MADIWANI BUMBULI WAPEWA SOMO.
(Katibu wa January Makamba(Hoza Mandia ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Milingano)
Na Raisa Said, Bumbuli
MADIWANI
wa Halmashauri ya Bumbuli, wilayani Lushoto wametakiwa kusimamia ipasavyo
maazimio na mikakati wanayopitisha katika vikao vyao ili kuwaletea
maendeleo wananchi wa Jimbo hilo.
Ushauri huo
umetolewa na Mbunge wa Jimbo la Uchaguzi la Bumbuli, January Makamba
akizungumza katika mahojiano na waandishi wa Habari hivi karibuni kufuatia
kikao maalumu cha wajumbe wa Kamati ya Madiwani wa CCM kilichoitishwa kwa niaba
yake na Katibu wake Hoza Mandia.
Mbunge huyo
amesisitiza kuwa madiwani wanapaswa kusimamia maazimio waaliyoyapitisha katika
kikao hicho ili kuiharakisha maendeleo kwa wananchi wa eneo hilo ambalo limebahatika kuwa Halmashauri
kamili.
Katika maazimio
hayo madiwani walimshauri Mbunge ajipangie utaratibu wa kuwasIliana kwa simu na
madiwani angalau kila baada ya wiki au kadri atakavyoona inafaa zaidi ili
kupata taarifa na kujua changamoto gani zilizopo katika jimbo hilo.
Pia waliazimia
kuwa kero zote za wananchi zinazohusui miradi ya maendeleo ziwasiklishwe kwa
kupitia vikao husijka na madwani wahusike kumuona mkurugenzi ili kupata majibu
ya ufumbuzi wa kero hizo
Kikao hicho pia
kiliazimia kuwa kila diwani awe amekamilisha na kuwasilisha taarifa ya
utekelezaji wa ilani ya CCM kwenye vikao husika ndani ya mwezi mmoja na
nakala ya taarifa hiyo iliyopitishwa iwasilishwe kwa katibu wa CCM wilaya na
kwa mbunge.
Mbunge huyo
alisisitiza kuwa hayo yote yaliyoazimiwa yasimamiwe kwa faida ya wananchi na
Chama cha mapinduzi.
Post a Comment