skip to main |
skip to sidebar
Mwigizaji wa kike katika tasnia ya
filamu Bongo Aunty Ezekiel akiwa anauguza jeraha la kidonda baada ya kudaiwa kujeruhiwa na chupa katika ukumbi wa starehe wa Club Billicanas jijini Dar es Salaam.
MWIGIZAJI wa kike katika tasnia ya
filamu Bongo Aunty Ezekiel imeripotiwa kupata majeraha katika mkono wake
wa kushoto baada ya kuchimbwa na chupa yenye ncha kali, sakata hilo la
hatari lilitokea Club Billicanas wakati wa show iliyokifanyika hapo
chini ya Madam Wema Sepetu chanzo chetu kimetuhabarisha.
Chanzo cha ugomvi hadi leo bado
kitendawili baada ya kutoka fununu kuwa uenda ugomvi huo unahusishwa na
kumgombea bwana yaani mwanaume ambaye waliwahi kumgombea siku za nyuma
lakini kupigana kidogo ambapo mmoja alitoka nduki na kuacha msala
ukitulia. CHANZO http://mwanahabariuswazi.blogspot.com
Chanzo chetu bado kinafuatilia tukio hilo kwa ukaribu kisha
tutakujuza kulikoni hadi nyota wetu kutaka kuharibiwa show yake ambayo
ndio inapa ajira katika uigizaji, tunampa pole kwa majeraha yaliyompata ,
huku tukisubiri atusimulie sakata leo hakuwa tayari kupokea simu yetu.
Copyright © 2011.
TANGA LEO - All Rights Reserved
Post a Comment