Featured Post Today
print this page
Latest Post

Chama cha CUF wilayani Mkinga chaweka mkakati mzito


Na Oscar Assenga, Mkinga
CHAMA cha Wananchi CUF wilayani Mkinga kimeelezea mikakati yake ya kufanya mikutano ya hadhara katika kata zote zilizopo wilayani humo lengo likiwa kukiimarisha chama hicho pamoja na kujiandaa na uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 ili kuchukua kata zote.

Akizungumza hivi karibuni,Mwenyekiti wa Chama hicho,Mauya Kileo amesema anaamini lengo lao litafanikiwa kutokana na kukabalika vilivyo na wananchi maeneo mbalimbali wilayani humo kitendo ambacho kiliwawezesha chama hicho kupata kata saba kati ya 21 zilizopo.

Kileo amezitaja kata ambazo zimechukuliwa na chama hicho wilayani humo kuwa ni Mtimbwani, Kwale, Manza, Boma, Doda, Moa na Duga Sigaya na kueleza mikakati yao ni kuongeza idadi ya kata kwenye uchaguzi huo mkuu kwani hilo linawezekana kutokana na mshikamano walionao.

Aidha aliwataka wanachama wa chama hicho kuendelea kuonyesha mshikamano ili kuweza kufanikisha malengo yao ya siku moja kuongoza halmashauri yaweze kufanikiwa.
0 comments

King Majuto: Njaa, shida za wananchi zinanilazimu nigombee Ubunge Tanga Mjini 2015

King Majuto: Njaa, shida za wananchi zinanilazimu nigombee Ubunge Tanga Mjini 2015


Na Kambi Mbwana, Dar es Salam
MSANII wa filamu na vichekesho wa muda mrefu hapa nchini, Amri Athuman maarufu kama King Majuto, amesema hali ya Tanga ilivyokuwa sasa na ugumu wa maisha unamlazimisha aingie kwenye siasa kwa ajili ya kuwania Ubunge mkoani Tanga.
Msanii wa vichekesho Tanzania, Amri Athuman, maarufu kama King Majuto, pichanii, aliuhakikishia mtandao huu nia yake ya kuwania Ubunge mwaka 2015 kwa tiketi ya CCM

Majuto anataka kugombea Ubunge katika Jimbo la Tanga mjini, ambapo kwa sasa lipo chini ya Mbunge wake Omar Nundu, jambo linaloanza kuibua maswali kede kede miongoni mwa wadau wa sanaa wanayempenda mzee Majuto.

Mbunge wa Tanga Mjini, Omar Nundu, pichani.
Akizungumza na Handeni Kwetu mapema wiki hii, King Majuto alisema kwamba atagombea Ubunge kwa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), chama anachokipenda na kukiheshimu kwa kiasi kikubwa mno kutokana na mfumo wake wa uongozi.
Alisema watu wamekuwa wakiishi maisha magumu na yenye kukatisha tamaa, hivyo ni wakati wake sasa kuingia katika ulingo huo ili amalizie wakati wake kwa ajili ya kuwapatia maisha mazuri wananchi wa Tanga na Tanzania kwa ujumla.
“Kuna watu wanaweza kusema labda njaa ndio inayonifanya niingie kwenye siasa na kutaka kuwania nafasi kubwa ya Ubunge, ila lazima wajuwe kuwa sina njaa kwakuwa kazi ninayoifanya inanipa fedha za kutosha na maisha yangu ni mazuri.

“Nina mpangilio mzuri wa kazi zangu, bado naheshimika kwa kiasi kikubwa na kazi zangu zinapendwa, ila kuingia kwenye siasa ni kwasababu nina malengo mazuri na wanananchi wa Tanga Mjini na Tanzania kwa ujumla, hivyo hakuna wa kunizuia,” alisema Mzee Majuto.
“Kwa sasa nipo sawa zaidi na malengo yangu hayo naoamba Mungu yafanikiwe bila kuogopa majina ya wanasiasa waliokuwapo au wanaoweza kupambana na mimi katika nafasi hiyo, tukianza ndani ya CCM na baadaye Uchaguzi Mkuu,” aliongeza Majuto.
Kauli ya King Majuto inaweza kuleta picha ya kupendeza kwa wadau wa sanaa Tanzania, huku akiwa ni miongoni mwa wasanii wanaokubalika kwa kiasi kikubwa mno. Bila shaka kwa kauli hiyo inaongeza ugumu wa siasa za mwaka 2015 huku kila mmoja akiona ana uwezo wa kuwania nafasi mbalimbali za kisiasa hapa Tanzania.
0 comments

EPHRAIM KIBONDE APATA AJALI MLIMANI CITY

EPHRAIM KIBONDE APATA AJALI MLIMANI CITY

Ephraim Kibonde akishuka kwenye gari baada ya ajali.
..Akilikagua gari lake.
Trafiki akiwa eneo la ajali.
Gari la Kibonde likiwa eneo la ‘round about’ ya kuelekea Mlimani City baada ya ajali.
Fundi akirekebisha gari hilo baada ya ajali.
Mtangazaji wa Clouds FM, Ephraim Kibonde amepata ajali ya gari leo asubuhi  katika barabara ya Sam Nujoma kwenye ‘round about’ ya kuelekea Mlimani City. Gari alilokuwa anaendesha Kibonde aina ya Toyota Carina lenye nama za usajili T 733 BVE limeharibika kwa mbele katika ajali hiyo.
(Picha: Chande Abdallah / GPL)
0 comments

STEPHEN WASIRA "SINA UFUNGUO WA IKULU, SIWEZI MCHAGULIA RAIS NANI WA KUONANA NAYE"

STEPHEN WASIRA "SINA UFUNGUO WA IKULU, SIWEZI MCHAGULIA RAIS NANI WA KUONANA NAYE"

*Asema hampangii Rais nani aonane naye
*Mtikisiko mkubwa watarajiwa bungeni Dodoma
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wasira, amesema hana mamlaka ya kumchangulia Rais nani akutane naye.

Alitoa kauli hiyo katika mahojiano na Rai yaliyofanyika Jumanne wiki hii ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam kuhusu hali ya siasa nchini katika kipindi ambacho umma wa Watanzania unasubiri kusainiwa kwa Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya Kikwete.

“Taarifa kwamba naweza kumwambia Rais Kikwete aonane na huyu au asionane na yule si za kweli, Rais ana mamlaka yake, ana ofisi yake binafsi, pia yeye ni kama baba hivyo mtu yoyote bila kujali itikadi ana haki ya kuonana na Rais.


“Ninachofahamu muswada ukija Rais atasaini kwa sababu taratibu na kanuni zote zimefuatwa, lakini kama wenzetu wanahitaji kumuona Rais ni sawa, na amesikia wito na amekubali. Tusubiri matokeo ya mazungumzo,” alisema.

-Mtanzania
0 comments

sakata la kodi ya simu


Fatma Karume 75d49
Wanasheria Fatma Karume (kulia) na Beatus Malima wanaowakilisha Chama cha Walaji nchini wakijadiliana na mawakili wa Serikali, Alesia Mbuya (wa pili kushoto) baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kuahirisha kesi ya kupinga kukatwa kodi ya Sh, 1,000 kwa kila simcard ambayo ilipitishwa na Bunge la Bajeti la mwaka huu wa fedha wa 2013/149 
0 comments

Vyombo vya habari kutowaandika Mukangara, Mwambene

Vyombo vya habari kutowaandika Mukangara, Mwambene

WanahabariClip_1f73f.jpg

Wadau wa habari nchini wametangaza msimamo wa kutotangaza wala kuandika habari zinazomhusu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela Mukangara pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Habari(Maelezo), Assah Mwambene kama sehemu ya kupinga mwenendo wa serikali wa kuvifungia vyombo vya habari.

Wadau hao kutoka taasisi mbalimbali za habari wamesema kuwa pamoja na kilio cha muda mrefu cha kuitaka serikali kufuta Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976, lakini hakuna jambo lolote lililofanyika mbali ya kuendelea kuviandama vyombo hivyo.

Katika taarifa yao, wadau hao wamesema pia wamesikitishwa na tabia iliyoonyeshwa na Dk Mukangara na Mwambene kuchukua uamuzi wa kuyafungia magazeti ya Mwananchi na Mtanzania bila kuyasikiliza na kupotosha umma juu ya jambo hilo.

"Kwa msingi huo, wadau tumeamua kwamba tutasitisha kuandika, kutangaza na kupiga picha shughuli zozote zitakazowahusisha au kuratibiwa na Dk Mukangara na Mwambene hadi hapo itakapotangazwa vinginevyo. Adhabu hiyo inaanza mara moja kuanzia leo," imesema sehemu ya taarifa hiyo.

Aidha taarifa ya wadau hao imesema kuwa wataendelea kupinga Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 kwa kutumia njia mbalimbali ikiwemo kuongeza nguvu ya kisheria mahakamani kwenye kesi iliyofunguliwa na Kampuni ya Hali Halisi Publishers Ltd, mwaka 2009 inayopinga sheria hiyo.
Taasisi zilizoshiriki kwenye uamuzi huo ni pamoja na Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari (Moat), Jukwaa la Wahariri (TEF), Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika-tawi la Tanzania (Misa-Tan) na Baraza la Habari Tanzania (MCT).

Nyingine ni Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC), Klabu ya Waandishi wa Habari ya Dar es Salaam (DCPC) na Tanzania Human Rights Defenders (THRDC).
Chanzo>mwananchi mtandaoni
0 comments
 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger