Featured Post Today
print this page
Latest Post

MZEE MANDELA AREJEA NYUMBANI KWAKE PRETORIA KUTOKA HOSPITALINI KIMYA KIMYA.

http://guardianlv.com/wp-content/uploads/2013/06/Nelson-Mandela-Winnie-Jac-001.jpgRAIS wa zamani wa Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela amerejea nyumbani kwake mjini Johannesburg kimya kimya baada ya kulazwa hospitali mjini Pretoria kwa muda mrefu.
Mandela mwenye umri wa miaka 95 alilazwa hospitali tangu Juni 8 mwaka huu baada ya kupata maambukizi katika map
afu.
Hali ya afya yake wiki iliyopita ilitajwa kuwa ‘mbaya lakini imara’ na haikutolewa taarifa tena kuhusiana na afya yake.
Maambukizi ya ugonjwa wake yanasemekana kuhusishwa na kipindi cha karibu miongo mitatu aliyokaa gerezani baada ya kufungwa kutokana na harakati zake za kupinga ubaguzi wa rangi nchini humo.
0 comments

MAJIMAREFU ATOA MIFUKO 50 YA SARUJI KITUO CHA POLISI MAGOMA

MAJIMAREFU ATOA MIFUKO 50 YA SARUJI KITUO CHA POLISI MAGOMA

MBUNGE wa Jimbo la Korogwe Vijijini,Stephen Ngonyani "Maji Marefu"mwenye shuti akipata maelekezo kutoka kwa Afisa Tarafa ya Magoma Haji Mbaruku kuhusu ujenzi wa kituo cha Polisi cha Tarafa hiyo wakati alipokitembelea jana,Picha na Oscar Assenga,Korogwe.
0 comments

DIAMOND NA LINAH WANASWA WAKITOMASANA HADHARANI


Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amenaswa na msanii mwenzake, Esterlina Sanga ‘Linah’ wakiwa kwenye mapozi ya kimahaba ambayo yametafsiriwa vibaya.
 

Katika tukio hilo lililojiri juzikati kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora ndani ya Tamasha la Serengeti Fiesta, Diamond alishuhudiwa akiwa amempakata Linah ndani ya basi huku mikono ya jamaa huyo ikishika maeneo nyeti.
 

Mara baada ya kutimba uwanjani hapo wakitokea hotelini tayari kwa kufanya shoo, Diamond na Linah walibaki kwenye basi wakiwa wamepakatana na hata msichana huyo alipomaliza shoo yake kali mishale ya saa 3: 00 usiku, alirejea mikononi mwa Diamond ambaye alimpachika mapajani.


Kwa mujibu wa mashuhuda, kama kweli mchumba wa Diamond, Penniel Mungwilwa ‘Penny’ anakubali mambo kama hayo, basi atakuwa na roho ngumu au moyo wa chuma.
 
Siyo mara ya kwanza Diamond na Linah kuripotiwa wakiwa wamepozi kimahaba kwani mwaka jana walifanya hivyo wakiwa jijini Mbeya hivyo kutafsiriwa kuwa inaonekana ni katabia kao kabaya wanakaendekeza.
0 comments

RWANDA YAPELEKA WANAJESHI 1700 KUWASAIDIA WAASI WA M23 BAADA YA KUELEMEWA NA JWTZ ( MONUSCO)

RWANDA YAPELEKA WANAJESHI 1700 KUWASAIDIA WAASI WA M23 BAADA YA KUELEMEWA NA JWTZ ( MONUSCO)


KIKUNDI cha waasi cha M23 kinachopambana na jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), kimeripotiwa kupigwa vibaya na kutikisa nguvu za kikundi hicho kutokana na baadhi ya wapiganaji wake kuripotiwa kupoteza maisha.
 
Mapigano baina ya M23 na Jeshi la Serikali ya DRC linalosaidiwa na Kikosi Maalumu cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa (MONUSCO), yameibuka upya ndani ya wiki hii.
 
Habari za kiintelijensia  zinasema kuwa, kutokana na shambulio hilo, Serikali ya Rwanda imelazimika kuingilia kati kusaidia waasi hao kwa kupeleka bataliani mbili zenye jumla ya askari 1,700 huko DRC, ili waweze kukabiliana na nguvu ya majeshi ya JWTZ, DRC, Monusco na Brigedi ya Majeshi ya Kulinda Amani ya Umoja wa Mataifa yenye mamlaka ya kujibu mapigo (FIB).

Kwa mujibu wa vyanzo hivyo vya habari, Rwanda imepeleka bataliani hizo mbili zenye askari 850 kila moja saa 48 zilizopita na kwamba wamevuka mpaka kuingia DRC katika eneo la Kibumba, lakini wanashindwa kusonga mbele.
 
Habari zaidi zinasema sababu ya Rwanda kupeleka askari wake hao ni kusaidia M23 ambao walipigwa sana Agosti 23 na 27, mwaka huu katika eneo la vilima vya Kibati na  kuikimbia ngome yao.
 
“M23 walitandikwa sana Agosti 23 na 27 katika eneo la vilima vya Kibati, na kulazimika  kuikimbia ngome yao, ndio maana sasa hivi Rwanda imepeleka batalioni zao kuwapa nguvu, lakini wanashindwa kusonga mbele maana hawajielewi kwa sababu ya kipigo walichopata,” kilisema chanzo kimoja cha habari.
 
Kwa mujibu wa vyanzo hivyo vya habari, eneo la Kibati ndilo eneo kubwa la M23 ambalo wamekuwa wakitumia kuhifadhi silaha zao za kivita, lakini wakati wa mapambano majeshi ya JWTZ , DRC, MUNUSCO na FIB yalisambaratisha kabisa ngome hiyo ya waasi.
 
FIB inaundwa na askari wengi wa Afrika Kusini na Tanzania. Habari zaidi zinasema kwa sasa majeshi ya DRC, Monusco na FIB yanawasubiri kwa hamu askari hao wa Rwanda kuingia uwanja wa vita ili kukabiliana nao kama walivyokabiliana na waasi wa M23.
 
“Taarifa tulizonazo hivi sasa Rwanda inajiuliza iwapo isonge mbele kupambana au irudi nyuma, ikifikiria pia kipigo walichopata M23,” kilisema chanzo kimoja cha habari. 

Inaelezwa kwamba, kutokana na kipigo walichopata M23 siku chache zilizopita kimepelekea Rwanda kujikuta ikikiri na kusema ukweli juzi kuwa inakisaidia kikundi hicho cha waasi.

0 comments

SABABU ZA (KAGAME) RWANDA KUIKACHA BANDARI YA DAR HIZI HAPA

SABABU ZA (KAGAME) RWANDA KUIKACHA BANDARI YA DAR HIZI HAPA 

SIRI ya wateja wakubwa wanaotumia Bandari ya Dar es Salaam, wakiwemo wa nchi jirani kama Rwanda kutishia kujitoa na kwenda kutumia bandari za nchi nyingine, imefahamika, Tanzania Daima Jumapili limebaini.

Siri hiyo inaelezwa kusababishwa na Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), kuwa na mpango wa kuanzisha tozo mpya kuanzia Oktoba mwaka huu kwa wateja wanaoingiza mizigo yao nchini pamoja na kasi ndogo ya utendaji ukilinganisha na bandari za nchi jirani.

Tozo hiyo mpya inayopigwa ni ya ufuatiliaji mizigo bandarini kwa njia ya mtandao (Electronic Cargo Tracking Note).

Hatua ya Rais Kagame kuikacha Bandari ya Dar es Salaam kunadaiwa kusababishwa na kulegalega kwa mahusiano kati ya Tanzania na Rwanda, lakini duru za siasa zinabainisha kuwa rais huyo alishaitahadhalisha serikali kuboresha utendaji wa TPA na kupunguza vikwanzo vya kibiashara kutoka 24 hadi 12.

Imeelezwa kwamba tozo hiyo ya e-CTN itaathiri mapato ya bandari za Tanzania kutokana na kuwa washindani wake wote hawana tozo hizo ikiwamo bandari za Mombasa, Walvis bay, Nacala, Maputo na Durban, ambazo zimekuwa zikichukua wateja wengi wa bandari za Tanzania wakiwamo wale wa nchi za Burundi, Rwanda, Zambia, DRC na Malawi.

Vyanzo vya habari vimeeleza kuwa kodi hiyo imeibua utata mkubwa baada ya kuwapo njama za kulazimisha kuwapo kwake pamoja na pingamizi kutoka kwa wadau na hata baadhi ya watendaji serikalini.

Taarifa za uhakika ndani ya mfumo wa bandari zilizothibitishwa na baadhi ya wadau, zinaeleza kwamba TPA ambao wamekwisha kuingia mkataba na kampuni moja ya Ubelgiji, iitwayo Antaser BVBA imeendelea na mchakato wa kuanzisha tozo hiyo.

Pamoja na pingamizi kutoka kwa wadau na hata ndani ya TPA yenyewe, bado kuna taarifa za kwamba uongozi wa mamlaka hiyo unaendelea na mchakato wa kuanza tozo hiyo ya e-CTN Oktoba mosi mwaka huu na baadhi ya watendaji wake wanapanga kwenda Ubelgiji kufanya maandalizi ya mwisho kabla ya utekelezaji wake.

Tozo hiyo ya e-CTN ni kwa ajili ya ufuatiliaji wa mzigo kutoka nchi inakotoka kwa njia ya mtandao, kazi ambayo wadau wanasema hufanywa na kampuni za meli na zile za wakala wanaosafirisha mizigo hiyo na si dhamana ya TPA ambao jukumu lao ni kupokea mizigo kutoka kwenye meli (cargo handling) na kuifadhi kwa muda ikisuburi wateja kuichukuwa.

“TPA walitakiwa wawasilishe pendekezo hili la e-TCN kwa Sumatra ambao kwa mamlaka waliyonayo wawaite wadau wote watoe mapendekezo yao kama uwepo wa kitu kama hiki utaleta tija kwa wadau wote wanaotumia bandari ya Dar es salaam. Kutokana na hila na pengine ufisadi uliojificha ndani. Gharama zake zitakwenda kwa mlaji wa mwisho!  TPA kazi yake ni kupokea mizigo kutoka kwenye meli (Cargo handling) na kuifadhi kwa muda ikisuburi wateja waje kuichukuwa aidha wao wenyewe au kwa kutumia mawakala wao wa forodha.

“TPA wanatakiwa ku kuibana  mizigo ikiwa ndani ya bandari na si kutoka bandari nyingine duniani ( ports of loadings) mpaka final destination ya mizigo bila " carriers" yaani shipping lines/ agents kuhusika na pia wenye mizigo (Cargo Owners) yaani importers/ C&F agents kuhusishwa!!.  Hapa kuna kitu kilichojificha,” anasema mdau ambaye anafanya biashara ya uwakala wa meli.

Tayari kumeibuka utata kuhusiana na huo mradi wa Electronic Cargo Tracking Note baada ya wadau kushitukia njama za kuwazunguka kwa njia ya kughushi muhstasari wa kikao wenye nia ya kuhalalisha mradi huo.

Utata huo umeibuka baada ya wadau kubaini kuwapo kwa kikao kilichofanyika Mei 30, 2013 kikiwashirikisha baadhi yao na baadaye kuandika muhstasari (nakala tunayo) ambao uliandikwa majina ya watu ambao hawakuhudhuria akiwamo Mwenyekiti, Otieno Igogo.

Igogo alibaini kuwapo kwa njama hizo na baadaye ‘kuvamia’ kikao kingine kilichoitishwa bila ya yeye kualikwa kilichofanyikia Agosti 29, 2013, ambacho alikiongoza na kutamka wazi kuwa jina lake pamoja na baadhi ya hoja za kikao cha Mei 30, 2013 vilighushiwa na hivyo kwa kauli moja wajumbe kufanyia marekebisho muhtasari.

Miongoni mwa hoja zilizoghushiwa katika muhtasari wa kikao hicho ni hoja ya kwamba wajumbe walijadili na kuridhia mpango wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kuanzisha tozo kwa ajili ya huduma za Electronic Cargo Tracking Note (e-CTN), na katika kikao cha wiki hii, wadau walirekebisha muhtasari huo na kukemea waliohusika na kughushi.

Mwakilishi wa Chama cha Mawakala wa Meli (TASAA), Paul Kirigini, ambaye ni mjumbe wa vikao hivyo alithibitisha kuwapo kwa tatizo katika muhtasari wa kikao cha Mei 30, 2013 ambao uliandaliwa katika mazingira tata kwa kuorodhesha watu ambao hawakuhudhuria na baadhi kuandika kwamba waliomba udhuru wakati hawakuwa wamealikwa akiwamo yeye.

“Mimi sikualikwa lakini wameandika kwamba sikuhudhuria kwa kuomba udhuru. Nilikuwapo Dar es Salaam na hata kama nisingekuwapo tungetuma mwakilishi wa TASAA, lakini hawakutuita na wakaandika kwamba tuliomba udhuru. Kibaya zaidi hata Igogo ambaye alipaswa kuwa mwenyekiti wa kikao hicho hakuwapo lakini wakaandika ndiye aliendesha hicho kikao,” anasema Kirigini.

Igogo ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati Ndogo ya Wadau wa Bandari,  hakuweza kupatikana jana kuzungumzia sakata hilo, lakini ilielezwa kwamba ameridhika baada ya muhtasari huo kufanyiwa marekebisho na kuazimiwa kwamba vikao vyote lazima wadau wajulishwe kabla ya kuitishwa.

Mjumbe mwingine ambaye anatajwa jina lake kuingizwa bila ya yeye kuwapo ni Stephen Ngatunga, ambaye naye aliomba kufanyika kwa marekebisho hayo katika kikao cha Alhamisi wiki hii.

Mwakilishi wa TPA, ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Teknohama, Phares Magesa, anaelezwa kuwa ndiye aliyemuwakilisha Mkurugenzi Mkuu wake, Madeni Kipande, ambaye hata vikao vilivyoitishwa na SUMATRA alishindwa kuhudhuria.

Mara baada ya kutokea malalamiko kuhusiana na Electronic Cargo Tracking Note, wadau walilazimisha kuitishwa kwa kikao kilichoongozwa na SUMATRA, lakini uongozi wa TPA ulishindwa kuhudhuria vikao vilivyoitishwa Julai 17 na Julai 22 mwaka huu.

Katika vikao hivyo viwili vya Julai, SUMATRA iliungana na wadau kuitaka TPA kuwashirikisha kabla ya kufikia maamuzi ya kuingiza tozo zozote zitakazoweza kuathiri wateja wanaotumia bandari za Tanzania ikiwamo bandari ya Dar es Salaam.

Mradi huo wa e-CTN unaelezwa na wadau kuweza kupandisha gharama za uingizaji wa mizigo bandarini hadi kufikia dola milioni 100 kwa mwaka kwa kutumia takwimu za mizigo ya makontena kwa mwaka 2012, ukiondoa mizigo mingine kama magari, nafaka na mafuta.

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ameshaingilia kati changamoto ndani ya Bandari ya Dar es Salaam na aliitisha kikao cha wadau kilichoahirishwa ghafla kutokana na kuingiliana na majukumu mengine ya kitaifa.
Tanzania Daima

 

0 comments

DAYNA ADAI DIAMOND KAMUIBIA WIMBO WAKE WA MY NUMBER ONE.

DAYNA ADAI DIAMOND KAMUIBIA WIMBO WAKE WA MY NUMBER ONE.

Msanii wa muziki wa bongo fleva Dayna Nyange mwenye maskani yake mjini Morogoro,ambaye pia ni msanii pekee wa kike anafanya vizuri kutoka Morogoro
alisema “Kukweli ni nimekwazika sana  pia imeniuma,kwani sikutarajia msanii kama Diamond anaweza KUIBA  nyimbo yangu na kwenda kuifanya yeye.Unajua nilikuwa nataka nimshirikishe kwenye nyimbo yangu ambayo nimefanya kwa Shedy Clever pale Tabata,hivyo nikarekodi demo,nikamtafuta na kumpatia ili aweze kusikia na kujua jinsi gani ataweza kuimba.
Baada ya muda ya nikamtafuta tena vipi ili tufanye kabisa ile nyimbo,ndipo akaanza kusema yupo bize nisubiri lakini.Lakini nashangaa sasa hivi nakisikia tena ile nyimbo ameeimba yeye tena alafu kibaya zaidi ametumia beat ile ile  pia na mashairi yale yale.
Kiukweli alichokifanya sio kitu kizuri,kwani watu wote tunatafuta maisha sasa yeye ameangalia zaidi maslahi yake.Na usiku wa jana ndio ametoka kuitambulisha rasmi video ya wimbo huo.
Nilikuwa namheshimu sana ila kwa hili nashindwa kusema kitu maana imenigusa sana,nyimbo yangu ilikuwa inaitwa my number one. Mpaka sasa bado sijajua nifanye kitu gani nipo katika kufikiri cha kufanya.
0 comments

Mechi za Leo Jumapili ligi kuu Uingereza...!

Mechi za Leo Jumapili ligi kuu Uingereza...! 

prediksi-liverpool-vs-manchester-united-epl-2013-14_b42ff.jpg
15:30 Liverpool vs Manchester United (P.T)

West-Brom-v-Swansea-1727337_33482.jpg
15:30 West Bromwich Albion vs Swansea City

18:00 Arsenal vs Tottenham Hotspur

 

0 comments
 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger