|
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akitambulishwa kwa baadhi ya viongozi wa Kenya na
Naibu Rais wa Kenya Mhe William Ruto walipowasili kwa pamoja katika
uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi leo Ijumaa
January 24, 2014. |
|
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiweka sahihi katika kitabu cha wageni huku
akishuhudiwa na Naibu Rais wa Kenya Mhe William Ruto na balozi wa
Tanzania nchini Kenya Mhe Batilda Buriani walipowasili kwa pamoja
katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi leo
January 24, 2014. |
|
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Naibu Rais wa Kenya Mhe William
Ruto walipowasili kwa pamoja katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo
Kenyatta jijini Nairobi leo |
|
Viongozi
hawa walikutana jijini Amsterdam, Uholanzi, na kupanda ndege moja
kuelekea nyumbani. Rais Kikwete, aliyetua Nairobi kwa muda, alikuwa
akitokea Davos, Uswisi, alikokuwa kwenye ziara ya kikazi ambayo
ameikatisha ili kujiunga na wananchi wa jimbo la Chalinze katika msiba
wa Mbunge wa jimbo hilo Marehemu Said
Bwanamdogo, ambaye amefariki dunia alifariki dunia Januari 22, 2014
katika wodi ya Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Upasuaji wa Mishipa ya
Fahamu (Moi) alikokuwa akitibiwa. Mazishi yamepangwa kufanyika leo
nyumbani kwa marehemu Miono, Bagamoyo.
PICHA NA IKULU
|
Posted by
Unknown
5:37 AM