Washauri wa rais Obama wakutana kuijadili Syria
Washauri wa rais Barack Obama watakutana katika ikulu ya Marekani ya
White House mwishoni mwa wiki hii kujadili nafasi mbali mbali za nchi
hiyo, ikiwa ni pamoja na hatua za kijeshi, dhidi ya serikali ya Syria.
Washauri wa rais Barack Obama watakutana katika ikulu ya Marekani ya
White House mwishoni mwa wiki hii kujadili nafasi mbali mbali za nchi
hiyo , ikiwa ni pamoja na hatua za kijeshi , dhidi ya serikali ya Syria.Mjadala huo utahusu iwapo serikali ya Syria ilitumia silaha za kemikali katika shambulio mapema wiki hii.
Rais Barack Obama
Uamuzi bado
Lakini afisa huyo ambaye amezungumza kwa masharti ya kutotajwa jina, ametahadharisha dhidi ya matarajio kuwa uamuzi wowote wa mwisho huenda unaweza kutolewa katika duru hii ijayo ya majadiliano.
Wakati huo huo wizara ya ulinzi inayaweka tayari majeshi yake iwapo rais Barack Obama ataamua kuchukua hatua ya kijeshi dhidi ya Syria, amesema waziri wa ulinzi wa Marekani Chuck Hagel siku ya Ijumaa.
Waziri wa ulinzi wa Marekani Chuck Hagel
Lakini amekataa kutoa taarifa zaidi kuhusiana na wapi majeshi ya Marekani yatawekwa pamoja na vifaa huku kukiwa na hali ya kuongezeka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria.
"Wizara ya ulinzi inawajibu wa kumpa rais uwezekano kwa kila aina ya hali," Amesema Hagel.
Manowari ya jeshi la Marekani
Amesema wakati afisa wa wizara ya ulinzi akisema kuwa jeshi la majini litapanua uwapo wake katika bahari ya Mediterranean kwa kuweka meli ya nne ikiwa na uwezo wa kubeba makombora.
Kikosi cha sita cha jeshi la Marekani , kikiwa na wajibika katika bahari ya Mediterranean , kimeamua kuibakisha manowari ya USS Mahan katika eneo hilo badala ya kuiruhusu kurejea nyumbani katika bandari ya Norfolk , jimboni Virginia.
Manowari nyingine tatu hivi sasa zimewekwa katika eneo hilo, USS Gravely , USS Barry na USS Ramage. Meli zote nne za kivita zina makombora kadha ya Tomahawk.
Meli hizo za ziada zinairuhusu wizara ya ulinzi kuchukua hatua za haraka iwapo Obama ataamuru shambulio la kijeshi.
"Rais ameitaka wizara ya ulinzi kutoa mapendekezo mbali mbali. Pamoja na hayo , wizara ya ulinzi iko tayari na imekuwa tayari kutoa uwezekano wa aina yoyote kwa rais wa Marekani ," Hagel amesema.
Ndege ya kivita ya jeshi la marekani F-35
Magazeti ya Marekani yamekuwa yakieleza kuwa kuna hali ya kutokubaliana ndani ya utawala wa Marekani kuhusiana na hatari ya kujiingiza katika vita vingine katika mashariki ya kati.
Post a Comment