Na Oscar Assenga, Tanga.
CHAMA cha Mapinduzi CCM
wilaya ya Tanga kinatarajia kufanya mkutano wa hadhara katika kijiji cha Pande
B kata ya Kiomoni jijiniTanga lengo likiwa kuwashukuru wananchi kwa kukiwezesha
chama hicho kupata ushindi katika uchaguzi serikali ya kijiji hicho uliofanyika
hivi karibuni.
Katibu wa Siasa, Uenezi
wa Chama hicho wilaya ya Tanga, Lupakisyo Kapange alisema mikutano hiyo
itafanyika Jumamosi wiki hii eneo la Lwande na baadae jioni watafanyia kwenye kitongoji cha
Kivuleni katika kata hiyo ambapo viongozi mbalimbali watapata nafasi ya
kuzungumza na wananchi hao.
Kapange alisema ushindi
wa chama hicho unaonyesha jinsi gani wananchi walivyokuwa na imani kwao
kutokana na kazi kubwa wanayoifanya kuwaletea maendeleo katika nyanja mbalimbali
ikiwemo ujenzi wa zahanati na barabara.
Katika uchaguzi huo wa
serikali ya Kijiji cha Pande B wapiga kura waliokuwa wamejiandikisha walikuwa
ni 686 waliopiga kura ni 674,zilizoharibika ni 97 hivyo kura halali kuwa ni 577
ambapo kati ya hizo,Chama cha Mapinduzi (CCM)kilipata kura 418,Chama cha
Wananchi (CUF) kilipata kura 128 na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA
)walipata kuwa 31.
Kwa upande wa wajumbe wa
Halmashauri ya Kijiji cha Pande B Chama cha Mapinduzi kilifanikiwa kupata
wajumbe 11 ambao ni Ally Jabiri,Ally Mohamed, Kauli Makame,Yakwesa
Samweli,Salim Kibwana,Salim Bakari, Ally Mchaga,Said Abdallah,Mtoa
Bakari,Hussein Salim na Said Kilo.
Aidha alisema chama
hicho kitaendelea kushirikiana na wananchi katika maeneo mbalimbali wilayani
hapa ili kuhakikisha wanaharakisha kasi ya maendeleo yao pamoja na kueleza sera
za chama hicho.
Hata hivyo Kapange
aliwashukuru wananchi wote wa wilaya ya Tanga kwa kuungana na mkoa katika
shughuli mbalimbali za kiserikali na kichama ikiwemo mapokezi makubwa ya
viongozi wa kitaifa .
Post a Comment