skip to main |
skip to sidebar
Hii ya binti wa miaka 14 kujifungua Mapacha watatu Kenya umeisoma yote?
Radio
station ya Kenya ‘Radio Maisha’ imeripoti kwamba wauguzi katika
hospitali kuu ya Bungoma nchini humo wamepigwa na butwaa baada ya
msichana mwenye umri wa miaka 14 kujifungua mapacha watatu.
Madaktari katika hospitali hiyo wanasema kuwa watoto hao
wako katika hali nzuri ya afya japo mama yao bado anaonekana kuwa
mnyonge.
Afisa wa baraza la kaunti ya Bungoma anayesimamia afya Grace
Khayota, aliwaongoza maafisa wengine wa kaunti hadi hospitali hiyo
kuwaona watoto hao ambapo sasa mama wa watoto hao Mwanarahab Wamukoya
ambae ni msichana wa miaka 14, ameomba Wasamaria kumpa usaidizi kwenye
kuwalea watoto.
Taarifa kwenye sentensi nyingine imesema binti huyu wa miaka
14 amepata watoto hao kutokana na uhusiano wa kimapenzi kati yake na
mpenzi wake ambae ni mvulana wa miaka 16.
Copyright © 2011.
TANGA LEO - All Rights Reserved
Post a Comment