Featured Post Today
print this page
Latest Post

Mashine za TRA zazua balaa.. Mbeya wagoma kuzinunua, vurugu zazuka.....!

Mashine za TRA zazua balaa.. Mbeya wagoma kuzinunua, vurugu zazuka.....!

Mabomu ya machozi yalipigwa ili kuzuia wafanyabiashara wasilete vurugu

7024725_orig_b85b7.jpg

Maduka yakiwa yamefungwa

2503579_orig_f146a.jpg
Wafanyabiashara hao walichoma matairi ili kuwazuia polisi wasiweze kuwafikia
Na Kenneth Ngelesi

WAFANYABIASHARA mkoani Mbeya wamezua kizaazaa wakigoma kufungua maduka wakipinga agizo la Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) linalowataka kununua mashine za kielektroniki kwa ajili ya kukatia risiti za wateja pindi wanapowauzia bidhaa.

Katika sokomoko hilo lililotokea jana na kusababisha taharuki kwa muda kadhaa, wafanyabiashara hao wanadai kuwa gharama za mashine zitolewe na serikali.

Eneo la Soko la Sido ambalo lina wafanyabiashara wengi na tegemeo katika uchumi wa Jiji la Mbeya, walifunga biashara zao kwa muda usiojulikana.

Kadhia hiyo inakuja siku moja tangu Mkuu wa Mkoa huu, Abbas Kandoro, akutane na viongozi wa wafanyabiashara kutoka Soko la Sido na kuwataka viongozi kuwataarifu wenzao wasitishe mkutano ambao walitaka kuufanya jana katika uwanja wa Shule ya Msingi Ruanda Nzovwe.
Kandoro alifikia uamuzi wa kukutana na viongozi hao baada ya kupata taarifa kupitia gari la matangazo ambalo lilikuwa likipita na kuzunguka katikati ya jiji na kuwataka wafanyabiashara hao kufunga maduka na kufika mkutanoni ili kujadili suala zima la mashine hizo.

Taarifa zinadai kuwa baada ya Kandoro kusikia matanagzo hayo, aliliagiza Jeshi la Polisi kumkamata dereva wa gari hilo pamoja na Mwenyekiti wa Soko la Sido na kuwaweka rumande kwa muda usiojulikana.
Baada ya wawili hao kuwekwa ndani, lilitolewa agizo la kuzunguka tena mitaani kwa kutumia gari hilo ili kuwatangazia wafanyabiashara hao kuwa mkutano huo umesitishwa.

Uamuzi wa kusitisha mkutano huo ulipuuzwa na wafanyabiashara hao ambao jana waliendelea na maandilizi ikiwa ni kukodi gari jingine la matangazo kupita mitaani kuwahimiza wenzao kujitokeza kwa wingi. Hatua hiyo iliufanya uongozi wa mkoa kuwasambaza polisi mitaani kuzuia mkutano huo. Mabomu ya machozi na maji ya kuwasha vilitembezwa kwa wafanyabiashara hao ambao walikuwa wamekusanyika huku maduka yao yakiwa yamefungwa.

Mabomu hayo ya polisi yaliwaathiri wanafunzi wa Shule ya Msingi Kagera na kuwafanya wataharuki na kuanza kukimbia hovyo huku wengine wakizirai.

Kufuatia hali hiyo, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Ayoub Kiwanga, Ofisa Mtendaji wa Kata ya Ilomba, Erasto Mwakaponda na Diwani wa kata hiyo, Dickson Mwakilasa, walikubaliana kuwakabidhi wanafunzi hao kwa wazazi wao waliofika shuleni hapo kuwajulia hali baada ya kupokea taarifa za kupigwa mabomu.
Wakizungumza na Tanzania Daima, wafanyabiashara hao walisema kuwa wanashindwa kuelewa nguvu kubwa ambayo inatumiwa na polisi wakati hakuna vurugu zozote katika eneo hilo.

Alex Oswald, kwa niaba ya wenzake alisema kuwa wao waliamua kufunga maduka kwa hiari yao na kwamba lengo la mkutano lilikuwa kutoa msimamo wa kuiomba serikali itoe mashine hizo bure.
Naye Peter Tweve, alisema kuwa kimsingi wao hawajagoma kutumia mashine hizo bali wanataka wawekewe bure, kwani si kila mfanyabiashara anaweza kuinunua mashine hiyo ambayo kwa sasa inauzwa kwa sh 800,000.

Alipotafutwa Kandoro kuelezea tukio hilo, aligoma akisema kuwa yupo katika kikao, pia Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani, simu yake iliita bila kupokewa.
Wiki moja iliyopita, Mkurugenzi wa Elimu ya Kodi wa TRA, Richard Kayombo, alitoa taarifa kuwa wafanyabiashara wenye mapato ya zaidi ya sh 45,000 kwa siku wanapewa hadi Oktoba 14, mwaka huu wawe wamenunua mashine hizo.
0 comments

Meza ya magazeti leo alhamisi Oktoba 3

Meza ya magazeti leo alhamisi Oktoba 3

DSC 0011 c3260
DSC 0012 8e34e
DSC 0013 e6179
DSC 0014 c24b6
DSC 0015 f18c6
DSC 0016 6789d
DSC 0017 602a2
DSC 0018 9c80b
DSC 0019 b9490
DSC 0020 5323bDSC 0021 146a3
0 comments

siku ya wazee duniani yasherehekea tanga

siku ya wazee duniani yasherehekea tanga

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASHIRIKI KILELE CHA MAADHIMISHO YA SIKU WAZEE DUNIANI NA WAZEE WA KOROGWE MKOA WA TANGA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya Wazee waliohudhuria katika sherehe za Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani, baada ya kuhutubia katika sherehe hizo zilizofanyika kwenye Uwanja wa Mandu, Korogwe Mkoani Tanga leo  Picha na OMR
 Akivishwa vazi la Asili.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya Wazee.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia katika sherehe za Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani,yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Mandu, Korogwe Mkoani Tanga leo
0 comments

CHELSEA YAKUTANA NA KIBONDE, YAKIFANYIZIA HASWAA KUJENGA HESHIMA, FABREGAS AING'ARISHA BARCA, BALOTELLI AINUSURU AC MILAN KULALA KWA AJAX

CHELSEA YAKUTANA NA KIBONDE, YAKIFANYIZIA HASWAA KUJENGA HESHIMA, FABREGAS AING'ARISHA BARCA, BALOTELLI AINUSURU AC MILAN KULALA KWA AJAX

At the double: Ramires celebrates his second goal of the night to make it 3-0 to Chelsea
  Mawili: Ramires akishangilia bao lake la pili katika ushindi wa 3-0 wa Chelsea
 
  MABAO mawili ya Ramires moja kila kipindi, moja la wenyeji kujifunga na moja la Frank Lampard yamempa furaha kocha Mreno, Jose Mourinho baada ya Chelsea kuichapa Steaua Bucharest mabao 4-0 katika Ligi ya Mabingwa usiku huu.

FIne finish: Ramires fires home his second of the night in a comfortable win for Chelsea
Ramires akifunga bao lake la pili 
Sidelined: Fernando Torres limped off with a knee injury after just 11inutes to be replaced by Samuel Eto'o
Fernando Torres alitolewa nje baada ya kuumia dakika ya 11 na nafasi yake kuchukuliwa na Samuel Eto'o
Poacher's effort: Ramires pokes home to break the deadlock before celebrating (below)
Ramires akifunga bao la kwanza kabla ya kwenda kushangilia na Juan Mata (chini)
Ramires celebrates with Juan Mata
Striker's touch: Chelsea's Samuel Eto'o shoots before the ball is put into the net for an own goal
Bado wamo: Shuti la Samuel Eto lilimbabatiza mchezaji wa Steaua akajifunga
Salt in the wounds: Frank Lampard (left) celebrates his injury-time goal to make it 4-0
Pati la ushindi: Frank Lampard (kushoto) akishangilia bao lake la dakika za majeruhi lililohitimisha ushindi mnono wa 4-0

Katika mchezo mwingine, bao pekee la Fabregas dakika ya 75 lilitosha kuipa ushindi wa ugenini, Barcelona wa 1-0 dhidi ya Celtic nchini Scotland.
Barcelona: Valdes, Dani Alves, Pique, Bartra, Adriano, Xavi, Busquets, Iniesta, Fabregas/Tello dk78, Pedro/Sanchez dk74 na Neymar.
Celtic: Forster, Lustig/Forrest dk70, van Dijk, Ambrose, Izaguirre, Matthews, Brown, Mulgrew, Samaras, Commons/Pukki dk86, Stokes/Kayal dk70.
Heading in: Cesc Fabregas (floored) connected with Alexis Sanchez's cross to loop his effort beyond Fraser Forster
Kichwa, nyavuni: Cesc Fabregas (chini) aliunganisha krosi ya Alexis Sanchez kumtungua Fraser Forster
The man in the middle: Barcelona rush to congratulate goalscorer Fabregas
Sherehe: Barcelona wakimpongeza mfungaji wa bao lao pekee, Fabregas
Sealing the deal: Fabregas punches the air after firing Barca ahead
Anatisha: Fabregas akipiga ngumi hewani baada ya kuipa ushindi Barca

Katika mchezo mwingine, bao la dakika mwishoni mno la mkwaju wa penalti wa Mario Balotelli limeinsuru AC Milan kulala baada ya kupata sare ya 1-1 na Ajax katika Kundi H.
Waholanzi walifikiri wameshinda baada ya bao la kichwa la Stefano Denswil dakika ya 90, lakini kulikuwa kuna zali la Balotelli aliyechezewa rafu na Mike van der Hoorn kwenye eneo la hatari na mwenyewe akaenda kufunga kwa tuta..
Easy does it: Mario Balotelli was composed enough to roll in a late, late penalty for AC Milan at Ajax
Mkombozi: Mario Balotelli akifunga kwa penalty dakika za lala salama kuinusuru AC Milan kulala kwa Ajax
Easy does it: Mario Balotelli was composed enough to roll in a late, late penalty for AC Milan at Ajax
Fungeni midomo yenu: Mario Balotelli akipongezwa na wenzake kwa kazi nzuri

Schalke inaongoza kundi E kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Basel, bao pekee la Julian Draxler dakika ya 54.
Washindi wa pili wa msimu uliopita, Borussia Dortmund walipata pointi zao za kwanza baada ya kuifunga Marseille ambayo haina pointi hadi sasa mabao 3-0.
Dortmund iliyofungwa na Napoli wiki mbili zilizopita, ilipata mabao yake kupitia kwa Robert Lewandowski dakika ya 19 na 79 kwa penalti na Marco Reus dakika saba baada ya kuanza kipindi cha pili.
0 comments

GARETH BALE NJE LEO REAL MADRIDI IKIPIGANA ULAYA, MAN UNITED NAYO KUMKOSA RIO DHIDI YA SHAKHTAR

GARETH BALE NJE LEO REAL MADRIDI IKIPIGANA ULAYA, MAN UNITED NAYO KUMKOSA RIO DHIDI YA SHAKHTAR

WINGA Gareth Bale ataukosa mchezo wa leo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya FC Copenhagen kutokana na tatizo lake la majeruhi kuendelea katika maisha yake mapya Real Madrid.
Mchezaji huyo ghali duniani alifanya mazoezi peke yake gym jana, wakati wachezaji wenzake wengine wakijiandaa na mechi hiyo ya Kundi B na hakutajwa katika kikosi cha kocha Carlo Ancelotti.
Ilitarajiwa kocha huyo Mtaliano angemrejesha kikosini baada ya kipigo cha mwishoni mwa wiki kichoifanya sasa Real Madrid izidiwe pointi tano na Barcelona katika ligi ya kwa
 
Out: Gareth Bale will have to wait for his first start in the Champions League for Real Madrid
Nje: Gareth Bale ataukosa mchezo wa leo wa Real Madrid katika Ligi ya Mabingwa
Concern: The winger has struggled with a thigh problem in recent weeks
Uangalizi: Winga amekuwa akisumbuliwa na maumivu ya misuli ya paja siku za karibuni

Lakini Bale hayuko tayari kuitikia wito wa kocha wake, kutokana na maumivu ya misuli ya paja la kushoto aliyoyapata siku 11 zilizopita wakati akipasha misuli moto kwa ajili ya mechi dhidi ya Getafe na kumfanya aondolewe kikosi cha kwanza.
Re-think: Carlo Ancelotti will now have to consider his options... but at least he has Cristiano Ronaldo (below)
Anafiiri mara mbili: Kocha Carlo Ancelotti atalazimika kufikiri kwa kina, angalau anaye Cristiano Ronaldo (chini)
Re-think: Carlo Ancelotti will now have to consider his options... but at least he has Cristiano Ronaldo (below)
Bale na Cristiano Ronaldo katika moja ya mechi za timu hiyo

Naye beki Rio Ferdinand ataukosa mchezo wa timu yake, Manchester United dhidi ya Shakhtar Donetsk kutokana na maumivu ya nyonga.
Lakini kocha wa United, David Moyes amemtukuza mshambuliaji Robin van Persie kama mchezaji bora zaidi kuwahia kufanya naye kazi.
"Tumewaacha wachezaji au mmoja,"alisema Moyes. "Rio Ferdinand, Anderson, Fabio na Wil Zaha hawapo nasi. Sijawahi kumtumia Rio popote, lakini amepata matatizo ya nyonga. Si makubwa,".
Out: Moyes confirmed that Rio Ferdinand would not travel to Ukraine
Nje: Moyes amethibitisha Rio Ferdinand hatasafiri kwenda UkraineUpbeat: Wayne Rooney and Robin van Persie share a joke during Manchester United training
Wa mbele tishio: Wayne Rooney na Robin van Persie wakitaniana wakati wa mazoezi ya Manchester United jana
0 comments

SERIKALI YAZIDI KUIKOMALIA MAGAZETI YA MWANANCHI, MTANZANIA.

Assa Mwambene.

KWA mara nyingine serikali imeendelea kuandama vyombo vya habari viwili ilivyovifungia wiki iliyopita, magaz
eti ya Mwananchi na Mtanzania.

Jana ilitishia kuchukua hatua kali dhidi ya gazeti la Rai (dada wa Mtanzania) ikisema iko tayari kulifunga iwapo litaendelea kuchapishwa katika siku tofauti na Alhamisi.

Kupitia kwa Mkurugenzi wa Habari (MAELEZO), Assah Mwambene, serikali jana ilisema haitaki kuliona gazeti la Mwananchi mtandaoni kama ambavyo hailitaki mitaani.

Mwambene alipiga marufuku magazeti hayo kuonekana popote, kwa njia yoyote, kabla hayajamaliza kifungo.

Mwambene alisema kuwa gazeti la Mwananchi baada ya kufungiwa limeendelea kutoa habari zake kupitia tovuti ya gazeti lao kinyume cha amri iliyotolewa na kwamba serikali imewaandikia kuwataka kuacha mara moja la sivyo watalazimika kuchukua hatua kali zaidi.

“Kampuni ya New Habari 2006 baada ya kufungiwa moja ya magazeti yake, imeanza  kuchapisha gazeti la ‘Rai’ kila siku tangu  Septemba 29, mwaka huu bila ya kibali cha Msajili wa Magazeti,” alisema.

Hata hivyo, amri ya serikali ya kuzuia Rai kutoka kila siku hasa baada ya Mtanzania kufungiwa siku nne zilizopita, imekumbana na upinzani mkali kutoka kwa uongozi wa New Habari.

Akizungumza na Tanzania Daima Jumatano kwa njia ya simu, Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Hussein Bashe, alisema kuwa kauli ya mkurugenzi wa MAELEZO inaonyesha bayana jinsi serikali ilivyokusudia kuiangamiza kampuni yake.

Bashe alimshambulia Mwambene akidai kuwa huenda mkurugenzi huyo hajui sheria za kuendesha makampuni au ana nia mbaya na tasnia ya habari nchini kwa sababu Rai imesajiliwa na ina kibali cha kutolewa kila siku.

“Rai ni gazeti lililosajiliwa kutoka kila siku kwa kibali cha serikali kilichotolewa na msajili wa magazeti Desemba 22, 1994 kwa barua yenye kumb: IH/TN/283/12. Barua hiyo inasema: ‘Yah kuchapicha gazeti la Rai kila siku’ na kutiwa saini na Dominica C. Haule, kwa niaba ya Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo).

Hata hivyo, Mwambene pamoja na kukiri barua hiyo, amedai kuwa ilitolewa kwa kampuni ya Habari Corporation, na sio New Habari (2006) Ltd, iliyonunua hisa za Habari Corporation. TANZANIA DAIMA.

Mwambene alisema kwa msingi huo, Rai haiwezi kuchapishwa kila siku kama anavyojaribu kusema Bashe katika utetezi wake.

Hata hivyo, Bashe alionekana kushangazwa na kauli ya mkurugenzi huyo na kuhoji uelewa wake kuhusiana na sheria za biashara za kununua na kuuza kampuni.

Alihoji ikiwa kampuni ilinunua hisa zote, itashindwaje au kuzuiwa vipi kuendelea na uendeshaji wa shughuli ikiwa imenunua mali zote na hivyo kuwa halali kuendeleza shughuli zinazotakiwa.

“Sisi tulichofanya ni kuitaarifu tu idara ya habari kwamba sasa tutaendelea na kuchapa kila siku na tulifanya hivyo Jumamosi. Sasa tunashangaa anaendelea tena kutusakama. Kuna nini hapa?” alihoji Bashe kwa mshangao.

Mwambene alisema kuwa serikali  imeyafungia  magazeti ya hayo kwa kuzingatia  Sheria ya Magazeti ya Mwaka 1976 na kanuni zake za mwaka 1977.

Alisema kuwa umma unapaswa kufahamu kuwa serikali  haikukurupuka  kufungia magazeti hayo, baada ya kufuata taratibu zote za msingi ikiwemo kuwasikiliza wahusika.

“Mwananchi limefungiwa kwa muda wiki mbili kuanzia  Septemba 27, mwaka huu, na Mtanzania limefungiwa kwa muda wa miezi mitatu au siku 90 kuanzia  Septemba 27, mwaka huu,” alisema.

Aidha, serikali imelaumiwa kwa tamko lake la kulitaka gazeti la Mwananchi kutowekwa mtandaoni mambo ambayo wachunguzi wanasema yalipaswa kufanywa na mamlaka ya mawasiliano (TCRA), ambayo ndiyo yenye mamlaka na mambo ya mitandao nchini kama kulikuwa na ukiukwaji uliofanyika.

Wadau  wanasema tofauti za kimajukumu kati ya Idara ya Habari na Mamlaka ya Mawasiliano nchini ziko bayana ndio maana hata Rais Jakaya Kikwete alitofautisha Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, huku nyingine inayohusisha mambo ya mitandao ikiwa chini ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia.

Hatua hiyo ya serikali imezidisha mpasuko mkubwa kati ya utawala na vyombo vya habari, mashirika ya kiraia ndani na nje ya nchi.

Taasisi na mashirika hayo yamelaani hatua hiyo, huku yakiitaka serikali kuacha kuzuia haki ya wananchi ya kujieleza na kupokea habari na mengine yakienda mbali zaidi na kutuhumu kuwepo kwa hujuma ya kuwanyima wananchi habari zinazoendelea kujiri katika mchakato wa Katiba au kuwapa yale ambayo serikali inawachagulia wananchi ili wasome.

Padre wa Kanisa Katoliki aliyekuwa mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino Dk. Joseph Matumaini amesema, “Idara ya Habari Maelezo imepitwa na wakati, hivyo ifutwe au kama haitafutwa vyombo vya habari viunde chombo kiingine kitakachotenda haki ili kuiacha idara hii kwa maslahi ya serikali ambayo yameonekana kuwa sio maslahi ya umma.”
0 comments

MBIO ZA MWENGE WA HURU JIJINI MBEYAN TAYARI KUZINDUA MIRADI YA MAENDELEO.

mkuu wa mkoa wa mbeya Abbas Kandoro akiapa kuwa ameupokea salama mwenge wa uhuru kama alivyokabidhiwa na mkuu wa mkoa wa Njombe jana.

 mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akimkabodhi mwenge mkuu wa wilaya ya Mbeya dk Norman Sigala ambaye ataukimbiza mwenge huo kwenye halmashauri yake.
Mkuu wa wilaya ya mbeya Dk Norman Sigala akikiri kuupokea mwenge huo
viongozi mbalimbali wa mkoa wa Njombe na wilaya ya Makete wakielekea kwenda kuukabidhi mwenge huo kwa mkoa wa jirani wa Mbeya (picha zote na Edwin Moshi)
0 comments

HII NI MAALUM KWA WADADA NA WAMAMA WANAOTAKA WAWE MABIKRA TENA!! TAHADHARI.

HII NI MAALUM KWA WADADA NA WAMAMA WANAOTAKA WAWE MABIKRA TENA!! TAHADHARI.

wengi hujiuliza  kama  kuna dawa  ya  asili  ya  kurejesha  bikira  kwa wanawake.

 Haipo  dawa  ya  asili  inayo  weza  kurejesha  bikira  kwa  mwanamke.
Dawa  zilizopo ni dawa  za  kichina, na  side  effects  zake  ni  kubwa  sana. 

Kwa  mujibu  wa  tafiti  mbalimbali  za  kitaalamu, mwanamke  anaye  tumia  dawa za  kichina  kwa  ajili  ya  kurejesha  bikira  yake  anajiweka  katika   hatari  kubwa sana  ya  kupatwa  na  ugonjwa  wa  kansa kutokana  na  kemikali  mbalimbali zinazo  patikana  katika  dawa  hizo.

USHAURI  WETU : 
Tunashauri  usitumie  dawa  za kichina  kwa  ajili  ya  kurejesha  bikira  kwa  sababu madhara  yake  ni makubwa sana.

UTUMIE  DAWA  GANI?: 
Hakuna  dawa  ya  kurejesha  bikira, dawa  za  asili  zilizopo  ni  dawa  zinazo  fanya kazi  ya  kuufanya  uke  kuwa  tight  sana  lakini  hauwi  bikira.  
Bikira  ikishatoka  haiwezi  kurudi  tena.
0 comments

MKE WA WAZIRI ATAPELIWA MIL. 280

MKE WA WAZIRI ATAPELIWA MIL. 280

Ikupa Mwakanjuki, mke wa waziri wa zamani wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, marehemu Brigedia Adam Mwakanjuki, ametapeliwa shilingi milioni 280.

Waliomtapeli Ikupa ni vijana wanne ambao inadaiwa ni matapeli wazoefu jijini Dar es Salaam na kwenye baadhi ya mikoa ya Tanzania, wakitumia ‘triki’ ya uganga wa kienyeji.

Vijana hao wakijifanya waganga wa kienyeji, walimfuata Ikupa na kumwambia kwamba wangeweza kumfanya atajirike zaidi kwa njia za mizimu.

Watuhumiwa wote wanne wa utapeli huo wameshakamatwa lakini gazeti hili limepata majina ya wawili, wa kwanza akifahamika zaidi kwa jina la Silver na mwingine ni Mwang’ombe .

Chanzo chetu kilisema kuwa baada ya mwanamke huyo kupewa maneno ya ulaghai, aliingilika lakini akawa hana fedha ambazo ‘waganga’ hao walizihitaji.

“Mama aliposema hana fedha, wale matapeli walimwambia anazo mali ambazo anaweza kuuza na kupata kiasi cha fedha kinachohitajika,” kilisema chanzo chetu na kuongeza:

“Mama alisema analo shamba, wakamshawishi auze. Mama naye sijui aliwekewa nini, akawa anafanya kila kitu kutokana na maelekezo ya wale matapeli.

“Kweli aliuza shamba lakini fedha zote alikabidhi kwa wale matapeli. Siku zikapita, haoni mabadiliko yoyote, ghafla akamuona Mwang’ombe anaendesha gari la kifahari aina ya Toyota Land Cruiser Prado.

“Hapo ndiyo akashtuka, Mwang’ombe bila woga, akarudi tena kwa mama akamwambia zinahitajika fedha nyingine kwa ajili ya sadaka kwa yatima.

“Akiwa na wenzake, wakamshawishi auze shamba lingine zipatikane japo shilingi milioni 100 ili maisha yaanze kubadilika kwa kasi. Hapo ndipo akatushirikisha ndugu, tukagundua huo ni utapeli. 

Tukaamua kulifikisha hili suala kwenye vyombo vya sheria.”
Habari zaidi zinasema kuwa Ikupa kwa ushawishi wa ndugu zake, alifikisha malalamiko yake mpaka makao makuu ya jeshi la polisi na inadaiwa kuwa IGP Said Mwema aliagiza ma-RPC wote kufanya juu chini na kuwaweka nguvuni watuhumiwa.

“Hii ishu ni ya juu, sisi tumetumwa tuwakamate, tukishafanikiwa tutawakabidhi watuhumiwa kwa maofisa upelelezi makao makuu,” mmoja wa maofisa wa jeshi la polisi Kinondoni, alilinong’oneza gazeti hili.

Septemba 18, mwaka huu, saa 8 usiku, Mwang’ombe bila kujua kama yupo mtegoni, alipaki Prado lake lenye namba za usajili T940 CLX, Corner Bar, Sinza Afrika Sana, Dar es Salaam.

Alipopaki hapo, alichagua kiti ili apate ‘kuzila bata zake’ lakini eneo hilo, alikuwepo kaka mdogo wa Ikupa ambaye alitoa taarifa polisi na mara moja, gari lake likazingirwa kabla ya mtuhumiwa huyo kukamatwa na kufikishwa Kituo cha Polisi Kijitonyama, Mabatini.

Uwazi lilikuwepo wakati Mwang’ombe anakamatwa Corner Bar na lilipofuatilia, liligundua kwamba mtuhumiwa huyo alimtaja Silver kwamba naye ni mhusika.

Oparesheni ikitekelezwa na maofisa upelelezi makao makuu, ilifanikisha kukamatwa kwa Silver eneo la Kimara Baruti, usiku huohuo na siku iliyofuata, watuhumiwa wengine wawili walitiwa nguvuni kisha shauri likarejeshwa Oysterbay kwa utekelezaji wa mkondo wa kisheria.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP Camillius Wambura, alilithibitishia gazeti hili kwamba tukio hilo lipo mezani kwake.

“Tupo kwenye uchunguzi, kuna vitu tunakamilisha halafu baadaye tutafanya mawasiliano na ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa ajili kwenda mahakamani,” alisema Wambura.

Ikupa alipopigiwa simu, alipokea mtu wake wa karibu ambaye alisema: “Kama mama atataka kuzungumza na wewe atakupigia.”

Baada ya hapo hakupokea tena simu.
Utapeli kwa njia za uganga, mitandao ya simu, katika mashine za fedha (ATM) na kadhalika, umekuwa ukishika kasi nchini ingawa jeshi la polisi limekuwa likijipambanua kwamba linashughulikia kwa nguvu kubwa.
0 comments

Extra Bongo wamlilia marehemu Watuguru

Extra Bongo wamlilia marehemu Watuguru

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
BENDI ya Extra Bongo, imestushwa na kifo cha mpiga gitaa wa bendi ya WK sound, Joseph Watuguru, aliyefariki juzi na kupangwa kuzikwa leo Kongowe jijini Dar es Salaam.
Marehemu Jose Watuguru kushoto enzi za uhai wake.
Watuguru aliwahi kutamba na bendi kadhaa hapa nchini, ikiwamo ile Mchinga Sound akiwa na wakali mbalimbali, hasa Mwinjuma Muumini maarufu kama kocha wa Dunia.
Mkurugenzi wa Extra Bongo, Ally Choki.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa bendi ya Extra Bongo, Ally Choki, alisema kuwa kifo cha Watuguru ni pengo katika tasnia ya muziki wa dansi nchini.
Alisema marehemu alifariki kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya TB, huku akiacha mke na watoto wawili na msiba wake upo nyumbani kwa kaka yake Kongowe.

“Watuguru ni miongoni mwa wanamuziki waliokuwa na uwezo mkubwa hapa nchini, hivyo kifo chake ni pengo katika ramani ya muziki huo na wengi tutamlilia.
“Mpiga gitaa huyo mwenye uwezo wa aina yake amepangwa kuzikwa kesho, hivyo sisi kama Extra Bongo, tumeguswa na msiba wake na hakika tutaendelea kumuombea mema zaidi huko aendako,” alisema.
Mbali na Exta Bongo, wadau na wanamuziki mbalimbali, akiwamo Muumini nao waliguswa na msiba huo kiasi cha kumuongelea marehemu kutokana na kujadili kipaji chake kwenye kona ya muziki.
0 comments

Khamis Tambwe mabao aumwa tumbo ghalfa

Khamis Tambwe mabao aumwa tumbo ghalfa

Na Kambi Mbwana, Dar es Salaam
DAKTARI wa timu ya Simba, Yasin Gembe, amesema mshambuliaji wao Khamis Tambwe, amepata mvurugiko wa tumbo hivyo kukosa kufanya mazoezi ya asubuhi na wenzake.
Muda wote wa mazoezi, Tambwe alikuwa nje ya uwanja, hivyo kuzua hofu kwa wadau na mashabiki wa timu ya Simba wanaokoshwa na kasi ya mshambuliaji huo ndani ya uwanja.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Gembe alisema kuwa mshambuliaji wao Tambwe aliamka vibaya kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya ghafla ya tumbo.

Alisema hata hivyo maradhi hayo si tatizo la kumfanya asiwe mzima kwa siku mbili na kuongeza kuwa afya yake itatengemaa haraka kwa ajili ya kuwapo uwanjani mwishoni mwa wiki pale timu yake itakapovaana na Ruvu Shooting, Jumamosi, katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
“Tambwe anaendelea vizuri baada ya kupata tatizo la kuumwa tumbo, ila hali yake haitampa wakati mgumu kuingia uwanjani kucheza na timu ya Ruvu Shooting Jumamosi katika Uwanja wa Taifa.
“Mbali na Tambwe, pia majeruhi Henry Joseph na Issa Rashid wote wamepona na wameanza mazoezi jana na wenzao, hivyo nadhani hii ni hatua nzuri kwa Simba,” alisema.
Mechi ya Simba na Ruvu Shooting inasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka wa Simba, wenye hamu ya kuona timu yao inaendelea kufanya maajabu kwa kushinda ili ijiweke katika nafasi nzuri kileleni.
0 comments

SEREKALI YAZIDI KUYAANDAMA MAGAZETI LINGINE LAPIGWA MKWAEA MZITO

SEREKALI YAZIDI KUYAANDAMA MAGAZETI LINGINE LAPIGWA MKWAEA MZITO

KWA mara nyingine serikali imeendelea kuandama vyombo vya habari viwili ilivyovifungia wiki iliyopita, magazeti ya Mwananchi na Mtanzania.

Jana ilitishia kuchukua hatua kali dhidi ya gazeti la Rai (dada wa Mtanzania) ikisema iko tayari kulifunga iwapo litaendelea kuchapishwa katika siku tofauti na Alhamisi.

Kupitia kwa Mkurugenzi wa Habari (MAELEZO), Assah Mwambene, serikali jana ilisema haitaki kuliona gazeti la Mwananchi mtandaoni kama ambavyo hailitaki mitaani.

Mwambene alipiga marufuku magazeti hayo kuonekana popote, kwa njia yoyote, kabla hayajamaliza kifungo.

Mwambene alisema kuwa gazeti la Mwananchi baada ya kufungiwa limeendelea kutoa habari zake kupitia tovuti ya gazeti lao kinyume cha amri iliyotolewa na kwamba serikali imewaandikia kuwataka kuacha mara moja la sivyo watalazimika kuchukua hatua kali zaidi.

“Kampuni ya New Habari 2006 baada ya kufungiwa moja ya magazeti yake, imeanza  kuchapisha gazeti la ‘Rai’ kila siku tangu  Septemba 29, mwaka huu bila ya kibali cha Msajili wa Magazeti,” alisema.

Hata hivyo, amri ya serikali ya kuzuia Rai kutoka kila siku hasa baada ya Mtanzania kufungiwa siku nne zilizopita, imekumbana na upinzani mkali kutoka kwa uongozi wa New Habari.

Akizungumza na Tanzania Daima Jumatano kwa njia ya simu, Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo, Hussein Bashe, alisema kuwa kauli ya mkurugenzi wa MAELEZO inaonyesha bayana jinsi serikali ilivyokusudia kuiangamiza kampuni yake.

Bashe alimshambulia Mwambene akidai kuwa huenda mkurugenzi huyo hajui sheria za kuendesha makampuni au ana nia mbaya na tasnia ya habari nchini kwa sababu Rai imesajiliwa na ina kibali cha kutolewa kila siku.

“Rai ni gazeti lililosajiliwa kutoka kila siku kwa kibali cha serikali kilichotolewa na msajili wa magazeti Desemba 22, 1994 kwa barua yenye kumb: IH/TN/283/12. Barua hiyo inasema: ‘Yah kuchapicha gazeti la Rai kila siku’ na kutiwa saini na Dominica C. Haule, kwa niaba ya Mkurugenzi wa Idara ya Habari (Maelezo).

Hata hivyo, Mwambene pamoja na kukiri barua hiyo, amedai kuwa ilitolewa kwa kampuni ya Habari Corporation, na sio New Habari (2006) Ltd, iliyonunua hisa za Habari Corporation.

Mwambene alisema kwa msingi huo, Rai haiwezi kuchapishwa kila siku kama anavyojaribu kusema Bashe katika utetezi wake.

Hata hivyo, Bashe alionekana kushangazwa na kauli ya mkurugenzi huyo na kuhoji uelewa wake kuhusiana na sheria za biashara za kununua na kuuza kampuni.

Alihoji ikiwa kampuni ilinunua hisa zote, itashindwaje au kuzuiwa vipi kuendelea na uendeshaji wa shughuli ikiwa imenunua mali zote na hivyo kuwa halali kuendeleza shughuli zinazotakiwa.

“Sisi tulichofanya ni kuitaarifu tu idara ya habari kwamba sasa tutaendelea na kuchapa kila siku na tulifanya hivyo Jumamosi. Sasa tunashangaa anaendelea tena kutusakama. Kuna nini hapa?” alihoji Bashe kwa mshangao.

Mwambene alisema kuwa serikali  imeyafungia  magazeti ya hayo kwa kuzingatia  Sheria ya Magazeti ya Mwaka 1976 na kanuni zake za mwaka 1977.

Alisema kuwa umma unapaswa kufahamu kuwa serikali  haikukurupuka  kufungia magazeti hayo, baada ya kufuata taratibu zote za msingi ikiwemo kuwasikiliza wahusika.

“Mwananchi limefungiwa kwa muda wiki mbili kuanzia  Septemba 27, mwaka huu, na Mtanzania limefungiwa kwa muda wa miezi mitatu au siku 90 kuanzia  Septemba 27, mwaka huu,” alisema.

Aidha, serikali imelaumiwa kwa tamko lake la kulitaka gazeti la Mwananchi kutowekwa mtandaoni mambo ambayo wachunguzi wanasema yalipaswa kufanywa na mamlaka ya mawasiliano (TCRA), ambayo ndiyo yenye mamlaka na mambo ya mitandao nchini kama kulikuwa na ukiukwaji uliofanyika.

Wadau  wanasema tofauti za kimajukumu kati ya Idara ya Habari na Mamlaka ya Mawasiliano nchini ziko bayana ndio maana hata Rais Jakaya Kikwete alitofautisha Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, huku nyingine inayohusisha mambo ya mitandao ikiwa chini ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia.

Hatua hiyo ya serikali imezidisha mpasuko mkubwa kati ya utawala na vyombo vya habari, mashirika ya kiraia ndani na nje ya nchi.

Taasisi na mashirika hayo yamelaani hatua hiyo, huku yakiitaka serikali kuacha kuzuia haki ya wananchi ya kujieleza na kupokea habari na mengine yakienda mbali zaidi na kutuhumu kuwepo kwa hujuma ya kuwanyima wananchi habari zinazoendelea kujiri katika mchakato wa Katiba au kuwapa yale ambayo serikali inawachagulia wananchi ili wasome.

Padre wa Kanisa Katoliki aliyekuwa mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino Dk. Joseph Matumaini amesema, “Idara ya Habari Maelezo imepitwa na wakati, hivyo ifutwe au kama haitafutwa vyombo vya habari viunde chombo kiingine kitakachotenda haki ili kuiacha idara hii kwa maslahi ya serikali ambayo yameonekana kuwa sio maslahi ya umma.”

-Tanzania Daima
0 comments
 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger