Featured Post Today
print this page
Latest Post

MKUU WA MKOA MOROGORO AONGOZA MAMIA KUMZIKA MKE WA MBUNGE WA JIMBO LA MOROGORO KUSINI.‏

MKUU WA MKOA MOROGORO AONGOZA MAMIA KUMZIKA MKE WA MBUNGE WA JIMBO LA MOROGORO KUSINI.‏

 Mkuu wa mkoa akimpeleka Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mh  Innocent Kalogeris  kupokea mwili wa mpendwa mke wake,kulia ni dada wa mbunge huyo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh Dr Joel Bendera Leo amewaongoza mamia ya wananchi wa mkoa wa Morogoro kumzika Mke wa Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini, Mh lnocenti Kalogeris watu mbali mbali wakiwemo wabunge,wakuu wa mikoa wa staafu na watu mashuhuri wamefurika nyumbani kwa mbunge huyo ambaye pia ni mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Morogoro CCM 


 Marehemu Elizabeth Kapoloma enzi za Uhai wake , Bi,Elizabeth Kapoloma alifariki Alhamisi Kwa Ugonjwa Moyo.
 Mwili wa marehemu ukiwasili nyumbani kwake kwajili ya Heshima za Mwisho na Ibada kabla ya Mazishi leo


                       


  Mkuu wa mkoa wa Morogoro Mh Dk Joel Bendera akimbembeleza Mume wa marehemu Mhe lnocent Kalogeris
0 comments

NOOIJ ATARAJIA MECHI YA WAZI DHIDI YA MSUMBIJI

NOOIJ ATARAJIA MECHI YA WAZI DHIDI YA MSUMBIJI

NA BONIFACE WAMBURA,MAPUTO.
Kocha wa Taifa Stars, Mart Nooij amesema anakiamini kikosi chake ambacho kesho (Agosti 3 mwaka huu) kinacheza mechi ya marudiano ya raundi ya pili ya michuano ya Afrika dhidi ya Msumbiji (Mambas).
Mechi hiyo ndiyo itakayoamua ni timu ipi kati ya Tanzania na Msumbiji itakayoingia hatua ya makundi ya michuano ya Afrika kwa ajili ya kutafuta tiketi za Fainali itakayofanyika mwakani nchini Morocco.
Katika mechi ya kwanza iliyochezwa jijini Dar es Salaam wiki mbili zilizopita timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2. Timu itakayosonga mbele itaingia kwenye kundi lenye timu za Cape Verde, Niger na Zambia.
Akizungumza hapa Maputo, Nooij amesema anaamini kikosi chake kitacheza vizuri zaidi kuliko kilivyofanya jijini Dar es Salaam kwa vile hakitakuwa katika shinikizo la washabiki ambalo mara nyingi hufanya wachezaji wasijiamini.
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imefikia katika hoteli ya Pestana Rovuma ikitokea Johannesburg, Afrika Kusini ambapo ilifanya maandalizi yake mwisho, na itafanya mazoezi leo (Agosti 2 mwaka huu) saa 9 alasiri Uwanja wa Taifa wa Zimpeto ambao ndiyo utakaotumika kwa mechi ya kesho.
Kikosi hicho cha timu ya Taifa leo imeandaliwa chakula cha jioni na Balozi wa Tanzania hapa Msumbiji, Shamim Nyanduga.
Wachezaji Mbwana Samata na Thomas Ulimwengu nao wameungana na timu leo asubuhi hapa Maputo wakitokea Lubumbashi katika klabu yao ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
Mechi itakayochezeshwa na waamuzi kutoka Uganda wakiongozwa na Dennis Batte itaanza saa 9 alasiri kwa saa za hapa ambapo nyumbani Tanzania itakuwa saa 10 jioni.
Wachezaji waliopo katika kiosi cha Taifa Stars hapa Maputo ni Aggrey Morris, Aishi Manula, Amri Kiemba, Deogratias Munishi, Erasto Nyoni, Haruna Chanongo, Himid Mao, John Bocco, Kelvin Yondani, Khamis Mcha, Mbwana Samata, Mwinyi Kazimoto, Mrisho Ngasa, Nadir Haroub, Oscar Joshua, Ramadhan Singano, Said Moradi, Shabani Nditi, Shomari Kapombe, Simon Msuva na Thomas Ulimwengu.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
MAPUTO
0 comments

Mashambulizi ya Israel yawaua watu 100

Mashambulizi ya Israel yawaua watu 100

 
Gaza. 
Maafisa wa matibabu katika eneo la Gaza wanasema kuwa zaidi ya wapalestina 100 wameuawa na makombora ya Israel tangu kukiukwa kwa makubaliano ya kusitisha vita siku ya ijumaa.
Vifo vingi vimetokea katika eneo la Rafah kusini mwa Gaza ambapo wanajeshi wawili wa Israel waliuawa na mwengine wa tatu kudaiwa kutekwanyara baada ya kuvamiwa na wapiganaji wa Hamas.
Kundi la wapiganaji wa kipalestina Hamas limesema kuwa halina habari zozote kuhusu mwanajeshi aliyetoweka Hadar Goldin na kwamba huenda aliuawa katika mapigano.
0 comments

ANCELOTTI AMENENA MAN CITY ITALAMBA DUME IKIMSAJILI LAMPARD

ANCELOTTI AMENENA MAN CITY ITALAMBA DUME IKIMSAJILI LAMPARD 

440788_heroa

BOSI wa Real Madrid, Carlo Ancelotti anaamini Manchester City itakuwa imelamba dume kama itamsajili kiungo mkongwe Frank Lampard ambaye yuko mbioni kujiunga Etihad kwa mkopo. 

Kiungo huyo mwenye miaka 36 aliachwa na Chelsea majira haya ya kiangazi mwaka huu baada ya mkataba wake kumalizika na alisaini mkataba wa miaka miwili na New York City FC mwezi juni mwaka huu.

Manchester City na New York Yankees wote wana hisa za umiliki wa New York.

 

0 comments

KIONGOZI TFF ASHUHUDIA YANGA SC ‘INAVYOLALIWA’ MSUMBIJI, ASEMA...

KIONGOZI TFF ASHUHUDIA YANGA SC ‘INAVYOLALIWA’ MSUMBIJI, ASEMA... 

Kidau kushoto akiwa na raia wa Msumbiji aliyenunua jezi ya Yanga SC mjini Beira          

 Na Mahmoud Zubeiry, MAPUTO
MJUMBE wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Wilfred Kidau leo ameshuhudia namna klabu ya Yanga SC inavyohujumiwa nchini Msumbiji.
Asubuhi ya leo, Kidau ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya TFF akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Maputo, nchini hapa alikutana kijana mmoja akiwa amevalia jezi Yanga ambayo amenunua kwa watu wanaouza bila idhini ya klabu hiyo.
Kidau alifika Uwanja wa Ndege kuwapokea washambuliaji Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe ya DRC waliokuja kujiunga na Taifa Stars kwa ajili ya mchezo dhidi ya wenyeji, Msumbiji kesho

 Kijana huyo raia wa Msumbiji, Magnum alisema kwamba jezi hiyo aliinunua Beira na anafahamu kwamba Yanga SC ni timu ya Tanzania, lakini haijui.
“Nimependa jezi nzuri, rangi nzuri nikanunua,”alisema kijana huyo ambaye alifika uwanja wa ndege kupata huduma za kibenki.
Alisema amenunua jezi hiyo kwa thamani ambayo ni sawa na fedha za Tanzania Sh. 15,000 na kwamba watu wengine pia wananunua kwa wingi na kuvaa jezi hizo nchini Msumbiji.
Kidau alisema kwamba Yanga SC na watani wao Simba SC wanapoteza fedha nyingi kutokana na kupuuza bishara ya jezi na bidhaa nyingine zenye nembo zao.
“Sasa watu ambao wanajua kama hii ni bishara nzuri, ndiyo wanajipatia fedha nyingi kirahisi namna hii, hii ni biashara kubwa sana, klabu nyingi Ulaya zinanufaika mno kwa biashara hii,”alisema kiungo wa zamani wa Milambo ya Tabora, Simba SC na timu ya Taifa, Taifa Stars.
Pamoja na ukweli huo kwamba jezi za timu ni biashara inayoziingizia fedha nyingi hata klabu kubwa Ulaya, lakini bado viongozi wa Yanga SC  hawajaonyesha kutaka kutumia fursa hiyo kuinufaisha klabu yao kiuchumi.
Jezi za Yanga pamoja na mahasimu wao, Simba SC zinapatikana karibu Afrika Mashariki yote na nchi nyingine jirani ikiwemo Msumbiji.
Wapembuzi yakinifu wa masuala ya biashara hiyo wanaamini, kwa mwaka Simba na Yanga zinakosa si chini ya Sh. Milioni 500 kila klabu kwa kupuuza biashara ya jezi pekee.

 

0 comments

SIMBA SC YALAMBA SH MILIONI 60 AZAM FC MAUZO YA KAPOMBE, SHOMARY SASA MCHEZAJI HALALI CHAMAZI

SIMBA SC YALAMBA SH MILIONI 60 AZAM FC MAUZO YA KAPOMBE, SHOMARY SASA MCHEZAJI HALALI CHAMAZI

Shomary Kapombe sasa ni mchezaji halali wa Azam FC





Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
SIMBA SC imepokea Sh. Milioni 60 kutoka kwa Azam FC na imemuidhinisha kiungo huyo anayeweza kucheza nafasi za ulinzi pia kujiunga na mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Makamu wa Rais wa Simba SC, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba suala la Kapombe limemalizika na sasa kwa baraka zote huyo ni mchezaji halali wa Azam FC.
“Tumekwishamalizana na Azam FC, Kapombe sasa ni mali yao,”amesema Kaburu na kuongeza; “Na sisi pia tumetekeleza wajibu wetu kwa kuwapa mgawo wao Morogoro Youth Football Academy, (Sh. Milioni 9),”.

Wakati Simba SC inamsajili Kapombe kutoka kituo hicho cha soka Morogoro miaka mitatu iliyopita, walifikia makubaliano akiuzwa na Wekundu hao wa Msimbazi wapate asilimia 15 ya mauzo.
Azam FC ilimnunua Kapombe kwa Euro 43,000 kutoka AS Cannes na mbali na kuwalipa Simba Milioni 60 kama asilimia 40 ya fedha walizotoa kwa klabu ya Ufaransa kumnunua nyota huyo, pia wanatakiwa kumlipa wakala Dennis Kadito asilimia 20. 
Kadito ndiye aliyempeleka Ufaransa Kapombe baada ya Simba SC kukubali kumtoa bure, kwa matarajio akiuzwa Ulaya itapata mgawo mzuri.
Kaburu amekabidhi hundi ya Sh. Milioni 9 kwa Morogoro Youth Football Academy kama sehemu ya mgawo wao wa mauzo ya Kapombe Azam FC


Kapombe alikwenda Ufaransa katikati ya mwaka jana kujiunga na klabu hiyo ya Daraja la Nne, lakini Novemba mwaka huo aliporejea kuichezea Tanzania katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Zimbabwe hakutaka tena kurudi Ulaya.
Machi mwaka huu, akaanza kufanya mazoezi na Azam FC kabla ya mwezi uliopita kusaini Mkataba wa miaka mitatu na mabingwa hao wapya wa Ligi Kuu nchini.





0 comments
 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger