Featured Post Today
print this page
Latest Post

MAONYESHO YA KIMATAIFA YA BIASHARA JIJI LA TANGA

MAONYESHO YA KIMATAIFA YA BIASHARA JIJI LA TANGA



 Na Peter Mtulia, Tanga.



Halmashauri ya jiji la Tanga imetoa wito  kwa  wakazi  wake kupitia maonesho ya biashara ya kimataifa yanayoendelea  kwenye viwanja vya Tangamano mkoani hapa kuwa wananchi wapate kutembelea banda lao ili waweze kupata taarifa sahihi kuhusu mji wa Pongwe pamoja na mambo ya usafi wa Mazingira .

     Hayo yamesemwa na mwoenyeshaji wa maonesho haya kwa niaba yah alma shauri Juma Mkombozi wakati akizungumza na redio huruma  viwanjani hapo kuhusu utoaji wa huduma yao kwenye maonyesho hayo ya kimataifa .

  Aidha amesema kuwa lengo la wao kushiriki kwenye maonesho ni kueleza kazi   zao   na shughuli zote za halamashauri kwa wananchi ili wapate ufafanuzi    juu ya mambo ambayo hawayafahamu .

Akielezea shughuli za halmshauri amesema kuwa ni pamoja na  fursa  na maeneo ya uwekezeji yliyopo ktika jiji la Tanga  na kutolea ufafanuzi   wa  shughuli  za wadau wa maendeleo ya jiji.

Sanjari na hayo amesema wakazi wa jiji la hawana budi kutambua kuwa halmshauri  inendelea kufanya jitihada zake kufanikisha kuwa Tanga Televisheni  itaanza  kutumika baada ya muda mfupi  hivyo  wananchi wameombwa kuwa na subira.
 
0 comments

WAZEE MKOA WA TANGA WALIA NA USAWA

WAZEE MKOA WA TANGA WALIA NA USAWA




Na Peter Mtulia, Tanga.
 
BARAZA la wazee mkoani tanga limeiomba serikali kutunga sheria  ambayo itasaidia kuleta hali ya usawa, ulinzi  na usalama kwa wazee ili kuwaondolea changamoto  mbalimbali wanazokumbana nazo katika jamii.

Rai hiyo imetolewa na katibu  wa umoja huo [TARINGO] mkoani hapa ferdolin mbunda wakati akizungumza na redio huruma ofisini kwake amesema kutokana na wazee wengi kutotendewa haki katika jamii serikali haina budi kuingilia kati suala hili kwa kuweka sheria za kuwajali wazee.

Aidha amesema serikali  itoe elimu kwa jamii ili iweze kujua umuhimu wa  wazee kwa kuwajali zaidi ki afya kwa kuweka vituo maalum ambayo yatasaidia  upatikanaji  wa matibabu kwa urahisi ili waweze kuepukana na foleni pale wanapofika mahospitalini.

Wazee hao wameiomba serikali iweke pensheni ya jamii na pensheni ya kawaida ambayo itasaidia wazee kupata huduma za matibabu kupitia maafao ya huduma hizo ili waweze kukidhi mahitaji yao.
0 comments

DENGUE HAIPO TANGA.



DENGUE HAIPO TANGA.

Na Peter Mtulia.

WIZARA ya afya na ustawi wa jamii, kupitia serikali Mkoani Tanga imekanusha madai ya yanayo enezwa wa wananchi juu ya kuwepo wagonjwa wanaougua homa ya  dengue mkoani hapa.

Akizungumzia uvumi wa kuenea kwa ugonjwa huo Mganga Mkuu Mkoa wa Tanga Asha Mahita, amewaambia waandishi wa habari kuwa may 12 walipokea mgonjwa aliyeonesha dalili za ugonjwa huo hatahivyo baada ya kufanyika vipimo ikaonekana hana ugonjwa huo.

Mahita amesema kuwa hata baada ya kufanyika mawasiliano katika wilaya zote za mkoa wa Tanga tarifa za kitabibu zimethibitisha hakuna mgonjwa aliyedhaniwa kuugua Dengue

Hata hivyo Mganga mkuu amewataka wananchi kutosita kuchunguza afya zao katika vituo vya afya pale inapoonekana dalili za ugonjwa huo na kutilia mkazo umuhimu wa kuendelea kufanyIKa usafi wa mazingira ili kuzuia uwezekano wa mbu wa Aedes anaeambukiza ugonjwa huo kuzaliana.
0 comments

WILAYA YA HANDENI YAJIZATITI KTK UZALISHAJI WA CHAKULA



WILAYA YA HANDENI YAJIZATITI KTK UZALISHAJI WA CHAKULA.

Na Peter Mtulia.

WILAYA ya Handeni mkoani Tanga imetangaza kuwa haitaomba tena chakula cha mtaada kutoka serikali kuu kwa msimu ujao kutokana na matarajio ya kuvuna kiasi kingi cha mazao yakiwemo mahindi na ufuta ikilinganishwa na miaka mingine iliyopita.

Mkuu wa wilaya ya Hendeni mkoani Tanga Bw. Muhingo Rweyemamu alitoa kauli hiyo wakati wa ziara yake ya kuwatembelea wakulima katika vijiji mbalimbali vya wilaya hiyo kuangalia utekelezaji wa maagizo ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya hiyo ya kumtaka kila mwananchi kulima kwa bidii na kupanda kwa kufuata maelekezo ya wataalam.

Akiwa katika mashamba ya wakulima wa vijiji vya Manga, Kwamsisi, Kang’anta, Madebe, Misima, Sindeni, Mzeri na Mbagwi wilatyani Handeni, Mkuu huyo wa wilaya Bw. Rweyemamu alisema katika msimu ijao, wilaya hiyo haitaomba tena chakula cha msaada kwa vile wana uhakika wa kuvuna chakula cha kutosha.

Amesema pamoja na kwamba mvua zinazoendelea kunyesha nchini kote zimekuwa zikileta madhara kwa baadhi ya maeneo, lakini kwa wilaya ya Handeni mvua hizo zimeleta neema na faraja kwa wakulima kutokana na kuimarika kwa mazao yao mashambani.

Bw. Rweyemamu  amesema karibu ya maeneo mengi wilayani humo, wamepata mavuno ya kutosha hasa mahindi na ufuta.

Naye Afisa Kilimo wa Wilaya ya Handeni mkoani Tanga Bw. Yibarik Chiza, amesema kuwa wakulima wengi katika wilaya hiyo wamelima kwa kutumia trekta na majembe ya kukokotwa kwa wanyamakazi jambo ambalo amesema litawaongezea ufanisi mkubwa msimu huu.
 
Na kwa upande wao baadhi ya wakul;ima wilayani humo wamesema chakula kitakachopatikana msimu huu wilayani humo hakijawahi kupatikana zaidi ya miaka 30 iliyopita.


0 comments

WAFANYABIASHARA WA SOKO LA TANGAMANO WALILIA HUDUMA YA CHOO.



WAFANYABIASHARA WA SOKO LA TANGAMANO WALILIA HUDUMA YA CHOO.



Sanura Nyangasa /Veronica Julius

Wafanyabiashara wa gulioni maarufu la tangamano wameiomba halimashauri ya jiji la tanga  kuwapatia huduma ya choo kwani imekuwa ni tatizo kubwa  kwa wanaohitaji huduma ya choo katika eneo hilo.

Hayo  yamesemwa na RAJABU SAIDI ambaye nimfanyabiashara wa nguo katika soko hilo katika mahojiano na kituo hiki ambapo   amesema kuwa ukosefu wa choo katika gulio hilo imetokana na choo kilichopo kwa sasa kutumiwa na viongozi tu na kupelekea wafanyabiashara kulazimika kutoka nje ya eneo hilo kufuata huduma hiyo muhimu.

Naye HUSENI AWADHI ambaye pia ni mfanyabiashara  katika  soko hilo amesema viongozi wa jiji la Tanga hawawathamini wafanyabiashara  wadogowadogo (wamachinga) na badala yake kuwajali wafanyabiashara wakubwa.

Sambamba na hayo mama SHEILA ambaye pia ni mfanyabiashara wa soko hilo hakusita kutoa ushauri kwa kusema  wanaomba kujengewa choo katika eneo hilo kwani imekuwa usumbufu kwa upande wao kutokana kulazimika kutoka mbali na biashara zao kufata huduma hiyo muhimu.
0 comments

SEREKALI YAOMBWA KUWASAIDIA VIJANA KUPATA AJIRA



SEREKALI YAOMBWA KUWASAIDIA VIJANA KUPATA AJIRA

Na Rose Sempeho

Kutokana na Vijana wengi kukosa Ajira Serikali imeombwa kutoa fursa za Ajira kwa Vijana ili waweze kujikwamua kiuchumi na kimaendeleo hali itakayopelekea vijana hao kutopotea kimaadili.

Rai hiyo imetolewa na Wafanyakazi wa Kampuni ya Amboni Plantation,Deo Peter Mungia na Gauwa Nyumbwe katika mahojiano na Redio Huruma jijini Tanga ambapo wamesema serikali itoe fursa kwa vijana ili waweze kujikwamua na Umasikini na kujitenga na makundi hatarishi kamavile Wizi Ujambazi na mengineyo ambayo hayaruhusiwai katika Jamii.

Aidha wamesema Vijana wawe mastari wa mbele katika kufanya shughuli za halali ambazo zitawasaidia wao wenyewe kupata kipato chao kwa njia ya halali kama matakwa ya Mungu yanavyosema.

Naye Bi Suzana Sinza ambaye ni mfanyakazi wa Halmashauri ya jiji la Tanga kitengo cha Afya na kinga amasema  ni wajibu wa kila kijana kujua umihimu wake katika jamii kwa kufanya shughuli za kujitolea , kujitunza na kujithamini katika kazi zao kwa kutambua wao ni nani katika jamii.

Sambamba na hayo amewataka vijana kutochagua kazi bali kufanya kazi yoyote ile halali kwani wao ni wategemewa wakubwa katika Taifa la kesho.
0 comments
 
Copyright © 2011. TANGA LEO - All Rights Reserved
Proudly powered by Blogger