Featured Post Today
print this page
Latest Post

HALI YA USALAMA YAZIDI KUZOROTA JAMUHURI YA AFRIKA YA KATI

HALI YA USALAMA YAZIDI KUZOROTA JAMUHURI YA AFRIKA YA KATI

GIGI_3b22b.jpg
Waasi wa kundi la kikristo la Anti Balaka katika Jamhuri ya Afrika ya Kati wametishia kuwaua mamia ya waislamu wanaojificha katika kanisa moja kama hawataondoka nchini humo katika kipindi cha wiki moja ijayo.

Wanajeshi wa kulinda amani wapatao 30 kutoka Cameroon walilazimika hapo jana kufyatua risasi hewani ili kuwatawanya wapiganaji wa Anti Balaka waliokuwa wamekusanyika nje ya kanisa hilo la Kikatoliki wakipania kuwaua waislamu hao ambao wamekimbilia katika kanisa hilo kuokoa roho zao.

Milio hiyo ya risasi iliwaogofya watoto waliokimbia kujinusuru na vilio vya watu hao waliojawa na uoga vilisikika vikirindima katika kanisa hilo.Wanajeshi hao wa kulinda amani kwa sasa ndiyo tegemeo la pekee kwa waislamu hao wapatao 800 dhidi ya kushambuliwa na magenge yanayotaka kuwaua.


Wapiganaji wa Anti Balaka tayari walionekana wakiwa na mitungi ya lita 40 ya petroli ambayo wametishia kutumia kulichoma kanisa hilo.Kasisi wa kanisa hilo Justin Nary ambaye anatoa hifadhi kwa waislamu hao anajua analengwa na waasi hao.

Waasi walizingira kanisa kuwasaka waislamu
Kasisi Nary amesema wapiganaji hao wa Anti Balaka wamemtishia maisha mara nne kwa kumulekezea mtutu wa bunduki na wamempigia simu kumuonya kuwa punde tu wanajeshi wa kulinda amani wataondoka,watamuua.

Baadhi ya wanaotafuta hifadhi katika kijiji hicho cha Guen wametoroka baada ya kiasi ya waislamu 70 kuuawa katika siku za hivi karibuni.Waislamu na wakristo walikuwa wakiishi kwa amani tangu jadi hadi kundi la waasi la kiislamu kutoka Kaskazini mwa nchi hiyo lilipoipindua serikali na kulitumbukiza taifa hilo katika ghasia.

Kundi hilo la kiislamu la Seleka linashutumiwa kwa mauaji katika vijiji vya wakristo katika taifa hilo.Viongozi waliosaidiwa na Seleka kuingia madarakani walipoondolewa madarakani mwezi Januari,ilichochea mashambulizi ya kulipiza kisasi kutoka kwa kundi lililoibuka la Anti Balaka.

Mauaji yaripotiwa katika miji mingine
Mji mkuuu Bangui ambao ulikuwa ni kitovu cha maasi na ghasia tangu mwezi Desemba kwa sasa hali inaonekana kudhibitiwa kwa kiasi fulani lakini mauaji yanayofanywa kwa misingi ya kidini yanaendelea kuripotiwa katika miji mingine nchini humo.
Majeshi ya Ufaransa na ya umoja wa Afrika yaliyoko nchini humo kudhibiti hali hayatoshi kukidhia mahitaji ya kiusalama na kiulinzi yanayohitajika kwa dharura.

Umoja wa Mataifa umeiomba Jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua kabambe na za dharura kuisaidia Jamhuri ya Afrika ya Kati kujikwamua kutoka kwa mzozo mbaya unaotishia kulisambaratisha taifa hilo.

Bunge la Ufaransa hii leo linatarajiwa kupiga kura kuidhinisha kuendelea kusalia kwa jeshi lake nchini humo hadi mwezi Februari mwaka ujao wakati ambapo Jamhuri ya Afrika ya Kati itafanya chaguzi.

Waziri wa ulinzi wa Ufaransa Jean Yves Le Drian amekiri kuwa itachukua muda mrefu kuliko walivyotarajia kurejesha udhabiti nchini humo kutokana na kiwango cha juu cha uhasama na ghasia.Maelfu ya watu wameuawa tangu Desemba na zaidi ya watu milioni moja wameachwa bila makaazi.
Chanzo, dw.de.com/swahili. R.M
0 comments

OPERESHENI DHIDI YA WAASI WA UGANDA ADF

OPERESHENI DHIDI YA WAASI WA UGANDA ADF

UGANDA_98bb6.jpg
 Waasi wa Uganda ADF.

Operesheni zinaendelea katika wilaya ya Beni, jeshi la serikali limetangaza kuwa, operesheni hizo, zimelipelekea jeshi hilo kuyakomboa maeneo kadhaa, toka mikononi mwa waasi.
Operesheni dhidi ya waasi wa Uganda ADF wanaojihifadhi katika misitu
ya wilaya ya Beni mashariki mwa jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zikiwa zinaendelea,huku wanajeshi wakiwa wamepelekwa katika eneo hilo, raia wa mji na wilaya za Beni wameanza kulalamikia usalama wao,kutokana na jinsi wanavyo nyanyaswa na wanajeshi wa serikali. Ili kukomesha vitendo vya unyanyasi wa raia, jeshi la Congo limelivalia njuga suala hilo.
Mwandishi wetu John Kanyunyu na ripoti kamili kutoka Beni. Kusikiliza ripoti hiyo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Chanzo, dw.de.com/swahili. R.M
0 comments

BILIONI 2.4 ZAHITAJIKA UKARABATI WA MIUNDOMBINU SHULE YA SEKONDARI TANGA SCHOOL

BILIONI 2.4 ZAHITAJIKA UKARABATI WA MIUNDOMBINU SHULE YA SEKONDARI TANGA SCHOOL


(Pichani ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Luteni Mstaafu Chiku Gallawa akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake)
 
NA OSCAR ASSENGA,TANGA
 
JUMLA ya sh. Bilioni 2.4 zinahitajika kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu katika shule ya sekondari ya Tanga School iliyopo mkoani Tanga kutokana na uchakavu ilionao baadhi ya majengo kwenye shule hiyo.

Shule hiyo inahitaji ukarabati wa miundombinu iliyokuwepo tokea mwaka 1967 ikiwemo madarasa,maabara,karakana, maktaba, mabweni,bwalo na zahanati ambazo ukarabati huo utaifanya kuonekana na muonekano mpya.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Luteni Mstaafu Chiku Gallawa wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake ambapo amesema maeneo mengine yanayohitajika ukarabati ni viwanja vya michezo,nyumba za walimu ,Jengo la Utawala,Chumba cha Kompyuta na duka na Mgahawa wa shule pamoja na gari la shule.


Gallawa ameongeza kuwa maeneo mengine ni miundombinu ya maji taka,uzio wa shule,uwekaji wa solar power,ufungaji wa security lights,ujenzi wa ofisi ya serikali ya wanafunzi,upakaji rangi wa majengo ya shule na ujezi wa miundombinu ya kuvuna na kuhifadhi maji.
wa kwanza kulia ni Mwandishi wa gazeti la Citizen mkoa wa Tanga,George Sembony ambaye ni miongoni mwa wanafunzi waliosoma kwenye shule ya sekondari ya Tanga School akiwa na walimu wakuu waliopitia shule hiyo na wa sasa.
 Amesema kazi ya kukarabati imepangwa kufanyika kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza itagharimu bilioni 1.4 ambayo itafanya ukarabati wa mabweni ya wasichana na wavulana,samani za madarasa, maktaba, maabara, bwalo,uzio wa shule na nyumba.
Aidha ameongoeza maeneo mengine kuwa ni Jengo la Utawala,Maegesho ya magari,miundombinu ya majitaka,ukarabati wa barabara ikiwemo zahanati kufanyiwa ukarabari katika awamu hii wakati awamu ya pili itagharimu  zaidi ya bilioni 1.
 
Mafundi wakiendelea na ufundi wao kwenye shule hiyo kwenye eneo la karakana.



Akizungumza mkakati wa upatikanaji wa fedha hizo,Mkuu huyo wa mkoa amesema kamati maalumu ya kuratibu zoezi zima imeundwa katika mkoa wa Tanga chini yake ikiwahusisha baadhi ya wakuu wa shule hiyo waliopita na aliyeko madarakani,wataalamu mbalimbali na wajumbe wa bodi kwa kuanzia.
baadhi ya majengo yaliyopo kwenye shule hiyo yanavyoonekana wakati mtandao huu ulipotembelea shuleni hapo
 Kamati hiyo imependekeza mikakati kwa ajili ya kupata fedha hizo ikiwemo kuwakutanisha watu wote walisoma au kufanya kazi shule hiyo pamoja na kutafuta wahisani mbalimbali ndani na nje ya mkoa.
Suala lengine litakalo fanyika ni kuandaa matamasha mbalimbali ikiwemo wazazi za walezi wa wanafunzi waliopo shule hiyo ambapo kamati hiyo itakutana na wadau walisoma shuleni hapo Machi 15 mwaka huu kwenye ukumbi wa bwalo la shule hiyo.

Baada ya mkutano huo makubaliano yataelezwa kwa wadau na mpango wea utekelezaji utaandaliwa

Shule hiyo ilianzishwa mwaka 1895 chini ya utawala wa kijerumani ambapo shule hiyo hapo awali ilijengwa mjini eneo la mkwakwani ambapo hivi sasa kuna shule ya sekondari Old Tanga.
0 comments

Wakulima wilayani Handeni waaswa kulima mazao ya biashara na chakula

Wakulima wilayani Handeni waaswa kulima mazao ya biashara na chakula



Na Mwandishi Wetu, Handeni

WANANCHI wilayani Handeni, mkoani Tanga, wameaswa kulima maza ya biashara na chakula ili kuwaondolea balaa la njaa linalowakumba kila mwaka kutokana na kutegemea kilimo cha aina moja, yakiwamo mahindi.
 
Mkuu wa Wilaya Handeni, Muhingo Rweyemamu, pichani.
 
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Muhingo Rweyemamu katika mahojiano maalum wilaya Handeni mkoani Tanga, ikiwa ni sera na mipango kabambe ya kuweka sawa jambo hilo kwa maendeleo ya wananchi wa Handeni na Tanzania kwa ujumla.


DC Muhingo alisema kuwa wakazi wengi wa Handeni wanategemea kilimo cha mahindi kama zao la biashara na chakula, jaambo linalowafanya kila wakati watu wengi wakabiliwe na njaa na kuwafanya waishi kwa tabu wakati wote.

“Ofisi yangu inajitahidi kuwaelimisha wananchi wengi waone ipo haja sasa ya kulima mazao mengi ya biashara, ukizingatia kuwa sasa wengi wao wanategemea mahindi kama zao la chakula na baadaye huuza kwa mahitaji yao.

“Naamini yapo mazao mengi ambayo endapo yatalimwa kwa wingi, mahindi yatahifadhiwa kwa ajili ya chakula wao na familia zao, maana suala la njaa Handeni linatokea kwasababu kuna mapungufu mengi, hasa ya chakula kuwa haba,” alisema.

Kwa mujibu wa Muhingo, elimu ya ziada kwa wananchi na wakulima wote kwa ujumla inahitajika wilayani humo ili watu wazoee kulima mazao mbalimbali, ukiwamo ufuta, maharage na mengineyo kwa ajili ya biashara na kuweka akiba ya chakula kwa zao la mahindi.
0 comments

NAIBU WAZIRI MAKAMBA ATAKA WANAWAKE KUJIUNGA NA VIKUNDI

            
Raisa Said, Bumbuli.
 MBUNGE wa Jimbo la Bumbuli, January  Makamba amewataka wanawake na vijana wa Jimbo hilo kuanzisha vikundi vya ujasiriamali ili waweze kupata mikopo kutoka taasisi mbalimbali likiwemo shirika la Maendeleo la Bumbuli.
 
Akizungumza kwa niaba  ya  Makamba,Makamu Mwenyekiti  wa Halmashauri  hiyo Bakari Kavumo wakati  wa  uzinduzi  wa kikundi  cha  Tumaini (VIKOBA)  kilichopo  kata   ya Soni alihimiza uanzishwaji wa vikundi na kwamba kufanya hivyo kutawarahisishia upatikanaji mikopo na misaada kwa wahisani.

Pia Mbunge  huyo  alichangia  shilingi 3. milioni  kama  mtaji  wa  kuendesha  kikundi hicho  ambacho kimezinduliwa  katika  jimbo  lake lengo  kubwa  kuwakomboa  wanawake  na umaskini. 

 
Alisema ni vema wananchi hao wakaanzisha  vikundi  maalumu ambavyo vitafahamika kisheria na hivyo kuwa njia mbadala ya kujinasua na umasikini badala ya kutegemea shughuli za mtu mmoja mmoja.
 
Makamba ambae  pia ni  Naibu  Waziri wa  Mawasiliano  Sayansi  na  Teknolojia  aliahidi kusimamia vikundi hivyo na kuhakikisha kuwa akinamama na vijana waliyojiunga wanapata mikopo kutoka Shirika hilo la Maendeleo ya Jimbo la Bumbuli (BDC).

Alisema atatekeleza hayo ikiwa ni miongoni mwa ahadi zake alizozitoa wakati wa kuomba ridhaa ya ubunge kwa wakazi wa Jimbo hilo na kwamba licha ya mikopo hiyo atahakikisha kuwa sekta zote muhimu zinapata mabadiliko huku akiwa na  nia  kuwakwamua  wana  bumbuli  kiuchumi.


Shirika la Maendeleo la Bumbuli lilianzishwa rasmi mwaka juzi na  Mbunge wa Jimbo hilo, January Makamba kwa ajili kuratibu na kuharakisha maendeleo kwa wananchi wa jimbo hilo.

Taasisi ya Utoaji Mikopo ya shirika hilo, BDC-MFI imeanzishwa kama chombo cha kuziba pengo lililopo la ukosefu wa mitaji na vyombo vya utoaji mikopo kwa ajili ya wajasiriamali wa kawaida.
                        MWISHO
0 comments

MWANAHARAKATI ATAKA SERIKALI KUSITISHA MCHAKATO WA KATIBA

MWANAHARAKATI ATAKA SERIKALI KUSITISHA MCHAKATO WA KATIBA 

 

 


Raisa  Said, Tanga
 
Katika hatua inayotishia mchakato wa upatikanaji katiba mpya, mwanaharakati mmoja wa Tanga amefungua shauri linaloitaka serikali kusitisha mchakato  hadi hapo itakapofanyia marekebisho ya masuala ambayo amedai kuwa yanakiuka katiba ya sasa, utawala bora, uwazi, demokrasia na haki ya kijamii.

Mwanaharakati huyo, Dr. Muzamil Kalokola, ambaye ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Kuhifadhi Mawazo ya Mwalimu Nyerere alifungua shauri hilo juzi katika Mahakama Kuu jijini Tanga dhidi ya  Waziri wa Sheria na Masuala ya Katiba Kama mdaiwa wa Kwanza, Tume ya Mabadiliko ya Katiba, kama mdaiwa wa Pili na Mwanasheria wa Serikali kama mdaiwa wa tatu.

Mdai huyo anataka Mahakama itoe  amri kumzuia Waziri wa Sheria na Masuala ya Katiba kutoendelea na mchakato huo hadi hapo shauri hilo litakaposikilizwa.

Pia ameitaka mahakama kutoa amri na  kutamka kwamba Tume ya Mabadiliko ya Katiba imekiuka katiba ya sasa kwa kutoa uwezo ambao juu ya uwezo wao wa kikatiba hususan masuala ambayo yanayohusiana na orodha iliyoko katika Nyongeza ya pili ya Katiba hiyo.

Dr. Kalokola pia ameiomba Mahakama kutamka kwamba uteuzi wa wabubnge wa Bunge la Katiba haukufuata misingi mikuu ya demokrasia kitu ambacho kimeathiri uhalali wa Bunge hilo.

Mwanaharakati huyo ameiomba mahakama kutupilia mbali uteuzi wa wajumbe wa Bunge hilo kwa kutofuata misingi ya demokrasia na uwakilishi.

Katika shauri hilo ameitaka mahaka kuliazimisha Tume ya Mabadiliko ya Katiba kutumia uwezo na wajibu wake kusahihisha udhaifu katika masuala yote ambayo yanakikuka katiba katika muda ambao utatolewa na Mahakama hiyo.

Mwanaharakati huyo pia amezungumzia posho za wabunge hao na kuitaka mahakama kuzikataa kwa sababu zitakua mzigo kwa kiuchumi kwa taifa.

MWISHO
0 comments

MSICHANGANYE MAPENZI NA MASOMO-RC.

MSICHANGANYE MAPENZI NA MASOMO-RC.

NA OSCAR ASSENGA,MUHEZA.

MKUU wa Mkoa wa Tanga,Luteni Mstaafu,Chiku Gallawa amewataka wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wilayani hapa kuacha kujiingiza kwenye mapenzi wakiwa mashuleni kwani hali hiyo itawafanya kushindwa kufikia malengo yao.

Gallawa alitoa kauli hiyo  wakati akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya Potwe kwenye ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo,kusikiliza kero za wanannchi kupitia mikutano ya hadhara kwenye kata na vijiji mbalimbali wilayani hapa.

Alisema wanapaswa kutumia vizuri muda wao wakiwa shuleni kwa kujisomea kwa bidii ikiwemo kupenda masomo ya sayansi ili waweze kuongeza kasi ya wataalamu wa masomo hayo kwa siku zijazo kitendo ambacho kitaongeza hamasa ya wenzao wengine.



    "Hakikisheni mnatumia vizuri muda wenu kwa kusoma kwa bidii kwani hiyo ndio silaha pekee ambazo itawainua kimaisha na kuwakwamua na umaskini walionao kwenye jamii zenu na Taifa kwa ujumla ikiwemo kuacha kujiingiza kwenye mapenzi 'Alisema RC Gallawa.

Akizungumzia suala la upandaji wa miti,Mkuu huyo wa mkoa aliagiza vitalu vya miti kwa shule za msingi na sekondari kuhakikisha wanapanda miti ipatayo 4000 ili kusaidia kuepukana na ukosefu wa mvua na uharibifu unaosababishwa na upepo mkali.

Awali akizungumza kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mkuu wa wilaya ya Muheza,Subira Mgalu alisema wilaya hiyo imeanzisha msako maalumu wa kusaka wazazi ambao hawajawapeleka watoto wao shuleni waliofaulu.

Mgalu alisema ikibainika wanafunzi hao wameozeshwa wazazi
watachukuliwa hatua kali ikiwmo kufikishwa kwenye vyombo vya sheria ili kuweza kukomesha vitendo vya aina hiyo wilayani humo.
      

"Mh.Mkuu wa Mkoa Tumeweka utaratibu wa kutoza faini ya sh.elfu moja kwa wanafunzi watoro ambapo fedha hizo huhesabiwa kwa kila siku aliokosa na hupelekwa kwenye uchangiaji wa ujenzi wa maabara "Alisema DC Mgalu.
0 comments

PICHA: Ajali mbaya mlima Sekenke - Lori la Mafuta lateketeza wanne kwa moto!

PICHA: Ajali mbaya mlima Sekenke - Lori la Mafuta lateketeza wanne kwa moto!

 Kuna ajali mbaya sana imetokea mlima Sekenke muda huu na watu 4 amefariki dunia.Ajali hiyo ilitokea wakati gari la mafuta kufeli breki na kuingia darajani na kulipuka moto.

Ni ajali mbaya sana ambayo ni vigumu kuielezea.




Wanainchi wakiangalia Lori baada ya kuungua

Mabaki ya Lori hilo bada ya kuteketea kabisa na moto jioni hii

Baadhi ya wasafiri wakitazama lori lililongua jioni hii



Bonde la mlima sekenke linavyoonekana na baadhi ya miti imeunguaa


Hii ni njia ya mlima sekenke

Haya ni mabaki ya mwili wa mmoja ya watu walikuwam kwenye Lori hiloo

Moto ukimalizikia kwa mbaliii kama inavyoonekana 

0 comments

Ummy: Nitavalia njuga bei ya gesi

Ummy: Nitavalia njuga bei ya gesi

NAIBU Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Ummy MwalimuNAIBU Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Ummy Mwalimu, ameahidi kulivalia njuga suala la bei za nishati ya gesi kwa lengo la kuhakikisha kila mwanamke wa Kitanzania ananufaika na nishati hiyo.
 
Naibu Waziri huyo alisema hayo alipokuwa akifungua warsha ya mafunzo kwa madiwani wanawake kutoka halmashauri zote za Mkoa wa Tanga yalioandaliwa na Taasisi isiyo ya kiserikali ya Tawode.
Alisema kina mama wengi wamekuwa wakitumia mkaa katika matumizi yao ya nyumbani  kutokana na kushindwa kumudu gharama za nishati ya  gesi ambayo kwa hivi sasa bei yake iko juu.
“Kwa kweli nitalivalia njuga suala hili sitakubali kumuona mwanamke wa Kitanzania akitaabika kutumia mkaa na ikiwa tuna majiko ya gesi tushushe  gharama za majiko haya, ili kuwe na urahisi wa matumizi ya nyumbani,” alisema Ummy.
Mkurugenzi wa Tawode, Fatuma Hamza, alisema mafunzo hayo yana lengo la kuwafundisha viongozi wanawake kujua mbinu za utawala bora kwa maendeleo ya wanawake na taifa kwa ujumla.
Alisema kutokana na msingi huo, taasisi hiyo imeweka kipaumbele cha juu suala la utawala bora na usawa wa jinsia, ili kufanikisha mageuzi ya kisiasa, kiuchumi na kijamii kupitia utekelezaji wa progamu mbalimbali.
Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego, aliwataka madiwani hao wanawake kuhakikisha wanakuwa na mshikamano kwa upande wa kuwatetea wanawake katika bajeti zinazopangwa na halmashauri zao.
Chanzo;tanzania daima
0 comments

TANZANIA YAANDALIWA MAOMBEZI MAALUM YA AMANI

TANZANIA YAANDALIWA MAOMBEZI MAALUM YA AMANI 

 Na Kenneth John

Kituo cha nyumba ya maombezi kimeandaa kongamano maalum lenye dhamira ya kuombea kampeni za uchaguzi mbalimbali ikiwemo uchaguzi mkuu mwaka 2015, pamoja na mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya unaoendelea kwa lengo la kudumisha amani ya nchi.

Akizungumza na waandisha wa habari jijini Dar es salaam muanzilishi na msimamizi wa kituo hicho Apostle Patrick Kayimbi Emmanuel amesema kuwa katika kampeni za uchaguzi kinachofanya kazi sana ni ulimi, kwa maana ulimi ndio unaongea , na pale ulimi usipokuwa na nguvu ya Mungu unaweza kuvuruga amani ya nchi , hivyo wameona ni vyema kuombea uchaguzi wa nchi pamoja na kiungo hicho muhimu , ili kuepusha kutoweka kwa amani.
Ulimi usipotawaliwa na nguvu za mungu utaleta vurugu kubwa sana baada ya kampeni maana familia moja na nyingine hawatapatana tena “Alisema Apostle Patrick.

Aidha ameongeza kuwa watanzania wasifunge mikono kwaajili ya kufurahia amani iliyopo sasa, bali wazidi kuomba amani kwani maombi pekee ndiyo yanaweza kuleta maisha ya amani na utulivu nchini.

Akizungumzia kuhusiana na mchakato wa katiba Apostle Patrick amesema mchakato wa katiba ni miongoni mwa mambo watakayo yaombea kwenye kongamano hilo ni pamoja na mchakato wa katiba, kwa lengo la kuhakikisha katiba ya faida na yenye Baraka kwaajili ya wananchi wote watanzania inapatikana .Halikadharika Apostle ameipongeza tume ya katiba mpya pamoja na Mhe; Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuwapatia watanzania haki ya kushiriki katika mchakato huo, kitu ambacho Apostle Patrick amesema huwa hakifanyiki katika nchi nyingi, na hivyo kuwaomba wananchi kupokea katiba jinsi itakavyoletwa mara baada ya tume kumaliza kazi yake.
Ameongeza kuwa endapo watanzania wote watamlilia Mungu basi mwaka huu utakuwa ni mwaka wa ushuhuda kwa nchi, lakini pia amesema hata vyama vya siasa vitatafautiana kwa sera zao ila lugha zao zitakuwa ni moja.

Sambamba na hayo Apostle Patrick ameiomba serikali kuwasaidia kuanzisha kituo cha watoto yatima, kwa lengo la kuwasaidia watu mbalimbali ambao wamekuwa wakifika kituoni hapo wakiwa na shida mbalimbali huku wakihitaji msaada.Na pia ametoa wito kwa viongozi wa dini mbalimbali pamoja na vyama vya siasa kuzidi kuhubiri amani ndani ya nchi.

Ikumbukwe kwamba kongamano hilo litafanyika Tabata Ugombolwa na litaanza rasmi februari 16 na kuhitimishwa Machi 2 , huku likijumuisha viongozi mbalimbali wa kimataifa ambao ni Bishop Drabraham Mandrandelle(Canada),Prophet Fordger Coetzee(Namibia),Apostle Peter Mwanga(Zambia),Evangelist Freddy Kayimbi(DR Congo) pamoja na Bishop Elie Kabengele(Kenya) Sambamba na mtumishi wa Mungu Peter Mitimingi.

 

0 comments

PILIKAPILIKA ZIKIWA ZINAENDELEA KTK SOKO LA SAMAKI DEEP SEA JIRANI NA BANDARI YA TANGA, SAMAKI WANAONEKANA KUWA ADIMU KUTOKANA NA UPEPO MKALI UNAOVUMA BAHARINI.

PILIKAPILIKA ZIKIWA ZINAENDELEA KTK SOKO LA SAMAKI DEEP SEA JIRANI NA BANDARI YA TANGA, SAMAKI WANAONEKANA KUWA ADIMU KUTOKANA NA UPEPO MKALI UNAOVUMA BAHARINI.








0 comments
KARIBU TANGA, KAZI NA MAPUMZIKO.


WADAU WA BLOG YA TANGA LEO WAKIWA WAMEPOZI ENEO LA DEEP SEA JIRANI NA BANDARI YA TANGA KAMA WALIVYOKUTWA NA BLOG HII ASUBUHI YA LEO



0 comments

AZAM YAANZA AFRIKA, YAWAKALISHA WAMAKONDE CHAMAZI LICHA YA KUBEBWA NA MAREFA ILE MBAYA

AZAM YAANZA AFRIKA, YAWAKALISHA WAMAKONDE CHAMAZI LICHA YA KUBEBWA NA MAREFA ILE MBAYA

Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
AZAM FC imepata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Ferroviario de Beira ya Msumbiji katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali Kombe la Shirikisho Afrika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam jioni hii.
Shukrani kwake mshambuliaji kutoka Ivory Coast, Kipre Herman Tchetche aliyefunga bao hilo pekee dakika ya 41 baada ya kutengewa pasi nzuri ya kichwa na Mganda Brian Umony na kufumua shuti kali.
Mchezo ulikuwa mkali dakika zote 90 na mashambulizi yalikuwa ya pande zote mbili.
Wachezaji wa Azam wakimpongeza Kipre Tchetche leo Chamazi

Mshambuliaji wa Ivory Coast, Kipre Tchetche na Mganda Umony kwa pamoja na Mzanzibari Khamis Mcha ‘Vialli’ walikuwa mwiba kwa safu ya ulinzi ya Ferroviario.  
Kipindi cha pili, Ferroviario walicharuka zaidi na Azam nao walipoteza nafasi kama tatu za kufunga mabao mwanzoni. 
Refa Mutaz Abdelbasit Khairalla na wasaidizi wake Waleed Ahmed Ali na Aarif Hassan Eltom wote kutoka Sudan walionekana kabisa kuwapendelea wageni katika maamuzi yao. 
Dakika ya 70 beki mmoja wa Ferroviario aliunawa mpira wazi wazi kwenye eneo la hatari kufuatia shuti la Kipre Tchetche mbele ya refa, lakini akapeta. 
Kiungo mkabaji wa Ferroviario, de Beira akipiga tik tak dhidi ya mshambuliaji wa Azam FC, Brian Umony leo Chamazi
Kipre Tchetche akimtoka beki wa kushoto wa Ferroviario, Emidio Matsinhe leo

Matokeo hayo yanamaanisha Azam itakuwa na kazi ngumu katika mchezo wa marudiano wiki mbili zijazo nchini Msumbiji, wakitakiwa kulazimisha sare ili kusonga mbele.
Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Mwadini Ali, Erasto Nyoni, Malika Ndeule, Aggrey Morris, Said Mourad, Kipre Balou, Salum Abubakar, Himid Mao, Khamis Mcha/John Bocco dk61, Kipre Tchetche na Brian Umony/Jabir Aziz dk81.
Ferroviarrio; William Manyatera, Zefanis Matsinhe, Emidio Matsinhe, Abrao Cura/Kiki Simao, Edson Morais, Reinildo Mandava, Valter Mandava/Hery Antony, Antonio Machava, Manuel Fernandes, Mario Sinamunda na Manuel Correia/Dje Buzana.  
0 comments

SIMBA SC YAKALISHWA NA MIGAMBO MKWAKWANI

SIMBA SC YAKALISHWA NA MIGAMBO MKWAKWANI

Na Oscar Assenga, Tanga
SIMBA SC imelala bao 1-0 jioni ya leo mbele ya Mgambo Shooting Uwanja wa Mkwakwani, Tanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Kwa mara nyingine leo kipa Ivo Mapunda amefungwa bao rahisi, baada ya kumtemea mpira mshambuliaji Fully Maganga dakika ya 29 kufuatia mpira wa adhabu.
Wachezaji wa Simba SC walipambana sana kujaribu kusawazisha bao hilo tangu hapo, lakini Mgambo Shooting leo walisimama imara kuhakikisha wanaondoka na pointi tatu.

Kwa matokeo hayo, Simba SC inabaki na pointi zake 31 baada ya kucheza mechi 17, wakati Mgambo inatimiza pointi 12 na inaendelea kushika mkia.
Kikosi cha Simba SC leo kilikuwa; Ivo Mapunda, Haruna Shamte/Ramadhani Chombo ‘Redondo’ dk57, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Joseph Owino, Donald Mosoti, Jonas Mkude, Amri Kiemba, Awadh Juma/Uhuru Suleiman dk62, Ramadhani Singano ‘Messi’, Amisi Tambwe na Ali Badru/Haroun Chanongo dk46.
Mgambo Shooting; Saleh Tendega, Bashir Chanache, Salim Kipaga, Bakari Mtama, Novaty Lufunga, Mohamed Samatta, Peter Mwalyanzi, Bolly Ajali, Fully Maganga Malima Busungu.
0 comments

Vigogo wilayani Handeni wafikishwa mahakamani kwa ufisadi wa Milioni 600

Vigogo wilayani Handeni wafikishwa mahakamani kwa ufisadi wa Milioni 600




Na Mwandishi Wetu, Handeni.
 
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wilayani Handeni mkoani Tanga,imewapandisha kizimbani watumishi 12 wa halmashuri hiyo wakiwatuhumu kutumia nyaraka mbalimbali ambazo ni hati za malipo (payment voucher) na kujipatia fedha isivyo halali. Watumishi waliofikishwa mahakamani ni aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo Mpangalukela Tatala, Erasto Vicent ambaye alikuwa injinia wa maji, 

Mkurugenzi wa kampuni iliyokuwa ikifanya utafiti wa kutafuta maji Beda Joseph, Julius Mhando ofisa maendeleo ya jamii, Ofisa Afya wa wilaya Benson Bundala na Maajabu Kambi aliyekuwa mhasibu wa halmashauri hiyo. 

Wengine ni fundi bomba Shabani Mfundo na Ahmad Buraa, Raphael Nkoba aliyekuwa ofisa Afya na sasa ni ofisa afya halmashauri ya mji Handeni, Michael Mosha mkaguzi wa ndani, Hemed Kandarua aliyekuwa dereva na Violeth Swai ambaye ni ofisa elimu sayansi Kimu. 

Akiwasomea mashitaka hayo Mwendedsha Mashitaka wa Takukuru Samwel Gabriel akisaidiwa na Sweetbert Rwegasira mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya Handeni Patrick Maligana, alisema kuwa katika mwaka 2005 hadi 2007 kwa nyakati tofauti watumishi hao walitumia hati za malipo,(payment voucher) na kujijazia na kumdanganya mwajiri wao kuwalipa pesa kwa ajili ya kazi mbalimbali wakati kazi hizo hazikufanyika kama walivyoomba.

Mwendesha mashitaka huyo alisema kuwa kutokana na kitendo hicho watuhumiwa hao waliisababishia serikali hasara ya Sh. 654,944,492.37 kwa kutumia hati za malipo ya uwongo wakiwa na lengo la kumdanganya mwajiri wao.
“Mheshimiwa hakimu kutokana na kitendo hicho watuhumiwa hawa waliisababishia serikali hasara ya Sh. 654,944,492.37 kwa kutumia hati za malipo ya uwongo wakiwa na lengo la kumdanganya mwajiri wao ambapo pesa hizo ni miongoni mwa fedha ambazo zilitolewa na benki ya Dunia kwa ajili ya kufadhili mradi wa kuchimba visima virefu wilaya Handeni,” alisema.

Baada ya watuhumiwa hao kusomewa makosa mbalimbali 49 na la 50 la jumla la kuchukua fedha za safari zikiwa hewa, mwanasheria huyo alisema dhamana ipo wazi na masharti ya dhamana lazima yazingatiwe chini ya kifungu cha 148 (5) cha sheria ya uhujumu uchumi chenye mashariti ya kuwa mtuhumiwa anatakiwa kutoa kiasi sawa na thamani ya mali ya kesi inayomkabili, hivyo kutakiwa watoe milioni 54 kila mmoja. 

Alisema kila mshitakiwa anatakiwa kulipa nusu ya mali anayotuhumiwa nayo ikiwa ni kuanzia shilingi milioni 10 atatakiwa kulipa nusu yake hivyo washitakiwa hao kwa kuwa wanadaiwa kiaisi cha shilingi milioni 600 walitakiwa kila mmoja kulipa shilingi milioni 54 papo hapo na mdhamini pia anatakiwa kutoa fedha hiyo. 

Baada ya wanasheria hao kuwasilisha maombi hayo, hakimu Maligana, alisema kwamba kutokana na vifungu vya sheria ya dhamana vilivyotolewa na takukuru inambidi kuchukua siku saba kusoma sheria hiyo kabla ya kutolea uwamuzi wake, hivyo watumiwa hao walirejeshwa rumande hadi 13 mwezi huu. 

Washitakiwa wote walikana mashitaka lakini walirudishwa tena rumande kutokana na hakimu kuomba muda wa kupitia sheria hiyo na kusema kuwa hawezi kutoa jibu la papo kwa hapo ni lazima afuatilie katika kesi kama hizo kuwa ni maamuzi gani yanachukuliwa.

“Kwanza naomba kuagiza washitakiwa wasiokamatwa wakamatwe haraka,waliohospitali watasomewa mashitaka yao huko huko na mliobaki hapa siwezi kusema mtapata dhamana au hapana kwani nahofia kufanyakazi kiholelaholela ila nipate muda wa kujiridhisha na na vifungu hivi harafu baadae ndio nitoe maamuzi hivyo watuhumiwa wote watarudi rumande hadi tarehe 13 mwezi huu,”alisema Maligana. 

Watuhumiwa kadhaa walijitetea kuwa wanamatatizo hivyo wanaomba kusaidiwa kupata dhamani lakini hakimu alisema kuwa haiwezekani kutokana na vifungu vilivyotajwa vinambana kutoa ruhusa hiyo. waliofikishwa mahakamani walikuwa tisa kutokana na kwamba Mosha amelazwa katika hospitali ya wilaya baada ya juzi kukamatwa kisha kupata mshituko uliosababisha alazwe hospitali, huku Tatala ametolwa taarifa kwamba amelazwa Muhimbili na Lyimo hajapatikana na anatafutwa huku hakimu akisisitiza watu hao watafutwe.
0 comments

NMB WAMKABIDHI NAIBU WAZIRI UMMY VITANDA SABA KWA AJILI YA VITUO VYA AFYA JIJINI TANGA LEO

NMB WAMKABIDHI NAIBU WAZIRI UMMY VITANDA SABA KWA AJILI YA VITUO VYA AFYA JIJINI TANGA LEO

NAIBU WAZIRI WA OFISI YA MAKAMU RAIS MAZINGIRA UMMY MWALIMU AKIZUNGUMZA WAKATI WA AKIPOKEA VITANDA SABA KUTOKA KWA BENKI YA NMB LEO AMBAPO VITANDA HIVYO VINA GHARAMA YA SH.MILIONI 5

KUSHOTO NI MENEJA WA NMB TAWI LA MADARAKA MKOANI TANGA JUMA MPIMBI AKIMKABIDHI VITANDA NAIBU WAZIRI OFISI YA  RAIS MAZINGIRA UMMY MWALIMU WANAOSHUHUDIA NI MEYA WA JIJI LA TANGA OMARI GULEDI NA MBUNGE WA JIMBO LA TANGA,OMARI NUNDU

WAKINA MAMA WAKIOJITOKEZA WAKATI WA MAKABIDHIANO YA VITANDA HIVYO LEO


MKUU WA WILAYA YA TANGA,HALIMA DENDEGO AKIZUNGUMZA KWENYE HAFLA HIYO YA MAKABIDHIANO LEO KWENYE KITUO CHA AFYA MAKORORA JIJINI TANGA.

VITANDA VILIVYOKABIDHIWA LEO NA BENKI YA NMB KWA NAIBU WAZIRI W OFISI YA MAKAMU WA RAIS MAZINGIRA UMMY MWALIMU KWA AJILI YA KUJIFUNGULIA WAKINA MAMA.

MENEJA WA NMB TAWI LA MADARAKA MKOANI TANGA JUMA MPIMBI AKITOA HOTUBA YAKE WAKATI WA MAKABIDHIANO YA VITANDA SABA VILIVYOTOLEWA NA BENKI HIYO KWA NAIBU WAZIRI OFISI YA RAIS MAZINGIRA UMMY MWALIMU KWA AJILI YA AKINA MAMA WAJAWAZITO WAKATI WAKIJIFUNGUA LEO

NAIBU WAZIRI WA OFISI YA  RAIS MAZINGIRA UMMY MWALIMU AKIFURAHIA JAMBO MARA BAADA YA MAKABIDHIANO HAYO LEO

NAIBU WAZIRI OFISI YA MAKAMU WARAIS MAZINGIRA UMMY MWALIMU KULIA AKIPOKEA VITANDA SABA KUTOKA KWA NEMEJA WA BENKI YA NMB TAWI LA MADARAKA JUMA MPIMBI LEO AMBAVYO NI MAHUSUSI KWA AJILI YA AKINA MAMA WAJAWAZITO WAKATI WA KUJIFUNGUA KWENYE KITUO CHA AFYA MAKORORA LEO
0 comments

MAGEREZA MKOA WA TANGA YAANZA MAANDALIZI YA UKARABATI WA OFISI MPYA ZA UTAWALA, JIJINI TANGA

MAGEREZA MKOA WA TANGA YAANZA MAANDALIZI YA UKARABATI WA OFISI MPYA ZA UTAWALA, JIJINI TANGA

 Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga, Naibu Kamishna wa Magereza Edither Malya(wa pili kulia) akielezea hatua mbalimbali za Maandalizi ya ukarabati wa Jengo la Ofisi za Utawala za Magereza Mkoa wa Tanga(wa kwanza kulia) ni Afisa Habari wa Jeshi la Magereza, Mkaguzi wa Magereza Deodatus Kazinja alipotembelea kujionea hatua mbalimbali za ukarabati unaoendelea leo Februari 7, 2014 Jijini Tanga.
 Muonekano wa mbele wa Jengo la Kikoloni ambalo linalotarajiwa kukarabatiwa kwa ajili ya Ofisi za Utawala za Magereza Mkoa wa Tanga. Jengo hilo hapo awali lilitumika kama Kituo Kikuu cha Polisi Mkoa wa Tanga ambapo hivi sasa Jeshi la Magereza tayari limeanza ukarabati wa jengo hilo. Wa kwanza katika picha ni Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga, Naibu Kamishna wa Magereza Edither Malya akiwa ameongozana na baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza leo Februari 07, 2014 Jijini Tanga.
 Tofali ambazo zimefyatuliwa kwa ajili ya ukarabati wa Jengo la Ofisi za Utawala za Magereza Mkoa wa Tanga. Ukarabati huo wa Ofisi mpya za Utawala unaanza hivi karibuni Jijini Tanga na utasimamia kwa karibu na Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga.
 Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga, Naibu Kamishna wa Magereza Edither Malya akiongoza Kikao kazi Ofsini kwake pamoja na baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wanaofanya kazi Ofisi ya Magereza Mkoa wa Tanga leo Februari 07, 2014 alipotembelewa Ofsini kwake na timu ya Maafisa Habari kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Dar es Salaaam(hawapo pichani)
Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga, Naibu Kamishna wa Magereza Edither Malya(wa tatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wanaofanya kazi Magereza Mkoa wa Tanga baada ya kutembelea sehemu mbalimbali ya maandalizi ya ukarabati wa Ofisi  Mpya za Utawala za Magereza Mkoa wa Tanga leo Februari 07, 2014(wa Nne kulia) ni Mnadhimu Mkuu wa Magereza Mkoa wa Tanga, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Augustino Mboje
(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
0 comments
 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger