Featured Post Today
print this page
Latest Post

KINANA AHITIMISHA ZIARA TANGA

KINANA AHITIMISHA ZIARA TANGA


 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye wakiwapungia mkono wananchi walipokuwa wakiwasili kwenye mkutano wa hadhara kwenye Uwanja wa Tangamano, jijini Tanga jioni ya leo, alipokuwa akihitimisha ziara ya siku 11 katika Mkoa wa Tanga.
Kinana akihutubia umati wa watu kwenye mkutano wa hadhara, jijini Tanga leo.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Kinana akipanda ngazi kwenda jukwaani wakati wa mkutano huo.
 Bajaji zikiongoza msafara wa Kinana kwenda kwenye mkutano wa hadhara.
 Msafara wa pikipiki ukiongoza msafara wa Kinana jijini Tanga.


 Bodaboda zikiongoza msafara wa Kinana
Kinana akipiga Saluti ikiwa ni ishara ya kuwasalimia wananchi katika mkutano huo
 Sehemu ya umati wa wananchi wakiwa katika mkutano huo
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia mkutano wa hadhara jijini Tanga
Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara na kuelezea miradi mbalimbali iliyotekelezwa kwa kufuata Ilani ya Uchaguzi ya 2010
wa Jimbo la Tanga Mjini, Omari Nundu akielezea jinsi miradi ilivyotekelezwa  katika jimbo hilo
Kinana akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wapinzani walioamua kujiunga na CCM katika mkutano huo wa hadhara
Kinana akivalishwa kanzu aliyopewa na wazee wa Tanga baada ya kufurahishwa na hotuba yake
Wazee wa Tanga wakimpatia zawadi ya kiti maalumu Kinana
Wananchi wakiwa na hamu ya kupeana mkono na Kinana baada ya mkutano kumalizika
Kinana akiwa katika vazi alilopewa zawadi na wazee wa Tanga baada ya kufurahishwa na hotuba yake
Kinana akiondoka baada ya kumaliza mkutano
0 comments

COASTAL UNION YAWAFUNDISHA SOKA NDANDA,YAWAFUNGA BAO 2-1 MKWAKWANI LEO

COASTAL UNION YAWAFUNDISHA SOKA NDANDA,YAWAFUNGA BAO 2-1 MKWAKWANI LEO

KIKOSI CHA COASTAL UNION KILICHOIPIGA NDANDA SC MABAO 2-1 UWANJA WA CCM MKWAKWANI.




TIMU ya Coastal Union ya Tanga leo imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ndanda SC ya Mtwara katika pambano la Ligi kuu soka Tanzania bara .

Mchezo huo ulichezwa kwenye uwanja wa CCM Mkwakwani ambap ulikuwa na kasi kutokana na timu zote ksuhambuliana kwa zamu.

Mabao ya Coastal yalifungwa na Joseph Mahundi akimaliza pasi ya Hamisi Mbwana "Kibacha" na bao la pili likifungwa na Hussein Sued aliyemaliza krosi ya Razack Khafani.
  
Bao la kufutia machozi la Ndanda FC lilifungwa dakika ya 57 kupitia Nassoro Kapamba kwa njia ya penati iliyotokana na mchezaji wa Coastal Union Sabri Rashid kuunawa mpira eneo la hatari na mwamuzi wa mchezo huo Amoni Paul kutoka Mara kuamuru ipigwe penati hiyo.
0 comments

Nimenusurika kupigwa na Wazanzibari mara mbili bungeni

Nimenusurika kupigwa na Wazanzibari mara mbili bungeni



Mbunge Ali Keissy akitolewa nje ya Ukumbi wa Bunge na walinzi.

Mbunge wa Nkasi Kaskazini mkoani Rukwa, Ally Keissy amesema kuwa katika uhai wake akiwa katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Bunge la Katiba hawezi kusahau alivyonusurika kupata kipigo kutoka kwa wabunge wa Zanzibar.
Alizungumza hayo katika mahojiano maalumu na gazeti hili yaliyotaka kujua historia ya maisha yake kabla na baada ya kuwa mbunge, hali ya kisiasa na Mchakato wa Katiba ulivyokuwa.Keissy alisema kuwa alinusurika mara mbili kupigwa na wabunge hao, huku wakimtolea lugha za kejeli na matusi.

"Kitu ambacho siwezi kukisahau nikiwa bungeni tangu mwaka 2010 mpaka sasa ni matukio mawili ya kutaka kupigwa. Moja ni katika Bunge la Jamhuri ya Muungano na jingine katika Bunge Maalumu la Katiba; ...haya siwezi kuyasahau kamwe," alisema mbunge huyo.

Keissy aliongeza: "Unajua unapokuwa bungeni, hakuna haja ya kuonyesha ubabe, unashindana kwa hoja na unajibiwa kwa hoja. Kama mimi nimetoa hoja, basi nanyi mjenge hoja kwa kunijibu, lakini kukimbilia kutaka kunipiga siyo suluhisho."

Anakumbuka matukio hayo akieleza kuwa mosi ni lile lilitokea Mei 26 mwaka huu ambapo alinusurika kupigwa baada ya kutoa maneno yaliyodaiwa kuwa ya kashfa kwa wabunge wa Zanzibar wakati wa akichangia Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

"Tukio la pili lililotokea mwezi uliopita (Septemba), wakati wa vikao vya Bunge Maalumu la Katiba, nilinusurika kipigo baada ya kupinga Rais wa Zanzibar kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Muungano,"alisema Keissy.

Akichangia mjadala wa Katiba, mbunge huyo asiyeisha vituko alisema kuwa haiwezekani Rais wa Zanzibar kuwa Makamu wa Rais wa Muungano kwa kuwa hakuchaguliwa na wananchi wa Tanzania Bara jambo lililozua tafrani bungeni.
Hata hivyo, Keissy alisema kuwa pamoja na matukio hayo na vitisho vingine, hatasita, wala kuogopa kusema analoamini kuwa ni kweli.

"Kamwe sitaogopa, nitaendelea kusema ukweli, nitaendelea kujenga hoja kwa kile ninachokifahamu na watu wanaotaka kunipinga wawe wakipinga kwa hoja, hapo nitakuwa tayari kuwasikiliza,"alisema.

Historia ya maisha yake

Keissy alizaliwa wilayani Nkasi, Mkoa wa Rukwa 15-Oktoba-1954. Alihitimu darasa la nane, Sumbawanga Middle School mwaka 1965.
Baada ya kumaliza darasa la nane, alianza kufanya shughuli mbalimbali hasa biashara za magari ya kubeba mizigo, mabasi ya abiria na maduka ya kuuza bidhaa mbalimbali.
0 comments

Elimu ya awali Tunduru na changamoto zake

Elimu ya awali Tunduru na changamoto zake

Mwalimu wa darasa la awali wa Shule ya Msingi Nakayaya, Teckla Milanzi (kulia) akiwa na wanafunzi wake eneo ambalo hutumika kama darasa la wanafunzi hao.
Mwalimu wa darasa la awali wa Shule ya Msingi Nakayaya, Teckla Milanzi (kulia) akiwa na wanafunzi wake eneo ambalo hutumika kama darasa la wanafunzi hao.

 WADAU wa elimu nchini Tanzania wanaamini kwa kiasi kikubwa kwamba endapo elimu ya awali (chekechea) nchini Tanzania itatolewa katika misingi inayostahiki itakuwa ni njia moja wapo madhubuti ya kuimarisha ubora wa elimu. Hii ndiyo maana wanaendelea kupaza sauti wakiitaka serikali kupitia vyombo husika kuboresha kwanza elimu ya awali kabla ya kupanda ngazi nyingine za juu. Huenda kilio hiki cha wadau wa elimu kimeanza kusikika serikalini.

Kwani tayari Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi iliagiza tangu mwaka 2010 kuwa kila shule zake za msingi ni lazima lianzishwe darasa la awali ili kuwenza kuwaandaa wanafunzi kuingia na darasa la kwanza.
Awali elimu hii ilikuwa ikitolewa kwa kiasi kikubwa na taasisi na vikundi mbalimbali na hata watu binafsi nje ya shule za msingi, tena kwa hiyari. Kwa sasa sera na miongozo ya elimu inatamka wazi kuwa nilazima kila shule ya msingi iwe na darasa la awali kwa ajili ya elimu hiyo muhimu. 

Changamoto kubwa iliyoibuka kwa sasa baada ya utekelezaji wa agizo hilo ni namna elimu hiyo inavyoendeshwa kwa kusuasua kwenye baadhi ya shule za Serikali. Hivi karibuni mwandishi wa makala haya alitembelea baadhi ya shule za msingi zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru kuangalia hali ya utekelezaji wa zoezi hilo.

Uchunguzi ulibaini zipo shule ambazo licha ya kusajili wanafunzi wa awali kila mwaka hazina madarasa ya kusomea kwa watoto hao, hali ambayo inafanya wanafunzi hao wadogo kufundishwa katika mazingira magumu na kudhohofisha lengo zima la utoaji wa elimu hiyo. Wapo wanafunzi ambao hulazimika kufundishiwa nje, yaani chini ya mti ama kwenye magofu (majengo ya shule ambayo hayajakamilika) iwe madarasa au nyumba za walimu.

Teckla Milanzi ni mwalimu wa darasa la awali, Shule ya Msingi Nakayaya. Anasema kimsingi wanafunzi wa darasa la awali shuleni hapo wanasomea chini ya mti kwa kuwa hawana darasa maalum kwa wanafunzi hao. Anasema wakati wa mvua ama jua kali mara nyingine hulazimika kuhairisha masomo kwa siku kutokana na hali ya hewa.

Baadhi ya wanafunzi wa darasa la awali katika Shule ya Msingi Tunduru Mchanganyiko wakiwa darasani kama walivykutwa na mwandishi wa makala haya hivi karibuni.

Baadhi ya wanafunzi wa darasa la awali katika Shule ya Msingi Tunduru Mchanganyiko wakiwa darasani kama walivykutwa na mwandishi wa makala haya hivi karibuni.

Anasema anashukuru kwa sasa wanajihifadhi kwenye jengo moja ambalo linaendelea na ujenzi shuleni hapo, jengo ambalo hata hivyo mara baada ya ujenzi kukamilika na wahusika kukabidhiwa darasa watarudi kusomea chini ya mti kama ilivyo ada. 

Hata hivyo, anasema licha ya changamoto hiyo darasa hilo halina vitabu kwa ajili ya kufundishia wanafunzi, bali kuna nakala moja moja kwa baadhi ya masomo ambavyo vilitafutwa kwa jitihada za mwalimu mwenyewe. “Mfano kwa vitabu vya Kiswahili, Kiingereza, Sayansi na Hisabati kuna nakala moja moja tu, ambazo hutumiwa na mwalimu mwenyewe.
Anasema darasa hilo licha ya kuwa na changamoto kedekede hata kwenye mgao wa fedha zinazoletwa shuleni kila mara halimo hivyo hakuna kinacholetwa tofauti na wanafunzi wengine,” anasema Bi. Teckla Milanzi. 

Kwa upande wake, Mwalimu Christina Komba wa darasa la awali Shule ya Msingi Tunduru Mchanganyiko anasema madarasa ya elimu ya awali Wilayani Tunduru yanakabiliwa na changamoto nyingi. Anabainisha kuwa madarasa mengi likiwemo lake hawana vitabu wala miongozo ya namna ya ufundishaji kabisa zaidi ya kila mwalimu anayefundisha kubuni nini afundishe kila uchao. “…Kwanza licha ya kutokuwa na vifaa vingine hatuna chumba maalumu cha wanafunzi hawa (darasa) kwa sasa tunatumia jengo la darasa ambalo bado linaendelea na ujenzi na hata hivyo jengo hili halijengwi kwa ajili ya wanafunzi wa awali,” anasema mwalimu Christina Komba.

Wanafunzi wa darasa la awali katika Shule ya Msingi Nakayaya, wakiwa katika darasa lao.

Wanafunzi wa darasa la awali katika Shule ya Msingi Nakayaya, wakiwa katika darasa lao.[/caption] “Madarasa ya elimu ya awali hayana vitabu, hayana miongozo…huwa tunaanzima au ukipata hela yako wewe binafsi unaenda kununua kitabu kimoja au viwili ili uweze kuwasaidia watoto.
Na baadhi ya masomo hayana vitabu kabisa hata ukienda madukani katika Wilaya yetu (Wilaya ya Tunduru) vitabu kama Haiba na Michezo, pamoja na Sanaa hazipo kabisa madukani. Anasema uongozi wa juu wilayani unalitambua hilo.

Batadhari Mkwela ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Nanjoka anasema usajili wa wanafunzi wa awali kila mwaka huongezeka japokuwa bajeti ya kuendesha elimu hiyo ni changamoto. “…Darasa la awali linahitaji vitendea kazi lakini havipo, hatuna vifaa kama vitabu vya kutosha, vyenzo za kufundishia, hakuna bajeti hata ya vifaa hivi toka Serikalini, hatuna madawati maalum kwa ajili ya wanafunzi wa awali,” anasema Mkuu huyo wa Shule ya Nanjoka. Hadija Makamla ni mwalimu wa darasa la awali Shule ya Msingi Majengo. Mwalimu huyu ambaye amehitimu kozi ya kufundisha darasa hilo, anasema anavyo baadhi tu ya vitabu vinavyoitajika katika darasa hilo. Anabainisha kuwa darasa hilo lina jumla ya wanafunzi 48 lakini hutumia darasa la wanafunzi wa kawaida maana hawana darasa lililojengwa maalum kwa wanafunzi wa awali. “…Ninazo nakala chache kwa ajili ya mwalimu tu ila wanafunzi hawana hata kimoja…lakini kuna masomo mengine sina vitabu kabisa kama vile Sanaa na Haiba ya Michezo sina kabisa hata mimi,” anasema mwalimu Makamla. “…Unajua watoto kwa kiasi kikubwa wanajifunza kwa vitendo, picha na uhalisia, sasa huenda tunavyowapa ni vikubwa zaidi au vidogo sana kwa sababu ya kubuni mada kwa baadhi ya masomo. Dorothea George ni mwalimu wa darasa la awali shule ya Msingi Nanjoka Wilayani Tunduru. Yeye anasema japokuwa hakuwahi kufanya kozi ya ualimu wa awali kwa sasa amekabidhiwa darasa hilo kulifundisha katika shule yake. 

Anasema darasa hilo kwa sasa lina wanafunzi 98 ambao wanasomea darasa moja chini ya mwalimu mmoja. Anasema licha ya darasa hilo kuwa na madawati kadhaa lakini si maalum kwa ajili ya wanafunzi wa awali bali ni ya wanafunzi wa kubwa, hata hivyo bado kuna watoto wanalazimika kukaa chini kwa kile kukosa madawati ya kutosha katika shule hiyo. 

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Majengo, Madina Mkali anasema uendeshaji wa darasa la awali shuleni hapo ni wa kusuasua kutokana na changamoto anuai zinazowakabili. Hakuna bajeti inayoingia kuisaidia elimu hiyo, ispokuwa mwaka huu waliletewa madawati kumi kwa ajili ya elimu ya awali. 

Kaimu Ofisa Elimu Wilaya ya Tunduru, Abdul Kazembe akizungumza na mwandishi wa makala haya (hayupo pichani) ofisini kwake hivi karibuni.

Kaimu Ofisa Elimu Wilaya ya Tunduru, Abdul Kazembe akizungumza na mwandishi wa makala haya (hayupo pichani) ofisini kwake hivi karibuni. “…Uendeshaji elimu ya awali hapa ni wa wastani kwa kweli kutokana na changamoto zinazotukabili, kwanza vifaa vya kuwafundishia watoto hawa ni tatizo na wazazi kwa eneo hili wamekuwa hawana mwamko wa elimu hii kabisa. 

Kwanza hawachangii michango ya chakula kama inavyotakiwa ili mtoto apate chochote awapo shuleni,” anasema mwalimu Mkali. Anabainisha kuwa watoto pia wanatakiwa kupata uji wawapo shuleni lakini uchangiaji kwa wazazi nao umekuwa tatizo kubwa. “…Wapo wanaochangia wengine wanagoma tunasukumana hivyo hivyo na mambo yanasonga mbele…lakini kutokana na uchangiaji duni kuna baadhi ya siku wanapata uji na sikunyingine hawanywi kutokana na ugumu wa michango,” anasema mwalimu George.
Mwenyekiti wa Kamati ya Shule ya Msingi Tunduru Mchanganyiko, Adam Hausi katika mazungumzo na mwandishi wa makala haya anasema uendeshaji wa elimu ya awali katika shule hiyo ni juhudi binafsi za mwalimu wa darasa hilo. Anasema darasa hilo halina bajeti yoyote kutoka serikalini hivyo hakuna vitabu na vitendea kazi vingine vinavyohitajika. “…Vitendea kazi ndio tatizo kabisa, ila mwalimu anafundisha kwa jitihada zake na darasa linaendelea. Alafu lina idadi kubwa sana ya wanafunzi (84) na anafundisha peke yake…,” anasema Hausi. 

Anasema uboreshaji elimu ya msingi ni suala la ushirikiano kati ya Serikali na jamii yenyewe lakini wakati mwingine Serikali inakwamisha juhudi hizo kwa kushindwa kuwajibika ipasavyo baadhi ya maeneo. “…Mfano sisi tulijenga madarasa mawili kwa nguvu za wananchi hadi yamekamilika ilipofika suala kuezekwa tokaomba msaada wa Serikali pamoja na kumaliziwa ili yaanze kutumika ilikuwa kazi kweli tulizunguzwa sana hadi tukaanza kuyatumia hivyo hivyo,” alisema. 

Bi. Thabita Farara ni Mkazi wa Kata ya Mringoti Mashariki anasema bado mwamko wa elimu ya awali kwa wazazi ni mdogo, maana wazazi wengi wamekuwa wakijiandaa na darasa la kwanza tu kumuandikisha mtoto. Kwa upande wake Asha Komba Mkazi wa Tunduru Stendi anasema yeye anaitambua elimu ya awali na kuikubali lakini ni ile inayotolewa na shule binafsi kama za taasisi. 

Lakini ile inayotolewa kwenye shule za Serikali ni tatizo kubwa maana hazizingatii ubora wa elimu zaidi ya kuwalundika watoto tu darasani. “…Mimi naitambua elimu ya awali na watoto wangu wote wamepitia lakini huwa tunawapeleka kwenye chekechea za taasisi mbalimbali kama zinazomilikiwa na makanisa majeshi na zinginezo maana huku ndiyo kidogo mtoto anaandaliwa…kule Serikalini kwanza unakuta darasani wapo kibao alafu muda wote wanacheza tu si kujifunza,” anasema Bi. Komba.

Abdul Kazembe ni Kaimu Ofisa Elimu Wilaya ya Tunduru, anasema kwa sasa kila shule ya msingi sera inaelekeza lazima iwe na darasa la awali. Anasema hata katika usajili wa wanafunzi wa darasa la kwanza kwa sasa watoto wa mwanzo kusajiliwa ni wale waliopata elimu ya awali katika shule husika. “…Kwa hiyo kuna umuhimu wa kila shule kuwa na darasa la awali…changamoto sasa inakuja kwenye vitendea kazi, kwa mwaka 2013 na kurudi nyuma uwepo wa ‘capitation’ ulikuwa pia unaelekeza watoto wa awali wapo mule na hata tunapotoa takwimu za awali tulianza na ‘pre-primary’ (wanafunzi wa awali) hivyo wenyewe wapo, tatizo hapa ni ujaji wa pesa yenyewe ya ‘capitation’ haitimii kama inavyo elekeza, yaani ile wastani ya kwamba kila mtoto apate shilingi 10,000 kwa mwaka hautimii,” anasema. 

Anatolea mfano mwaka 2013/14 kiwango cha fedha ambacho kilitakiwa kuja katika halmashauri ya wilaya hiyo ni zaidi ya milioni 366.7. Kiwango hiki ni kile kilichoidhinishwa katika bajeti tu lakini ukirudi kwenye mahitaji halisi ni zaidi ya kiasi kilichoidhinishwa. Anasema kilichokuja ni zaidi ya milioni 196.5 fedha ambayo ni karibia nusu ya kiasi kilichopitishwa kwenye bajeti. Anabainisha hilo ndilo tatizo kubwa kwani hata fedha ambazo zimepitishwa haziji kama ilivyopitishwa kwenye bajeti.

“…Kwa hiyo unaweza kuona kwamba ni ngumu kuigawa fedha hii katika matumizi maana kwanza haitoshi na pili hata kilichotegemewa kuja ni pungufu zaidi tena sana, sasa sijui unaweza kugawa kila shule ipate shilingi ngapi…kwani haitoshelezi,” anasema. 

Anasema kwa upande mwingine miundombinu ya madarasa ni changamoto kubwa. Kwa mwaka 2013 idadi ya mahitaji ya madarasa kwa wilaya nzima ilikuwa ni 1,715 lakini ukiangalia vyumba vya madarasa vilivyopo ni kama 900 na kitu na mengine ni ya muda mrefu sana kiasi ambacho yanaelekea kuchakaa jambo ambalo pia yanapungua. Aidha anaeleza kuwa ukienda kwenye bajeti ya ujenzi wa madarasa mapya milioni 171 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa na miundombinu mbalimbali kiasi hiki cha fedha waweza kuta kinauwezo wa kujenga madarasa kama nane tu. 

Kiasi hicho cha fedha ni pamoja na ujenzi wa nyumba tano za walimu. Na kiasi hicho cha fedha za ujenzi ni pamoja na kumalizia miradi viporo za nyumba za walimu na vyumba vya madarasa. Anasema upungufu wa vyumba vya madarasa eneo hilo ni karibia madarasa 800. “Sasa kwa ujumla unaweza kuona kuwa miundombinu pale shuleni haitoshelezi, ni jambo la kawaida kuona walimu wakiacha ofisi itumike kama darasa au darasa litumike kama ofisi. 

Huku kwa awali ni changamoto zaidi maana licha ya upungufu wa vyumba hata wazazi hasa vijijini wanashindwa kuchangia chakula (uji) kwa watoto wao unaweza kukuta wameandikishwa wengi Januari lakini kila muda unavyozidi kwenda watoto wanapungua na unaweza kukuta hadi mwezi Juni darasa linapotea kabisa kwa utoro,” anasema. Kazembe anabainisha kuwa kuna jumla ya shule za msingi 144 katika wilaya hiyo, huku shule zilizo na vyumba maalumu vya madarasa ya awali zikiwa 16 tu. 

Anasema shule nyingine zote hazina vyumba vya madarasa ya awali na matokeo yake ama wanatumia madarasa ya msingi kwa kupishana. Anaongeza kuwa uhamasishaji wa ujenzi wa madarasa ya awali na umuhimu wa elimu hiyo unatolewa kwa walimu, wazazi na kamati za shule kupitia vikao mbalimbali ambapo mara nyingi uongozi uhimiza wazazi kuchangia zaidi nguvu zao katika kukamilisha ujenzi wa madarasa ya awali, utengenezaji wa madawati na upatikanaji wa chakula cha mchana na uji shuleni. “…lakini tunaangalia sana chakula maana watoto hata kwenye mti wanaweza kukaa wakasoma endapo wanamadawati pale au wamekaa chini kwenye kivuli, japokuwa si mazingira mazuri sana shuleni…lakini wakiwa na chakula hata utoro unapungua,” anasema. Anasema kwa mwaka 2013 serikali ilikumbuka kuleta fedha kwa ajili ya ununuzi madawati ya wanafunzi wa awali, fedha ambazo tulizigawa na kununua baadhi ya vitabu vya awali na madawati kwenye shule ambazo zinamadarasa hai ya awali. 

Shule zilizonufaika na mgao huo ni shule za mjini Tunduru tu ambazo nyingi ndizo zenye madarasa hai ya awali. Anasema ili kukabiliana na hali ya upungufu wa walimu wa awali; imepitishwa walimu wa gredi ‘A’ kufundisha madarasa hayo kwa kuwa wao mafunzo yao katika kozi hujumuisha ufundishaji darasa la awali, tangu walioitimu mwaka 2013. 

“…sasa wakati mwingine unaweza kukuta mwalimu ni gradi A na kimsingi yeye anao uwezo wa kufundisha darasa la awali, lakini wengine hawakubali hadi aone ana cheti kabisa maalumu cha kufundisha darasa la awali…ukimuuliza huyu atakwambia yeye hana taaluma ya kufundisha awali jambo ambalo si sawa,” anasema Ofisa Elimu huyo wa Msingi. “..Kwa suala la vitabu kweli hii ni changamoto, hapo nyuma tulikuwa tunanunua vitabu wenyewe wakini kwa sasa TAMISEMI wenyewe moja kwa moja wananunua na kuvileta.
Sasa huku kwetu ni nadra sana kuona wazabuni wetu wanaleta vitabu vya awali kwa sababu soko lake ni dogo sana kutokana na idadi ndogo ya uwepo wa elimu hii ya awali eneo husika,” anasema. Hata hivyo umeona unafuu maeneo ya mjini mzazi anatambua umuhimu wa elimu hivyo anaweza kuchonga dawati kwa ajili ya mtoto wake lakini kwa vijijini hali ni mbaya zaidi. Mzazi ukimwambia achangie dawati anakushangaa na pia haoni umuhimu huo.

“…Nikwambie unajua Wilaya ya Tunduru mzazi mtoto wake akifeli anafurahi sana…tena baadhi wanaona kama ni sherehe, kwanza wakifanya mtihani tu wa la saba barabarani akina mama wanashangilia wanaona wametua mzigo, unaweza kujiuliza wazazi wanaoshangilia inamaana walikuwa wakiona ni adhabu watoto wao kuwa shule? 

Lakini pia mtoto akisha faulu kwenda shule hapelekwi hadi DC aunde kamati, atembee na hakimu na polisi kukamata wazazi wanaogoma kusomesha watoto watishiwe ndo wanakubali kusomesha…lakini kitendo cha wazazi kukamatwa kushikiliwa kwa kushindwa kuwapeleka watoto shule wamegeuka na kuwarubuni watoto wao wasifaulu,” anasema. Anabainisha kuwa ni kweli Serikali ina jukumu la elimu, lakini mzazi kwa upande wake anajukumu zaidi, kuangalia mtoto wake anapata elimu gani na ya kiwango gani na kama mzazi hayupo tayari basi haiwezekani na wakati mwingine inakuwa ngumu. Kimsingi jitihada za kuhakikisha upatikanaji wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia watoto wa awali zipo, lakini upatikanaji wa fedha ndio. Salum Mtutula ni Mbunge wa Tunduru Kusini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mbunge huyu katika mahojiano anakiri kuwa elimu ya awali ni muhimu na msingi mzuri wa mtoto kielimu. 

Anasema mtoto anapopata elimu nzuri ya awali huwa na msingi mzuri kielimu katika masomo yake ya mbele. “…Ili mtoto apate elimu bora ni lazima apate elimu ya awali inayostahiki…hakiwa na msingi mbaya wa elimu ya awali kuna uwezekano mkubwa way eye kufanya vibaya pia,” anasema Mtutula. Hata hivyo anaishauri Serikali kuingiza suala hili katika sheria na kanuni zake kuwa kila shule ya msingi inapoanzishwa ianze na darasa la awali kwanza ndipo madarasa mengine yafuate.
“…Mimi nitafurahi kama suala hili tutaliweka kwenye sheria au kanuni zetu kuwa kila shule ya msingi inapoanzishwa basi lazima ianze na darasa la awali ndipo madarasa mengine yafuate iwe shule za Serikali au binafsi,” anasema Mbunge Mtutula.
*Imeandaliwa na: www.thehabari.com
0 comments

NANI MTANI JEMBE 2 YAZINDULIWA RASMI JIJINI DAR




TAARIFA KUTOKA KILIMANJARO PREMIER LAGER.


Awamu ya pili ya kampeni ya Nani Mtani Jembe imezinduliwa leo kwa waandishi wa habari na itazinduliwa kwa wadau wa Simba na Yanga kesho tarehe 4 Oktoba 2014 katika viwanja vya Leaders Club jijini Dar es salaam na itajulikana kama Nani Mtani Jembe 2.

Akiongea katika mkutano na waandishi leo, George Kavishe, Meneja wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager, alisema, “Dhumuni la kampeni yetu ya pili ya Nani Mtani Jembe ni kuisogeza Kilimanjaro Premium Lager karibu na wateja wake na wananchi na kuhamasisha ushindani kati ya mashabiki wa Simba na Yanga kwa kushindanisha mamilioni ya mashabiki wa  klabu hizi nchi nzima kwa kipindi cha wiki kumi kuanzia Oktoba hadi Disemba.


Alisema, “kampeni hii itazinduliwa  na mlolongo wa matukio ambapo tukio la pili litakuwa ni uzinduzi rasmi kwa wadau jijini Dar es salaam ambapo Nani Mtani Jembe 2 itatambulishwa kwa wadau na mashabiki wa Simba na Yanga. Uzinduzi huu utafuatiwa na hafla fupi za kuzindua kampeni hii katika viwanda vyote vya  bia ya TBL nchini katika mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza, Mbeya, Moshi na Arusha lengo likiwa ni kuongeza uelewa wa wafanyakazi wa TBL kuhusu Nani Mtani Jembe 2 ili waweze kuwa mabalozi wazuri. Pamoja na kampeni hiyo, tutakuwa na uzinduzi wa kipindi cha  televisheni  kiitwacho “Kili Chat ”ambacho kitarushwa hewani kwa muda wa wiki kumi kikijumuisha watu maarufu nchini ili kuitangaza Nani Mtani Jembe 2 zaidi na kuhakikisha  uwanja wa Taifa unajaa  siku ya mechi. ”

Akieleza utaratibu wa kampeni hiyo, Kavishe alisema kampeni hiyo itahusisha mashabiki wa Simba na Yanga ambapo jumla ya shilingi milioni 100 zitatolewa na kugawanywa kama ifuatavyo;
a) Shilingi milioni 20 itakuwa zawadi ya fedha kwa ajili ya mechi ya Nani Mtani Jembe 2, ambapo timu itakayoshinda itaondoka na kitita cha shillingi milioni 15 na shillingi milioni 5 zitatolewa kwa timu itakayofungwa mechi.
b) Kampeni hiyo itaendeshwa kwa njia ya sms ambapo mashabiki watapiga kura kwa njia ya sms na shilingi milioni 80 zitagawanywa kati ya timu hizo mbili. Kwa hiyo kila timu itaanza na shillingi milioni 40 kwenye benki maalum  mtandaoni kwa ajili ya shindano.

Kavishe alisema kwa kila bia ya Kilimanjaro Premium Lager yenye ujazo wa  500ml mnunuzi atakuta namba maalum chini ya kizibo cha bia hiyo, namba hizo atazitumia kutuma  sms kwenda kwenye namba maalum 15415.

Alendelea kusema kuwa ni lazima mnunuzi aandike kwenye sms kuwa yeye ni shabiki wa timu ipi kwa kuandika neno SIMBA au YANGA ikifuatiwa na namba zilizopo chini ya kizibo, na anapotuma sms ataweza kupunguza shilling 10,000 kwenye benki ya timu pinzani na kuweka kiasi hicho kwenye timu yake.

Mwisho wa kampeni hiyo kila klabu itakuwa imeongeza au kupoteza kiasi cha fedha kwa timu pinzani, kulingana na jinsi mashabiki walivyopiga kura.

 Alisema, “kwa mfano, kama mashabiki wa Simba watapiga kura zaidi ya mashabiki wa Yanga itamaanisha kwamba Simba itashinda na kupata fedha zaidi kutoka kwenye kiasi cha milioni 80, hivyo hivyo kwa mashabiki wa Yanga kama watapiga kura zaidi kuliko mashabiki wa Simba itamaanisha Yanga itapata fedha zaidi ”

Kampeni hii inatarajiwa kuongeza chachu ya ushindani kati ya mashabiki wa Simba na Yanga kwa kuwapa fursa mashabiki kuonyesha mapenzi yao kwa timu zao. Kampeni hii itafungua mlango kwa  Kili kuendelea kuwa karibu zaidi na mashabiki na vilevile itazisaidia klabu hizi kuongeza idadi ya mashabiki na kuimarisha ushabiki na mapenzi kwa timu zao.

Mbali na kampeni ya sms, Nani Mtani Jembe 2 itahusisha mashabiki wa klabu za Simba na Yanga katika  promosheni mbalimbali na kuwawezesha kushinda zawadi mbalimbali kila wiki pamoja na fedha taslimu. Kampeni hii itafika kileleni mwezi Disemba ambapo itahitimishwa na mechi ya Nani Mtani Jembe 2 kati ya Simba na Yanga katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam mbele ya mashabiki wa timu hizo. IIi timu ziweze kujiandaa vizuri, kila timu itapata kiasi cha shilingi milioni 30 kwa ajili ya maadalizi ya mechi hiyo zikiwa ni ongezeko kutoka shilingi milioni 20 za mwaja jana.
0 comments

PPF KUWAFIKISHA WAAJIRI MAHAKAMANI

PPF KUWAFIKISHA WAAJIRI MAHAKAMANI

NA MWANDISHI WETU,TANGA.
MFUKO wa pensheni wa PPF umesema utawafikisha mahakamani waajiri ambao hawapeleki michango kwa wakati kwani hali hiyo inasababisha usumbufu kwa wateja wao.
Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni na Meneja wa Kanda ya Kinondoni, Tanga na Pwani, Zahara Kayugwa wakati wa semina ya waajiri wa sekta mbalimbali jijini hapa.
Alisema hatua hiyo inaweza kusaidia waajiri kufikisha michango ya wafanyakazi wao kwa wakati.
“Kwa kweli inatubidi tuchukue hatua, kwa sababu unakuta mfanyakazi anakuja kudai mafao halafu mwajiri amechangia asilimia tano tu, sasa wateja wanatuona kama sisi ni wababaishaji… hatutawavumilia tena," alisema Kayugwa.
Aidha, akifungua semina hiyo Katibu Tawala Mkoa wa Tanga, Salim Chima, alisema Serikali inatambua na kuthamini mchango wa sekta ya hifadhi ya jamii nchini, hasa katika suala zima la kukuza na kuimarisha uchumi.
0 comments

KINANA AWASILI TANGA MJINI NA KUPOKEWA KWA SHANGWE.

KINANA AWASILI TANGA MJINI NA KUPOKEWA KWA SHANGWE.

 
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akivuka na kivuko cha MV.Pangani kuelekea Wilaya ya Tanga mjini ambapo anatazamiwa kukagua miradi mbali mbali na kushiriki ujenzi wa maendeleo,wengine pichani ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (kushoto) na Mwenyekiti wa CCM Pangani Ndugu Hamis Mnegero.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi wa Pangani baada ya kuvuka na MV.Pangani

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi waliojitokeza kumuaga wakati akielekea Tanga mjni.
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa kata ya Kigombe ,Pangani ambapo  aliwaeleza lazima kuwa makini katika kuchagua viongozi wa kijiji kwani wengi wamekuwa wakiuza ardhi ya wananchi kiholela na kusababisha matatizo makubwa ya ardhi.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mbunge wa Tanga mjini Mh.Omari Nundu wakati wa mapokezi katika kata ya Marungu wilaya ya Tanga mjini.
 Wananchi wa kata ya Marungu wakifurahia ujio wa Katibu Mkuu wa CCM kwenye kata yao
 Wasanii wa Tanga All Star wakionyesha ujuzi wa kuimba na kucheza wakati wa mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimia wakazi wa kata ya Marungu
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokea kadi za wanachama wa CUF na Chadema wa kata ya Marungu walioamua kurudi CCM,zaidi ya wanachama 60 wa kata ya Marungu kutoka upinzani wamejiunga CCM .
  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha kadi za wanachama wa CUF na Chadema wa kata ya Marungu walioamua kurudi CCM,zaidi ya wanachama 60
 Bibi Saumu Ngoma mama mzazi wa Diwani wa kata ya Marungu Ndugu Bakari Mambeya akirudisha kadi ya CUF kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  na kujiunga na  CCM.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kuezeka ofisi ya CCM kata ya Marungu.
 Wazee wa kijiji cha Machui kata ya Tangasisi wakiwa kwenye mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambapo alishiriki kutoa kadi za mfuko wa afya ya jamii na kushiriki ujenzi wa nyumba ya mganga.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana  akiwasalimu wakazi wa kijiji cha Machui kata ya Tangasisi wilaya ya Tangamjini.
  
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa nyumba ya mganga wa kijiji cha Machui katika kata ya Tangasisi

 
 Katibu Mkuu wa CCM akisalimiana na Wazee waasisi wa CCM Tanga mjini kwenye mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Tanga mjini.

 
Mzee Athumani Makalo (wa kwanza kulia) akiwa na wazee waasisi ndani ya ukumbi wa mkutano Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Tanga mjini.
 
0 comments

KAMPENI YA HAKI YA UCHUMI KATIKA MASWALA YA KILIMO YAENDESHA MDAHALO

KAMPENI YA HAKI YA UCHUMI KATIKA MASWALA YA KILIMO YAENDESHA MDAHALO

Meneja wa Kampeni haki ya Uchumi kutoka Oxfam Eluka Kibona akifungua Mdahalo huo na mafunzo juu ya Kujenga hoja ya upatikanaji wa Chakula na haki ya chakula, Kufuatilia upatikanaji wa haki kwenye Rasilimali za Ardhi na matumizi yake,na kuhamasisha uwekezaji kwa wakilima wadogo wadogo Hususani wanawake kwenye Muktadha wa mabadiliko ya Tabia nchi, katika kampeni ya GROW   
Mmoja wa washiriki wa Semina hiyo akielezea matarajio yake akiwa kama Mama shujaa wa Chakula na Mkulima mwanamke Jinsi ambavyo wameweza kusaidiwa na Oxfam kufikia malengo yao katika kilimo na kuwa wakulima Bora wenye mfano wa Kuigwa

Mshindi wa Maisha Plus 2012 Bernick Kimiro akitoa mchango wake Jinsi kilimo kinavyo weza kumsaidia mwanamke na kufikia Malengo yake.(P.T)

Mshindi wa Mama shujaa wa Chakula 2014 , akiendelea kuchukua Maoni mbalimbali , Mchango na mawazo ya watu mbalimbali katika Mdahalo huo.

Oscar Munga kutoka Forum CC akitoa ufafanuzi wa kina juu ya mahusiano ya kilimo na mabadiliko ya Tabianchi, Pia alizungumzia ni namna gani watu wanaweza kujikomboka katika kilimo na kuendana na Mabadiliko ya Tabianchi.

Balozi wa Oxfam kupitia kampeni ya GROW Khadija Mwanamboka akielezea umuhimu wa kilimo bora na uwezeshaji wa wanawake katika kupata haki za Ardhi lakini pia jinsi gani Mwanamke anaweza kujikomboa katika kilimo na kuwa wanawake wanahaki sawa katika swala zima la kumiliki Ardhi.

Wa kwanza kulia ni mmoja wa aliyekuwa mshiriki wa Mama Shujaa wa Chakula 2014 kutoka Zanzibar akitoa Mchango wake kuhusu Umiliki wa Ardhi na kuelezea jinsi gani wanawake wasivyo na haki ya Ardhi hiyo, na kuomba kwamba nao ni binadamu na wanahaki sawa ya kumiliki ardhi hiyo


Wakili Joseph Chiobola ambaye ni Afisa Programu kutoka Haki Ardhi akitoa ufafanuzi wa kina juu ya haki za watu kumiliki Ardhi, pia alieleza kwa kina sababu za watu mbalimbali kugombania Ardhi na kueleza namna gani Migogoro ya Ardhi inatokea na Njia za kuimaliza Migogoro hiyo.


Mkamiti Mgawe kutoka Oxfam Akichangia Jambo katika Mdahalo huo 



Afisa Ushawishi wa Ardhi kutoka Oxfam Naomi Shadrack akiendelea kutoa muongozo katika mdahalo huo.



Mchoraji Maarufu wa Katuni Muhidini Msamba akitoa mchango wake juu ya mada ambayo ilikuwa inahusu mazao kuto kuwa na thamani kuwa ndio moja ya chanzo cha wakulima waliowengi kutoka Tanzania kukosa  Masoko katika mazao yao, aliongeza ushauri kuwa kunahitajika nguvu ya ziada ili kujikwamua katika swala hilo kwa ujumla 



Mama Shujaa wa Chakula 2012 akitoa ushuhuda wake jinsi Kampeni ya Grow inayoendeshwa na Oxfam Jinsi walivyo weza kumpa Shamba ambalo mpaka sasa Linamsaidia yeye pia watu wengine kupitia elimu anayoitoa ya Shamba Darasa kwa wakazi wa eneo analoishi huko Morogoro. na kusisitiza kuwa na matumizi Bora ya Ardhi.


 
Mmoja wa Washiriki Akichangia Mada juu ya rushwa kuwa ni kikwazo kikubwa sana kwa wakulima na kuwa kuna Baadhi yao wanamazao mazuri lakini kutokana na kuwa mkulima mdogo anashindwa kuuza mazao yake na badala yake anayeuza mazao hayo ni Mkulima mkubwa ambaye huweza kutoa hongo na Mazao yake kununuliwa kirahisi 



Mshindi wa Shindano la Maisha Plus 2014 Boniface akitoa maelezo na kuchangia katika Mdahalo huo 



Tajiel Urioh kutoka Forum CC akihitimisha Mdahalo huo





Washiriki wakiendelea kufuatilia kwa makini Mdahalo huo 



 Kila mmoja akiwa makini kuhakikisha anapata Somo na kulielewa ili apate kwenda wafundisha na wengine.


 Washiriki wakiwa katika Mdahalo huo
0 comments
 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger