Kilimo cha michikichi kutekelezwa Kisarawe;
SHIRIKA la Maendeleo la Taifa (NDC) limesaini makubaliano ya kuendeleza mradi wa michikichi katika Kijiji cha Kimala Misale wilayani Kisarawe katika Mkoa wa Pwani na Kampuni ya Naval Bharat PTE Ltd (NBS) ya Singapore. Mkurugenzi wa NDC, Gideon Nasari akizungumza baada ya makubaliano hayo kuwa mradi huo utagharimu Sh bilioni 160 katika eneo la hekta 10,000
Alisema mbali na kulima michikichi, pia kutaanzishwa kiwanda cha kuchakata mafuta yanayotokana na michikichi.
"Mradi huu utasaidia kupunguza vitendo vya kusafirisha michikichi kwenda nje ya nchi kwa ajili ya kuchakatwa na kupunguza uagizaji wa mafuta hayo kutoka nje ya nchi," alisema Nasari.
Alisema kati ya hekta 10,000 za mradi huo, hekta 2,000 zitawanufaisha wakazi wa Kijiji cha Kimala Misale na masalia ya michikichi yatazalisha umeme wa megawati 10.
NDC itawekeza katika mradi huo kwa asilimia 20 wakati NBS itawekeza kwa asilimia 80, alisema.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa NBS, Devineni Ashwin alisema mradi huo utaanza mara moja tathmini ya mazingira itakapofanyika na kupata vibali.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, Adam Ng'imba alisema wilaya hiyo imekubaliana mradi huo utekelezwe kwa sababu inaamini utakuwa na mafanikio.
Chanzo:mtanzania

Post a Comment