MWANAHARAKATI ATAKA SERIKALI KUSITISHA MCHAKATO WA KATIBA
Raisa Said, Tanga
Katika hatua
inayotishia mchakato wa upatikanaji katiba mpya, mwanaharakati mmoja wa Tanga
amefungua shauri linaloitaka serikali kusitisha mchakato hadi hapo itakapofanyia marekebisho ya masuala
ambayo amedai kuwa yanakiuka katiba ya sasa, utawala bora, uwazi, demokrasia na
haki ya kijamii.
Mwanaharakati huyo,
Dr. Muzamil Kalokola, ambaye ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Kuhifadhi Mawazo ya
Mwalimu Nyerere alifungua shauri hilo juzi katika Mahakama Kuu jijini Tanga
dhidi ya Waziri wa Sheria na Masuala ya
Katiba Kama mdaiwa wa Kwanza, Tume ya Mabadiliko ya Katiba, kama mdaiwa wa Pili
na Mwanasheria wa Serikali kama mdaiwa wa tatu.
Mdai huyo anataka
Mahakama itoe amri kumzuia Waziri wa
Sheria na Masuala ya Katiba kutoendelea na mchakato huo hadi hapo shauri hilo
litakaposikilizwa.
Pia ameitaka mahakama
kutoa amri na kutamka kwamba Tume ya Mabadiliko
ya Katiba imekiuka katiba ya sasa kwa kutoa uwezo ambao juu ya uwezo wao wa kikatiba
hususan masuala ambayo yanayohusiana na orodha iliyoko katika Nyongeza ya pili
ya Katiba hiyo.
Dr. Kalokola pia
ameiomba Mahakama kutamka kwamba uteuzi wa wabubnge wa Bunge la Katiba
haukufuata misingi mikuu ya demokrasia kitu ambacho kimeathiri uhalali wa
Bunge hilo.
Mwanaharakati huyo
ameiomba mahakama kutupilia mbali uteuzi wa wajumbe wa Bunge hilo kwa kutofuata
misingi ya demokrasia na uwakilishi.
Katika shauri hilo
ameitaka mahaka kuliazimisha Tume ya Mabadiliko ya Katiba kutumia uwezo na
wajibu wake kusahihisha udhaifu katika masuala yote ambayo yanakikuka katiba
katika muda ambao utatolewa na Mahakama hiyo.
Mwanaharakati huyo
pia amezungumzia posho za wabunge hao na kuitaka mahakama kuzikataa kwa sababu zitakua
mzigo kwa kiuchumi kwa taifa.
MWISHO
Post a Comment