Balozi za Tanzania zatumia fedha vibaya : Kabwe
Mwenyekiti wa kamati ya bunge ya hesabu za serikali na mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe amesema balozi karibu zote za Tanzania zina utumiaji mbaya wa fedha za umma yaani matumizi bila utaratibu kufuatwa.
Ameeleza kwamba tatizo lililopo ni tatizo la kimfumo au kimuundo hususan kwenye wizara ya mambo ya nje na kujikuta mahesabu ya balozi yamekuwa na matatizo.
Kwahiyo anaeleza kuwa kamati yake ilichofanya kwanza imeagiza ukaguzi maalum kwa wizara ya mambo ya nje ili pia mdhibiti mkuu na mkaguzi wa hesabu za serikali awasilishe kitu kinachoitwa ukaguzi wa mfumo ili kuweza kujua ni nini kamati yake inaweza kufanya ili wizara ya mambo ya nje isiwe na hoja za ukaguzi nyingi kama ambavyo imetokea hivi sasa.
Akifafanua kwamba ukijumlisha kwa ujumla balozi zote dunia nzima kuna jumla ya hoja za thamani ya shilingi bilioni 5 na kwa hiyo sehemu kubwa moja ya tano ya hizo zote ziko ubalozi mmoja tu wa Washington hapo aliongeza.
Lakini inawezekana kana kwamba ni mfumo tu ulivyokaa inakuwa ni vigumu kwa mabalozi kuweza kuwajibisha zile fedha wanazopewa na fedha ambazo zinakuwa zimekusanywa na fedha nyingi zinazofanyiwa ubadhirifu ni zile ambazo zimekusanywa kwa ajili ya visa na kadhalika ameongeza ukaguzi huu utawapa suluhisho la kudumu kwamba tatizo hili lisijirudie tena.
Na balozi zilizotajwa kuwa na matatizo zaidi ni New York, Canada , Ujerumani, Malaysia,Ubelgiji, London, NewDelhi na Beijing.
Na akijibu swali kuhusu kubainika kuwa kuna ubadhirifu na watu wamehusika alisema "lazima kuwe lazima na uwajibikaji kwa sababu Tanzania hivi sasa kila siku ukisikiliza radio, ukaangalia televisheni, ukasoma magazeti habari unazozipata ni habari za matumizi mabaya ya fedha , lakini yakiibuliwa nini kinachofuata?" aliuliza.
Ndio maana tunataka kila anayehusika na matumizi mabaya lazima achukuliwe hatua akitolea mfano mwaka jana kamati ya hesabu za mashirika ya umma ilipelekea takriban mawaziri wanane kufukuzwa kazi ikiwa kati yao ni manaibu waziri wawili na mawaziri sita kufukuzwa kazi kwasababu za ubadhirifu.
Akisisitiza kwamba ikifanyika kwa mwaka mzima na watu wakawajibishwa kutokana na hesabu mbovu anaamini kwamba watakuwa mfumo mzuri wa uwajibikaji na watu wataanza kuthamini fedha za umma.
Post a Comment