Sheikh Sharrif Ahmed; Rais Anayedhibiti Maeneo Jirani Na Ikulu..
Ni Rais wa Somalia. Kwa hakika, kwa
sasa ndiye Rais wa nchi ya Kiafrika mwenye wakati mgumu sana. Na katika
shida zake, Sheikh Sharrif ameonekana, si mara moja, akitua Dar Es
Salaam, kwenye Ikulu ya JK. Kwa Sheikh Sharrif aliye matatizoni, kufunga
safari ya Dar kwa JK ni kama kwenda kwa Obama! Kuna tofauti kubwa na
Mogadishu.
Kiukweli Sheikh Sharrif Ahmed hana
eneo kubwa la nchi ambalo anaweza kusema kuwa analidhibiti. Kuna wakati
ikasemwa, kuwa anadhibiti maeneo jirani tu na Ikulu yake ya Mogadishu.
Huko kwengine kuna ' Mabwana wa Vita'.
Na sasa ni ' pasua' kichwa ya Al
shabaab. Tofauti na inavyoonekana nje, Al shaabab hawajawa na nguvu za
kutisha sana. Isipokuwa, wakiachwa wakue, ni ' pasua' kichwa si tu kwa
Somalia, bali kwa nchi zetu hizi.
Shambulizi la Wastgate ni ishara za Al
Shabaab wanaoanza kuota mapembe. Kuna mantiki ya Marais wa nchi jirani
na Somalia ikiwamo Tanzania, chini ya mwevuli wa AU na UN, kufanya
jitihada za kuungana katika kupanga mikakati ya kumsaidia Sheikh Sharrif
Ahmed.
Wamsaidie ili Somalia itawalike. Na
kwa kufanya hivyo, kutaharakisha vita ya kuisambaratisha Al Shabaab,
ambayo kimsingi, haina sapoti ya Wasomalia wengi.
Wikiendi Njema.
Maggid.
Posted by
Unknown
11:01 PM