SIMBA SC WAZUIWA KUCHEZA NA ASHANTI KESHO HADI WALIPE MILIONI 25, ‘MPIGANAJI’ RAGE AINGIA MSITUNI KUINUSURU KLABU
Na Mahmoud Zubeiry, Posta
SIMBA SC imetakiwa kulipa Sh. Milioni 25 kama gharama za uharibifu wa viti katika vurugu ambazo mashabiki wa timu yake walifanya timu yao ikimenyana na Kagera Sugar, Oktoba 31, mwaka huu Uwanja wa taifa, Dar es Salaam na kutoka sare ya 1-1.
Adhabu hiyo imetolewa na Bodi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na tayari Simba SC wamekabidhiwa barua- na wameambiwa hawataruhusiwa kukanyaga nyasi za Uwanja wa Taifa kesho kumenyana na Ashanti United kabla ya kulipa fedha hizo.
Lakini Simba SC wameistaajabu barua waliyopewa wakisema ina mapungufu kwa sababu haina mchanganuo wowote na mbaya zaidi muda uliobaki ni mchache kuelekea mechi ya kesho- maana yake hautatoa fursa ya mjadala.
Mwenyekiti wa Simba SC, Alhaj Ismail Aden Rage sasa anataka kutumia kipaumbele chake cha kuwa Mbunge (Tabora Mjini CCM) akiwa na uwezo wa kuzungumza moja kwa moja na Mawaziri, kujaribu kuifanya adhabu hiyo isifanye kazi kesho hadi hapo mijadala itakapochukua nafasi.
Kikubwa Simba SC wanasema barua haina michanganuo na hata wakitafakari uharibifu ulitokea wanaona hauendani na gharama wanayotakiwa kulipa. BIN ZUBEIRY inafahamu Simba SC haina nia ya kuepuka adhabu, bali inataka mchanganuo ili kujiridhisha.
Pamoja na hayo, Simba SC wanalalamika kupewa adhabu mara mbili- kwanza wanachama wake wamekamatwa na sasa wapo Rumande kutokana na vurugu hizo, na wakati huo huo wanatakiwa kulipa gharama za uharibifu.
Simba SC wenyewe wanaamini hii ni sawa na kuadhibiwa mara mbili, jambo ambalo wanasema ni kinyume cha sheria.
Baada ya Kagera kusawazisha bao dakika ya pili ya muda wa nyongeza baada ya kutimia kwa dakika 90 na kupata sare ya 1-1, Uwanja wa Taifa, uligeuka eneo la vita baina ya Polisi mashabiki wa Simba SC.
Baada ya Salum Kanoni kukwamisha nyavuni mkwaju wake wa penalti, mashabiki wa Simba waliokuwa viti vya Rangi ya Bluu na Chungwa, walianza kung’oa viti na kuvitupia uwanjani.
Malalamiko ya Simba SC ni kwamba, mchezaji aliyesababisha penalti ya Kagera aliuingiza mpira kwa mkono katika eneo la hatari na akajiangusha- lakini refa akatoa penalti. Na katika mchezo huo huo refa huyo huyo aliwanyima penalti Simba SC baada ya beki wa Kagera kuushika mpira kwenye eneo la hatari.
Mara baada ya viti kuanza kurushwa, Polisi walianza kupambana na mashabiki hao kwa kuwatupia mabomu ya machozi, ndipo wakaanza kukimbia. Makocha na wachezaji wa Simba kwa pamoja waliwafuata waamuzi kuwalalamikia- hali ambayo ilifanya watolewe kwa kusindikizwa na Polisi.
Bao la Simba lilifungwa na mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Amisi Tambwe dakika ya 45 baada ya kupokea pasi nzuri ya Betram Mombeki na kumpiga chenga beki Salum Kanoni, kabla ya kumchambua kipa Hannington Kalyesebula.
Wakati Simba inatozwa faini ya Sh. Milioni 25, yenyewe ilipata mgawo wa Sh. 7,242,252.45 kutokana na jumla ya Sh. 32,726,000 zilizopatikana kwenye mechi hiyo.
Ligi Kuu inatarajiwa kuendelea kesho kwa JKT Ruvu kumenyana na Coastal Union, Ashanti United na Simba, Kagera Sugar na Mgambo Shooting, na Ruvu Shooting vs Mtibwa Sugar, wakati keshokutwa Azam itacheza na Mbeya City, Yanga itacheza na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati Rhino itakuwa mwenyeji wa Tanzania Prisons hizo zikiwa mechi za kukamilisha mzunguko wa kwanza.

Ustadh umeiponza timu kulimwa faini ya Sh. Milioni 25, unaisaidiaje sasa? |
Lakini Simba SC wameistaajabu barua waliyopewa wakisema ina mapungufu kwa sababu haina mchanganuo wowote na mbaya zaidi muda uliobaki ni mchache kuelekea mechi ya kesho- maana yake hautatoa fursa ya mjadala.
Mwenyekiti wa Simba SC, Alhaj Ismail Aden Rage sasa anataka kutumia kipaumbele chake cha kuwa Mbunge (Tabora Mjini CCM) akiwa na uwezo wa kuzungumza moja kwa moja na Mawaziri, kujaribu kuifanya adhabu hiyo isifanye kazi kesho hadi hapo mijadala itakapochukua nafasi.
Kikubwa Simba SC wanasema barua haina michanganuo na hata wakitafakari uharibifu ulitokea wanaona hauendani na gharama wanayotakiwa kulipa. BIN ZUBEIRY inafahamu Simba SC haina nia ya kuepuka adhabu, bali inataka mchanganuo ili kujiridhisha.
Rage anapambana adhabu isifanye kazi kesho |
Pamoja na hayo, Simba SC wanalalamika kupewa adhabu mara mbili- kwanza wanachama wake wamekamatwa na sasa wapo Rumande kutokana na vurugu hizo, na wakati huo huo wanatakiwa kulipa gharama za uharibifu.
Simba SC wenyewe wanaamini hii ni sawa na kuadhibiwa mara mbili, jambo ambalo wanasema ni kinyume cha sheria.
Baada ya Kagera kusawazisha bao dakika ya pili ya muda wa nyongeza baada ya kutimia kwa dakika 90 na kupata sare ya 1-1, Uwanja wa Taifa, uligeuka eneo la vita baina ya Polisi mashabiki wa Simba SC.
Baada ya Salum Kanoni kukwamisha nyavuni mkwaju wake wa penalti, mashabiki wa Simba waliokuwa viti vya Rangi ya Bluu na Chungwa, walianza kung’oa viti na kuvitupia uwanjani.
Lakini hakuna wasiwasi, ikishindikana mwenye Simba yake, Zacharia Hans Poppe atalipa, Milioni 25 kitu bwana! |