Featured Post Today
print this page
Latest Post

Matumaini ya amani Ukraine kwa mkutano wa Minsk

Matumaini ya amani Ukraine kwa mkutano wa Minsk


 Mapigano yamepamba moto mashariki mwa Ukraine, kuelekea mkutano wa Belarus, unaowaleta pamoja viongozi wa Ufaransa, Ujerumani, Urusi na Ukraine. Rais Barack Obama alizungumza na Vladimir Putin kuelekea mkutano huo. 


Kansela Angela Merkel, marais Francois Hollande, Vladimir Putin na Petro Poroshenko wanatarajiwa mjini Minsk baadae siku ya Jumatano, kwa mazunugumzo muhimu juu ya mgogoro nchini Ukraine. Ikiwa mazungumzo hayo yatashindwa kuleta muafaka, vikwazo zaidi vya Umoja wa Ulaya dhidi ya Urusi vinatarajiwa. Marekani pia inatafakari kulipatia silaha jeshi la Ukraine ikiwa hakutakuwa na hatua zozote katika mazungumzo.
Kabla ya mkutano huo ikulu za White House na Kremlin ziliripoti juu ya mazungumzo kwa njia ya simu kati ya marais Obama na Putin. Kwa mujibu wa Whote House, Obama alisisitiza umuhimu kwa rais Putin kutumia fursa ya mazungumzo ya Minsk kufikia suluhu ya amani. Kremlin ilisema viongozi hao wawili wlikubaliana juu ya haja ya kuwa na suluhu ya kisiasa kwa mgogoro wa ndani wa Ukraine.
Pushilin (kulia) alisema aliwasilisha mapendekezo kwa wawakilishi wa serikali ya Kiev. Pushilin (kulia) alisema aliwasilisha mapendekezo kwa wawakilishi wa serikali ya Kiev.
Ni mapema mno kwa usitishaji mapigano
Wajumbe wa upatanishi kutoka Ukraine, waasi wanaowania kujitenga, Urusi na shirika la usalama na ushirikiano barani Ulaya OSCE, waliweka msingi wa mazungumzo ya leo katika majadiliano ya karibu masaa mawili mjini Minsk jana. Licha ya taarifa za usitishaji mapiagano, ilibainika baadae ni hatua kidogo sana zilizopigwa.
"Ni mapema mno kuzungumzia usitishaji mapigano,"alisema Denis Pushilin, mjumbe wa ujumbe wa wanaotaka kujitenga. Aliongeza kuwa waasi wamewasilisha pendekezo juu ya namna ya kusonga mbele na kwamba walikuwa wanasubiri majibu, bila kubainisha undani wa mapendekezo hayo.
Na taarifa zinazotoka Ukraine zinasema mashambulizi ya waasi yamewauwa wanajeshi 19 wa Ukraine na kuwajeruhi wengine 78 katika mji wa Dibalseve. Mapigano mengine makali jana Jumanne yaliripotiwa kuuwa zaidi ya raia 10 na wanajeshi katika mji wa Kramatasorsk. Wakati mapigano yakiendelea, waziri wa mambo ya nje ya Ujerumani Frank-Walter Steinmeier aliwatolewa mwito wanaohusika kujizuwia wakati wanadiplomasia wakifanya kazi.
"Ukweli kwamba mkutano huo unafanyika siyo uthibitisho wa mafanikio. Ndiyo maana nazisihi, na nazitaraji Moscow na Kiev kuyachukulia kwa uzito, na kutumia nafasi hii, kwa kuzingatia kitisho kilichoko mbele yetu cha mgogoro wa kijeshi," alisema waziri Steinmeier.
Kansela Angela Merkel, rais Francois Hollande walipozungumza na rais Vladimir Putin mjini Moscow. Kansela Angela Merkel, rais Francois Hollande walipozungumza na rais Vladimir Putin mjini Moscow.
Mpasuko barani Ulaya
Mgogoro huo umesababisha mpasuko miongoni mwa mataifa ya Ulaya, na kuitikisa dhana ya mshikamano usiyoyumbishwa wa mataifa ya Atlantic. Ufaransa na Ujerumani zimeweka chini matarajio ya juhudi zao mpya za amani. Rais wa Ufaransa Francois Hollande alisema viongozi hao walikuwa wanaongoza mazungumzo hayo kwa dhamira ya kufanikiwa, lakini bila ya kuwa na uhakika wa iwapo wataweza kutimiza lengo hilo.
Vita hivyo na miaka kadhaa ya rushwa iliyokithiri vimeipeleka nchi hiyo kwenye kingo za kufilisika, ambapo sarafu yake iliporomoka wiki iliyopita. Ukraine inajadiliana mkopo wa uokozi na shirika la fedha la kimataifa IMF, na duru zilisema mkopo huo huenda ukapanuliwa kwa kiasi kikubwa na kuipatia nchi hiyo kiasi cha dola bilioni 40 za msaada.
Mwandishi: Iddi Ssessanga/dpae, rtre,DW
Mhariri: Elizabeth Shoo
0 comments

RAIS KIKWETE AHUDHURIA MAZISHI YA MAMA MZAZI WA JAJI AUGUSTINO RAMADHANI, DAR ES SALAAM

RAIS KIKWETE AHUDHURIA MAZISHI YA MAMA MZAZI WA JAJI AUGUSTINO RAMADHANI, DAR ES SALAAM

Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakitoa heshima za
mwisho kwa mwili wa Marehemu Bibi Bridget Ramadhani, Mama Mzazi wa
Jaji Augustino Ramadhani,  wakati wa mazishi Ijumaa February 6, 2015
huko Kimara King’ongo jijini Dar es salaam. jky2 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakijumuika na
waomboilezaji wengine  katika mazishi ya Marehemu Bibi Bridget
Ramadhani, mama Mzazi wa Jaji Augustino Ramadhani,  wakati wa mazishi
Ijumaa February 6, 2015 huko Kimara King’ongo jijini Dar es salaam.
jky3 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiweka udongo
kwenye kaburi la  Marehemu Bibi Bridget Ramadhani, mama Mzazi wa Jaji
Augustino Ramadhani,  wakati wa mazishi Ijumaa February 6, 2015 huko
Kimara King’ongo jijini Dar es salaam. jky4 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiweka shada
kwenye kaburi la  Marehemu Bibi Bridget Ramadhani, mama Mzazi wa Jaji
Augustino Ramadhani,  wakati wa mazishi Ijumaa February 6, 2015 huko
Kimara King’ongo jijini Dar es salaam.

0 comments

Rais Kikwete aongoza mazishi ya Bi.Tajiri Tanga

Rais Kikwete aongoza mazishi ya Bi.Tajiri Tanga

jk1.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka udongo katika kaburi la marehemu Bi.Tajiri Abdallah Kitenge wakati wa mazishi yaliyofanyika katika makaburi ya Chumbageni mjini Tanga.Marehemu Bi.Tajiri ni mama wa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama Bwana Rashid Othman. jk2 
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Bwana Rashid Othman wakati wa mazishi ya Mama yake Bi.Tajiri Abdallah Kitenge yaliyofanyika katika makaburi ya Chumbageni mjini Tanga jana(picha na Freddy Maro)

0 comments

IVORY COAST BINGWA AFCON 2015

IVORY COAST BINGWA AFCON 2015

Mabingwa wapya wa Kombe la Mataifa Afrika 2015, Ivory Coast wakipozi na kombe
Straika wa Manchester City, Wilfried Bony akiwa amembeba shujaa wa Ivory Coast Boubacar Barry (katikati), aliyefunga penalti ya mwisho.
Nahodha wa Ivory Coast, Yaya Toure akifurahia ubingwa.
0 comments

MAJIJI KUMI SALAMA YA KUISHI DUNIANI


Tafiti zimesema haya ndio MAJIJI salama zaidi duniani kwa kuishi… (PICHAZ)

0_CATERS_Hong_Kong_Extreme_Selfies_08-800x498
Kila mtu anapenda kuwa mahali penye ulinzi na usalama wa uhakika, kama ndio hivyo basi moja ya sifa ambayo tunatakiwa kuiangalia sana mahali tunapoishi ni ishu ya usalama wa uhakika.
Katika moja ya vitu ambavyo nimeona nikusogezee ujue ni hii ya list ya majiji ambayo ni salama zaidi duniani
Vigezo ambavyo viliangaliwa hapa ni pamoja na ulinzi wa kisasa (vitu kama CCTV camera, scanners), ulinzi na usalama wa afya za watu, ulinzi na usalama wa miundombinu kama majengo, barabara na usalama wa mtu binafsi.
Watafiti wa The Economist Intelligence Unit wametoa idadi ya majiji hayo 50 salama zaidi duniani kwa kuishi, katika hayo kutoka Afrika ni jiji moja tu limeingia kwenye nafasi ya 47, Johhanesburg Afrika Kusini.
Hapa nimekuwekea haya kumi bora mtu wangu.
No. 1: Tokyo, Japan
No. 2: Singapore, Singapore
No. 3: Osaka, Japan
No. 4: Stockholm, Sweden



No. 5: Amsterdam, Netherlands

No. 6: Sydney, Australia
Zurich
No. 7: Zurich, Switzerland
No. 8: Toronto, Canada
No. 9: Melbourne, Australia
No. 10: New York, Marekani
Nitaendelea kukusogezea kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia
0 comments

Yanga yapaa kileleni mwa Ligi Kuu.


Yanga yapaa kileleni mwa Ligi Kuu. 
 
 yangaaa

Ligi kuu ya soka nchini Tanzania bara imeendelea hii leo kwa mchezo mmoja uliopigwa kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam ukiwakutanisha Wenyeji Yanga na Mtibwa Sugar toka Morogoro .
Katika mchezo huo Yanga waliibuka na ushindi wa mabao mawili bila katika mchezo ambao walitawala kuanzia mwanzo hadi mwisho na wangeweza kushinda kwa idadi kubwa ya mabao .
Yanga walifunga mabao yote mawili kupitia kwa Kiungo mshambuliaji  Mrisho Khalfan Ngassa ambaye alifunga mabao mawili baada ya kuingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya mshambuliaji raia wa Liberia Kper Sherman .
Huu unakuwa ushindi wa pili mfululizo kwa Yanga baada ya kushinda mchezo wao dhidi ya Coastal Union kwa bao moja .
Matokeo haya yanawafanya yanga wapande  kwenye kilele cha ligi kuu ya Tanzania bara wakiwa na idadi ya pointi 25 wakiwazidi mabingwa watetezi Azam Fc kwa pointi tatu .
0 comments
 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger