Marekani yapima mikakati ya kijeshi dhidi ya Syria

Marekani yapima mikakati ya kijeshi dhidi ya Syria

Kufuatia shambulizi la silaha za sumu lililoua mamia nchini Syria, yaonekana muda wa kutafuta suluhu ya muafaka umekwisha. Marekani inaona msitari mwekundu umevukwa, na inapima uwezekano wa kuingilia kijeshi. 

Baada ya kutokea shambulizi linalodhaniwa kuwa la kemikali, ambalo liliwauwa mamia ya raia na kujeruhi zaidi ya 3000 nchini Syria kwa mujibu wa shirika la misaada la madaktari wasio na mipaka, mataifa mengi ya magharibi na hasa Marekani, yanaaamini kuwa rais Bashar al-Assad ndiye anawajibika kwa shambulizi hilo. Kwa sababu kwa miezi kadhaa rais wa Marekani, Barack Obama, alionya kuwa matumizi ya silaha za kemikali yatamaanisha kuwa msitari mwekundu umevukwa, katika mazingira haya, laazima utawala wa Assad uchukuliwe hatua nzito. Kwa mujibu wa vyanzo vya Usalama vya Marekani, Ikulu ya mjini Washington inajadili njia tatu za kuchukuwa.

Eneo la kuzuiwa kuruka ndege linaweza kuwasaidia pakubwa waasi.  
 Eneo la kuzuiwa kuruka ndege linaweza kuwasaidia pakubwa waasi.
 
Eneo lisiloruhusiwa ndege kuruka

Njia ya kwanza ni kuweka eneo lisiloruhusiwa ndege kuruka nchini Syria, hii ikimaanisha kuwa Wamarekani watazipiga marufuku ndege na helikopta za utawala katika baadhi ya maeneo. Hii itamaanisha kuwa vikosi vya Assad havitaweza tena kuwashambulia waasi kupitia angani. Hans-Joachim Schmidt, kutoka taasisi ya amani na utatuzi wa migogoro ya Hessian, anasema hatua hii ingekuwa ya msaada mkubwa kwa waasi kwa sababu "Assad hangeweza kuwashambulia waasi kwa kutumia helikopta na ndege zake za kivita. Hii ingewanufaisha moja kwa moja waasi."


Lakini Paul Rogers, mtaalamu wa masuala ya usalama kutoka shirika la ushauri la Oxford Reseach Group la Uingereza, anasema Marekani laazima izime mifumo ya ulinzi wa angani ya Syria, jambo ambalo anasema litakuwa ghali na la hatari sana kwa kuzingatia kuwa Urusi iliahidi kuipatia Syria mitambo ya kisasa. Juu ya wasiwasi huo, Hans-Joachim Schmidt anasema ikiwa kweli Urusi imekwisha iuzia Syria mitambo hiyo ya kisasa, basi Wamarekani watapata taabu sana. Lakini anasema haoni uwezekano mkubwa kwa Marekani kutumia mkakati huu, kwa sababu utawavuta zaidi katika mgogoro huu, kitu ambacho serikali ya Marekani haitaki. Wakati huo huo, kanda isiyoruhusiwa kuruka ndege laazima iidhinishwa na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, na huko Urusi na China bila shaka zitatumia kura ya turufu kuizuia.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry ametoa matamshi yanayoashiria mashambulizi dhidi ya Assad yako njiani.  
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry ametoa matamshi yanayoashiria mashambulizi dhidi ya Assad yako njiani.
 
Mashambulizi dhidi ya maeneo ya kimkakati

Njia nyingine ni kushambulia maeneo ya kimkakati kwa makombora na maroketi kama vile viwanja na njia za kurukia ndege, na hivyo kudhoofisha uwezo wa jeshi la angani la Syria. Marekani ina meli kadhaa za kivita na nyambizi katika bahari ya Mediterannean, ambazo zinaweza kutumiwa kutekeleza mashambulizi ya namna hii na kufanya vigumu kwa ndege kuruka na kutua.


Lakini uharibifu kwa njia za ndege unaweza kukarabatiwa haraka. Schmidt anaiona njia hii kuwa ndiyo yenye uwezekano mkubwa zaidi wa kutumiwa, licha ya ukweli kuwa nayo itahitaji kuidhinishwa na baraza la usalama. "Wamarekani hawataki kujiingiza moja kwa moja katika mgogoro huu, hivyo shambulio la kijeshi lingekuwa ishara yenye ufanisi, japokuwa yenye mipaka, ya kuzuia matumizi zaidi ya silaha za kemikali," anafafanua mtafiti wa amani na utatuzi wa migoro Hans-Joachim Schmidt.
 
Kuwapatia waasi silaha

Njia ya tatu inaweza kuwa kuwapatia silaha waasi. Hadi sasa Marekani haijawapatia msaada wa silaha waasi, ukiachilia mbali misaada ya kawaida kama vile vifaa vya tiba. Lakini Rogers anasema waasi wamekuwa wakipokea vifaa vya kijeshi kutoka Saudi Arabia na Umoja wa falme za Kiarabu kupitia Uturuki na Jordan. Lakini anasisitiza kuwa uwezekano wa waasi kupatiwa silaha moja kwa moja na Marekani ni mdogo sana, kwa sababu watahitaji kupewa mazoezi kwanza kabla hilo halijafanyika. Hofu nyingine 

 kuhusiana na hili, ni silaha hizo kuangukia mikoni mwa kundi lenye itakadi kali la Al-Nusra Front.

Rais Bashar al-Assad akisalimiana na wanajeshi wake mjini Damascus hivi karibuni.  
 Rais Bashar al-Assad akisalimiana na wanajeshi wake mjini Damascus hivi karibuni.
 
Na diplomasia je?

Lakini Uingiliaji wa tahadhari bado unabaki kuwa uingiliaji, na kwa hivyo Marekani bado inasita kufanya hivyo, kwa kuzingatia madhara yake. Tayari rais Bashar al-Assad ameonya kuwa hatua yoyote ya kuingilia kati kijeshi itasababisha moto utakaoizingira kanda nzima ya mashariki ya kati. Iran nayo inaweza kuliimarisha kundi la Hezbollah dhidi ya Israel na kundi la Taliban linaweza kuzidisha mashambulizi dhidi ya maslahi ya Marekani.

Schmidt kwa hivyo anapendekeza njia ya nne ambayo haizungumzwi katika vyombo vya habari kwa sasa: Shinikizo la diplomasia. Hata hivyo, mtaalamu huyo anahisi kuwa uamuzi wa kuishambulia Syria kijeshi umekwisha chukuliwa na kinachosubiriwa ni lini na vipi. Kinachoonekana sasa ni kwamba Marekani inatafuta washirika katika operesheni hii.

 

Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger