HII NDIO ADHABU ALIYOPEWA MRISHO NGASA.
Mwenyekiti wa Kamati ya Sheria na
Hadhi za Wachezaji, Alex Mgongolwa amesema kamati yake haikumhoji winga
wa Yanga, Mrisho Ngassa ilijitosheleza na maelezo ya kimaandishi.
Ngasa amefungiwa kucheza mechi sita
za mashindano na kutakiwa kuilipa Simba kiasi cha Sh45 milioni kufuatia
kubainika kusajili mikataba ya klabu mbili kwa wakati mmoja.
Klabu yake ya Yanga imekata rufaa
kupinga uamuzi huo, ambapo pamoja na mambo mengine inaona mchezaji wake
hakupewa haki ya kujieleza kufuatia tuhuma alizokuwa akikabiliwa nazo.
Lakini jana wakati Mwenyekiti,
Mgongolwa akizungumza na gazeti hili alisema kamati yake inafanya kazi
na vielelezo vya maandishi, hivyo hawakuona sababu ya kumwita Ngasa.
“Kimsingi, watu wanatakiwa kufahamu,
sisi kama kamati tunatumia maelezo ya maandishi ambayo ndio
vithibitishoi vyetu, na kama ushahidi wa vielelezo utakuwa na upungufu
ndipo tunapomwita mchezaji,” alisema Mgongolwa. Akifafanua alisema:
“Kuna wachezaji wengi usajili wao umeonekana kuwa na matatizo, lakini
hatukuwai kuwahoji.”
SOURCE: MWANANCHI
SOURCE: MWANANCHI
Post a Comment