Mshindi wa nyumba Airtel akikabidhiwa funguo;
Meneja Masoko kanda ya kusini, Beda Kinunda akimkabidhi funguo mshindi wa kwanza wa nyumba ya airtel yatosha kutoka Iringa, Silvanus Juma. (HM)
Meneja
Mahusiano wa Airtel, Jackson Mmbando akimkabidhi akimkabidhi cheti cha
ushindi, mshindi wa kwanza wa nyumba ya airtel yatosha kutoka Iringa,
Silvanus Juma, katikati ni mkewe Veronica Silvanus.
Meneja
Mahusiano wa Airtel, Jackson Mmbando (katikati) akieleza jinsi shindano
hilo linavyofanyika kwa wananchi waliokuwepo ukumbi wa MR Hoteli wakati
wa kumkabidhi cheti cha ushindi na funguo, mshindi wa kwanza wa nyumba
ya airtel yatosha kutoka Iringa, Silvanus Juma (Kushoto) na kulia ni
Meneja masoko kanda ya kusini, Beda Kinunda.
MSHINDI wa nyumba ya kwanza ya Airtel Yatosha yenye thamani ya Sh65m kutoka Kampuni ya mitandao ya simu za mkononi Airtel, Silvanus Juma amekabidhiwa rasmi funguo yake
baada ya kuibuka mshindi kupitia promosheni maalumu ya Airtel yatosha shinda nyumba 3.
Makabidhiano ya funguo hiyo yalifanyika kwenye hoteli ya MR mkoani Iringa ambapo alikabidhiwa funguo pamoja na cheti kinachoonesha kwamba yeye ni mshindi wa kwanza wa nyumba katika nyumba tatu zinazoshindaniwa kupitia promosheni ya Airtel Yatosha.
Juma ni mhasibu wa Taasisi ya Maendeleo ya Wanawake na Watoto waliopo vijijini Meneja.
Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando alisema makabidhiano ya funguo ni ya awali lakini Alhamisi ya wiki hii Silvanus Juma atakabidhiwa rasmi nyumba yake iliyopo
maeneo ya Kigamboni jijini Dar es salaam.
Alisema Airtel inayo furaha kubwa kumkabidhi mshindi wao huyo zawadi hiyo na itaendelea kutoa zawadi zilizo bora kwa wateja wake nchi nzima kupitia promosheni mbalimbali zinazoendeshwa na Kampuni hiyo.
"Kama alivyo na furaha mshindi wetu ndivyo na sisi tunavyofurahi na hii sio kikomo bado kuna zawadi mbalimbali kwa wateja wa Airtel nchi nzima na cha muhimu ni wao kujiunga na vifurushi mbalimbali vinavyopatikana kwenye promosheni hii ya ya Airtel yatosha shinda
nyumba 3. mbalimbali za Airtel ili kushinda," alisema Mmbando.
Mpaka sasa Airtel imeweza kutoa zawadi mbalimbali kwa wateja wake nchi nzima ambapo imetoa shilingi milioni 37 kwa washindi 37 na inaendelea na promosheni hiyo ambayo inadumu kwa siku 90, sambamba na hilo nyumba mbili kati ya tatu zilizopo Kigamboni bado zinashindaniwa kupitia promosheni hiyo ya Airtel yatosha, shinda nyumba 3.
Akielezea furaha yake Juma alisema zawadi hiyo ya nyumba ni bahati ya kipekee ambayo hakuitarajia hapo awali na hata alipopigiwa simu hakuamini kwa sababu alijua kitu kama hicho hakiwezekani na hawezi kupata nyumba katika msimu kama huo.
"Nilipopigiwa kwanza nilijua ni utani, pengine mtu amejisikia tu kunitania lakini nilipigiwa tena na hapo ndipo nilipoanza kuamini. Nawashukuru sana Airtel kwa zawadi hii na ni kielelezo wazi kuwa Airtel ni mtandao unaojali na kuthamini wateja wake," alisema Juma.
Juma alipatikana baada ya kuchezeshwa kwa droo ya kwanza katika makao makuu ya Airtel Dar es salaam mwisho wa mwenzi wa saba mwaka huu ilyopelekea Bw. Juma kuibuka mshindi wa kwanza katika promosheni hiyo. Chanzo: Hakimu Mwafongo, mjengwablog, Iringaa
Post a Comment