MAKAMBA , KINANA NA WENGINE WACHANGIA
Raisa Said, lushoto.
Zaidi ya Sh. Mil. 41 zimechangwa kwa
ajili ya ujenzi
wa kanisa katika Chuo cha Kumbukumbu ya Sebastian Kolowa (SEKOMU), wilayani Lushoto
katika juhudi za kuwasogezea huduma karibu wanafunzi na
jamii inayozunguka katika chuo
hicho.
Kwa
mujibu wa Makamu
Mkuu wa Chuo hicho, Dk Aneth Munga kati ya
fedha hizo, Sh. mil.22 zilichangwa na Mbunge wa Jimbo la Bumbuli, January Makamba
kwa kushirikiana na baadhi ya Mawaziri, wabunge pamoja
na Katibu Mkuu wa
CCM, Abdulahman Kinana.
Munga
alisema kuwa fedha
zilizochangwa zinawapa matumaini makubwa
ya kutimiza ndoto ya ujenzi wa
kanisa ambao alisema
ili kukamilika kwa ujenzi zinahitajika Sh. Bil.3.
Dk. Munga
alisema kuwa kujenga
si jambo rahisi na kwamba michango
walioipata ni mwanzo
wa ujenzi huo.
Makamu Mkuu
wa Chuo
huyo alitaja sababu za kumualika
Makamba kuwa ni pamoja na mchango wake
katika shughuli za kijamii na kujitoa
kuwa mtetezi wa
amani. Dr. Munga alisema kuwa mara
nyingi ameonekana akisisitiza
juu ya upendo na amani kwa
watanzania.
Kwa upande wake, Makamba, ambaye pia ni Naibu Waziri
wa Mawasiliano Sayansi alisema kujengwa
kwa kanisa hilo ni
chachu katika jamii ya wanafunzi
walioko chuoni hapo pamoja
na wananchi waishio
maeneo ya jirani.
Pia alisisitiza juu ya umuhimu wa kudumisha amani
na upendo uliopo ili Baraka
za
Mwenyezi Mungu ziendelee
kutawala nchini.
Mwisho
Post a Comment