Featured Post Today
print this page
Latest Post

Waziri Mukangara awafunda maafisa mawasiliano serikalini

Waziri Mukangara awafunda maafisa mawasiliano serikalini

Waziri Habari Utamaduni na Michezo, Dkt Fennellah Mukangara, akizungumza katika kikao cha Maafisa Habari na Mawasiliano wa serikalini, mkoani Tanga. 
 
Na Oscar Assenga, Tanga.

WAZIRI wa Habari,Vijana ,Utamaduni na Michezo Dokta Fenella Mukangara ametoa wito
kwa Maafisa Mawasiliano wa Serikali kwenye wizara, Idara na Taasisi za serikali kuendelea kujifunza kwa weledi mambo mbalimbali yatakayosaidia kuleta tija katika kutekeleza majukumu yao ya kusimamia mawasiliano kwenye maeneo yao ya kazi.

Mukangara ametoa wito huo jana wakati wakifungua kikao cha kazi cha maafisa mawasiliano kutoka maeneo mbalimbali hapa nchini kilichofanyika kwenye ukumbi wa Hotel ya Tanga Beach Resort Mkoani Tanga.
    
NAIBU KATIBU MKUU WA WIZARA YA HABARI VIJANA,UTAMADUNI NA MICHEZO PROF.ELISANTE OLE GABRIEL AKIZUNGUMZA KWENYE KIKAO HICHO KABLA YA KUMKARIBISHA WAZIRI.

Amesema maafisa hao wamepewa jukumu kubwa la kuiwezesha serikali kuipitia ofisi zao kufanya mawasiliano na umma kupitia vyombo vya habari kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu sera na miradi inayotekelezwa na serikali yenye lengo la kustawisha maendeleo kwa watanzania.


Amesema kimsingi wasemaji wa wizara ,idara na taasisi wao ndioa wasemaji wakuu badala ya watendaji wakuu wa sehemu zenu za kazi hivyo serikali inatimiza wajibu wake wa kutoa haki ya msingi ya wananchi kupata habari hususani zinazohusu utekelezaji wa shughuli mbalimbali serikalini.
 

Waziri huyo amesema kikao hicho kimebeba kauli mbiu isemayo "Matumizi ya mitandano ya Tehama na mitandao katika kuimarisha mawasiliano ya serikali kwa umma  ambapo amewaasa washiriki kutumia fuksa hiyo ya kuwepo mitandao ya kijamii ili kukidhi kiu ya jamii ya kupatiwa taarifa mbalimbali za kuelimishwa na kuburudishwa.

0 comments

TAHADHARI MTU MMOJA AFARIKI DUNIA BAADA YA KUJERUHIWA NA MAMBA MKOANI TANGA...!

TAHADHARI MTU MMOJA AFARIKI DUNIA BAADA YA KUJERUHIWA NA MAMBA MKOANI TANGA...!

Moja ya majeraha makubwa kwenye mwili wa marehemu yaliyopelekea kifo chake
Mtu mmoja amefariki dunia baadaa ya kujeruhiwa na mamba Korogwe mkoani  Tanga,Jina la marehemu halikuweza kufahamika mara moja.....!

Wanainchi wa eneo la la kijiji cha Korogwe wakiwa wameuzunguka mwili wa marehemu.


0 comments

MAKAMBA , KINANA NA WENGINE WACHANGIA

MAKAMBA , KINANA NA WENGINE WACHANGIA

          
 
 
Raisa Said, lushoto.
 Zaidi ya Sh. Mil. 41 zimechangwa  kwa  ajili  ya  ujenzi  wa  kanisa katika Chuo  cha Kumbukumbu ya  Sebastian Kolowa (SEKOMU), wilayani Lushoto katika juhudi za kuwasogezea  huduma  karibu wanafunzi  na  jamii  inayozunguka  katika chuo  hicho.

Kwa  mujibu  wa  Makamu  Mkuu wa  Chuo hicho, Dk Aneth  Munga  kati  ya  fedha  hizo, Sh. mil.22  zilichangwa na Mbunge wa Jimbo la Bumbuli, January  Makamba  kwa  kushirikiana  na   baadhi  ya Mawaziri, wabunge  pamoja  na  Katibu  Mkuu wa  CCM, Abdulahman Kinana.

Munga  alisema  kuwa  fedha  zilizochangwa zinawapa  matumaini  makubwa  ya kutimiza  ndoto  ya  ujenzi wa  kanisa  ambao  alisema  ili kukamilika  kwa  ujenzi zinahitajika  Sh. Bil.3.

Dk. Munga  alisema  kuwa  kujenga  si  jambo rahisi na kwamba  michango  walioipata  ni   mwanzo  wa  ujenzi  huo.

Makamu  Mkuu wa  Chuo  huyo alitaja sababu za  kumualika Makamba kuwa ni pamoja na  mchango  wake  katika  shughuli za kijamii na  kujitoa  kuwa  mtetezi  wa  amani. Dr. Munga alisema kuwa mara  nyingi  ameonekana  akisisitiza  juu ya upendo  na  amani kwa  watanzania.

Kwa upande wake, Makamba, ambaye pia ni Naibu  Waziri  wa  Mawasiliano  Sayansi alisema  kujengwa  kwa  kanisa  hilo ni  chachu  katika  jamii ya  wanafunzi  walioko chuoni  hapo  pamoja  na  wananchi  waishio  maeneo  ya  jirani.

Pia alisisitiza juu ya  umuhimu wa kudumisha  amani  na  upendo  uliopo  ili  Baraka  za  Mwenyezi  Mungu  ziendelee  kutawala nchini.
                                  Mwisho
0 comments

BUMBULI WALIA NA UPUNGUFU WA WATUMISHI

BUMBULI WALIA NA UPUNGUFU WA WATUMISHI

{Beatrece  Msomisi  ambae  ni Mkurugenzi  wa  bumbuli   akipokea  zawadi}
Raisa Said, Bumbuli.
 
 Halmashauri  ya Bumbuli  mkoani  Tanga inakabiliwa na  tatizo kubwa la upungufu wa watumishi jambo ambalo linakwamisha utendaji wa kazi katika Halmashauri hiyo mpya.

Akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri hiyo kilichofanyika Bumbuli mwishoni mwa wikli hii, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauiri hiyo,  Beatrice Msomisi alisema kuwa Halmshauri hiyo ina upungufu mkubwa wa  watumishi ambao alisema kuwa unaathiri shughuli za kazi.

 Msomisi alisema kuwa wakati Halmashari hiyo inaanzishwa ilipewa watumishi 28 ikiwa ni pamoja na madereva.  “Watumishi waliopo hivi sasa ni 1308 ambapo  mahitaji ni  2094  hivyo upungufu  uliopo ni watumishi  786 idara  zilizopo katika halmashauri hiyo zinahitaji watumishi wa kutosha kuendesha shughuli zao za maendeleo,” alisema Mkurugenzi huyo.

Ili kukabiliana na changamoto hiyo, Mkurugenzi huyo alisema kuwa imebidi achukue hatua kadhaa kuhakikisha kuwa kazi zinakwenda kama ipasavyo.

Mkurugenzi huyo  alisema  katika  halmashauri  hiyo  mpya  inakabiliwa  hasa  katika  idara  ya Biashara,  Idara ya Ardhi, Idara  ya  Nyuki pamoja  na  Idara ya  ushirika ambazo  idara  hizo  hazina  mtumishi hata  mmoja.
Hata hivyo  Msomisi alisema  kuwa  mpaka sasa  kuna wakuu wa  idara  wanne  na  wengine  wanakaimu  idara  zingine  na  waliobaki ni watumishi  wa  kujitolea ambapo alisema  kitengo  cha  mwanasheriasheria  wa  Halmashauri  wameajili mmoja kwa  mkataba.
wakati  huo huo  mkurugenzi  huyo  aliwataka  wananchi  wa  Bumbuli  kutoa  ushiriano kwa  watumishi  waliopo lengo likiwa kutoa huduma  bora  na  kuharakisha maendeleo ya kila  mmoja  yanapatikana  pamoja  na  kukuza  uchumi  wa  Bumbuli kwa  ujumla.
           MWISHO
0 comments

MJI WA HANDENI KUTUMIA ZAIDI YA TSH BIL. 7 KWA MWAKA 2014/15

MJI WA HANDENI KUTUMIA ZAIDI YA TSH BIL. 7 KWA MWAKA 2014/15


{Mkurugenzi  Mji wa  Handeni    Thomas Mzinga  pichani}Add caption
            Raisa  Said, Handeni

Baraza la Halmashauri Mji wa Handeni limepanga kutumia jumla ya Sh. Bilioni 7.92 kwa ajili ya shughuli mbalimbali za maendeleo na utawala kwa mwaka wa fedha 2014/2015.

Kwa mujibu wa mapendekezo ya bajeti yaliyopitishwa na kikao cha Baraza la Halmashauri hiyo, kati ya fedha hizo Sh. milioni.503.19 zimepangwa kutuimika kwa ajili kutekeleza miradi mbalimbali za maendeleo kwa mwaka huo wa fedha.

Akisoma mapendekezo hayo katika kikao hicho kilichofanyika makao makuu ya Halmashauri hiyo, Chanika, Handeni , Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri,Thomas Mzinga alisema vyanzo vikuu vya fedha za utekelezaji wa miradi ni ruzuku kutoka serikali kuu na wahisani.

Mzinga  alisema  bajeti ya  mwaka  2014/2015 imeandaliwa  kufuatiwa  malengo makuu  saba  ambayo ni  Huduma  ya  ukimwi  kuboreshwa na  maambukizi  mapya  kupunguzwa ,  kuboresha upatikanaji wa  huduma za  jamii,  kuimarisha  shudghuli za  utawala  bora pamoja  kuboresha udhibiti wa  majanga.
Mingine ni miradi ya  kuimarisha  huduma  za  kijamii jinsia  na  kujenga  uwezo  wa  jamii na  kuongeza  idadi  na ubora  wa huduma  za  jamii na  miundombinu .


Mkurugenzi huyo  alisema  kuwa  mbali ya fedha  hizo  pia  wanapeleka  maombi  maalum  nje  ya  ukomo  wa  bajeti  yenye  thamani  ya  Tshs. 2,374,000,000 kati ya  hizo  mil.1.5  zitatumika  katika  kujenga  jengo  la  utawala  na  mil. 624,000,00/= zitatumika  katika  kujenga vyumba 13 vya  maabara pamoja  na  mil. 250,000,000/= zitatumika  katika  kununua  gari  la  Mkurugenzi  na  gari  la Idara  ya  mipango  .
Akizungumzia juu ya changamoto zilizojitokeza katika utekelezaji wa  bajeti ya  2013/2014 ,
 alisema kuwa kuchelewa kwa fedha za  matumizi ya  kawaida  kutoka  serikali kuu (Hazina).

Alitaja chanhamoto nyingine kuwa ni kutopata fedha  za  maendeleo  kwa  wakati  kutoka  hazina (fedha  hizi  zinapitia Halmashauri  ya  wilaya  zinapotumwa).
                     MWISHO
0 comments

MCT WATEMBELEA TANGA PRESS CLUB.

MCT WATEMBELEA TANGA PRESS CLUB.

MWENYEKITI WA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA TANGA(TANGA PRESS CLUB)KUSHOTO AKIZUNGUMZA NA MAAFISA KUTOKA BARAZA LA HABARI TANZANIA (MCT) WA KWANZA KULIA NI THERESA CHILAMBO NA ANAYEFUATA NI ANITHA MENDOZA.





MRATIBU WA TANGA PRESS CLUB NEEMA KHATIBU KULIA AKIFURAHIA JAMBO NA OFISA WA MCT ANITHA MENDOZA MARA BAADA YA KUTEMBELEA KLABUNI HAPO LEO

HAPO MMOJA WA MAAFISA HAO,ANITHA MENDOZA  KUSHOTO ALIYESIMAMA AKIZUNGUMZA NA MRATIBU WA TANGA PRESS CLUB NEEMA KHATIBU.

HAPA MAAFISA HAO WAKIANGALIA PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI YA WANAHABARI KLABUNI HAPO


MWENYEKITI WA KLABU YA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA TANGA(TANGA PRESS CLUB)HASANI HASHIM KATIKATI AKITOA MAELEKEZO WA PICHA HIZO KWA MAAFISA HAO WA MCT WALIOTEMBELEA KLABUNI HAPO LEO.

0 comments
 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger