Waziri Mukangara awafunda maafisa mawasiliano serikalini
Amesema maafisa hao wamepewa jukumu
kubwa la kuiwezesha serikali kuipitia ofisi zao kufanya mawasiliano na
umma kupitia vyombo vya habari kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu sera
na miradi inayotekelezwa na serikali yenye lengo la kustawisha
maendeleo kwa watanzania.
Amesema kimsingi wasemaji wa wizara ,idara na taasisi wao ndioa wasemaji
wakuu badala ya watendaji wakuu wa sehemu zenu za kazi hivyo serikali inatimiza wajibu wake wa kutoa haki ya msingi ya
wananchi kupata habari hususani zinazohusu utekelezaji wa shughuli
mbalimbali serikalini.
Waziri huyo amesema kikao hicho kimebeba kauli mbiu isemayo "Matumizi ya
mitandano ya Tehama na mitandao katika kuimarisha mawasiliano ya
serikali kwa umma ambapo amewaasa washiriki kutumia fuksa hiyo
ya kuwepo mitandao ya kijamii ili kukidhi kiu ya jamii ya
kupatiwa taarifa mbalimbali za kuelimishwa na kuburudishwa.
Post a Comment