Wakikaidi ukandamizaji unaofanywa na serikali ya mpito inayoungwa mkono
na jeshi, kundi la Udugu wa Kiislamu na washirika wao wametangaza kuwa
watafanya maandamano katika maeneo karibu tisa katika mkuu wa
Misri,Cairo.
Waungaji mkono wa rais aliyeondolewa madarakani Mohammed Mursi wanapanga kufanya maandamano mengine mjini Cairo leo Jumapili(18.08.2013), na kuongeza hofu ya umwagikaji zaidi wa damu baada ya mamia ya watu kuuwawa wiki hii.
mapambano katika msikiti wa al-Fath17.8.2013
Maandamano hayo yanakuja wakati serikali inatafakari kulivunjia kabisa kisheria kundi la Udugu wa Kiislamu na waendesha mashtaka wanawahoji wafuasi 250 wa Mursi kuhusiana na mauaji na madai ya ugaidi.
serikali inawashutumu viongozi wa makundi ya Kiislamu kwa kuchochea ghasia na imeahidi kupambana na kile ilichokiita , "nguvu za ugaidi na uharibifu".
Ghasia zilianza siku ya jumatano wakati majeshi ya usalama yalipowaondoa kwa nguvu waandamanaji katika maeneo mawili makubwa ya waandamanaji wanaomuunga mkono rais aliyeondolewa madarakani Mohammed Mursi mjini Cairo. Kiasi ya watu 750 wameuwawa katika hatua hiyo ya jeshi pamoja na ghasia zilizofuatia nchi nzima.
Ndani ya msikiti wa al-Fath mjini Cairo 17.8.2013
Shutuma kali.
Ukandamizaji dhidi ya waandamanaji wa makundi ya Kiislamu umesababisha shutuma kali kutoka kwa jumuiya ya kimataifa, hususan kutoka bara la Ulaya na Marekani. Hata hivyo , mataifa ya ghuba yameeleza kuunga kwao mkono watawala wa mpito nchini Misri.
Mazishi katika kanisa la Coptic mjini Cairo
Ban amewataka waandamanaji mitaani na maafisa kuwa na uvumilivu wa hali ya juu na kuelekea haraka katika kupunguza ghasia hizo. Wakati huo huo polisi ya Misri imewaondoa waandamanaji wa Kiislamu kutoka katika msikiti mjini Cairo jana Jumamosi baada ya mapambano ikiwa ni pamoja na kurushia risasi, wakati idadi ya vifo katika siku hizo nne za machafuko ikifikia 750.
Majeshi ya usalama yaliwaondoa waungaji mkono wa rais aliyeondolewa madarakani Mohammed Mursi kutoka msikiti wa Al-Fath, huku kundi kubwa la watu wenye hasira likijaribu kuwapiga watu hao wakiwaita magaidi.
Mapambano hayo yamekuja wakati serikali ikisema kuwa watu 173 wameuwawa katika muda wa saa 24 zilizopita , na kufikisha idadi ya watu waliouwawa nchi nzima kufikia 750 tangu siku ya Jumatano, wakati polisi walipowaondoa waandamanaji kwa nguvu katika makambi mawili ya watu wanaomuunga mkono Mursi katika mji mkuu.
Post a Comment