Wanaume
wawili nchini Kenya wameibuka na mbinu isiyo ya kawaida ya kupata
suluhu ya kupigania mwanamke ambaye wote wanampenda kwa kusaini mkataba
wakikubaliana kuishi nae kwa zamu.
Silvester Mwendwa ni mmoja wa wanaume hao. Ameeleza BBC kwanini binafsi anamuhusudu mwanamke huyo.
Mmoja ya wa wanaume hao alisema haoni ubaya wowote kwa yeye na mwenzake kumuoa mwanamke mmoja.
Amehoji sheria ya sasa inayoruhusu wanaume kuoa wanawake wengi na wakati huo huo kuharamisha mpango kama huo kwa kina mama.
Sylvester Mwendwa anasema wazazi wake wamekubali na mpango wake na wako tayari kumtolea mahari.
Wanaume hao wawili walikubali kumuoa mwanamke huyo baada ya kugundua kwamba kumbe wote wana uhusiano wa kimapenzi naye.
Na kumbe mwanamke huyo alikuwa ameahidiana na kila mmoja wao kwamba angefunga nao ndoa bila ya wao kujuana.
Lakini
walipogunduana , ilikuwa ni ugomvi kwa mara kwa mara lakini mwanamke
huyo alipoambiwa amchague mnmoja wao, alishindwa. Akasema anawapenda
wote wawili.
Na
baada ya hapo watatu hao waliafikiana kusaini mkataba ambao utaruhusu
wanaume hao wawili kuishi na mwanamke huyo kama bwana na bibi ila kila
mmoja wao atakuwa na wakati wake wa 'kwenda kumjulia hali.'
Vile
vile mkataba huo unawashurutisha kugawana majukumu yote ya nyumbani
ikiwa ni pamoja na kuwalea watoto na kutowabagua kwa kuwa wote watakuwa
na haki sawa.
Hata
hivyo kwa mujibu wa sheria za kenya ni haramu kwa mwanamke kuolewa na
wanaume wawili na mkataba huo sasa umeibua mjadala mkali wa kisheria,
huku sheria mpya ya ndoa ikitarajiwa kujadiliwa na kuidhinishwa bungeni.
Post a Comment