WARSHA KUHUSU KUENEA KWA HALI YA JANGWA NA UKAME NA MAENDELEO ENDELEVU YA ARDHI YAANZA MJINI BAGAMOYO
Sehemu ya wajumbe wa warsha ya mafunzo kuhusu kuenea kwa hali ya jangwa na ukame na maendeleo endelevu ya ardhi mjini Bagamoyo wakiskliza hotuba iliyokuwa ikitolewa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Injinia Angelina Madete
Kaimu Mkurugenzi wa mazingira ofisi ya Makamu wa Rais bibi
Magdalena Mtenga akimkaribisha mgeni Rasmi Injinia Angelina
Madete aweze kufungua warsha ya mafunzo kuhusu kuenea kwa
hali ya jangwa na ukame na maendeleo endelevu ya ardhi mjini
Bagamoyo
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Injinia Angelina
Madete akifungua warsha ya siku mbili kwa wafanyakazi kutoka
sekta mabalimbali za Serikali juu ya mafunzo kuhusu
kuenea kwa Hali ya jangwa na ukame na maendeleo endelevu ya
ardhi mjini Bagamoyo leo
Wajumbe wa warsha ya mafunzo kuhusu kuenea kwa hali ya
jangwa na ukame na maendeleo endelevu ya ardhi mjini
Bagamoyo leo wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi
katika warsha hiyo Injinia Angelina Madete
Naibu
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Injinia Angelina Madete amesema
ukame umekuwa tatizo kubwa linaloleta athari katika swala zima la
mazingira katika nchi zinazoendelea ikiwamo Tanzania.
Inakadiriwa
kuwa aslimia 73 ya nchi za Afrika zimepunguza uwezo wa kuzalisha
chakula kunakotokana na ukame jambo linalosababisha kuwepo upungufu
mkubwa wa chakula.
Madete
ameyasema hayo leo mjini Bagamoyo wakati wa ufunguzi wa warsha
ya siku mbili kuhusu kuenea kwa hali ya jangwa na ukame wa maendeleo
endelevu ya ardhi.
Alitaja
baadhi ya mikoa iliyoathiriwa na ukame ambayo ni Dodoma, Singida na
maeneo machache ya mikoa ya Shinyanga, Mara, Iringa, Manyara na Arusha.
Warsha
hiyo imewashirikisha wafanyakazi kutoka wizara mbalimbali za Serikali
kwa lengo la kuwaongezea uelewa juu ya umuhimu wa utunzaji wa mazingira
kwa lengo kuepuka janga la ukame.
Akiongea
katika warsha hiyo Injinia Madete alisema kuwa ukame unaleta umaskini
na pia ukame umechangia wananchi wengi kuhama maeneo yao na kwenda
sehemu zingine zisizo na ukame.
Aliendelea
kusema kuwa Serikali imechukua hatua mbalimbali kukabiliana na swala
hilo la ukame amabapo mwaka 1994 ilisaini Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa
Kupamabana na kuenea kwa hali ya jangwa na ukame (United Nations
Convetion to Combat Dessertification UNCCD)
Serikali
inatekeleza mkataba huo kupitia Programu ya Taifa ya kupambana na
kuenea kwa hali ya Jangwa na ukame (National Action Programme to Combat
Dessertification-NAP) ambapo kususdi kubwa la mkataba huu ni kuimarisha
maisha ya kila siku ya mwananchi wa kawaida aishiye kwenye sehemu za
Ukame.
Warsha
hiyo ya siku mbili imewashirikisha pia wadau wa mazingira kutoka sehemu
mbalimbali wakiwemo wafadhili kutoka Shirika la Maendeleo la Umoja Wa
Mataifa (UNDP)
Picha na Habari na Monica Sapanjo
Afisa Habari
Ofisi ya Makamu wa Rais
Post a Comment