SAFARI ZA MIKOANI SASA UTATA...! MALORI NA MABASI FUL MGOMO... CHEKI HAPA.
Na Goodluck Hongo.
SIKU moja baada ya Chama cha Wamiliki wa Malori
nchini (TATOA), kutangaza usimamish
aji huduma za kusafirisha mizigo
ndani na nje ya nchi kuanzia leo, Chama cha Wamiliki wa Mabasi yaendayo
Mikoani (TABOA), nacho kimetangaza usitishaji huduma zake (kusafirisha
abiria), kuanzia kesho
. Awali TATOA kilidai, lengo la kusitisha
huduma ni kupinga agizo la Serikali kupitia Waziri wa Ujenzi, Dkt. John
Magufuli kuondoa msamaha wa tozo ya uzito wa magari yaliyozidi asilimia
tano ya uzito unaokubalika kisheria.
Msemaji
wa TATOA, Bw. Elias Lukumay, alisema msamaha huo ulitolewa na Serikali
mwaka 2006 baada ya kamati ambayo iliundwa na Serikali ikishirikisha
kufanya ziara katika mizani na kubaini haziko sawa kwa maana ya
kutofautiana vipimo vyake.
Sababu nyingine iliyosababisha Serikali
kutoa msamaha huo ni ubovu wa barabara, matuta mengi yaliyosababisha
kuyumba kwa mzigo na mizani kutofanyiwa matengenezo.
Alisema uamuzi
huo wa Serikali haukuishirikisha TATOA kama ilivyofanya mwaka 2006 mbali
ya umuhimu wa sekta hiyo nchini hivyo ili kuepusha mgogoro na Serikali
pamoja na wafanyakazi wa mizani, wamekubaliana kupaki magari yao.
Wakati
TATOA ikitoa msimamo huo ambao utekelezaji wake unaanza leo, TABOA nao
wamemtaka Dkt. Magufuli kurudisha msamaha wa asilimia tano vinginevyo
wanasitisha huduma za kusafirissha abiria kwenda mikoa mbalimbali nchini
pamoja na nje ya nchi kuanzia kesho.
Akizungumza na Majira Dar es
Salaam jana, Katibu Mkuu wa TABOA, Enea Mrutu, alisema kitendo cha
kuondoa asilimia tano kutayafanya mabasi mengi kusafiri na abiria
wachache hivyo wamiliki wake kuingia hasara.
Alisema tangu kutolewa
kwa taarifa hiyo, kumekuwa na misururu mikubwa ya magari katika mizani
hivyo kusababisha usumbufu mkubwa kwa abiria na kumaliza safari zao muda
mbaya.
"Tunamuomba Dkt. Magufuli arudishe msamaha wa asilimia tano
aliouondoa, upo uwezekano mkubwa wa mabasi kusafiri na abiria wachache
hivyo kuingia hasara," alisema.
Alimtaka Dkt. Magufuli na Waziri wa
Uchukuzi Dkt. Harrison Mwakyembe, kutafakari uamuzi huo kwa kina ili
kutoka na jawabu la kurudisha msamaha huo kwani sekta hiyo inategemewa
na wananchi wengi wanaosafiri kila siku.
"Tumekuwa hatushirikishwi
katika masuala kama haya, kitendo cha Serikali kuyaruhusu magari aina ya
Noah yenye thamani ndogo kubeba abiria zaidi ya uwezo wake pia
hatukushirikishwa," alisema.
Wakati huo huo, Bw. Mrutu aliwataka
wamiliki wote wa mabasi kufika katika Ofisi za TABOA ili kuchukua fomu
kwa ajili ya kupunguziwa bima kwa asilimia tano.
Aliwataka na
wamiliki ambao hawajajiunga na TABOA,wafanye hivyo sasa ili waweze
kushirikiana katika mambo muhimu yanayohusu huduma wanayoitoa kwa abiria
Majira
Posted by
Unknown
8:11 AM