skip to main |
skip to sidebar
Elizabeth Kilindi,Tanga
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema),Dr Willbroad slaa amewaasa watanzania watambue kuwa
katiba ni uhai wa Taifa hivyo wawe huru kutoa maoni ili baadae iweze
kuwatetea na kuwalinda.
Dr. Slaa alisema hayo katika mkutano
wenye lengo la kukusanya maoni ya katiba mpya iliyofanyika katika
viwanja vya Tangamano jijini hapa ikiwa maelfu ya wananchi
walikusanyika kutoa maoni ambapo amesema chama hicho kitakusanya maoni
si chini ya milioni tano ili kuyapeleka kwa Jaji Warioba.
Aidha
alisema chama chake kimeamua kukusanya maoni kwani katiba si mali ya
chama bali ni ya watanzania wenyewe hivyo wameona ni vyema kuwakusanya
kwa pamoja kutoa maoni yao ambayo ni haki ya kila mtanzania.
Katibu
huyo alisema kuwa wenye mawazo ya kufanana wanauwezo wa kutengeneza
katiba hivyo tunaitaji katiba ambayo itawalinda watanzania na wala sio
itakayolinda chama chochote cha siasa.
Katika atua nyengine Dr
Slaa alisema katika katiba ya sasa imetumiwa vibaya na viongozi wa sasa
walioko madarakani na pamoja na kutowachukulia hatua wanaovunja maadili
kwa kuiba rasilimali za umma.
Sambamba na hayo aliweza kuongelea
umuhimu wa serikali tatu ambapo alisema kuwa itapunguzia ghalama za
uendeshaji wa serikali kwa kuokoa fedha nyingi kwani asilimia ya wabunge
na mawaziri itapungua kwa kiasi kikubwa.
Pia aliwata watanzania kuacha woga katika kudai haki kwani kufanya hivyo ni kutojitendea haki na hata mungu anakataza.
Naye
mjumbe wa kamati kuu wa chama cha demokrasia na maendeleo{chadema}
Mabere Marando alisema kuwa watahakikisha kwa kila njia kuwafikiwa
watanzania na kuwaelewesha rasimu ya katiba mpya na msimamo wa chama
hicho.
Hata hivyo alisema kuwa chama hicho kitawafikia wananchi
katika maeneo yao kuwaelewesha na kupata maoni na vyema kusema nini
wanataka kiwepo katika katiba hiyo mpya.
Copyright © 2011.
TANGA LEO - All Rights Reserved
Post a Comment