MWANAMKE ALIYEPIGWA RISASI ARUSHA AMPA WAKATI MGUMU RPC WA ARUSHA
Toka jana jioni wakazi wa jiji la Arusha wameendelea kuwa katika taharuki na minong'ono hapa na pale kutokana na tukio la kupigwa risasi binti mmoja aitwaye Violeth Mathias katika ofisi za TRA Arusha.Mwanadada huyu aliyeonesha jeuri ambayo haikutegemea si tu Arusha bali katika Taifa hili hasa lile la kwenda na kuchukua Bastola na kutaka kummaliza askari aliyekuwa akitimiza wajibu wake katika Bank ya CRDB. Kitendo hiki kimelfanya wakazi wa jiji hili kuwa na Maswali mengi kuliko majibu. Hasa juu ya anakota jeuri ama kiburi mwanadada huyu.
Viola alikwenda CRDB kuchukua pesa na kilichotokea yeye alipaki gari eneo lisiloruhusiwa kwa mazingira yale ya Bank. Hivyo askari Polisi alimfuata na kumwelekeza kwamba haruhusiwi kupaki gari eneo hilo ila yeye (Mwanadada) huyu hakutaka kusikiliza alichokuwa akiambiwa. Akashuka na kwenda bank ndani.
Hata hivyo Polisi alimfuata ndani ila cha kushanga mwanamke huyu akagoma tena. Ndipo Polisi kwa ajili ya usalama alirudi nje na kutoa upepo matairi yote ya gari kwa tahadhari. Cha kustaajabisha ni pale binti huyo aliporudi na kukuta hali hiyo alipoulizwa alijibiwa polisi ndiye aliyefanya hivyo. Alichofanya alienda kwenye gari lake na kutoka na bastola ati akitaka kumlenga yule askari polisi ndipo yule askari alipoaamu kujihami na kumshug begani.
Baada ya watu kuchunguza wakajua kuwa kiburi hicho anakitia kwa RC wa Arusha Bwa. Magesa Mulongo kwa kuwa anajipumzisha kwake. Wakazi wengi wa hapa wameshangazwa sana namna RC anavyozidi kuchafua nafasi yake hiyo na hata yule aliyempatia.
Cha kusikitisha zaidi ni RPC kuamua kukimbia waandishi wa habari baada ya waandishi kumfuata na kumtaka atoe maelezo juu ya hilo tukio. RPC kuona waandishi wa habari alimwamuru dereva kugeuza gari na kuondoka jambo lililopelekea waandishi wa habari kuamini kuwa RPC atakuwa amepokea maeleekezo toka kwa RC.
RPC alipopigiwa simu aliishia kusema anaelekea Hospitali kwa kuwa Sukari yake haiko sawa hili limepelekea kuaminika kuwa Mulongo anawaweka viongozi wenzie katika wakati mgumu kutokana na tabia zake hizi.
-Jamii Forums
Post a Comment