Featured Post Today
print this page
Latest Post

ANGALIA ERNIE BRANDTS ALIVYOONDOKA DAR KIMYAKIMYA


Kocha aliyetimuliwa Yanga, Ernie Brandts amechukua uamuzi wa kuondoka nchini kimyakimya.
Brandts aliondoka nchini juzi usiku na kuwasili nchini Uholanzi jana asubuhi.

Alipoulizwa sababu ya kuondoka kimyakimya huku akiwa ametangaza ataondoka usiku, Brandts alisema anaamini wazo lake lilikuwa zuri kiusalama.

“Sijui kwa nini nimekuwa na hofu, lakini nimeona hivi ni sahihi.
“Nashukuru niko hapa uwanja wa ndege na ninaondoka kurejea nyumbani.
“Mke na mtoto wangu wananihitaji na ninaamini kipindi hiki ndiyo bora cha kurejea nyumbani na kuwa pamoja na familia yangu,” alisema.
Brandts aliipa Yanga ubingwa na hadi anafukuzwa, Yanga ndiyo vinara wa msimamo wa Ligi Kuu Bara wakifuatiwa na Azam FC.
Alifukuzwa baada ya kikosi chake kuchapwa mabao 3-1 dhidi ya Simba katika mechi ya Bonanza la Nani Mtani Jembe iliyopigwa Desemba 21, mwaka jana.
0 comments

WAZANZIBARI WA SIMBA, BERKO KIVUTIO ZANZIBAR




Kocha Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic, juzi alimpanga kwa mara ya kwanza kipa wake mpya, Yaw Berko ambaye aliibuka kivutio kwenye mchezo wa Kombe la Mapinduzi dhidi ya KMKM.

Katika mchezo huo ambao mashabiki walikuwa wakimshangilia kipa huyo kwa nguvu kubwa dakika zote alizokuwa uwanjani, Simba ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 na kutinga robo fainali.
Kipa huyo aliweza kuchukua nafasi ya Ivo Mapunda ambaye amekuwa akicheza kwenye michezo mingi ya timu hiyo, lakini aliweza kuonyesha kiwango cha juu kwa kuokoa michomo mikali.
Mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Amani mjini Unguja, ulihudhuriwa na mashabiki wengi ambao walikuwa wakishangilia muda wote.
Simba iliweza kuutawala mchezo huo na kujipatia bao la mapema lililofungwa na Amri Kiemba katika dakika ya nne ya mchezo.
Hata hivyo, Loga alifanya jambo ambalo lilishangiliwa, ni baada ya kuwaanzisha wachezaji watatu Wazanzibar katika mchezo huo, jambo ambalo alisema ni kwa kuwa wana uzoefu na timu za huko.
Aliwaanzisha Abdulhalim Humud, Ali Badru na Adeyum Saleh ambao wote ni wazaliwa wa Zanzibar.
Kwa matokeo hayo Simba sasa inatarajiwa kuingia uwanjani leo kuvaana na Chuoni ya Zanzibar katika mchezo wa robo fainali.
0 comments

Waziri wa Ardhi,Nyumba na Makazi Profesa Anna Tibaijuka amemtaka Mwekezaji wa shamba la Mpunga la Kapunga[Kapunga Rice Project]kuachia hecta 1870 za Kijiji ili kumaliza mgogoro wa ardhi uliodumu kwa muda mrefu.

Waziri wa Ardhi,Nyumba na Makazi Profesa Anna Tibaijuka amemtaka Mwekezaji wa shamba la Mpunga la Kapunga[Kapunga Rice Project]kuachia hecta 1870 za Kijiji ili kumaliza mgogoro wa ardhi uliodumu kwa muda mrefu.

Waziri wa Ardhi,Nyumba na Makazi Profesa Anna Tibaijuka akiongea na wananchi wa Mbarali


Mmoja wa wakurugenzi, Mkurugenzi mtendaji Bwana Justin Vermaak akisoma taarifa fupi kwa waziri


Profesa Tibaijuka akipata maelekezo ya shamba  kutoka kwa mmoja wa wakurugenzi, Mkurugenzi mtendaji Bwana Justin Vermaak ambaye alimweleza kuwa suala la kuachia ardhi atakutana na wabia wenzake watano ili kutoa majibu muda mfupi ujao.






Waziri akivuka mto Chimara

Katika ziara hiyo waziri alijionea jinsi tani zaidi ya 1800 za mpunga uliovunwa na mwekezaji ukiwa umehifadhiwa nje ya maghala kutokana na kukosekana na soko ndani na nje ya nchi hivyo kufanya kiwanda kuendeshwa kwa hasara.




Waziri wa Ardhi,Nyumba na Makazi Profesa Anna Tibaijuka amemtaka Mwekezaji wa shamba la Mpunga la Kapunga[Kapunga Rice Project]kuachia hecta 1870 za Kijiji ili kumaliza mgogoro wa ardhi  uliodumu kwa muda mrefu.

Rai hiyo ameitoa alipofanya ziara katika shamba hilo ambalo liliuzwa hecta 7370 badala ya 5500 ambazo ndizo zilizostahili na kuacha hecta 1870 ambazo ni eneo la kijiji kabla ya kukabidhiwa shamba la NAFCO kabla ya kubinafsisha.

Ziara hiyo imefanywa na Waziri ili kujiridhisha baada ya kupokea mgogoro huo kwa muda mrefu bila majibu ya kuridhisha kutoka kwa watendaji wake hivyo kama Waziri mwenye dhamana lazima atoe majawabu yenye uhakika badala ya kuolea majibu ofisini.

Profesa Tibaijuka alikutana na Uongozi wa Serikali ya kijiji kabla ya kukutana na Mwekezaji na kuhitimisha kwa kufanya mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Kapunga ambao pia ulihudhuriwa na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Mbarali Matayo Mwangomo,Mkuu wa wilaya ya Mbarali Gulamhusein Kiffu na wataalam mbalimbali kutoka wilayani na mkoani.

Waziri Tibaijuka aliwashukuru wananchi wa Kapunga kwa uvumilivu wao kwani licha ya mgogoro kudumu muda mrefu hawajafanya vurugu zozote hivyo alimtaka Mwenyekiti wa kjiji hicho Ramadhan Nyoni kudumisha amani na upendo ili kumaliza mgogoro huo bila uvunjifu wa sheria.

Profesa Tibaijuka alipata maelekezo ya shamba hilo kutoka kwa mmoja wa wakurugenzi, Mkurugenzi mtendaji Bwana Justin Vermaak ambaye alimweleza kuwa suala la kuachia ardhi atakutana na wabia wenzake watano ili kutoa majibu muda mfupi ujao.

Hata hivyo Bwana Vermaak alibainisha kuwa shamba hilo linakabiliwa na changamoto ya wizi wa mbolea na mpunga kutoka kwa baadhi ya wananchi hivyo kuzorotesha uzalishaji wa mpunga.

Aidha Vermaak alimwambia Waziri kuwa kuharibiwa kwa miundo mbinu ya mifereji ya maji kilometa 14 kutoka mto Ruaha kumepelekea kupungua kwa maji katika shamba hilo hivyo kulazimika kulima chini ya kiwango.

Pia Bwana Vermaak amemwambia Waziri kuwa wanalazimika kukodisha mashamba kutokana na kuombwa na wananchi wa Kapunga ingawa hakuwa wazi juu ya mikataba ya ukodishaji kuokana na mashamba hayo kukodishwa kwa shilingi 2,880,000 kwa plot na kutakiwa kulipa mwekezaji tani 24 hadi 27 za mpunga baada ya mavuno.

Wananchi wameonekana kushindwa kumudu gharama za uendeshaji kauli iliyoungwa mkono na Diwani wa Kata ya Itamboleo mheshimiwa Lwitiko Mwangosi ambaye amesema kuwa licha ya kulipia shilingi 1,680,000 mwaka jana lakini hakupata kitu baada ya mwekezaji kuchukukua mpunga wote aliovuna.

Baada ya kukutana na uongozi wa kijiji na mwekezaji Waziri alihutubia wananchi na kuwaambia kuwa hivi sasa mgogoro haupo baada ya kumwomba mwekezaji kuachia hecta 1870 na kuwataka wananchi kuwa na subira kwani suala hilo halitachukua muda mrefu na kama atakaidi basi taarifa ataiwasilisha kwa Rais kwani ndiye mwenye dhamana ya kufuta hati miliki ya ardhi.

Katika mkutano huo wanachi walipata fursa ya kuuliza maswali ambapo Emmanuel Kapalamba alimwambia wazri kuwa vijana wamekosa ardhi ya kilimo hivyo kufanya maisha kuwa magumu kiuchumina pia kwamba hawpati huduma za umeme na maji licha ya miundo mbinu kupita katika kijiji chao.

Kwa upande wa wanawake walimweleza waziri kuwa kijiji hakina zahanati kutokana na iliyokuwapo kuporwa na mwekezaji hivyo kulazimika kutembea umbali wa kilomita 26 ili kupata huduma za afya katika hospitali ya Chimala.

Mkutano ulifungwa kwa waziri kuchukua baadhi ya changamoto za maji,umeme na kilimo kuzipeleka kwa mawaziri husika ili kupata ufumbuzi wa kudumu.

Katika ziara hiyo wazir alijionea jinsi tani zaidi ya 1800 za mpunga uliovunwa na mwekezaji ukiwa umehifadhiwa nje ya maghala kutokana na kukosekana na soko ndani na nje ya nchi hivyo kufanya kiwanda kuendeshwa kwa hasara ambapo baadhi ya hecta hazijalimwa na nyingine kufanya majaribio ya zao la soya kinyume na mkastaba.

Na Ezekia Kamanga 
Mbeya yetu
0 comments

Pitia tamko la Chadema dhidi ya kutekwa kwa mwenyekiti wao Temeke

Pitia tamko la Chadema dhidi ya kutekwa kwa mwenyekiti wao Temeke

 

 

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepokea kwa mshtuko taarifa za tukio la kutekwa, kuteswa na kuumizwa kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Temeke, Josephat Yona Patrick.

 Chama kupitia Kurugenzi ya Mawasiliano
na Uhusiano, mbali ya kukemea kwa nguvu zote tukio hilo la kihuni na mengine ya
namna hiyo yenye lengo ya ukatili dhidi ya binadamu, katika hatua ya sasa
kinapenda kusema yafuatayo juu ya tukio hilo ovu ;
1.   Jeshi la Polisi lifanye uchunguzi juu ya tukio hilo la kutekwa na kuteswa kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Temeke ili ukweli ujulikane na haki itendeke, kwa sheria kuchukua mkondo wake.

2.   Chama kinawataka wanachama na Watanzania kwa ujumla kutulia, hasa pale ambapo watu wenye hila na malengo yao, wanaanza kukihusisha chama na tukio hilo. Watambue kuwa pamoja na mtu yeyote kuwa kiongozi wa chama, bado anayo maisha yake na uhusiano na watu wengine katika jamii.

3.   Jeshi la Polisi linapaswa kuyachukulia uzito mkubwa na unaostahili matukio ya namna hii ambayo yanaanza kuota mizizi kutokana na watu waovu wanayoyatekeleza kutochukuliwa hatua za kisheria ambazo zingesaidia kuzuia yasitokee tena.

4.     Watanzania bado wanakumbuka kwamba hadi sasa Jeshi la Polisi limeshindwa kutoa taarifa za kina na kuchukua hatua za kisheria ambazo zingesaidia ukweli kujulikana na haki kutendeka katika matukio ya kutekwa na kuteswa kwa kiongozi wa madaktari Dk. Steven Ulimboka na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda. Hivyo ingesaidia kuzuia
matukio mengine kutokea.

5.   Ni kutokana na jeshi hilo kushindwa kuwajibika ipasavyo katika matukio mengine ya namna hiyo, watu waovu wanaweza kutumia mwanya wa kinachoendelea ndani ya CHADEMA kwa chama kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya wanachama wasio waadilifu, kufanya matukio ya namna hiyo ili kujenga taswira ya kukihusisha chama na uhuni huo unaobeba kila sifa ya kuitwa ukatili dhidi ya binadamu.

6. Aidha kushindwa kwa Jeshi la Polisi kuwajibika ipasavyo katika kufanya uchunguzi wa matukio hayo (yaliyotolewa kama mfano hapo juu) na mengine ya namna hiyo, jeshi hilo linazidi kujiweka katika wakati mgumu wakukwepa tuhuma za baadhi ya watendaji wake kujua na kushiriki masuala haya, hususan kwa kurejea tukio la kutekwa kwa Dkt. Ulimboka.

Imetolewa jana Jumanne, Januari 7, 2014 na;

Kurugenzi ya Mawasiliano na Uhusiano
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
0 comments
 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger