ARSENAL, BARCA zapangwa makundi ya KIFO LIGI YA MABINGWA
MABINGWA mara saba wa Ulaya, AC Milan, waliotolewa na Barcelona katika Ligi ya Mabingwa misimu miwili iliyopita, wamepangwa kundi moja na vigogo hao wa Katalunya katika hatua ya makundi msimu huu baada ya droo iliyopangwa jana. (HM)
Arsenal ambayo kocha wake Arsene Wenger anapambana kusajili jina kubwa kabla ya pazia kufungwa, imepangwa Kundi F pamoja na Marseille ya Ufaransa, Borussia Dortmund ya Ujerumani na Napoli ya Italia.
Mabingwa mara tisa, Real Madrid wamepangwa kundi moja na Juventus, B ambalo pia lina timu za Galatasaray and FC Copenhagen.
Mabingwa watetezi, Bayern Munich wamepangwa na CSKA Moscow, Manchester City na mabingwa wa Czech, Viktoria Plzen Kundi D, ambayo inawapa njia nyeupe ya kufuzu.
Chelsea, mabingwa wa misimu miwili iliyopita, wamepangwa na Schalke 04, FC Basle na Steaua Bucharest Kundi E, timu mbili ambazo ilizifunga kuelekea kutwaa taji la Europa League msimu uliopita.
Mabingwa mara tatu wa taji hilo, Manchester United imepangwa na Shakhtar Donetsk, Bayer Leverkusen na Real Sociedad katika Kundi A.
AC Milan na Barcelona wamekutana mara sita katika misimu miwili iliyopita na Wakalunya wameng'ara dhidi ya Wataliano.
Timu ya Serie A ilifungwa mabao 4-2 jumla katika hatua ya 16 Bora mwaka jana na 3-1 jumla katika Robo Fainali misimu miwili iliyopita, wakati timu hizo zilipokutana pia kwenye hatua ya makundi.
Timu hizo mbili zimepangwa katika Kundi H, sambamba na mabingwa mara nne Ajax Amsterdam na mabingwa wa 1967, Celtic, ambao walikutana na Barcelona katika hatua ya makundi msimu uliopita na kupata ushindi wa kukumbukwa wa nyumbani. Chanzo: binzubeiry
Post a Comment