BILIONI 2.4 ZAHITAJIKA UKARABATI WA MIUNDOMBINU SHULE YA SEKONDARI TANGA SCHOOL
(Pichani ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Luteni Mstaafu Chiku Gallawa akizungumza na waandishi wa habari leo ofisini kwake)
NA OSCAR ASSENGA,TANGA
JUMLA ya sh. Bilioni 2.4
zinahitajika kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu katika shule ya sekondari ya
Tanga School iliyopo mkoani Tanga kutokana na uchakavu ilionao baadhi ya
majengo kwenye shule hiyo.
Shule
hiyo inahitaji
ukarabati wa miundombinu iliyokuwepo tokea mwaka 1967 ikiwemo
madarasa,maabara,karakana, maktaba, mabweni,bwalo na zahanati ambazo
ukarabati huo utaifanya kuonekana na muonekano mpya.
Kauli hiyo imetolewa leo na
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Luteni Mstaafu Chiku Gallawa wakati akiongea na waandishi
wa habari ofisini kwake ambapo amesema maeneo mengine yanayohitajika ukarabati
ni viwanja vya michezo,nyumba za walimu ,Jengo la Utawala,Chumba cha Kompyuta
na duka na Mgahawa wa shule pamoja na gari la shule.
Gallawa ameongeza kuwa maeneo
mengine ni miundombinu ya maji taka,uzio wa shule,uwekaji wa solar power,ufungaji
wa security lights,ujenzi wa ofisi ya serikali ya wanafunzi,upakaji rangi wa
majengo ya shule na ujezi wa miundombinu ya kuvuna na kuhifadhi maji.
Amesema kazi ya kukarabati
imepangwa kufanyika kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza itagharimu bilioni
1.4 ambayo itafanya ukarabati wa mabweni ya wasichana na wavulana,samani za
madarasa, maktaba, maabara, bwalo,uzio wa shule na nyumba.
Aidha ameongoeza maeneo
mengine kuwa ni Jengo la Utawala,Maegesho ya magari,miundombinu ya
majitaka,ukarabati wa barabara ikiwemo zahanati kufanyiwa ukarabari katika
awamu hii wakati awamu ya pili itagharimu
zaidi ya bilioni 1.Mafundi wakiendelea na ufundi wao kwenye shule hiyo kwenye eneo la karakana. |
Akizungumza mkakati wa
upatikanaji wa fedha hizo,Mkuu huyo wa mkoa amesema kamati maalumu ya kuratibu
zoezi zima imeundwa katika mkoa wa Tanga chini yake ikiwahusisha baadhi ya
wakuu wa shule hiyo waliopita na aliyeko madarakani,wataalamu mbalimbali na
wajumbe wa bodi kwa kuanzia.
baadhi ya majengo yaliyopo kwenye shule hiyo yanavyoonekana wakati mtandao huu ulipotembelea shuleni hapo |
Kamati hiyo imependekeza
mikakati kwa ajili ya kupata fedha hizo ikiwemo kuwakutanisha watu wote
walisoma au kufanya kazi shule hiyo pamoja na kutafuta wahisani mbalimbali
ndani na nje ya mkoa.
Suala lengine litakalo
fanyika ni kuandaa matamasha mbalimbali ikiwemo wazazi za walezi wa wanafunzi
waliopo shule hiyo ambapo kamati hiyo itakutana na wadau walisoma shuleni hapo
Machi 15 mwaka huu kwenye ukumbi wa bwalo la shule hiyo.
Baada ya mkutano huo
makubaliano yataelezwa kwa wadau na mpango wea utekelezaji utaandaliwa
Shule hiyo ilianzishwa mwaka
1895 chini ya utawala wa kijerumani ambapo shule hiyo hapo awali ilijengwa
mjini eneo la mkwakwani ambapo hivi sasa kuna shule ya sekondari Old Tanga.
Post a Comment