Mwenyekiti wa CCM wilayani Handeni awalipua wapinzani
Na Rahimu Kambi, Handeni
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wilayani Handeni,
mkoani Tanga, Athumani Malunda, amesema wananchi wengi wamegundua kuwa wapinzani
hawana lengo zuri kwa maisha yao, ndio maana wanazidi kukiamini chama chao.
Mwenyekiti wa CCM wilayani Handeni, mkoani Tanga, Athumani Malunda, pichani.
Akizungumza na Handeni Kwetu Blog, wilayani hapa, Malunde
alisema kwa sababu hiyo, wanaamini kuwa CCM itaendelea kuwa mkombozi kwa
wananchi wote nchini.
Alisema mara kadhaa sera za viongozi wa upinzani zimeshindwa
kujitosheleza, sanjari na kufanya mambo mengi ya kuwagawa Watanzania.
Aidha alijaribu pia kuzungumzia mikakati kabambe ya
kuhakikisha kuwa wanachama wa CCM na Watanzania wote wanaendelea kuthamini
mchango wa chama chao kwa kuongoza serikali kwa ajili ya kuwapatia maisha bora
kwa kila Mtanzania.
“Tunashukuru kwakuwa wananchi wote wameelewa janja ya
wapinzani na namna wanavyotaka kuwayumbisha Watanzania.
“Hili ni jambo jema kwa viongozi wote na ifikie wakati kila
mtu aone namna ya kujiweka sawa na vyama vya upinzani, hasa kama kinachofanywa
ni kuwachanganya Watanzania,” alisema
Malunda, ambaye ni mwenyekiti wa CCM wilayani Handeni, mkoani Tanga.
Post a Comment