Featured Post Today
print this page
Latest Post

Mkuu wa Mkoa Tanga awataka Wanawake Wilayani Korogwe kuwashitaki Wanaume Walevi

Mkuu wa Mkoa Tanga awataka Wanawake Wilayani Korogwe kuwashitaki Wanaume Walevi



Wanawake Wilayani Korogwe wametakiwa kuwashitaki  kwa viongozi waume zao ambao  wanazitelekeza familia zao kwa  ajili ya ulevi.Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa Mhe. Gallawa wakati wa  mkutano wa hadhara wa wananchi wa kijiji cha Mafureta kilichopo Korogwe vijijini  ambapo aliwataka wanawake kutowaonea huruma  wanaume wenye kasumba ya kuzitelekeza familia zao kwa sababu ya ulevi.

Mhe. Gallawa  alionekana kukerwa na maisha duni ya wakazi hao wa mafureta  licha ya kuzungukwa na mazingira mazuri ya kilimo na kutaka kujua kulikoni, aliwapasha wananchi hao kuwa ardhi ni mali na kwamba hawakustahili  kuwepo kwenye lindi la umaskini.
Hata hivyo idadi kubwa ya watu waliofika kumsikiliza Mkuu huyo wa Mkoa walikuwa katika hali ya ulevi huku  watoto waliokuwepo kutokuwa na  viatu wala nguo zenye kuleta matumaini ya maisha bora kwa  mtanzania jambo lililomchefua sana .

“Akinamama toeni taarifa kwenye vyombo vya sheria kwa wababa wanaouza vyakula  na kwenda kulewa  pombe ama kuongeza nyumba ndogo  huku watoto hawana viatu wala vifaa vya shule” alisema Gallawa.

Kwa upande mwingine aliwataka wananchi kuachana na kilimo cha mazoea  ambacho alisema kuwa  hakiwezi kuwaletea mabadiliko  mazuri ya  kimaisha kwa kuwa hakina tija wala muelekeo.

Awali Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Korogwe, Lucas Mweri  wakati akijibu hoja ya  Mkuu wa Mkoa kuhusu mradi wa kijiji hicho, alieleza kuwa kijiji cha Mafureta ni miongoni mwa vijiji vilivyopata  fedha kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji na kwamba zaidi ya tsh, million 300 zilitolewa kuiimarisha.

Mweri alieleza kuwa jumla ya tsh million 300 zilitolewa kwenye skimu ya Mafureta kwa ajili ya ujenzi wa miundo mbinu na kuboresha thamani ya zao la mpunga na kwamba watakopeshwa pembejeo kwa kulipa wakati wa mazao pamoja na mkakati  wa barabara ya uhakika.

Naye Mbunge wa jimbo la Korogwe vijiji, Stiven Ngonyani (Profesa majimarefu) aliwataka wananchi hao kuchangia mambo ya maendeleo yao badala ya kuchanga fedha kwa ajili ya kuleta waganga wa jadi ambao hatima yake ni kusababisha migogoro na jamii kutengana.


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Korogwe Vijijini Bw. Lucas Mweri akijibu hoja ya mradi wa kilimo cha umwagiliaji kijijini hapo


Umati wa wanakijiji waliofika katika mkutano wa hadhara wakati wa ziara ya Mkuu wa Mkoa

Baadhi ya watoto waliofika kwenye mkutano wa hadhara

0 comments

SHULE MAARUFU ZA SEKONDARI MKOA WA TANGA


MAZINDE JUU

[IMGA0297.JPG]



KIFUNGILO


Shule ya Sekondari Kifungilo ilianzishwa mwaka 1935. Ilianza kama kituo cha kutunza watoto, baadaye ikawa shule ya Msingi, baadaye mwaka 1981 ilianza kutoa masomo ya Sekondari ikijulikana kama Shule ya Sekondari ya Wasichana Kifungilo. Mwaka 1996 kidato cha tano na sita kilifunguliwa.
Masta wa Damu Takatifu pia hutoa huduma katika Majimbo mengine. Haya ni Arusha, Moshi, Morogoro, Zanzibar na Nairobi. Pia hutoa huduma nchi za Zambia, Zaire, Zimbabwe, Afrika ya Kusini, Korea, Amerika, Kanada na Ulaya.
Nembo yao ni Mwana Kondoo wa Pasaka, Mkombozi wetu aliyekuwa tayari kujitolea kwa ajili ya wanakondoo.


TANGA SCHOOL


LWANDAI

 

GALANOS SECONDARY SCHOOL




 HANDENI SECONDARY



USAGARA SECONDARY



KIDELEKO






 ECKERNFORDE SECONDARY SCHOOL

 

 KOROGWE GIRLS
0 comments

BOSS WANGU ANATAKA KULALA NA MIMI HADI ASUBUHI KWA MILION 5

BOSS WANGU ANATAKA KULALA NA MIMI HADI ASUBUHI KWA MILION 5

Salam kwa wana jamvi wote! 
Napenda kutoa funzo moja hapa! Ila sio msimulizi mzuri sana lakini naamini nitaeleweka tuuu....
Mimi na rafiki yangu ambaye tumekuwa marafiki baada ya kuajiriwa siku moja hapa jijini! 
Kwa kweli, bila hata kumaliza mwenzi mmoja the big boss akaanza kutupa mawe kwa rafiki yangu huyu ila hakuniambia kama boss anataka kungonoka! Ila binti akamtolea nje!! 
Alipo ona yamashindikana kule si ndoo akaamua ahamie kwangu kujaribu bahati yake, mimi nisivyo na siri nikaona nimshirikishe huyu rafiki yangu si ndo akafunguka nami nikajua kuwa boss ana mchezo mchafu!! 
Nikamwambia hakuna dinner atakayo nialika nikaenda ila mwenzangu vi dinner alikuwa havikosi!
Ila anavyo sema rafiki yangu hajawahi ku do naye!!!!! 
Sasa wiki hii, boss kanivulia uvivu macho kodo kwangu kila wakati, mara ohooo leo umependeza sana ohoo you luk scorching gorgeous hajui mwenzie najua kuwa tabia yake ni hafu! 
Sasa jana si akanipigia simu after work twende kwa coffe enening coloessum, kwa kuwa ilikuwa mapema nikasema kwa nini niwahi home hivi! 
After those thoughts na maamuzi ya kwenda binti nikamwambia poa not a big deal, nikamtonya shosti yangu akaniambia usiogope nothing he shall do to you! Hao mpaka coloessum 
After coffee akasema twende ukaone mahali ninapoishi nkamwambia poa............ 
Kufika hapo, akaanza can we spend a night together tomorrow?
Nikamwambia what will be the reward? huwezi nikunja usiku mzima for nothing atiiiii, cause i know hakuna love!!
Boss aka offer 500,000/ nikamwambia labda millioni tano!!!!!
Kapanda mpaka 3.5 mil nikasema 5 mil cash final + HIV test!
Akasema hapana that is too much! nIkamwambia then call it a day and take me home!!!!!! 
Sasa this morning at work he texted me, the offer is granted come and pick your cash!!!!!!
Nimeenda kwa ofisi nikamwambia my mind has changed keep your dirty money with you!!!!! 
He looked at me with a surprise usoni, I told him i thought few days after the incident will i be able to work again and a thought mapenzi ofisini ni upuuzi mtupu!!!!! 
He said good thoughts, u re too emotional! 
He ended we shall be always frends & anything you nid just tell me will be glad to help!!!
0 comments

WAMAREKANI WADAI KUGUNDUA CHANJO INAYOANGAMIZA UGONGWA WA UKIMWI

WAMAREKANI WADAI KUGUNDUA CHANJO INAYOANGAMIZA UGONGWA WA UKIMWI

Washington. Wanasayansi nchini Marekani wamegundua chanjo ambayo wanaamini itaweza kuangamiza Virusi Vya Ukimwi (VVU) kwa binadamu.

Katika majaribio ya chanjo hiyo, wanasayansi hao wameelezea kuwa imeonyesha mafanikio kwa kuangamiza kabisa virusi wanaofanana na VVU kwa nyani.

Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) limechapisha kwenye tovuti yake kuwa baada ya kubaini hilo sasa wamekusudia kufanya majaribio ya chanjo hiyo kwa binadamu.

Likinukuu taarifa iliyochapishwa kwenye jarida la kisayansi linaloitwa; Nature, lilimnukuu Mwanasayansi wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba cha Oregon, nchini Marekani akisema walijiridhisha kuwa chanjo hiyo iliangamiza virusi vyote kwenye mwili wa nyani.

Virusi hao jamii yake inafanana sana na VVU wanajulikana kama Simian Immunodeficiency Virus (SIV) ikiwa na maana ni virusi vinavyosababisha upungufu wa kinga ya kujikinga na maradhi kwa nyani.

Taarifa za kisayansi zinaonyesha kwamba SIV ni virusi ambao wamekuwa wakienea kwa njia ya kujamiiana miongoni mwa vizazi vya nyani na vilibadilika baada ya kuambukizwa kwa binadamu vikawa vimezaa VVU.

Wanasayansi hao wanasema kati ya nyani 16 waliopewa chanjo hiyo, waliyoipa jina la Cytomegalovirus (CMV),tisa walipona kabisa maradhi ya SIV.

Mtaalamu wa Taasisi ya Chanjo na Jeni katika Chuo Kikuu cha Oregoni, ambaye alihusika kwenye utafiti huo, Profesa Louis Picker aliielezea chanjo hiyo kuwa ni ya kutia moyo ukilinganisha na nyingine ambazo zimewahi kufanyika.

“Katika chanjo nyingi ambazo ziliwahi kuonyesha mafanikio ya kuangamiza virusi ni kwamba kuna baadhi ya seli virusi walibakia,” alisema Profesa Picker, akifafanua:

“Lakini kwa chanjo hii tulichunguza sehemu nyingi nyeti katika mwili wa nyani tukagundua kwamba hakuna kirusi aliyebakia.”

Alisema chanjo yao wameiamini kutokana na uwezo wake wa kupenya maeneo mbalimbali ya mwili kiasi kwamba siyo rahisi kirusi kubakia.

Wanasayansi hao walisema kwa kawaida nyani ambaye ameambukizwa SIV hufa ndani ya kipindi cha miaka miwili.
0 comments

NIMEGUNDUA MPENZI WANGU NIMPENDAE NI "LESBIAN" JE NIMUACHE

NIMEGUNDUA MPENZI WANGU NIMPENDAE NI "LESBIAN" JE NIMUACHE


Dunia yetu kwa sasa imepata mabadiliko makubwa sana, kiasi cha kusababisha tamaduni na desturi zetu kuathiriwa na mabadiliko hayo.

Ingawa ni maeneo mengi yameathirika kutokana na athari za kiutandawazi, lakini kwenye hii mada ningependa kuzungumzia hawa wanawake "wasagaji" au "lesbian".

Binafsi ni miongoni mwa waathirika wa hayo mabadiliko ya kiutandawazi, kwa kuwa binti ambae nimempenda kwa kipindi cha hivi karibuni ndio michezo yake hiyo (usagaji), hivyo katika mahusiano yetu hapo awali, hali ilikuwa ngumu sana maana hata siku moja HAKUPENDA tuongelee mambo ya ngono (ingawa tayari ameni-sign in).

Licha ya hivyo, mara kwa mara amekuwa akizungumzia sana mabinti wenzake wakati wa mazungumzo yetu, ingawa nimekuwa nikijitahidi sana kumtoa kwenye mazungumzo hayo, ila yeye amekuwa akilazimisha tujadili mambo ya aina hiyo, hali iliyonipelekea nikawaulize hao rafiki zake kuhusu hali halisi ya mpenzi wangu. Majibu yalikuwa kama ambavyo nilitarajia (kuwa demu wangu ni lesbian).

Aidha, ikitokea nimetoka nae "out" kula nae raha kwenye maeneo ya starehe, kila aonapo rafiki zake ni lazima awatathmini kwa ukaribu mpaka watu walioko karibu yake wanatambua ni nini anafanya, mara nyingine uenda mbali zaidi mpaka kugusa wenzake maeneo ya makalio kwa kuwachapa kofi.

Sasa ndugu zangu wana MMU katika hali kama hii, jembe nifanye nini?, maana kiukweli ni fedheha kuwa na binti anaetamani wanawake wenzake ingawa nampenda, nifanye nini katika hali kama hii?

Source:Jamii Forums
1 comments

OKWI AJIUNGA NA URA KUSUBIRI HATMA YAKE KWA WAARABU - FIFA YAWAPA ETOILE MPAKA MWISHO MWA MWEZI HUU KUWALIPA MIL 480 SIMBA

OKWI AJIUNGA NA URA KUSUBIRI HATMA YAKE KWA WAARABU - FIFA YAWAPA ETOILE MPAKA MWISHO MWA MWEZI HUU KUWALIPA MIL 480 SIMBA


STRAIKA wa zamani wa Simba, Emmanuel Okwi amejiunga na URA ya Uganda ili kujiweka fiti akisubiri hatma yake kwenye klabu ya Etoile du Sahel ya Tunisia.
Okwi amegoma kuichezea Etoile du Sahel mpaka itakapommalizia malipo yake ya kusaini mkataba pamoja na kumlipa malimbikizo ya mishahara ya miezi mitatu.
“Nimetulia kwanza nione suala langu linaendaje na suluhisho ni nini. Ninataka sana kurudi uwanjani kucheza soka la ushindani,” alisema Okwi.
“Ishu ni kwamba hawajanimalizia pesa ya kusaini mkataba pamoja na mishahara yangu ya miezi mitatu sasa,” alisema Okwi ambaye anaendelea kujinoa na URA ingawa haruhusiwi kucheza mechi ya mashindano kwa sababu ana mkataba wa miaka mitatu na Etoile du Sahel.
Wakala wa mchezaji huyo amesema kwamba wanaendelea na mazungumzo na Etoile ili kutatua suala la Okwi ingawa habari za ndani zinasema kwamba anafanya mpango wa kumpeleka kwa mkopo kwenye klabu moja ya Daraja la Kwanza Ulaya.
Okwi aliitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Uganda na kucheza dhidi ya Senegal wiki iliyopita katika mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia na kushuhudia kikosi cha Kocha Sredojevic Milutin ‘Micho’ kikiambuliwa kipigo cha bao 1-0.
Wakati Okwi akiwa na malumbano hayo na klabu hiyo ya Tunisia, Simba ambayo ilimuuza nayo inasubiri malipo ya Sh480 milioni kutoka kwa Etoile du Sahel ambayo iliahidi kulipa fedha hizo kabla ya mwisho wa mwezi huu.
Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) limetoa mpaka mwisho wa mwezi huu Simba iwe imelipwa.
SOURCE: MWANASPOTI
0 comments

PADRI MAGAMBA AONGEZA IDADI YA WATU MAALUM KUMWAGIWA TINDIKALI NDANI YA MIEZI 10 WAKIWEMO VIONGOZI WA DINI VISIWANI ZANZIBARI.

Padri Joseph Magamba akiwa wodini akipatiwa matibabu. ZANZIBARI. 
PADRI wa Kanisa la Romani Katoliki Parokia ya Machui, Joseph Monesmo Magamba amemwagiwa tind
ikali na watu wasiojulikana katika Mtaa wa Mlandege jana jioni, Mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar.


Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Haji Hana alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba kiongozi huyo wa dini amelazwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja, akiendelea na matibabu baada ya kujeruhiwa usoni, kifuani na mikononi.
Hana alisema kwamba Padri Magamba (60) alikuwa akitokea katika duka la huduma za mawasiliano ya mtandao la Shine Shine saa 10.15 jioni na watu waliommwagia walimtega mlangoni kabla ya kufanya uhalifu huo na kutoweka kwenye vichochoro vya Mitaa ya Mtendeni na Mchangani.
Alisema polisi wamestushwa na tukio hilo kwa vile limetanguliwa na matukio matatu ya kumwagiwa tindikali kwa viongozi wa dini na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano wa kufanikisha kuwakamata watu wanaojihusisha na vitendo hivyo.
“Tumeanza kufanya uchunguzi ikiwemo kuchukua maelezo ya majeruhi, tungependa zaidi kupata msaada wa kitaarifa kwa watu walioona na wanaojua mahali walipo watu wanaofanya vitendo hivyo,” alisema Hana.
Mfanyakazi wa Duka la Huduma za Mawasiliano ya Mtandao, Rukia Yahya Abass alisema anamtambua Padri Magamba kama mteja wake wa muda mrefu na huja dukani hapo nyakati za asubuhi au jioni kwa ajili kupata huduma za mawasiliano.
Rukia alisema ameshtushwa kuona padri huyo baada ya kumaliza kupata huduma na kutoka nje akipiga mayowe ya kujeruhiwa.
“Nimezoea kumwita father au babu, ni mteja wangu kwa kweli, nilimwona akirudi tena ndani huku akiomba msaada, watu waliokuwa katika mtandao harakahara wakammwagia maji, alikuwa akilalamika kwa ukali wa maumivu,” alisema Rukia akiwa na huzuni.
Alisema wasamaria wema ndiyo waliomchukua na kumpeleka hospitali. Kabla ya tukio hilo alilipa gharama za huduma ambazo zilikuwa ni Sh2,000 na kurudishiwa chenji yake baada ya kutoa noti ya Sh10,000.
Daktari Jamal Adam ambaye pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Mnazi Mmoja alisema kwamba Padri Magamba amepatiwa huduma ya kwanza na anaonekana amejeruhiwa usoni, mikononi na kifuani.
“Ni mapema mno kusema ameathirika kwa kiasi gani kutokana na tukio hilo, tunaendelea na juhudi za kumtibu, ”alisema Dk Jamal.
Huu ni mfululizo wa visa vipatavyo vinne vya kikatili ambavyo vimefanyika Zanzibar, vikiwalenga watu maalumu katika kipindi cha miezi 10 iliyopita. MWANANCHI
0 comments

Lowassa akutana na Wanavyuo Tabora;

Lowassa akutana na Wanavyuo Tabora;

lowas1_b7b1a.jpg
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli, Mh. Edward Lowassa (katikati) akiongozana na baadhi ya Viongozi wa Chama cha Mapinduzi Mkoani Tabora, wakati alipokuwa akiwasili kwenye Ofisi za CCM Wilaya ya Tabora Mjini, mchana wa jana Septemba 13, 2013.
lowasa6_34980.jpg
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akizungumza machache kwenye mkutano wake wa Mkoa wa Tabora.
lowasa9_6f637.jpg
Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Tabora Mjini, Seif Gulamali akizungumza machache mbele ya Wanafunzi wa Vyuo mbali mbali Mkoani Tabora leo.
lowasa10_b9241.jpg
Baadhi ya wanafunzi hao kutoka Vyuo mbali mbali Mkoani Tabora, wakiuliza maswali.
0 comments
 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger