TANZANIA YAANDALIWA MAOMBEZI MAALUM YA AMANI
Na Kenneth John
Kituo
cha nyumba ya maombezi kimeandaa kongamano maalum lenye
dhamira ya kuombea kampeni za uchaguzi mbalimbali ikiwemo
uchaguzi mkuu mwaka 2015, pamoja na mchakato wa
upatikanaji wa katiba mpya unaoendelea kwa lengo la
kudumisha amani ya nchi.
Akizungumza
na waandisha wa habari jijini Dar es salaam muanzilishi na
msimamizi wa kituo hicho Apostle Patrick Kayimbi Emmanuel
amesema kuwa katika kampeni za uchaguzi kinachofanya kazi
sana ni ulimi, kwa maana ulimi ndio unaongea , na pale ulimi
usipokuwa na nguvu ya Mungu unaweza kuvuruga amani ya
nchi , hivyo wameona ni vyema kuombea uchaguzi wa nchi pamoja
na kiungo hicho muhimu , ili kuepusha kutoweka kwa amani.
“Ulimi
usipotawaliwa na nguvu za mungu utaleta vurugu kubwa sana
baada ya kampeni maana familia moja na nyingine hawatapatana
tena “Alisema
Apostle Patrick.
Aidha
ameongeza kuwa watanzania wasifunge mikono kwaajili ya
kufurahia amani iliyopo sasa, bali wazidi kuomba amani
kwani maombi pekee ndiyo yanaweza kuleta maisha ya amani na
utulivu nchini.
Akizungumzia
kuhusiana na mchakato wa katiba Apostle Patrick amesema
mchakato wa katiba ni miongoni mwa mambo watakayo yaombea
kwenye kongamano hilo ni pamoja na mchakato wa katiba, kwa
lengo la kuhakikisha katiba ya faida na yenye Baraka
kwaajili ya wananchi wote watanzania inapatikana .Halikadharika
Apostle ameipongeza tume ya katiba mpya pamoja na Mhe;
Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuwapatia watanzania haki ya
kushiriki katika mchakato huo, kitu ambacho Apostle Patrick
amesema huwa hakifanyiki katika nchi nyingi, na hivyo
kuwaomba wananchi kupokea katiba jinsi itakavyoletwa mara
baada ya tume kumaliza kazi yake.
Ameongeza
kuwa endapo watanzania wote watamlilia Mungu basi mwaka
huu utakuwa ni mwaka wa ushuhuda kwa nchi, lakini pia
amesema hata vyama vya siasa vitatafautiana kwa sera zao ila
lugha zao zitakuwa ni moja.
Sambamba
na hayo Apostle Patrick ameiomba serikali kuwasaidia
kuanzisha kituo cha watoto yatima, kwa lengo la kuwasaidia
watu mbalimbali ambao wamekuwa wakifika kituoni hapo wakiwa
na shida mbalimbali huku wakihitaji msaada.Na pia ametoa
wito kwa viongozi wa dini mbalimbali pamoja na vyama vya
siasa kuzidi kuhubiri amani ndani ya nchi.
Ikumbukwe
kwamba kongamano hilo litafanyika Tabata Ugombolwa na
litaanza rasmi februari 16 na kuhitimishwa Machi 2 , huku
likijumuisha viongozi mbalimbali wa kimataifa ambao ni Bishop
Drabraham Mandrandelle(Canada),Prophet Fordger
Coetzee(Namibia),Apostle Peter Mwanga(Zambia),Evangelist Freddy
Kayimbi(DR Congo) pamoja na Bishop Elie Kabengele(Kenya)
Sambamba na mtumishi wa Mungu Peter Mitimingi.
Post a Comment