BUMBULI WALIA NA UPUNGUFU WA WATUMISHI

BUMBULI WALIA NA UPUNGUFU WA WATUMISHI

{Beatrece  Msomisi  ambae  ni Mkurugenzi  wa  bumbuli   akipokea  zawadi}
Raisa Said, Bumbuli.
 
 Halmashauri  ya Bumbuli  mkoani  Tanga inakabiliwa na  tatizo kubwa la upungufu wa watumishi jambo ambalo linakwamisha utendaji wa kazi katika Halmashauri hiyo mpya.

Akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri hiyo kilichofanyika Bumbuli mwishoni mwa wikli hii, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauiri hiyo,  Beatrice Msomisi alisema kuwa Halmshauri hiyo ina upungufu mkubwa wa  watumishi ambao alisema kuwa unaathiri shughuli za kazi.

 Msomisi alisema kuwa wakati Halmashari hiyo inaanzishwa ilipewa watumishi 28 ikiwa ni pamoja na madereva.  “Watumishi waliopo hivi sasa ni 1308 ambapo  mahitaji ni  2094  hivyo upungufu  uliopo ni watumishi  786 idara  zilizopo katika halmashauri hiyo zinahitaji watumishi wa kutosha kuendesha shughuli zao za maendeleo,” alisema Mkurugenzi huyo.

Ili kukabiliana na changamoto hiyo, Mkurugenzi huyo alisema kuwa imebidi achukue hatua kadhaa kuhakikisha kuwa kazi zinakwenda kama ipasavyo.

Mkurugenzi huyo  alisema  katika  halmashauri  hiyo  mpya  inakabiliwa  hasa  katika  idara  ya Biashara,  Idara ya Ardhi, Idara  ya  Nyuki pamoja  na  Idara ya  ushirika ambazo  idara  hizo  hazina  mtumishi hata  mmoja.
Hata hivyo  Msomisi alisema  kuwa  mpaka sasa  kuna wakuu wa  idara  wanne  na  wengine  wanakaimu  idara  zingine  na  waliobaki ni watumishi  wa  kujitolea ambapo alisema  kitengo  cha  mwanasheriasheria  wa  Halmashauri  wameajili mmoja kwa  mkataba.
wakati  huo huo  mkurugenzi  huyo  aliwataka  wananchi  wa  Bumbuli  kutoa  ushiriano kwa  watumishi  waliopo lengo likiwa kutoa huduma  bora  na  kuharakisha maendeleo ya kila  mmoja  yanapatikana  pamoja  na  kukuza  uchumi  wa  Bumbuli kwa  ujumla.
           MWISHO
Share this article :

Post a Comment

 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger