku tatu, kutoa fursa kwa wananchi wa Afrika Kusini kutoa heshima zao za mwisho kwa kiongozi waliyempenda. Baadaye mwili wake utasafirishwa kwenda kuzikwa mahali alipokulia Mandela, Qunu.
Ibada ya kumkumbuka Mandela
Jana maelfu ya raia wa Afrika kusini kutoka matabaka yote na rika zote walishiriki katika ibada ya pamoja ya dini mbali mbali, ambayo ilifanyika mjini Cape Town mahali ambapo Mandela alitoa hotuba yake ya kwanza baada ya kuachiwa huru kutoka jela.
Mayor wa jiji la Cape Town Patricia de Lille alisema katika ibada hiyo kuwa watu wa mji huo, weusi kwa weupe, wahidi na wenye damu mchanganyiko, wanaungana kwa mshikamano kumuenzi Nelson Mandela na kukumbuka mchango wake kwa nchi yao.
Watu wa matabaka yote wamesononeshwa na kifo cha kipenzi wa dunia Nelson Mandela Watu wa matabaka yote wamesononeshwa na kifo cha kipenzi wa dunia Nelson Mandela
Askofu mkuu wa zamani wa kanisa la Angikani nchini Afrika Kusini Desmond Tutu ambaye kama Mandela naye ni mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Amani, akijipangusa machozi ya huzuni alimsifu Mandela na kusema alikuwa alama ya umoja tangu alipoachiwa huru kutoka gerezani.
Kifo cha Mandela chaiunganisha dunia
Nchi kadhaa ulimwenguni zilitangaza maombolezo kwa kifo cha Nelson Mandela. Bendera zilipeperushwa nusu mlingoti katika baadhi ya nchi hizo, zikiwemo za kiafrika, Marekani, Ufaransa na Uingereza, na kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York.
India ilitangaza siku tano za maombolezo, na mnara maarufu wa mjini Paris, Eiffel, ulimeremeta kwa rangi za bendera ya Afrika Kusini kwa heshima ya Madiba.
Pande zenye misimamo tofauti kihistoria zimezungumza kwa sauti moja kumsifu Mandela; Wapalestina na Israel, Dalai Lama na China, Marekani na Iran wote wamemsifu kuwa mtu aliyetetea haki na usawa.
Ibada ya kumuaga Nelson Mandela ambayo itafanyika Jumanne ijayo kwenye uwanja wa mpira mjini Johannesburg inatarajiwa kuwa mojawapo ya mikusanyiko mkubwa ya watu maarufu kuwahi kutokea.
0 comments

PESA ZA WATEJA WA M-PESA, TIGO PESA, AIRTEL MONEY NA Z-PESA WANAO FARIKI ZINAKWENDA WAPI?

PESA ZA WATEJA WA M-PESA, TIGO PESA, AIRTEL MONEY NA Z-PESA WANAO FARIKI ZINAKWENDA WAPI?

Kutokana na makampuni karibu yt ya simu Tz kuwa na huduma hz za mobile money, Je inapotokea mteja amefariki, makampuni yanawajibika vipi kuhusu kurudisha pesa za mteja wao kwa msimamizi wa mirathi au warithi? 

swali hiili linazingatia kuwa wateja wanaoweza kutwa na mauti kwa vyovyote wanaweza kuwa na akiba kidogo kwenye ac zao za mitandao ya simu wanayotumia!

Je kuna sheria yoyote ambayo imeweka bayana masuala haya?

kwa wenzetu walio kwenye makampuni ya simu tafadhali mtusaidie kwa hili!
naomba kuwasilisha kwa mjadala!
0 comments

MAJANGA:WAZIRI MUHONGO ASUSIA NDEGE, KISA KAKOSA FIRST CLASS SEAT

MAJANGA:WAZIRI MUHONGO ASUSIA NDEGE, KISA KAKOSA FIRST CLASS SEAT

WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, amegoma kusafiri na Watanzania wenzake kwenda nchini Algeria kwa daraja la kawaida baada ya kukosa daraja la kwanza, hivyo kuahirisha safari yake kwa siku moja, Tanzania Daima limebaini.

Profesa Muhongo ambaye amekuwa akionyesha dharau kwa Watanzania mara kadhaa, aligoma kusafiri katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam Jumapili ya Novemba 24, 2013, saa 10.45 akiwa na wenzake tisa kwenda kwenye safari ya kikazi nchini Algeria alikoenda baadaye.Moja ya kauli ya dharau iliyotolewa hivi karibuni na Waziri Muhongo ni pale aliposema wafanyabiashara Watanzania wana uwezo wa kuwekeza kwenye soda na juisi badala ya gesi na pia aliwahi kuwashambulia viongozi wa dini kwa kuwaita waongo.

Uchunguzi wa Tanzania Daima uliofanyika kwa siku kadhaa sasa, umethibitisha kwamba Muhongo alikuwa aondoke na ndege ya shirika la ndege la Emirates namba EK 726 kutoka Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere kupitia Dubai kwenda Algeria akiwa na tiketi ya daraja la kawaida bila kujua kabla ya kufika uwanjani hapo na kisha kuanza kumfokea kila aliyekuwa anamsemesha.

“Tiketi yake na wenzake kumi ilikuwa ni Economy Class (Daraja la Kawaida), lakini akakataa akitaka asafiri kwa First Class (Daraja la Kwanza). Alibembelezwa na wenzake na wafanyakazi wa Emirates na wale wa Uwanja wa Ndege lakini akagoma huku akifoka na wenzake wakataka kuahirisha safari.

Ikawa tena ni sisi kuwaomba wasafiri ili Bwana Mkubwa (Muhongo) atafutiwe nafasi kwa daraja analotaka.
“Walimbembeleza wakamwambia kwa kutumia ‘millage’ ya safari zake watambadilishia akiwa ndani ya ndege na kumuweka daraja la kwanza lakini alionekana ameshakuwa mkali na hakuwa anamsikiliza yeyote.“Baadaye tulifanikiwa kuwashawishi wenzake kuendelea na safari na yeye sijui aliondoka na ndege gani tena maana wakubwa wetu wana mambo sana,” anasema ofisa mmoja uwanjani hapo.

Taarifa za awali kuhusu sakata hili, ziliripotiwa siku hiyo katika mtandao wa jamiiforums.com zikieleza kwamba kitendo cha Waziri Muhongo cha kususia safari hiyo, kiliwakera baadhi ya wasafiri wakiwamo raia wa kigeni ambao walishangazwa na hatua hiyo ya kiongozi wa nchi maskini inayotegemea misaada kulazimisha kusafiri kwa daraja la kwanza, daraja ambalo viongozi wa mataifa makubwa hawaruhusiwi kusafiri bila sababu maalumu.

Taarifa hiyo kwenye mtandao wa JamiiForums. Com iliripotiwa hivi: “Kweli viongozi wa nchi hii wanatia aibu, wakati mawaziri wa Uingereza wanakataa First Class, hapa kwetu kimetokea kioja. Waziri wenu wa Nishati na Madini (Muhongo) ambaye anazidi kutulaza na joto na giza leo amewaacha hoi Watanzania pale alipofika mpaka Airport na akiwa anaboard akakuta anawekwa sehemu ya abiria wa daraja la kati, baada ya kuambiwa hayuko First Class akagoma na kutoka nje ya mlango. Wakati hayo yakiendelea kumbe ana wenzake zaidi ya tisa wako economy na wawili Bussiness Class, ghafla nao wakaanza kushuka.

“Hapo ndipo hekima za mmoja wa wahusika wa Airline (Emirates) akawaomba hao waende ili yeye akabadilishe aje kesho yake.” “Jamani kweli First Class inakushushia aibu hivi Profesa na bado unasema maisha magumu Tanzania!? Inaonekana zile buti za bora ulizivalia ukiwa form V na haya ndio madhara yake, mnapewa vyeo wakati maisha yalishawapiga; mnatafuta muafaka na Yesu mkiwa madarakani,” anaeleza mtu aliyewasilisha mada husika akijulikana kwa jina la Basiasi.

Basiasi alihoji sababu ya abiria wenzake ambao nao walikuwa wakisafiri kikazi kutaka kushuka na kusababisha hasara kwa serikali au wafadhili waliokata tiketi hizo. Kwa utaratibu wa kawaida abiria anayeahirisha safari baada ya kuwa ameshaingia ndani ya eneo la kusafiria (boarding) anaweza kupoteza kabisa tiketi au kulipishwa fedha nyingi zinazoweza kuwa sawa na kununua tiketi mpya.

“Hebu kuweni wastaarabu, sasa wale watu tisa walitaka kuwashusha kwa nini na kama wamekwenda, mlishindwa kuwaambia wabaki mpaka mkaanza kuleta aibu uwanjani? Inaonekena ndege mmeanza kupanda uzeeni; najiuliza kivipi unaletewa tiketi hata kama na ‘travel agency’ halafu unashindwa kuuliza au kukagua mpaka unaenda uwanjani na unapewa ‘boarding pass’ bado unashindwa kukagua ipi ‘bussiness class’ na ipi ‘first class’!” anahoji Basiasi. Abiria mmoja aliyenukuliwa na Jamiiforums alisema kwa waziri wa nchi kama Uingereza anatakiwa kutoa maelezo ya sababu za kusafiri na daraja la kwanza (first class) ikiwa atalazimika kufanya hivyo, vingine viongozi husafiri kwa madaraja ya kawaida.

Wakati Waziri Muhongo akisusia ndege kwa kukosa nafasi ya kusafiri na daraja la kwanza, baadhi ya mawaziri wanaofanya ziara mikoani na kusafiri kwa ndege, hulazimika kuyaagiza mashangingi yao kutoka Dar es Salaam hadi katika mikoa wanayokwenda kufanya ziara hizo hata kama yatatumika kwa siku moja.
0 comments

LIVE KUTOKA KIGOMA,DR.SLAA APAMBANA NA MAANDAMANO MAKUBWA YA KUMPINGA

LIVE KUTOKA KIGOMA,DR.SLAA APAMBANA NA MAANDAMANO MAKUBWA YA KUMPINGA


Kinachoendelea KIGOMA muda huu na hata kwenye kwenye Maandamano Makubwa ni hiki wanachama wa CHADEMA wakiandamana kupinga ujio wa Dr SLAA na viongozi wenzake mkoani.
Mods tunaomba postive na Negative Pictures anachokutana nacho Dr.slaa ziruhusiwe hapa Jukwaani,naona watu wamekaa kusifiana tu hapa.Ukweli ni Kwamba Dr.slaa amekutana na wakati Mgumu akiwa Kigoma.Picha zingine zitakuja na saambili Usiku ITV,TBC NA STAR TV wataonesha hali ya leo Kigoma walivyojitokeza Kupinga Ujio wa Dr.slaa.

0 comments

UPEPO MKALI WAEZUA PAA LA SHULE YA MSINGI LUGANGA

UPEPO MKALI WAEZUA PAA LA SHULE YA MSINGI LUGANGA

1 892ea
Wanafunzi wa shule ya msingi Luganga kata ya Ilolompya Tarafa ya Pawaga Mkoa wa Iringa, wakiangalia sehemu ya paa la chumba cha darasa lililo ezuliwa na upepo mkali hivi karibuni.
2 e40f4
Nyumba ya Mwalimu
4 10483
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Luganga wakicheza nje ya Darasa lililo ezuliwa
5 ff967
Wanafunzi Shule ya msingi Luganga wakiendelea na Masomo ndani ya Darasa lililo ezuliwa na Upepo mkali hivi karibuni,Picha na Said Ng'amilo.(HD)
0 comments

Chadema mkoani Kigoma kimenuka, watu waandamana kupinga ujio wa Katibu Mkuu Dk. Slaa

Chadema mkoani Kigoma kimenuka, watu waandamana kupinga ujio wa Katibu Mkuu Dk. Slaa

Wanachama na wafuasi wa Chadema wakiandamana katika mitaa mbalimbali ya kigoma ili kupinga ziara ya Katibu Mkuu wa Chadema Dk. Slaa mkoani humo pamoja na kupinga maamuzi yanayofanywa na Kamati kuu ya Chadema. Maandamano hayo yanaendelea hivi sasa. Taarifa zaidi tutaendelea kuwapatia kadri tutakavyozipata.
0 comments

KIGOMBE BINGWA WA KOMBE LA MKONGE CUP 2013

KIGOMBE BINGWA WA KOMBE LA MKONGE CUP 2013

Na Oscar Assenga,Tanga.

TIMU ya Shamba la Mkonge la Kigombe mkoani Tanga leo wameibuka na ubingwa wa Kombe la Mkonge Cup mara baada ya kuibamiza China Farm ya Morogoro mabao 4-3 katika mchezo wa fainali uliochezwa kwenye dimba la soka Mkwakwani.

Katika mchezo ambao ulikuwa mkali na wenye upinzani mkubwa ambapo mpaka timu zote zinakwenda mapumziko hakuna timu iliyoweza kuona lango la mwenzie,kipindi cha pili kilianza kwa kasi ya mashambulizi kwa timu zote.

Wakionekana kujipanga na kujiimarisha vilivyo,Kigombe waliweza kufanya mashambulizi ya kushtukiza langoni mwa China Farm na kufanikiwa kuandika bao lao la kwanza dakika ya 56 kupitia Said Yasin kwa njia ya penati iliyotokana na mshambuliaji wa China Farm kumchezea faulu eneo la hatari Abdallah Maduba.

Kutokana na hali hiyo ilimlazimu mwamuzi wa mchezo huo,Ibrahimu Kidiwa “Mdudu”kuamuru ipigwe penati na ndipo ilipofungwa kiufundi na mchezaji huyo ambaye pia aliweza kutengeneza nafasi nyingi kwa timu hiyo.

Baada ya bao hilo,China Farm waliweza kujipanga na kuanza kufanya mashambulizi ya ,mara kwa mara langoni mwa Kigombe na kuweza kufanikiwa kusawadhisha bao hilo dakika ya 70 kupitia kwa Peter Bukulu ambaye aliweza kuunganisha krosi iliyopigwa na Rashid Paulo.

Mpaka dakika 90 zinamalizika timu hiyo zilitoka nguvu sawa na kuongezwa dakika 30 na mwamuzi wa mchezo huo ambazo hazikuweza kuzaa matunda yoyote ndipo ilipoamuliwa kupigwa mikwaju ya penati.
Katika hatua hiyo ya matuta ndipo timu ya Kigombe ilipoweza kuibuka na ushindi kwa kufanikiwa kufunga penati 4-3 dhidi ya wapinzani wao China Farm kitendo ambacho kilipelekea mashabiki wa timu hiyo kulipuka kwa shangwe na nderemo uwanja mzima.

Akizungumzia mashindano hayo,Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano,Lai Mpuma alisema mwaka huu yalionekana kuwa na msisimuko mkubwa iliyotokana na timu nyingi shiriki kufanya maandalizi kabambe na hivyo kupelekea kutokutabirika kuwa nani atachukua ubingwa.
0 comments
 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger