Mwenyekiti wa CCM Kilimanjaro awapa neno wananchi kuhubiri Rasimu ya Katiba pamoja na kufanya kazi za kimaendeleo

Mwenyekiti wa CCM Kilimanjaro awapa neno wananchi kuhubiri Rasimu ya Katiba pamoja na kufanya kazi za kimaendeleo

Na Fadhili Athumani, Moshi
MWENYEKITI wa CCM mkoani Kilimanjaro, Iddi Juma, amewataka Watanzania kuacha kutumia tabia ya kutumia muda mwingi kujadili Katiba na badala yake kujikita katika shughuli za kuimarisha uchumi pamoja na kutatua kero za wananchi.
Kauli ya kiongozi huyo, imekuja wakati viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wamekuwa wakizunguka nchi nzima kuwahamasisha wananchi kutoa maoni yao juu ya Rasimu ya Katiba mpya hasa muundo wa serikali wanayoitaka.
Juma alisema kwa sasa kila mahali utakuta watu wakitumia muda mwingi wa wamekusanyana makundi makundi wakibishana kuhusu Rasimu ya Katiba hasa muundo wa serikali na kusahau kuwa kuna haja ya kujishughulisha ili kuimarisha uchumi wao na uchumi wa nchi.
Mwenyekiti huyo alisema  kujadili Rasimu ya Katiba bila kufanya kazi za maendeleo ni upuuzi utekelezaji Katiiba kunahitaji Fedha na hilo halitawezekana kama wananchi pamoja na Viongozi hawatazinduka na kuona haja ya kutmia muda wao vizuri.

“Viongozi sasa hivi sio wa Chadema, CCM, NCCR-Mageuzi, TLP, vingozi wa dini pamoja na Wananchi wanatumia muda mwingi kujadili ya Rasimu ya Katiba, utakuta watu wakiwa katika makundi wakibishana kuhusu Rasimu, Viongozi hasa hawa wenzetu wanazunguka kila mahali kuhamasisha maoni ya wananchi lakini wanasahau kuwahamasisha kufanya kazi”, alisema Juma
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Moshi Manispaa, Elizabeth Minde akizungumza baada ya chama hicho kutoa msaada wa fedha na vifaa vya nyumbani kwa waathirika wa janga la Moto lililotokea katika mtaa wa sabasaba kata ya Soweto, September 10 mwaka huu, alisema swala la muhimu ni kufanya kazi kwani mwenye njaa kamwe haitambui hata “ingepakwa rangi nyeupe”.
 
Mwenyekiti wa CCM, mkoani Kilimanjaro, Iddi Juma (katikati, aliyevaa kofia), Mwenyekiti wa CCM moshi Mjini, Elizabeth Minde (kushoto kwake) katibu wa CCM manispaa ya Moshi, Aluu Seigamba (kulia kwake) na baaadhi ya viongozi wa chama wakati wakikabidhi msaada kwa familia 12, wahanga wa moto katika mtaa wa sabasaba, kata ya Soweto manispa ya  Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Minde ambaye ni Mwanasheria kitaaluma alisema endapo uchumi wa nchi utayumba, katiba kama ilivyo sheria inaweza ikaonekana haifai hata kama ingekuwa vipengele vizuri kiasi gani.
Katika Hatua nyingine Watendaji wa ngazi za chini wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wamedaiwa kuhujumu ziara za vingozi wa juu wa CCM mkoani hapo pamoja na kukwamisha shughuli za chama katika maeneo wanayosimamia.
Malalamiko hayo yalitolewa jana na Wajumbe wa Mkutano wa Chama hicho katika ziara katika ziara ya Chama cha Mapinduzi katika Manispaa ya Mjini Moshi, Mkoani Kilimanjaro, Wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM mkoani hapa, Iddi Juma.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti huku wakionesha kuchoshwa na manyanyaso wanayopata mikononi mwa watendaji hao baadhi ya WanaCCM katika kata za Soweto, Shirimatunda Kilimanjaro na Karanga walidai watendaji hao wamekuwa wakihujumu ziara za vingozi wa juu wa chama hicho.
Katika mkutano na Wananachama wa Chama cha Mapinduzi katika Kata hizo, Baadhi ya Wajumbe wa mkutano huo waliwaanyoshea kidole watendaji wa ngazi za chini wakiwemo makatibu wa kata na wenyeviti wao kuwa kikwazo kikubwa katika ziara za viongozi wakuu wa chama hicho.
Malalamiko hayo yalikuja baada ya kuwepo kwa hali isiyokuwa ya kawaia ya kuwepo kwa mahudhurio duni ya wanachama pamoja na taarifa za ziara hiyo kutolewa wiki mbili kabla ambapo ilidaiwa kuwa kikwazo ni baadhi watendaji hasa watendaji wa kata za Karanga na Shirimatunda ambao wanadaiiwa kuendekeza rushwa katika utendaji wao.
Hali iyo ilijitokeza baada ya mkutano wa Mwenyekiti huyo katika kata ya karanga iliyojumuisha kata zote tatu za Karanga, Shirimatunda na Soweto kuhudhuriwa na wanachama wachache pamoja na taarifa za ziara ya kiongozi huyo kutolewa wiki tatu kabla ambapo idadi iliyohudhuria kilikuwa hakizidi wanachama mia.
Akizungumzia malalamiko hayo za wananchama hao, Iddi Juma ambaye alionesha kukerwa na hali hiyo, alisema kwa sasa CCM imejipanga kuhakikisha kila mtu anawajibika katkaeneo lake la kazi na kuahidi kufikisha malalamiko hayo katika sehemu husika ili wote wanaotuhmiwa wawajibishwe.
“Hali hii inasikitisha sana, wananchi wanatutegemea kama viongozi wao, Sifa ya kiongozi ni kuongoza katika harakati za kutatua kero za mwananchi sio kuzidisha kero hizo, tutahakikisha swala hili linafika sehemu husika na tutafuatilia”, alisema Juma
Naye Katibu wa CCM manispaa ya Moshi, Aluu Segamba alisema kuwa Chama hakitavumilia uona watu wachache wanainajisi Serikali na kuongeza kuwa watahakisha wanapambana na wahujumu uchumi.
“Watendaji wamekuwa wakilalamikiwa sana, kwa mfano watendaji wetu ambao tunawategemea kama chama tawala wameamua kutuoni jinsi gani wanavyoweza kuinajisi Serikali tena mbele ya macho yetu, mwakani tunaanza harakati za uchaguzi tunahitaji watu makini na hata hawa wanaofanya kazi kwa mazoea tutawatimua wote” alisema Segamba.
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger