NAIBU WAZIRI MAKAMBA ATAKA WANAWAKE KUJIUNGA NA VIKUNDI

            
Raisa Said, Bumbuli.
 MBUNGE wa Jimbo la Bumbuli, January  Makamba amewataka wanawake na vijana wa Jimbo hilo kuanzisha vikundi vya ujasiriamali ili waweze kupata mikopo kutoka taasisi mbalimbali likiwemo shirika la Maendeleo la Bumbuli.
 
Akizungumza kwa niaba  ya  Makamba,Makamu Mwenyekiti  wa Halmashauri  hiyo Bakari Kavumo wakati  wa  uzinduzi  wa kikundi  cha  Tumaini (VIKOBA)  kilichopo  kata   ya Soni alihimiza uanzishwaji wa vikundi na kwamba kufanya hivyo kutawarahisishia upatikanaji mikopo na misaada kwa wahisani.

Pia Mbunge  huyo  alichangia  shilingi 3. milioni  kama  mtaji  wa  kuendesha  kikundi hicho  ambacho kimezinduliwa  katika  jimbo  lake lengo  kubwa  kuwakomboa  wanawake  na umaskini. 

 
Alisema ni vema wananchi hao wakaanzisha  vikundi  maalumu ambavyo vitafahamika kisheria na hivyo kuwa njia mbadala ya kujinasua na umasikini badala ya kutegemea shughuli za mtu mmoja mmoja.
 
Makamba ambae  pia ni  Naibu  Waziri wa  Mawasiliano  Sayansi  na  Teknolojia  aliahidi kusimamia vikundi hivyo na kuhakikisha kuwa akinamama na vijana waliyojiunga wanapata mikopo kutoka Shirika hilo la Maendeleo ya Jimbo la Bumbuli (BDC).

Alisema atatekeleza hayo ikiwa ni miongoni mwa ahadi zake alizozitoa wakati wa kuomba ridhaa ya ubunge kwa wakazi wa Jimbo hilo na kwamba licha ya mikopo hiyo atahakikisha kuwa sekta zote muhimu zinapata mabadiliko huku akiwa na  nia  kuwakwamua  wana  bumbuli  kiuchumi.


Shirika la Maendeleo la Bumbuli lilianzishwa rasmi mwaka juzi na  Mbunge wa Jimbo hilo, January Makamba kwa ajili kuratibu na kuharakisha maendeleo kwa wananchi wa jimbo hilo.

Taasisi ya Utoaji Mikopo ya shirika hilo, BDC-MFI imeanzishwa kama chombo cha kuziba pengo lililopo la ukosefu wa mitaji na vyombo vya utoaji mikopo kwa ajili ya wajasiriamali wa kawaida.
                        MWISHO
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger