PATO LA MKOA WA TANGA LAONGEZEKA TOKA TRILIONI 1.78 HADI TRILIONI 2.009
Na Oscar Assenga
Pato
la Mkoa wa Tanga limeongezeka kutoka trilioni 1.78 hadi kufikia
trilioni 2.099 kwa mwaka 2012 ambapo ongezeko hilo ni sawa na asilimia
17.8.
Taarifa
hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Luteni Mstaafu Chiku Gallawa
wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Mkoani hapa desemba
30 mwaka huu kuhusiana na mafanikio ya Mkoa wa Tanga ya mwaka 2012 hadi
2013.
Gallawa
amesema katika ongezeko hilo Mkoa umechangia wastani wa asilimia 4.69
ya pato la Taifa ambalo ni Trilioni 44.7 kwa mwaka 2012 kulinganisha na
37.5 Trilioni kwa mwaka 2011.
Mkuu
huyo wa Mkoa alisema pia pato la mtu mmoja mmoja limeongezeka kutoka
wastani wa shilingi laki 8,86,343 mwaka 2011 hadi shilingi 1,26,432 kwa
mwaka 2012 ambapo wastani wa kitaifa ni shilingi 1,025,038 kiasi ambacho
Mkoa wa Tanga unashika nafasi ya nane kati ya mikoa 25 ya Tanzania bara
tangu mwaka 2010.
Aidha
katika utekelezaji wa malengo ya kukuza uchumi Mkoa wa Tanga umeandaa
mkakati wa kutekeleza miradi kwa kutumia mfumo wa tekeleza sasa kwa
matokeo makubwa kwa miaka 2013 hadi 2015.
Hata
hivyo Mkuu huyo wa Mkoa ameainisha vipaumbele katika maeneo ya kukuza
mapato kwa mtu mmoja mmoja kufikia wastani 1.5, kuendeleza huduma za
jamii za elimu
kwa kuongeza ufaulu kutoka asilimia 32 hadi 60 msingi na sekondari na
maji kufikia asilimia 50 ifikapo 2015 kwa kutoa huduma za maji kwa
umbali usiozidi mita 400 kutoka eneo la makazi.
Post a Comment