Featured Post Today
print this page
Latest Post

Mwakilishi wa UK Sports atembelea Wizara ya Habari

Mwakilishi wa UK Sports atembelea Wizara ya Habari

pix1_57c17.jpg
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Leonard Thadeo akifafanua jambo wakati wa mkutano wake na Mshauri Mwandamizi wa Shirika la UK Sports la Uingereza Bwana Elias Musangeya (kushoto) alipotembelea Wizarani hapo kwa ajili ya tathmini ya maendeleo ya mradi wa International Inspiration leo jijini Dar es Salaam.
pix2_ce8e8.jpg
pix2: Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa Henry Lihaya (kushoto) akielezea jambo huku Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Leonard Thadeo (kulia) na Mshauri Mwandamizi wa UK Sports Elias Musangeya (katikati) wakimsikiliza kwa makini. Mkutano huo umefanyika ikiwa ni sehemu ya tathmini ya maendeleo ya mradi wa International Inspiration.(P.T)
pix3_96c6b.jpg
pix3: Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Leonard Thadeo (kulia) na Mshauri Mwandamizi wa Shirika la UK Sports la Uingereza Bwana Elias Musangeya (kushoto) wakifurahia jambo walipokutana ofisini kwa Kaimu Katibu Mkuu huyo kwa ajili ya tathmini ya maendeleo ya mradi wa International Inspiration leo jijini Dar es Salaam.
pix4_20e92.jpg
pix4: Kutoka kulia Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Leonard Thadeo, Mshauri Mwandamizi wa Shirika la UK Sports la Uingereza Bwana Elias Musangeya, Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa Henry Lihaya na Mkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Michezo sehemu ya Usajili Bi. Mercy Rwezahura wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kikao cha tathmini ya maendeleo ya mradi wa International Inspiration kilichofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Picha zote na Frank Shija - WHVUM
0 comments

SERIKALI KUENDELEA KUWAJENGEA UWEZO WATAALAM KATIKA MASUALA YA MIKATABA

SERIKALI KUENDELEA KUWAJENGEA UWEZO WATAALAM KATIKA MASUALA YA MIKATABA

Picture_013_caa47.jpg
Picture 013- Afisa Habari wa ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bi. Asiatu Msuya akieleza kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu majukumu mbalimbali ya Divisheni ya Mikataba ikiwa ni pamoja na kutoa ushauri wa kitaalam katika masuala ya Mikataba na makubaliano yanayoihusu serikali,wakati wa mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bi. Zamaradi Kawawa.
Picture_028_ebdfc.jpg
Picture 028 -Mkurugenzi Msaidizi Divisheni ya Mikataba toka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali Bw. Edson Mweyunge akifafanua kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani)kuhusu utendaji kazi na mafanikio ya Divisheni hiyo katika masuala ya Mikataba,wakati wa mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bi. Zamaradi Kawawa.
0 comments

Wabunge wa EALA wapongeza hotuba ya Rais Kikwete.

Wabunge wa EALA wapongeza hotuba ya Rais Kikwete.

Jakaya-Kikwete_1dd20.jpg

Frank Mvungi-Maelezo
Wabunge wanaowakilisha Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki wamempongeza Rais Jakaya Kikwete kufuatia hotuba yake aliyoitoa Bungeni Dodoma tarehe 07/11/2013 kuhusu Mustakabali wa Jumuiya Hiyo.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa wabunge hao Mh. Adam Kimbisa wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.

Mh. Kimbisa amesema wabunge hao wanampongeza Mh. Rais kwa kuchukua fursa ya kuongea na Watanzania kupitia Bunge na kueleza masuala kadhaa baina ya Nchi wanachama na hali ya hivi sasa ndani ya Jumuiya.

Akifafanua zaidi Mh. Kimbisa amesemaMh. Rais amefanya uchambuzi wa kina kuhusu matatizo yaliyoikumba jumuiya ya Afrika Mashariki kufuatia mikutano mitatu iliyofanywa na nchi tatu za Kenya,Uganda na Rwanda ikiwatenga Tanzania na Burundi.

Alieleza zaidi kuwa wabunge wa bunge hilo wanaungana na Watanzania wengi kuhusu kuwepo kwa shirikisho la Afrika Mashariki lakini wanataka hatua hiyo isifanywe haraka bali kwa umakini mkubwa,sera ambayo pia Serikali ya Tanzania imeipa kipaumbele.

Pia alisema jambo la msingi ambalo mkataba wa uanzishwaji wa jumuiya umesema ni kuwa Jumuiya lazima iwe ni ya wananchi kwa manufaa ya wananchi na isiwe ya viongozi ambapo wananchi watashirikishwa katika kila hatua na kila ngazi ili waweze kushiriki kikamilifu kwa ajili ya maslahi yao.

Katika hatua nyingine wabunge hao waliipongeza Serikali kwa hatua iliyochukua kwa kuwarejesha makwao wahamiaji haramu kutoka Burundi,Rwanda,Uganda,DRC nchi nyingine ambao walitishia na kuharibu hali ya usalama na mazingira katika maeneo ya Mikoa ya Kagera,Geita na Kigoma.

Aidha wabunge hao wameiomba Serikali iendelee kusimamia suala hilo kwani baadhi ya wahamiaji haramu wameanza kurejea katika maeneo husika na wananchi wameanza kutoa malalamiko dhidi ya wahamiaji haramu.
0 comments

ILO YAENDESHA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI NA KUJIKINGA NA VVU KWA WANAWAKE CHALINZE

ILO YAENDESHA MAFUNZO YA UJASIRIAMALI NA KUJIKINGA NA VVU KWA WANAWAKE CHALINZE

SONY DSC

Mratibu Msaidizi wa Mradi wa Ukimwi ILO Getrude Sima (kushoto) akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi Kaimu Afisa Tarafa ya Chalinze kata ya Pera Bw. Rashid Kiwamba (kulia) kukabidhi vyeti kwa wahitimu wa mafunzo ya siku sita kuhusu maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kwa Wanawake wasiokuwa kwenye ajira rasmi na wanaoishi pembezoni katika juhudi za kudhibiti maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi.
Na Damas Makangale, Chalinze Moblog 
SHIRIKA LA KAZI DUNIANI (ILO) limeendesha mafunzo ya siku sita kuhusu maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kwa Wanawake wasiokuwa kwenye ajira rasmi na wanaoishi pembezoni katika juhudi za kudhibiti maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi. Moblog inaripoti.
Mradi huo wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) unalenga wanawake wote ambao wapo pembezoni wa barabara na mipakani kwa sababu wapo katika hali ya hatarishi.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Mkoa Pwani Wilayani Chalinze, Mratibu Msaidizi wa Mradi wa Ukimwi kutoka Shirika la Kazi Duniani (ILO) Getrude Sima amesema ndani ya siku sita mradi wa mapambano ya Ukimwi chini ya ILO umewafikia wanawake 120 katika kata za Pera, Chamakweza, Mpingo, Bwilingu, Msolwa na Mdaula.
SONY DSC

Mshauri wa Biashara wa shirika lisilokuwa la Kiserikali (NGO) TAPBDS Bi. Theresia Kato akifundisha wakinamama wa Chalinze (hawapo pichani) jinsi ya kuandika na kuandaa mchanganuo wa biashara katika mafunzo hayo ya siku sita yaliyoandaliwa na Shirika la kazi Duniani (ILO).

Amesema tangu mradi uanze kutekelezwa hapa nchini wakutoa mafunzo ya ujasiriamali na kujikinga na Virusi vya Ukimwi wameweza kuwafikia wanawake 220 nchi nzima katika maeneo ya pembezoni na mpakani kama vile Tunduma, Kyela na Namanga.

“Unajua wanawake wengi wanakuwa katika kundi hatarishi pale wanapokuwa katika maeneo ya mpakani na pembezoni mwa barabara kwa mfano Chalinze kwa sababu ya muingiliano wa watu hasa Madereva na Wafanyabiashara,” amesema Sima.

Sima ameongeza kuwa katika mradi huu wa mapambano ya Ukimwi malengo ni kumuelimisha Mwanamke ili ajitambue na aweze kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kwa kumfundisha stadi za maisha pamoja na ujasiriamali.

Amesema mradi unalenga wanawake wasiokuwa katik ajira rasmi ili kuongeza muamuko miongoni mwa wakinamama mitaani na vijijini ili waweze kukabiliana na vishawishi katika sehemu zao wanazoishi.
SONY DSC 
Bi. Theresia Kato akiwaelekeza washiriki namna ya kujaza fomu za kuombea mikopo kwa taasisi mbalimbali.

Kwa upande Mshauri wa Biashara toka shirika lisilo kuwa la Kiserikali TAPBDS, Theresia Kato amesema kuwa biashara ndogo ndogo ni muhimu katika kumjengea mwanamke uwezo wa kujiamini na kujitegemea.

“lazima wanawake waamuke ili waweze kuanzisha biashara zao na kuandika mchanganuo wa biashara na kutafuta mitaji kupitia taasisi mbalimbali za fedha hapa nchini,” amesema.
SONY DSC
Mratibu Msaidizi wa Mradi wa Ukimwi ILO Bi. Getrude Sima akisisitiza jambo kwa washiriki kuhusiana na mafunzo waliyoyapata yakawe chachu ya kuleta maendeleo.
SONY DSC
Picha juu na chini ni baadhi ya wakinamama wa Chalinze wakifuatilia mafunzo hayo yaliyomalizika mwishoni mwa wiki.
SONY DSC SONY DSC  
Mgeni rasmi Kaimu Afisa Tarafa ya Chalinze kata ya Pera Bw. Rashid Kiwamba akikabidhi vyeti kwa mmoja wa wahitimu wa mafunzo hayo.
SONY DSC  
Mwanamke wa Kimasai Paspen Kisota akipokea cheti chake baada ya kuhitimu mafunzo hayo.
SONY DSC
Picha juu na chini mgeni rasmi Kaimu Afisa Tarafa ya Chalinze kata ya Pera Bw. Rashid Kiwamba na Mratibu Msaidizi wa Mradi wa Ukimwi ILO Getrude Sima wakiwa kwenye picha ya pamoja na wahitimu.
SONY DSC SONY DSC
Fundi Sanifu wa Maabara ya Afya Bw. Rwezahura Merehiory akichukua damu kwa ajili ya vipimo vya VVU kwa mmoja wa washiriki wa semina ya mafunzo ya Ujasiriamali na Kupambana na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi iliyoratibiwa na shirika la Kazi duniani (ILO) wilaya ya Chalinze mwishoni mwa wiki.


0 comments

UKATILI WA KIJINSIA KWA WATOTO BADO IPO JUU TANGA.

UKATILI WA KIJINSIA KWA WATOTO BADO IPO JUU TANGA.

Na Oscar Assenga, Tanga.
IMEELEZWA kuwa hali ya uhalifu katika mkoa wa Tanga hasa kwenye makosa yanayohusu ukatili wa kijinsia na watoto inaonyesha bado upo juu huku jitihada kubwa zaidi zikihitajika kuweza kukabiliana nayo ili kuweza kutokomeza vitendo hivyo .

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga,Constatine Massawe aliyasema hayo wakati akizungumza hali ya ukatili wa kijinsia na watoto mkoa wa Tanga kwa kipindi cha kuanzia Mwezi Januari hadi Octoba mwaka huu na kueleza takwimu zinaonyesha kuwapo kwa makosa hayo ambayo yanaathiri sana afya ya mwili na akili kwa mwanadamu kitendo ambacho ni ukiukwaji
mkubwa wa haki za binadamu.

Massawe alisema takwimu hizo zinaonyesha katika kipindi hicho jumla ya kesi 308 za ubakaji zilirekodiwa katika vituo vya polisi mkoa wa Tanga ambapo kati ya hizo 148 bado zipo chini ya upelelezi ,100 zinaendelea mahakamani,13 zilipata ushindi kwa washtakiwa kupatiwa adhabu mahakamani wakati kesi nyengine 5 zilishindwa mahakamani na 42 zilifungwa katika vituo vya polisi kwa sababu mbalimbali ikiwemo kukosa ushahidi wa kuweza kupeleka kesi hizo kwa mwanasheria waserikali kwa hatua zaidi za  kisheria.

Aidha alisema ndani ya miezi kumi iliyopita jumla ya makosa ya kulawiti 46 yalirekodiwa katika vituo vya polisi mkoa wa Tanga ambapo kesi 18 zipo chini ya upelelezi ,kesi 16 zipo mahakamani,kesi 01
ilipata ushindi mahakamani kwa washtakiwa kupatiwa adhabu wakati moja ilishindwa mahakamani na kesi 10 zilifungwa katika vituo vya polisi kwa sababu mbalimbali.

Kamanda Massawe aliongeza kuwa katika makosa ya kutupa watoto yalirekodiwa 04 ambapo kesi zote nne zilifungwa kwa sababu mbalimbali
pamoja na kueleza katika kipindi hicho makosa ya wizi wa watoto yalirekodiwa matatu kwenye vituo vya polisi ambapo kesi 02 zinaendelea mahakamani wakati kesi 01 ilifungwa.

Akizungumzia mauaji yaliyotokana na wivu wa mapenzi/ugoni na mauaji majumbani kwa kipindi hicho yalikuwa ni matukio 16 na kutoa wito kwa
jamii kuacha kufanya vitendo vya ukatili wa  kijinsia kwani kufanya hivyo ni kuvunja sheria .
0 comments

Coastal Union U20 yaanza vema michuano ya Uhai.

Coastal Union U20 yaanza vema michuano ya Uhai.

 Yusuf Chuma (mwenye shati la mistari) akiangalia wenzake wakimenyeka leo asubuhi. Yusuf Chuma ni miongoni mwa mabeki walioingarisha Coastal Union U20 tangu mwaka juzi akishirikiana na Nzara Ndaro, Abdi Banda na Hamad Juma. kwa sasa Chuma, Banda na hamad wamepandishwa timu ya wakubwa. Alikuja kuwaangalia wenzake baada ya Ligi Kuu kusimama.

 Nzara Ndaro akiangalia wa kumpa mpira katika kipindi cha kwanza wakati huo timu imelala 1-0.

 Ayoub, beki mbili wa Coastal Unio  akitoa pasi kwa Raizin Hafidh (namba nne) huku Nzara Ndaro (nahodha wa Coastal) akiangalia kwa makini.

 Kiungo mshambuliaji wa Coastal Union Ally Ufudu akikokota mpira kuelekea lango la Azam.

 Yusuf Chippo akiwajibika uwanjani, hapa anawakemea vijana wake wasicheze mipira ya juu.

 Tunakwenda moja moja, ndiyo staili ya kocha Yusuf Chippo.

 Balaaaa... mchezaji mmoja anakabwa na kijiji.

 Penalt hii iliyoingizwa kimiani na Raizin Hafidh 'Boban' dakika ya 50 baada ya mchezaji wa Azam kuunawa mpira katika eneo la hatari.

 Wachezaji wa Coastal Union wakishangilia bao la kwanza lililofungwa kwa mkwaju wa penalt dakika ya 50.

 Nao ni na...

 Raizin Hafidh 'Boban' akiwa ameshampiga chenga golikipa wa Azam, anaelekea kupiga shuti kwa guu lake la kushoto kuhitimisha kilio kwa Azam dakika ya 55.

 Wachezaji wa Coastal Union wakishangilia bao la pili lililofungwa na Raizin Hafidh 'Boban'.

 Raizin Hafidh 'Boban' akitafuta mbinu za kumtoka mchezaji wa Azam huku mchezaji wa Coastal akiwa tayari kutoa msaada.



Kocha wa Coastal Union, Yusuf Chippo akizungumza na kiungo wa timu hiyo Ally Ufudu wakati mechi ikiendelea, leo asubuhi uwanja wa Karume Ilala jijini.
 

TIMU ya Coastal Union chini ya miaka 20 imeanza vema michuano ya UHAI U20 baada ya kuwachapa mahasimu wao wa muda mrefu Azam FC kwa mabao 2-1 yaliyoingizwa kimiani na kijana
Ilikuwa ni dakika ya 50 kipindi cha pili baada ya mchezaji wa Azam kuunawa mpira katika eneo la hatari Raizin Hafidh ‘Boban’ akakabidhiwa mikoba ya kupiga mkwaju wa penalt ambao ulitikisa nyavu za Azam huku golkikipa wa timu hiyo akibaki chini ameshangaa.
Bao hilo liliamsha shangwe katika uwanja wa Karume uliopo Ilala jijini Dar es Salaam, hali iliyoonyesha watazamaji wengi walikuwa upande wa Coastal Union.
Baada ya bao hilo kuingia wachezaji wa Azam walipoteza mwelekeo na kuruhusu mashambulizi ya mara kwa mara langoni mwao hali iliyompa mwanya ‘Boban’ ambaye alitokea upande wa kulia akamramba chenga beki wa Azam akaingia kwenye box dogo akakutana na golikipa wa Azam amezubaa, naye akamramba chenga na kumalizia kazi nzuri iliyotokana na juhudi zake binafsi kwa mguu wa kushoto.
Kuingia kwa bao la pili kulimaanisha kitu kimoja tu kwa Azam, kuhakikisha mvua hiyo ya mabao haiendelei. Hivyo wakaanza kucheza mchezo wa kujihami hali iliyowafanya kuendelea kushambuliwa mara kwa mara.
Hata hivyo wachezaji wa Coastal Union nao wakaanza kujisahau na kucheza kwa kujiamini huku wakionekana kuridhika na mabao hayo. Kutokana na mchezo huo ulioonyesha dharau na kujiamini vijana hao ambao mwaka jana walitawazwa kuwa kikosi bora cha michuano hiyo, walikosa mabao mengi ya wazi yaliyosababishwa na uzembe wa mabeki wao.
Katika kipindi cha kwanza Azam ambao ni mabingwa watetezi wa michuano hiyo baada ya kuwatoa Coastal Union mwaka jana walipata bao la mapema katika dakika ya 3 mfungaji akiwa Erick Haule, aliyetumia vema makosa ya mabeki wa Coastal Union na kumalizia krosi iliyopigwa kutoka upande wa kulia ikamkuta miguuni na kumbabatiza golikipa wa Coastal Union kasha ukaingia wavuni.
Bao hilo lilidumu mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza huku vijana wa Coastal Union wakiomba kipindi hicho kiishe mapema kutokana na mashambulizi waliyokuwa wakiyapata kutoka kwa wapinzani wao.
Katika hatua nyingine, ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Azam FC ndiwo ushindi wa kwanza kwa Coastal Union chini ya miaka 20 kwa vijana wenzao hao tangu walipoanza kukutana miaka minne iliyopita.
Aidha kwa mara tatu mfululizo Azam wamekuwa wakiwashinda Coastal Union kwa mikwaju ya penalt kwenye hatua ya mtoano, baada ya kutoka suluhu kwenye dakika za kawaida.
Kundi A lina timu nne za Coastal Union, Azam FC, Yanga na Mbeya City. Matokeo ya mechi inayochezwa sasa kati ya Yanga na Mbeya City ndiyo yataihakikishia Coastal Union kuongoza kundi kabla ya kutupa karata yake ya pili siku ya Jumanne dhidi ya Yanga katika uwanja wa Karume Ilala saa mbili asubuhi.
COASTAL UNION
NOV 17, 2013
DAR ES SALAAM, TANZANIA
0 comments

TMF YAANZA MAFUNZO YA UBORESHAJI WA UANDISHI WA MITANDAO YA KIJAMII.

TMF YAANZA MAFUNZO YA UBORESHAJI WA UANDISHI WA MITANDAO YA KIJAMII.

 Washiriki  wa mafunzo ya  uboreshaji wa  uandishi wa  mitandao  ya  kijamii kama blog  na mingine  wakiwa kwenye ukumbi wa dodoma hotel
 Ma bloga kutoka  mikoa  mbali mbali wakiwa katika darasa  la mafunzo ya uboreshaji uandishi wa mitandao ya kijamii chini ya  ufadhili wa TMF 
 

0 comments
 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger