PROGRAMU YA PAMOJA TUWALEE FHI 360 YATOA MSAADA WA BAISKELI 257 ZENYE THAMANI YA SH27.2MILIONI KWA WAHUDUMU WANAOWAHUDUMIA WATOTO WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA HATARISHI MOROGORO.

Mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera akikata utepe ikiwa ishara ya uzinduzi wa ugawaji wa baiskeli kwa wahudumu wanaowahudumia watoto wanaishi katika mazingira hatarishi wanaojitolea baada ya shirika la PROGRAMU YA PAMOJA TUWALEE FHI 360 kutoa msaada wa baiskeli 257 zenye thamani ya sh 27.2milioni katika katika wilaya za Morogoro, Morogoro Vijijini na Mvomero katika hafla iliyofanyika kwenye ofisi za mkuu wa mkoa wa Morogoro.PICHA JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM

Hapa Bendera akimkabidhi Sister Monica Mbiki kutoka kituo cha watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi kijiji cha Ngerengere wakati wa ugawaji wa baiskeli hizo.PICHA JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM

Bendera akiribu kuiendesha moja ya baiskeli hizo mara baada ya kuzindua ugawaji.PICHA JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM
Bendera akizungumza wakati wa uzinduzi wa ugawaji wa baiskeli hizo kwa wahudumu wanaowahudumia watoto wanaishi katika mazingira magumu wanaojitolea (hawapo pichani) baada ya shirika la PROGRAMU YA PAMOJA TUWALEE FHI 360 kutoa baiskeli hizo
Makamu Mkurugenzi PROGRAMU YA PAMOJA TUWALEE FHI 360, Levina Kikoyo akitoa taarifa mbele ya mkuu wa mkoa kulia na Katibu Tawala Msaidizi mkoa wa Morogoro, Lucas Mwaisaka (katikati) katika hafla hiyo.
PICHA JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM

Hawa ni sehemu ya wahudumu wa kujitolea nao wakifuatilia jambo katika hafla hiyo.PICHA JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM
Mwandishi mkongwe wa TBC 1 mkoa wa Morogoro Monica Lyampawe kushoto na Mwandishi wa Habarileo mkoa Morogoro John Nditi wakifuatilia matukio mbalimbali katika hafla hiyo. PICHA JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM
Baiskeli zikiwa zimepangwa katika mistari muda mfupi kabla ya mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera kukabidhi kwa wahusika. PICHA JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM
Baadhi ya wahudumu wanaowahudumia watoto wanaishi katika mazingira hatarishi wakisukuma lori aina ya fuso lililohesheni baiskeli za shirika la programu ya pamoja tuwalee FHI 360 ambazo zinatolewa msaada kwa wahudumu wa mkoa wa Morogoro ambao wanatoa huduma kwa watoto wanaishi katika mazingira hatarishi ambapo jumla ya baiskeli 257 zenye thamani ya sh 27.2milioni zilitolewa katika hafla iliyofanyika kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa wa Morogoro hivi karibuni.PICHA JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM
Sehemu ya baiskeli zikiwa zimepangwa tayari kwa kuwakabidhi wahusika.PICHA JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera wa pili kutoka kushoto akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali na shirika la PROGRAMU YA PAMOJA
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger