Mgombea udiwani mwaka 2010 kwa tiketi ya CUF sasa akichulia chama chake
ALIYEKUWA mgombea udiwani Kata
ya Kwamatuku, wilayani Handeni, mkoani Tanga, kwa tiketi ya Chama Cha Wananchi (CUF),
Mwamini Andrew, amesema haoni sababu ya kubaki katika chama kisichokuwa na
dhamira ya kuwaongoza Watanzania.
Mwamini Andrew, Mgombea Udiwani mwaka 2010 Kata ya Kwamatuku, wilayani Handeni, mkoani Tanga kwa tiketi ya CUF, pichani.
Mwamini ameyasema hayo wakati
hivi karibuni aliuhakikishia mtandao huu kuwa ameamua kuachana na CUF na kuamua
kurudi kuhamia katika Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Akizungumza na Handeni Kwetu
Blog, Andrew alisema kwamba Watanzania wanahitaji kuongozwa vyema na kupatiwa
maendeleo, hasa wale wanaoishi vijijini.
Alisema vyama vya siasa mfano
wa CUF haviwezi kuwa na jipya kiasi cha kuwakomboa Watanzania, hivyo kwake yeye
kuondoka ni jambo lenye mashiko kwa kiasi kikubwa.
“Niligombea udiwani kwa tiketi
ya CUF, lakini kwa sasa hamu sina kutokana na changamoto nyingi zinazokikumba
chama hasa mipango na ushirikiano kati ya wanachama na viongozi kukosekana.
“Naamini mipango yangu ilienda
vizuri, huku nikiamini kuwa lengo ni kufanikisha maendeleo kati ya wananchi na
serikali, sanjari na viongozi wa vyama vyote vya siasa,” alisema Andrew.
Kauli ya kijana huyo inaweza
kuwa mwiba mkal kutoka kwa vijana wanaoamini kuwa chama cha CUF kimepoteza
mvuto ndio maana wengi wamekuwa wakikihama kwa kasi ya ajabu.
Post a Comment