UVCCM WAPINGA SERIKALI TATU.
JUMUIYA ya Umoja wa Vijana Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga (UVCCM)imepinga mfumo wa kuwepo kwa serikali tatu na kueleza endapo mchakato wa uundwaji wake ufanyika utarudisha nyuma maendeleo ya watanzania pamoja na kuuvunja muungano uliopo baina ya Tanzania bara na visiwani.
Kauli hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana Mkoa wa Tanga(UVCCM)Abdi Makange wakati akizungumza katika kikao cha baraza hilo ambacho kilifanyika wilayani hapa na kuhudhuriwa na Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga,Gustav Mubba.
Makange alisema yenye anashangazwa na viongozi wa vyama vya upinzani vyenye sera ya kuridhia uwepo wa serikali tatu bila kuangalia athari ambazo zinaweza kutokea kwa wanannchi na jamii ambazo zinawazunguka.
"Binafasi nashangazwa sana na sera zinazotolewa na vyama vya upinzani hapa nchini kwa kuzungumzia uanzishwaji wa serikali tatu bila kuangalia kuna athari gani kwa wananchi wanaowaongoza "Alisema Makange.
Alisema maoni ambayo waliyatoa kuhusu uanzihwaji wa serikali tatu hawaamini kama yanatoka kwa wananchi na kueleza kuwa ni ya watu wachache wenye dhamira ya kuudhofisha muungano wetu ambao tulioachiwa na waasisi wa Taifa hili.
Mwenyekiti huyo aliwataka vijana waliopo ndani ya umoja huo kusimama kwenye mapendekezo ya chama cha mapinduzi kuwa serikali tatu haiwezekani kwa sababu itaongeza gharama za uendeshaji na kuwafanya wananchi kuendelea kuwa maskini.
Aidha aliwataka wananchi kuepukana na viongozi wasioitakia mema serikali yao kwa kuwa mstari wa mbele kuzungumzia suala hilo na kuwataka wajumbe hao watakaopata nafasi ya kwenda kwenye mabaraza ya katiba wakayazungumze hayo kwamba serikali tatu haiwezekani.
PICHA ZA MATUKIO YA BARAZA LA UVCCM MKOA WA TANGA JANA KOROGWE.
KATIBU WA CHAMA CHA MAPINDUZI MKOA WA TANGA,GUSTAV MUBBA AKITOA NENO KATIKA BARAZA HILO . |
MWENYEKITI WA UVCCM MKOA WA TANGA,ABDI MAKANGE AKIZUNGUMZA KATIKA KIKAO CHA BARAZA HILO AMBACHO KILIFANYIKA WILAYANI KOROGWE JANA. |
KATIBU WA CHAMA CHA MAPOINDUZI MKOA WA TANGA KUSHOTO GUSTAV MUBBA AKITETA JAMBO NA MWENYEKITI WA UVCCM MKOA WA TANGA ,ABDI MAKANGE JANA |
MAKAMANDA WA UVCCM WILAYA YA TANGA WAKIONGOZWA NA MWENYEKITI WAO,SALIM PEREMBE KUSHOTO WAKIMSIKILIZA KWA UMAKINI MWENYEKITI WA MKOA UVCCM JANA KWENYE BARAZA HILO. |
;Chanzo, tangarahablogspot.com
Post a Comment