WILSHERE ATIKISA KIBERTIKI ARSENAL...ASEMA ATAONDOKA WENGER AKIFUKUZWA.
KIUNGO Jack Wilshere amkandia wanaomponda Arsene Wenger na kusema atafikiria mustakabali wake Arsenal iwapo Mfaransa huyo ataondoka klabuni.
Wenger amejikuta katika wakati mgumu The
Gunners kwa kutosajili huku akiwakosa wachezaji aliowataka Gonzalo
Higuain, Wayne Rooney, Luis Suarez na Luiz Gustavo.
Kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Aston
Villa Jumamosi iliyopita kimesababisha mashabiki wa Arsenal, waitwao
Supporters' Trust kusema kwamba itakuwa vibaya kwa bodi kumpa Mkataba
mpya asiposajili hadi dirisha likafungwa.
Onyo: Jack Wilshere amesema ataangalia upya mustakabali wake Arsenal ikiwa Arsene Wenger ataondoka
Mgogoro: Wilshere ameponda kulaumiwa kwa Wenger
Wilshere, pamoja na hayo amesema kwamba atalazimika kuondoka Uwanja wa Emirates kama Wenger akiondoka.
"Nataka kushinda vitu na Arsenal na
ninataka kuwapo huko muda mrefu, lakini ikiwa kocha ataondoka, mambo
yatabadilika," alisema Wilshere akizungumza na Zapsportz.com.
"Arsenal ipo moyoni mwangu wakati wote
na kwa kusaini Mkataba kwa miaka mingine mitano inaonyesha ni jinsi gani
nimeshikamana nao na ni wajibu wao kuniwekea kila kitu vizuri.
Maandalizi: Arsenal itamenyana na Fulham Uwanja wa Craven Cottage mchana wa Jumamosi
"Arsene Wenger amekuwapo kwa miaka mingi na wakati wote ameshinda mataji. Sawa,
tumeporomoka mno kwa miaka mitano au sita iliyopita, lakini ni kocha
babu kubwa na watu ambao wanahoji uwezo wake ni wapuuzi.
"Amefuzu Ligi ya Mabingwa kwa miaka 16, hivyo nafikiri ni mtu sahihi kazini,".alisema.
Wenger aliiongoza Arsenal Jumatano usiku
kuichapa mabao 3-0 Fenerbahce nchini Uturuki, matokeo ambayo yanaiweka
timu katika nafasi ya kufuzu kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya
Mabingwa.
Miaka nane imepita sasa tangu The Gunners imeshinda taji na Wilshere ameanzisha kampeni za kumkingia kifua kocha wake.
Mwaka mwingine: Ushindi wa Arsenal Uturuki unaiweka timu katika nafasi ya kufuzu tena hatua ya makundi ya Lii ya Mabingwa
"Tumepoteza majina machache ya wachezaji
wa nguvu miaka ya karibuni na hiyo ni ngumu kwa klabu yoyote,"alisema
kiungo huyo mwenye umri wa miaka 21 wa England.
"Kwanza tulimpoteza Thierry Henry na kisha Cesc Fabregas, Samir Nasri na Robin van Persie. "Hiyo ni ngumu, hususan wakati Robin alipohamia kwa timu nyingine England, inatupa ugumu wa kushindana.
"Lakini sasa tumepata damu changa ya
wachezaji wa England wanaoibuka na kama tutakaa pamoja na kujenga kitu,
kisha tutashinda mataji katika miaka michache ijayo,".
Impoteza: Kuuza nyota kama Robin van Persie, Cesc Fabregas na Thierry Henry kumesababisha ugumu Arsenal, amesema Wilshere
Post a Comment